Makapuku Forum

Makapuku Forum

b6acdbd605b17370ac0fcd3cb2eac910.jpg
 
Muziki na Makosa

Ni wakati wingine tena tunakutana hapa hapa pa siku zote Makapuku wenzangu. Natamani kuwaita waheshimiwa makapuku lakini kila nikitaka kutamka hivyo ulimi unakuwa mzito, ulimi zege, maana wale waheshimiwa kule bungeni hawajui hata wanafanya nini na bado wanajiita waheshimiwa. Waheshimiwa wabaki mahakimu tu

na hii ndo sababu ya kuchukia kuitwa mkuu, maana kuna mkuu hana vyeti, mwingine kala rambirambi, mwingine alitaka kuhongwa na ACACICIA huku ndo akiwa kichwa kabisa na bahati mbaya si TAKOKURU wala TBS waliojitokeza kuangalia viwango. Wakuu wabaki walimu tu

Najua kabisa kutenda makosa ndo ubinadamu, uanamume na uanamke na si zaidi ya hapo. inakuwa mbaya sana pale unapofanya makosa na ukawiwa kabisa na nafsi kwamba umefanya makosa ila kwa kibri tu unajikausha na kuamua kusingizia wengine wasiotenda uliyotenda kuwa ndio waombe msamaha. yaani hii ni sawa na makanikia na sisiemu jumlisha uzalendo wa nchi yetu. Ipo siku, yana mwisho kama alivyowahi kusema Shafi katika Kuli.

Hivi naandika nini hapa, najishangaa lakini vidole vinazidi kutiririka tu kuelekea chini.

Les Wanyika ndo tunao leo humu kwenye muziki na utamu wa gitaa, unaikumbuka Shilingiu Yaua tena Maua, pamela na nyingine tamu nyingi? Well kama hukumbuki ngoja nikukumbushe kidogo.

Wanyika band zilikuwa zinaongozwa na Wakenya na Watz ambao miaka ya 70 walikimbia uchumi mbovu kwenye tasnia ya muziki nakwenda Kenya huko wakaanzisha band na kupata mafanikio makubwa ambayo hata hivyo hawakudumu sana. nawaongerea kina Kinyongas na Ngereza. siku nyingine tutawaangalia ndugu hawa ila leo tupate kibao chao matata sana

Ni clip ya YouTube, na kaa ukijua hiki si kipengele cha zilipendwa bali muziki na utamu wa gitaa


Asante Obe ubarikiwe
 
Aaa wapi! Wanawake wapo wa kulala nao tu lakini ukianza kutafuta yule mmoja wa mpaka kifo aisee ni zoezi pevu. Hasa ukiwa umeshamaliza vihitaji hivi vya msingi msingi kazi ni ngumu zaidi kwa sababu huwezi kujua kama mtu anakupenda wewe kama wewe au anapenda hivyo vihitaji hitaji vyako ulivyonavyo. Ni kusali na kuomba sana japo nadhani pia kwa hali ya sasa si lazima sana kuoa...Jaza Ujazwe!
Tatizo mmefunga macho ila mkifumbua tu hayo macho basi mtatuona na mkiacha hayo mambo yenu magumu kwetu
 
Aisee! Ni kiungo cha aina yo yote kinapokuwa transplanted? May be it is a moot question kwa vile hatujaweza bado kufanya transplant ya ubongo. Kuna mambo mengi bado hatuyajui kuhusu miili yetu, viumbe wengine na malimwengu kwa ujumla.

Kama jana hapa nilikuwa nawasikiliza wanasayansi wakijaribu kueleza maji yaliyojaza robo tatu ya uso wa dunia yalitoka wapi aisee ni kizungumkuti...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom