Makapuku Forum

HESABU 6

24."BWANA Akubarikie na kukulinda"

BABA Asante kutuamsha salama siku ya leo ,hatuna la kusema zaidi ya Asante,tunajikabidhi Mikononi mwako siku ya leo utuondoe katika hatari mbalimbali na ajali mbalimbali za mwili na za roho,utuopoe kila tuingiapo hatarini Mfalme wa Amani.

Ponya wagonjwa wape nguvu wafiwa wajane yatima wape tumaini la kudumu,wasaidie wenyechangamoto mbalimbali wakumbuke baraka zote tangu kuzaliwa hadi siku ya leo.

Mahali hapa MAKAPUKU tupate maarifa,tupate furaha,tupate faraja pawe kimbilio la wengi wenye mapenzi mema.

Tunakushukuru sana kwa baraka tele unazotujalia za marafiki,kazi ,chakula,Amani,mavazi,uhuru,upendo,mshikamano,masomo,maarifa ,uponyaji,kukujua wewe,kukupenda na kukuheshimu Baba hatuna mwingine kama wewe asante kwa kuwa hujawahi kuchoka kila siku umetenda mema na makuu kwetu.
Zidisha upendo mahali hapa ,tupe mshikamano na furaha ya kweli tusaidie tufahamu mahitaji ya kila mmoja wetu na kuombeana Amani

Walinde wasafiri wafike salama,wagonjwa wainuke katika vitanda na kupata kupona,wasio na makazi wape makazi ya kudumu ee BABA,wasio na ajira wape maarifa na mbinu bora za kuishi,boresha mahusiano ya familia,ndoa,uchumba kila mmoja ajue kusudi lako katika maisha.
Asante kwa ulinzi BABA,Tunaomba yote yafanyike katika utukufu wa jina lako takatifu jina la Yesu,Damu yake takatifu itufunike.
Amen

NAWATAKIA SIKU NJEMA SANA MBARIKIWE
 
Asante sana Husna.

Angalizo: katika hali yotote ile mama akijisikia ni mjamzito (amekosa siku zake za maua)kwa namna yoyote kama alikua anatafuta mtoto au imetokea tu bila taarifa ni muhimu kwenda hospitali,kufanyiwa vipimo maalumu vya awali vya ukuaji na maendeleo ya mtoto pia afya ya mama,bahati nzuri siku hizi utaalamu na vifaa vimeongezeka na hata inasaidia kuokoa mama na mtoto aliye tumboni na hatimaye atakayezaliwa...tusikae nyumbani kungoja dharura..nimeona watu wengi wakiokoa uhai kwa kuwahi hospitali na nimeona watu wengi wakipoteza uhai kwa kuchelewa kufika hospitali..dawa mbadala ni nzuri kukinga lakini kwa wajawazito zinahitaji uangalifu na ufuatuliaji wa karibu sana .

MUNGU ametupa nafasi ya kushiriki uumbaji kwa kukutana na mume , kubeba mtoto miezi tisa tumboni tuiheshimu hii zawadi ya uhai na tuitunze maana MUNGU AMETUHESHIMU.Kushiriki ulinzi,uhai na maendeleo ya mtoto,kuna mambo yanazuilika ukiwahi hospitali MBARIKIWE
 
Ubarikiwe Obe..hii MUZINA imenikumbusha mbali sana asante sana ngoja nirudie na Kurudia.
 
Katika dondoo za bbc. ...

Majeshi ya Iraq na Marekani yamesema wapiganaji wa Islamic State wameulipua msikiti mkubwa wa al- Nuri uliopo mjini Mosul na pamoja na mnara wake mkongwe uliodumu karne na karne.

Viongozi wandamizi wa mataifa makuu matano yanayojumuika katika ushirika wa bonde la mto Nile wanakutana nchini Uganda kujaribu kutanzua tofauti zilizosababishwa na mapatano ya Entebbe kuhusu matumizi ya maji yamto huo.

Wakimbizi kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo walioko katika kambi za wakimbizi nchini Rwanda wanalalamikia kupungua kwa idadi ya wanaohamishwa kutoka kambini na kwenda kuishi nchini Marekani.

Mahakama ya kikatiba nchini A-Kusini ambayo ndio yenye uamuzi wa juu kabisa leo itaamua iwapo kura ya siri inaweza kutumika bungeni kumuondoa rais Jacob Zuma madarakani .

Nchini Tanzania ,Dr.Askwari Hilonga mtaalamu wa masuala ya Uhandisi wa kemikali ameamua kutumia taaluma yake kutatua matatizo yanayosababishwa na maji kutokuwa safi na salama katika jamii inayomzunguka.

Uchafuzi wa mazingira ya ziwa Tanganyika kwa upande wa Burundi umekua ukitia wasiwasi mashirika ya kimataifa na hata ya raia wa nchi hiyo ya kulinda mazingira kwa ujumla.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…