Makapuku Forum


Alikuwa na umri wa miaka 62
Alizaliwa 1908
......

Wakati najisomeasomea elimu za darasani, nilivutiwa naye sana.
Hakujikita katika mambo hasi yanayomfanya mtu asifanikiwe, yeye aliamini kila mmoja wetu ana uwezo wa kufanikiwa kwa kuwa tu tuna vipawa tofauti, na hasa tukitia jitihada kuboresha maisha yetu. Aliandaa hii inayoitwa 'hierarchy of needs'.

Ili ufanikiwe, kuna ngazi lazima uzipande, na ngazi moja hufanya hamu ya kupanda zaidi.
Ngazi ya kwanza; Mahitaji ya kimwili na kiasili: Unahitaji kula , kunywa , malazi, kulala na kulalana. Physiological and biological needs

Ngazi II: Mahitaji ya kuwa salama, hapa anasema ili ufanikishe ndoto zako baada ya kuwa umeshiba kimwili na kiafya basi ni lazima uwe na uhakika wa usalama wako pindi unatekeleza majukumu ya kujitafutia kipato iwe shambani (kule kibiti /Rufiji ni ngumu), usiwe na hofu.

Ngazi ya III: Mahitaji ya mapenzi na kujinasibisha, hapa kila mmoja ana haki ya kupendwa, ukaribu (intimacy), kuaminiwa na kukubalika (love and belongingness)

Ngazi ya IV: Esteem needs , weee Mondray hebu njoo uweke link hapa ili kujua kwamba kuna hitaji la kujithamini, kutojiweka chini
Na ngazi ya tano ni kujitambua wewe ni nani na unajukumu gani. Hii utaifikia baada ya kuwa umepitia ngazi zote hizo.

Labda tu kwa kuongezea hapa, kuna hitaji/motisha ya utambuzi. Ukiweza kutambua na kuelewa kupitia maarifa tofauti uhakika wa kufanikiwa ni mkubwa tofauti na ukiwa bwege mtozeni, utatoswa hata na wanasiasa wajinga wa mwisho. Soma soma, angalia news, pitia Makapuku nk

Pia kuna motisha ya kujiweka smart, ndo maana watu hawakauki gym kujenga mwili , kujipodoa ukapodoka (aesthetic needs), kutafuta kakitambi kaheshima kama nilikonako.

Na pia kuna motisha ya kuwasaidia wengine kufanikisha ndoto zao (transcendence needs) hapa ndo unakutana na waombeaji wote, walimu na wewe Kapuku unayesoma hapa.
Well, nimeandika sana eeh. Pole na asante kwa kumsoma Mussolin5 na leo katika historia
 
 
Mama mchungaji unatakiwa uanze maombi maalum ili taifa liweze kulipa madeni y'a nnje n'a ya ndani tunakarbia trilion 100 sasa
Ukweli tunapaswa kuombea taifa letu ,mambo ni mengi mno ,mahali hapa tunaweza kuungana pamoja kuomba na kuona ukuu wa Mungu katika kila jambo

YAKOBO 5

16.b...kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana,akiomba kwa bidii.

17.Eliya alikua mwanadamu mwenye tabia moja nasisi,akaomba kwa bidii mvua isinyeshe,na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.

18.Akaomba tena,mbingu zikatoa mvua,nayo nchi ikazaa matunda yake.

Shalom
 
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…