
UFUNUO 3
8.Nayajua matendo yako,Tazama nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako,ambao hapana awezaye kuufunga,kwakuwa unazonguvu kidogo,nawe umelitunza neno langu,wala hukulikana jina langu

Mwana wa Mungu ,Baba anasema nawe anayajua matendo yako na amekuachia nafasi ya kuamua kuingia katika mlango alioacha wazi ili uweze kuwa na furaha na amani,MUNGU anatufahamu vizuri sana na anajua tunazo nguvu kidogo za kuishi maisha matakatifu na kuacha dhambi ili siku ya mwisho tukamwone na Kuishi naye milele,shida,changamoto ,magonjwa,dhiki,kukosa ada,kukosa chakula,kukosa kodi ya nyumba,kukosa kazi,kukosa mume,kukosa mke ,kukosa amani na tabu ni hila za shetani kutukwamisha kuingia mlango wa neema ambao ameufungua uko wazi...tunapaswa kuomba sana,kusoma neno la Mungu ili tuweze kumshinda shetani maana MUNGU ametupa nguvu hizo.Mchana huu wa leo nakualika ukaze mwendo,nguvu kidogo ulizonazo si haba ,zitakufikisha kwenye ufalme wa Mbinguni...Fanya bidii ya kushiriki yale yanayompendeza Mungu ili uingie kwenye mlango huu umshinde shetani...maana HAKUNA AWEZAYE KUUFUNGA...SHALOM..MCHANA MWEMA
