Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Jumapili Tulivu

Natumaini umekuwa na wikend njema sana, umejiandaa vya kutosha kuianza wiki mpya, wiki ya kazi. Na kama ilivyo ada, wiki ya kazi Makapuku tunaiheshimu na hata kama hatuna vocha huwa tunakopa salio all in all kufanya kazi na kupata nguvu ya kurudisha mkopo.

Upande wangu nimefurahika na yaliyojiri tangu asubuhi humu, magazeti na shululu , UF/BBC na anko wangu lee empire , historia na Jimena , kile kicard cha kila siku Sakayo bila kuwasahau makapuku wote ambao tumeshiriki katika mijadala kadha wa kadha. Bitoz tumemmiss leo lakini alikuwepo kwa chati, sala na Shunie imekosekana leo. hakijaharibika kitu.

Natamani nimtaje kila Kapuku lakini uwanja wangu ni mdogo sana, maana nimepewa para tatu tu za kupiga blah blah ila wakati mwingine nikipandwa na wazimu naendaga hadi 5 tegemana na siku au nimekula nini.

Muziki sasa, kuna sauti zinavutia kusikiza, na hutokuwa mbishi (ubishi ni kawaida yako mpenzi msomaji-ndo ujue hilo). Sikiza sauti ya kijana wa kizeenji AT na Stara Thomas, unataka kusikia sauti gani nyingine ufurahi? Ya mzee Jangala?

uwe na wakati mzuri na unajua kabisa Kapuku Forum ni sehemu bora kabisa kwa kuwa wewe upo. Na karibuni wageni wote (nimewasahau majina)


Binamu asante imfikie muhenga sakayo popote alipo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom