ZABURI 91
1.Aketiye mahali pa siri pake,Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
2.NitasemaBWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu,Mungu wangu nitakayemtumaini
3.Maana yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji na katika tauni iharibuyo.
4.Kwa manyoya yake atakufunika,Chini ya mbawa zake utapata kimbilio,Uaminifu wake ni ngao na kigao,
5.Hutaogopa hofu ya usiku,wala mshale urukao mchana,
6.Wala tauni ipitayo gizani,wala uele uharibuo adhuhuri.
Muwe na usiku mwema