Makao Makuu ya Tanganyika: Mapendekezo

Tanganyika ina Makao yake tayari; Ikulu ya Magogoni na Bunge Karimjee (hii ni mali na haki ya Watanganyika kama ilivyo Kisiwandui kwa Wazanzibari)). Serikali ya Shirikisho (Tanzania) Makao yake Makuu yawe Dodoma, kwasababu yalipendekezwa kipindi cha serikali ya Muungano wa Tanzania, pia ofisi za Bunge la muungano liiendele kuwa hilo la Dodoma kwani nalo limejengwa kipindi cha Muungano. Hakuna sababu ya Watanganyika kuanza kutafuta Makao Makuu wakati tayari tunayo.
 
Ndugu wAna bodi, Baada ya Tume ya Marekebisho ya Katiba kuja na pendekezo la Serikali Tatu, kuna mambo ya kuyatolea maamuzi, ikiwemo makao Makuu ya TANGANYIKA. Napendekeza Tabora, KWA nini? TANGANYIKA ilianza wakati wa Ukoloni wa Mjerumani, Mjerumani alidhamiria Tabora KUWA Makao Makuu ya TANGANYIKA , akaufanya Mkoa Mkubwa, Mpanda na Kahama zilikuwa ni Sehemu ya Tabora, na moja ya sababu ya kuichagua Tabora ni KUWA ki nchi iko strategically located.

nawasilisha
 
Sababu yako haina mashiko.
Kisa mkoloni alidhamiria hilo ndipo tucopy? je bado Mpanda na Kahama ziko Tabora hadi leo?

Unaposema Tabora iko 'strategically located' unamaanisha nini?
 
Sababu yako haina mashiko.
Kisa mkoloni alidhamiria hilo ndipo tucopy? je bado Mpanda na Kahama ziko Tabora hadi leo?

Unaposema Tabora iko 'strategically located' unamaanisha nini?
hiyo ni sehemu ya akili ndogo kuongoza akili kubwa, 7+7=15
nahisi mleta thread ni mwigulu.
 
Kaka hoja yako ni nyepesi na haina tija., Historia ya nchi hii imebebwa na mikoa mingi sana, kila mkoa umechangia kwa sehemu kuifanya Tanganyika kuwa hivi ilivyo leo, na si tabora peke yake.
 
Tabora shida zenu wenyewe hamziwezi shida za Watanganyika mtaziweza?? ONDOENI AKINA RAGE KWANZA NDO MLETE HOJA
 
Kilimanjaro ndiyo iwe makao makuu hasa Moshi pale.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Ndugu wAna bodi, Baada ya Tume ya Marekebisho ya Katiba kuja na pendekezo la Serikali Tatu, kuna mambo ya kuyatolea maamuzi, ikiwemo makao Makuu ya TANGANYIKA. Napendekeza Tabora, KWA nini? TANGANYIKA ilianza wakati wa Ukoloni wa Mjerumani, Mjerumani alidhamiria Tabora KUWA Makao Makuu ya TANGANYIKA , akaufanya Mkoa Mkubwa, Mpanda na Kahama zilikuwa ni Sehemu ya Tabora, na moja ya sababu ya kuichagua Tabora ni KUWA ki nchi iko strategically located.

nawasilisha

Mhmmm nafikiria
 
Ha ha haaa kuna wakati CHILIGATI kama sikosei yeye na wananchi wake walidai eneo moja huko Manyoni ni Katikati ya Tanzania (kisa) kuna wazungu waliweka Beacon tu LOL!
 
Kaka hoja yako ni nyepesi na haina tija., Historia ya nchi hii imebebwa na mikoa mingi sana, kila mkoa umechangia kwa sehemu kuifanya Tanganyika kuwa hivi ilivyo leo, na si tabora peke yake.
Kwa hiyo unataka mikoa yote iwe makao makuu?

Mtoa mada ametoa wazo hili kwa kujikita kihistoria zaidi!

Toa wazo mbadala!
 
Ha ha haaa kuna wakati CHILIGATI kama sikosei yeye na wananchi wake walidai eneo moja huko Manyoni ni Katikati ya Tanzania (kisa) kuna wazungu waliweka Beacon tu LOL!
Ubishi mwingine hauna mashiko,ni kweli manyoni ni katikati ya Tanganyika!
 
Kabla hatujapendekeza mkoa mwingine kuwa makao makuu ya nchi, tujiulize swali, kwani wale waliopendekeza Dodoma kuwa makao makuu walikuwa na sababu zipi? Lakini pia kueleza 7bu ya Tanga kuwa na historia nzito na Nyeti haina tija kwakuwa ni mikoa mingi yenye historia nyeti na existence ya Tanganyika + Tanzania. Dodoma ibaki kuwa makao makuu ya nchi yetu.

Dodoma tulishajaribu ikashindikana! Dar iendelee kuwa makao makuu ya TZ lakini Tanga ni mahala muafaka kuwa makao makuu ya Tanganyika mtarajiwa!
 
Dodoma yenyewe bado tunasuasua hatutaki kutoka Dar, nani hataki kuangalia meli zikiingia na kutoka? Tunazo tena upya Tabora? Nako tuweke mamlaka ya kujenga mji Mkuu? Bunge? Nk kwa uchumi upi? Maana tulionao tumeshindwa kuusimamia vizuri
 
Kila mkoa una historia, iringa watadai mkwawa alipambana na wakoloni, historia hiyo! Kule kilimanjaro chifu Mandara, historia hiyo! Vita ya majimaji nayo historia! Kagera nako chifu Rumanyika, tutakuwa na makao makuu kila mahali kihistoria, ingiza hoja ingine
 
Hoja ya tabora ina tija na wala si kuangalia historia tu, Tabora ni mji mzuri sana kwa serikali kujenga makazi yake si kama Dodoma, hali ya hewa ya Tabora si kama ya Dodoma.

Pia kuna sehemu nyingine kwa umuhimu wake tuziache pekee, makao makuu ya utalii yaende Moshi, Arusha ibaki na EAC, Dar acheni serikali ya muungano na makao makuu ya makampuni. Dodoma tuiache iwe makao makuu ya mabunge, Mbeya ni sehemu nzuri saana kuwa makao makuu ya kilimo, Mwanza Madini! Ikulu si vibaya ikaenda Tabora maana yaweza kuwa centre na hub ya kuendesha nchi.
 
Ubishi mwingine hauna mashiko,ni kweli manyoni ni katikati ya Tanganyika!

Haya Mkuu UMESHINDA!!! SUKA~MAHELA Manyoni pawe Makao Makuu ya Tanganyika,Sababu kuna Stesheni kubwa ya Saranda,Pako Mlimani Unaweza kuwaona Maadui wakiwa wanakuja kufanya Uvamizi,Nishati ya Umeme wa Upepo ipo hapo hapo nk.nk. Gari zikishindwa kupanda Mlima ule kuna wale jamaa waliopelekwa pale 1980's watasaidia kusukuma. LOL
 
Back
Top Bottom