Sawa tutakufikiria ikulu itakuwa mtaa wa ngapi, nasikia mtaa wa 7 watu wanapakimbia.Kama rasimu ya katiba itapitishwa kuna umuhimu mkubwa wa mkoa wa Tanga ufanywe kuwa makao makuu ya Tanganyika kwa sababu zifuatazo:
1- Tanga ina historia nzito na nyeti!
2- Tanga ina bandari kongwe na iko mahali strategia zaidi!
3- Tanga ni mji wa kwanza Tanganyika kupata hadhi ya manispaa!
4- Tanga ni mji uliostaarabika kwanza kabla ya miji mingine kwa kuwa na mahakama za mwanzo wakati wa Mjerumani!
ukichanganya na ujenzi wa kinidhamu wa mitaa ya Tanga, na sifa zingine nyingi zinaipa hadhi jiji hilo kuwa makao makuu ya Tanganyika ijayo! Dar es Salaam iendelee kuwa makao makuu ya Tanzania badala ya Dodoma!
Arusha ni mahali muafaka kabisa.
[1] Hali ya hewa ni nzuri
[2] Viongozi watakuwa na uwezo wa kuvaa suti katika kipindi kirefu cha mwaka bila kutumia AC na kuongeza gharama kwa walipa kodi.
[3] Arusha ni makao makuu ya EAC.Kwakuwa wizara ya EAC si suala la muungano tena baada ya kuzaliwa nchi ya Tanganyika hii itasaidia kupunguza gharama za usafiri maafisa wa serekali.