Makapuku Forum

Makapuku Forum

Hivi unajua kwamba mwanaume anayepitia bar au kwenye chomachoma akachukua nusu kuku akafunga kwenye mfuko akawahi nyumbani mapema ili ale yule kuku mdogo na mkewe na watoo wake wote ana akili, busara na hekima mara 1000 kuliko yule ambaye anapitia kwenye bar hiyohiyo na kuketi na kuchoma kuku watatu na mguu wambuzi ili ale na marafiki zake na akimaliza kushiba anabeua na kutoa pumzi safi na chafu huku akienda nyumbani kwa kuchelewa na tena akiwa mikono mitupu wakati huko nyumbani kwake wana mwezi hawajamnusa kuku. Sasa hapo ndipo utapingana na yule mhenga aliyesema "Akili ni nywele na kilamtu anazake" maana nahisi kunawengine wana upupu kichwani na sio akili #

Bar ninayoendaga mimi ina mbuzi na mishkaki ya kitimoto, ukibeba kuleta home wataugua gout, na mishkaki ya Mzee wa meza ni kharamu wakiwa hawajalewa. Sasa nitakuwaje sina akili
 
Briefly explanations rafiki nilishindwaga kuuelewa! Nieleweshe please

Cc Smart911
Huku ni kama familia zinaishi...yaani life linaendelea kila siku..

Kuna post;

Magazeti asubuhi.
Nukuu ya leo.
Historia
Update za Mpira
Update za habari
Did you knows
Unbelievable Facts
Stori
Upuuzi wa lee
Wimbo/video na unaelezewa woote.

Na stori zingine zozote na kupeana hali halisi ya maisha stori kibao

Wengine humu wanafahamiana nje ya jf..

Karibu feel at home.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom