Makapuku Forum

ZABURI 133

1 Tazama ulivyo vema na kupendeza Ndugu wakae pamoja kwa umoja

2 Ni kama mafuta mazuri kichwani Yashukayo ndevuni ndevu za Haruni Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake

3 Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni maana ndiko BWANA aliko amuru Baraka Naam uzima hata milele

Kupitia wimbo huu wa mfalme Daudi, tunakumbushwa kuwa na UMOJA katika maisha ya kila siku katika familia jamii na taifa MUNGU anapendezwa na UMOJA kama alivyodhihirisha katika UTATU wake wa BABA MWANA NA ROHO MTAKATIFU

MUNGU BABA asante kutuamsha tena asante kwa NENO "UMOJA"wewe uliye asili ya mema yote utupe huo UMOJA na UPENDO maishani mwetu utuimarishe kila mmoja kwa mwenzake katika familia na jirani zetu na hata taifa letu kipekee ulibariki kundi hili la MAKAPUKU lidumu katika kujifunza bariki kazi za mikono yetu biashara na wanaotutazama wauone Ukuu wako wapate kukutukuza katika jina la Yesu Kristo Amen Asante


NAWATAKIA JUMAPILI NJEMA IBADA NJEMA MBARIKIWE
 
Tunashukuru sana kwa neno
 
Amen
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…