Makao Makuu ya Tanganyika: Mapendekezo

Kadogoo

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,073
341
Kama rasimu ya katiba itapitishwa kuna umuhimu mkubwa wa mkoa wa Tanga ufanywe kuwa makao makuu ya Tanganyika kwa sababu zifuatazo:
1- Tanga ina historia nzito na nyeti!
2- Tanga ina bandari kongwe na iko mahali strategia zaidi!
3- Tanga ni mji wa kwanza Tanganyika kupata hadhi ya manispaa!
4- Tanga ni mji uliostaarabika kwanza kabla ya miji mingine kwa kuwa na mahakama za mwanzo wakati wa Mjerumani!
ukichanganya na ujenzi wa kinidhamu wa mitaa ya Tanga, na sifa zingine nyingi zinaipa hadhi jiji hilo kuwa makao makuu ya Tanganyika ijayo! Dar es Salaam iendelee kuwa makao makuu ya Tanzania badala ya Dodoma!
 
Arusha ni mahali muafaka kabisa.

[1] Hali ya hewa ni nzuri

[2] Viongozi watakuwa na uwezo wa kuvaa suti katika kipindi kirefu cha mwaka bila kutumia AC na kuongeza gharama kwa walipa kodi.

[3] Arusha ni makao makuu ya EAC.Kwakuwa wizara ya EAC si suala la muungano tena baada ya kuzaliwa nchi ya Tanganyika hii itasaidia kupunguza gharama za usafiri maafisa wa serekali.

Why not Kigoma.,

1. Lake Tanganyika is there so viongozi watapata nafasi ya kula samaki fresh toka ziwani!
2. Ni asili ya wanamuziki wengi wa bongo fleva, waheshimiwa viongozi wataburudishwa kiurahisi sana
3. Kuna Chikichi source nzuri ya mafuta
4. Kuna ............
 
TANGA ( TANGA - nyika)

Tunawaletea taarifa ya habari kutoka Tanga nchini Tanganyika.

Hii imekaa vizuri lakini ili ikae vizuri zaidi tubadilishe mkoa wa Dodoma uitwe Tanga na Tanga uitwe Dodoma ili kuubeba mkoa wa Tanga hadi katikati ya nchi.

AU makao makuu yawe KIGOMA karibu na ziwa Tanganyika.

kwa mtu anayejua kufikiri kwa kina atasema kwa nini isiwe dar es salaam au Dodoma ili kupunguza mvutano usio wa lazima wa umimi.
 
Kabla hatujapendekeza mkoa mwingine kuwa makao makuu ya nchi, tujiulize swali, kwani wale waliopendekeza Dodoma kuwa makao makuu walikuwa na sababu zipi? Lakini pia kueleza 7bu ya Tanga kuwa na historia nzito na Nyeti haina tija kwakuwa ni mikoa mingi yenye historia nyeti na existence ya Tanganyika + Tanzania. Dodoma ibaki kuwa makao makuu ya nchi yetu.
 
Warioba kaleta matatizo badala ya kutatua matatizo katiba ingetakiwa ituletee njia ya maendeleo badala ya kuongeza ukubwa wa serikali na haya mambo mengine ambayo ni gharama na hayana maana kwa taifa.
 
Wanakuambia hakuna tanganyika ila kuna tanzani bara na tanzania zanzibar,chezea tume wewe!
 
Kama rasimu ya katiba itapitishwa kuna umuhimu mkubwa wa mkoa wa Tanga ufanywe kuwa makao makuu ya Tanganyika kwa sababu zifuatazo:
1- Tanga ina historia nzito na nyeti!
2- Tanga ina bandari kongwe na iko mahali strategia zaidi!
3- Tanga ni mji wa kwanza Tanganyika kupata hadhi ya manispaa!
4- Tanga ni mji uliostaarabika kwanza kabla ya miji mingine kwa kuwa na mahakama za mwanzo wakati wa Mjerumani!
ukichanganya na ujenzi wa kinidhamu wa mitaa ya Tanga, na sifa zingine nyingi zinaipa hadhi jiji hilo kuwa makao makuu ya Tanganyika ijayo! Dar es Salaam iendelee kuwa makao makuu ya Tanzania badala ya Dodoma!
Sawa tutakufikiria ikulu itakuwa mtaa wa ngapi, nasikia mtaa wa 7 watu wanapakimbia.
 
Arusha ni mahali muafaka kabisa.

[1] Hali ya hewa ni nzuri

[2] Viongozi watakuwa na uwezo wa kuvaa suti katika kipindi kirefu cha mwaka bila kutumia AC na kuongeza gharama kwa walipa kodi.

[3] Arusha ni makao makuu ya EAC.Kwakuwa wizara ya EAC si suala la muungano tena baada ya kuzaliwa nchi ya Tanganyika hii itasaidia kupunguza gharama za usafiri maafisa wa serekali.

ha ha ha ha umenifurahisha sana coz umemjibu indirect ila hope amekuelewa
 
Ili kupunguza garama za mafuta ya magari ya wabunge wetu kutoka Dar, ni vizuri makao makuu ya Tanganyika yangekuwa Kwenye mji wa Starehe - MOROGORO. Pia kiusalama ni vizuri Ikulu mpya ijengwe Morogoro ili kukwepa kuwa kukaribu na nchi jirani ya Zanzibar, Maana ndugu zake Osama watakuwa wanakuja tutalii kule.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom