GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,100
Wanabodi, uteuzi wa Dkt. Mpango kuwa Makamu wa Rais ni kudhibiti matumizi ya serikali na mambo mengine ya uchumi
Hii kauli ya kudhibiti matumizi imesemwa na Rais Mama Samia mwenyewe kwanini amemchagua Dkt Mpango, Lengo kudhibiti matumizi ya serikali na baadhi ya sera za uchumi.
Makamu wa Rais Dkt Mpango nae amekazia kauli hiyo Kuwa watadhibiti matumizi yaani watapunguza matumizi ya serikali
Mimi sio mchumi(Economist) wala mtaalamu wa mambo ya Fedha(Finance).
Kuna njia kuu mbili tu za kuongoza Uchumi duniani kote ambao una vipengele baadhi vinatekelezwa na Benki kuu za nchi husika
1. Management of Public expenditure yaani matumizi jumla ya serikali kuyatanua au kuyaongeza ( Expansionary public expenditure policy) au kuyabana /kupunguza ( Contraction public expenditure policy).
2. Monetary policy Management, Hii mara nyingi inatekelezwa na Benki kuu za nchi husika ni sera inayohusu udhibiti wa Bei za bidhaa(Price stability) , Riba ya mabenk kukopa na kukopeshwa(Bank rate) , Mfumuko wa bei (Inflation).
Makamu wa Rais Dkt Mpango Philip ni muumini wa Contraction public expenditure yaani kubana matumizi ya serikali, Kumbuka ukibana matumizi ya serikali hakuna mzunguko wa pesa kwenye Uchumi, Hii sera imetekelezwa kwa miaka 5 chini ya Dkt Mpango kama Waziri wa Fedha, Na Ataendele nayo kama Makamu wa Rais kwa miaka mitano kwa maongezi yake mwenyewe Kuwa watadhibiti matumizi ya serikali.
Je athari zake ni zipi Kwa kubana matumizi wakati mlaji na mtumiaji mkubwa wa pesa ni Serikali?
Mosi, Sekta ya Fedha itatoa riba ndogo kwa watu walioweka pesa kwenye mabenki kwani Mabenki yakitaka kuikopesha serikali, Serikali itakopa kwa riba ndogo kwa kujiona ina pesa, Hivyo ni ngumu kwa Benk kukusanya pesa yaani deposit mobilisation kwani riba kwa wawekaji (Depositors))inakatisha tamaa.
Pili, Benki zitashindwa kukopesha na hata zikitaka kukopesha masharti yatakupa magumu sana kwa wakopaji kwani mzunguko wa pesa ni mgumu sana hivyo hakuna wa kupeleka pesa Benki za biashara.
Miaka mitano ya Hayati JPM kubana matumizi na Kutekeleza miradi ya serikali mzunguko wa pesa kwenye Uchumi Ulikuwa mgumu sana, Ni muda muafaka wa Makamu wa Rais kubadili mitazamo wa sera toka kubana matumizi ( contraction policy) na kuruhusu matumizi ( Expansionary policy) ili Kuongeza pesa au ujazo kwenye uchumi.
Tushindane kwa hoja linapofika suala la utaalamu tunaweka siasa pembeni na kujadili uhalisia.
Kila mtu ana kitu anachokiamini Katika taaluma yake, Mimi ni muumini wa sera za kuwafanya watu wale bata na kuwa na Furaha huku kwa mbali ukidhibiti Mfumuko wa bei.