Muziki na Makosa
Ni wakati wingine tena tunakutana hapa hapa pa siku zote Makapuku wenzangu. Natamani kuwaita waheshimiwa makapuku lakini kila nikitaka kutamka hivyo ulimi unakuwa mzito, ulimi zege, maana wale waheshimiwa kule bungeni hawajui hata wanafanya nini na bado wanajiita waheshimiwa. Waheshimiwa wabaki mahakimu tu
na hii ndo sababu ya kuchukia kuitwa mkuu, maana kuna mkuu hana vyeti, mwingine kala rambirambi, mwingine alitaka kuhongwa na ACACICIA huku ndo akiwa kichwa kabisa na bahati mbaya si TAKOKURU wala TBS waliojitokeza kuangalia viwango. Wakuu wabaki walimu tu
Najua kabisa kutenda makosa ndo ubinadamu, uanamume na uanamke na si zaidi ya hapo. inakuwa mbaya sana pale unapofanya makosa na ukawiwa kabisa na nafsi kwamba umefanya makosa ila kwa kibri tu unajikausha na kuamua kusingizia wengine wasiotenda uliyotenda kuwa ndio waombe msamaha. yaani hii ni sawa na makanikia na sisiemu jumlisha uzalendo wa nchi yetu. Ipo siku, yana mwisho kama alivyowahi kusema Shafi katika Kuli.
Hivi naandika nini hapa, najishangaa lakini vidole vinazidi kutiririka tu kuelekea chini.
Les Wanyika ndo tunao leo humu kwenye muziki na utamu wa gitaa, unaikumbuka Shilingiu Yaua tena Maua, pamela na nyingine tamu nyingi? Well kama hukumbuki ngoja nikukumbushe kidogo.
Wanyika band zilikuwa zinaongozwa na Wakenya na Watz ambao miaka ya 70 walikimbia uchumi mbovu kwenye tasnia ya muziki nakwenda Kenya huko wakaanzisha band na kupata mafanikio makubwa ambayo hata hivyo hawakudumu sana. nawaongerea kina Kinyongas na Ngereza. siku nyingine tutawaangalia ndugu hawa ila leo tupate kibao chao matata sana
Ni clip ya YouTube, na kaa ukijua hiki si kipengele cha zilipendwa bali muziki na utamu wa gitaa