Makapuku Forum

Makapuku Forum

Sijalalamika nilikuwa namkumbusha bitoz Ku,ungumza lugha yake ya asili

Mbona unajihami hivyo
Oh real? Unamkumbusha tu eeeh

Anyway, sijihami. Mine was just a simple observation kwa sababu mnalalamikia Wasukuma kama vile wao wamekuwa malaika katika taifa hili mpaka wanawakataza kuongea Kindali chenu. Taifa letu halitambui ukabila, ukanda wala udini; na hoja hizi za kuegemea mojawapo ya mambo haya, kwa maoni yangu ni mufilisi tu.
 
5982bb1ab81e4e7002dbf78ed4150021.jpg
 
Katika dondoo za bbc.

Zaidi ya watu laki moja na elfu arobaini nchini Kenya asilimia 60 ikiwa ni wanawake wanatarajiwa kufaidi mradi wa miaka mitano wa Umoja wa Ulaya, unaolenga kuimarisha kiwango, ubora na uuzaji wa mihogo katika soko la ndani na la kimataifa.

Jana wapenzi wa Soka katika ukanda wa Afrika Mashariki wameshuhudia mtanange kati ya Everton ya England na Gor Mahia inayojulikana kama KOGALO, ya Kenya.

Barabara kati ya Kenya na mpaka wa Ethiopia wakati mmoja iliogopwa sana kutokana na majangili waliokuwa wakiwapora watu na mifugo. Lakini sasa mji wa mpakani wa Moyale kaskazini mwa Kenya imebadilika na kuwa kituoa muhimu cha kibiashara kutokana na ujezi wa barabara kuu katika eneo hilo.

Simba waliotoroka kutoka katika mbuga ya wanyama ya kruger nchini A-Kusini.Sasa imethibitishwa simba hao wameuwawa na walinzi wa mbuga hiyo baada ya kushindwa kuwadhibiti

Nchini Rwanda kampeni za uchaguzi utakaofanyika mwezi wa 8,zinaanza kutimua vumbi leo na kudumu kwa siku 19.baadhi ya wagombea wanalalamika kuwa muda wa kunadi sera zao ni finyu sana ikizingatiwa na uwezo mdogo kifedha walio nao.

Watu watatu wameuwawa nchini Kenya siku ya jana katika shughuli ya kumwokoa afisa mkuu wa Serikali mikononi mwa Al Shabaab katina eneo la Lamu. Katibu wa kudumu katika wizara ya Kazi za Umma Mariam El Maawy na wengine watano walitekwa nyara na AL Shabaab katika barabara ya mpeketoni kuelekea Lamu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom