Makamu wa Rais Dkt. Mpango usibane sana matumizi, Maisha yatakuwa magumu zaidi

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,099
Wanabodi, uteuzi wa Dkt. Mpango kuwa Makamu wa Rais ni kudhibiti matumizi ya serikali na mambo mengine ya uchumi

Hii kauli ya kudhibiti matumizi imesemwa na Rais Mama Samia mwenyewe kwanini amemchagua Dkt Mpango, Lengo kudhibiti matumizi ya serikali na baadhi ya sera za uchumi.

Makamu wa Rais Dkt Mpango nae amekazia kauli hiyo Kuwa watadhibiti matumizi yaani watapunguza matumizi ya serikali

Mimi sio mchumi(Economist) wala mtaalamu wa mambo ya Fedha(Finance).

Kuna njia kuu mbili tu za kuongoza Uchumi duniani kote ambao una vipengele baadhi vinatekelezwa na Benki kuu za nchi husika

1. Management of Public expenditure yaani matumizi jumla ya serikali kuyatanua au kuyaongeza ( Expansionary public expenditure policy) au kuyabana /kupunguza ( Contraction public expenditure policy).

2. Monetary policy Management, Hii mara nyingi inatekelezwa na Benki kuu za nchi husika ni sera inayohusu udhibiti wa Bei za bidhaa(Price stability) , Riba ya mabenk kukopa na kukopeshwa(Bank rate) , Mfumuko wa bei (Inflation).

Makamu wa Rais Dkt Mpango Philip ni muumini wa Contraction public expenditure yaani kubana matumizi ya serikali, Kumbuka ukibana matumizi ya serikali hakuna mzunguko wa pesa kwenye Uchumi, Hii sera imetekelezwa kwa miaka 5 chini ya Dkt Mpango kama Waziri wa Fedha, Na Ataendele nayo kama Makamu wa Rais kwa miaka mitano kwa maongezi yake mwenyewe Kuwa watadhibiti matumizi ya serikali.

Je athari zake ni zipi Kwa kubana matumizi wakati mlaji na mtumiaji mkubwa wa pesa ni Serikali?

Mosi, Sekta ya Fedha itatoa riba ndogo kwa watu walioweka pesa kwenye mabenki kwani Mabenki yakitaka kuikopesha serikali, Serikali itakopa kwa riba ndogo kwa kujiona ina pesa, Hivyo ni ngumu kwa Benk kukusanya pesa yaani deposit mobilisation kwani riba kwa wawekaji (Depositors))inakatisha tamaa.

Pili, Benki zitashindwa kukopesha na hata zikitaka kukopesha masharti yatakupa magumu sana kwa wakopaji kwani mzunguko wa pesa ni mgumu sana hivyo hakuna wa kupeleka pesa Benki za biashara.

Miaka mitano ya Hayati JPM kubana matumizi na Kutekeleza miradi ya serikali mzunguko wa pesa kwenye Uchumi Ulikuwa mgumu sana, Ni muda muafaka wa Makamu wa Rais kubadili mitazamo wa sera toka kubana matumizi ( contraction policy) na kuruhusu matumizi ( Expansionary policy) ili Kuongeza pesa au ujazo kwenye uchumi.

Tushindane kwa hoja linapofika suala la utaalamu tunaweka siasa pembeni na kujadili uhalisia.

Kila mtu ana kitu anachokiamini Katika taaluma yake, Mimi ni muumini wa sera za kuwafanya watu wale bata na kuwa na Furaha huku kwa mbali ukidhibiti Mfumuko wa bei.
 
Kwa vyovyote vile wakifanya maisha magumu tutakula nao sahani moja, make wananchi hatutaelewa na pia unafaidika nini kufanya vitu ambavyo jamii unayoiongoza haikuelewi? Unapata faida gani?! Au huwa wanafurahia kuona raia wanalalamika?? Wanajiskia furaha Sana huenda.
 
Kwani?mpango ndio waziri wafedhwa?
Mkuu kama wewe ni mchumi toa hoja una uwezo gani wa kuelewa uchumi

Mimi sio mtaalamu sana lakini nimetumia lugha rahisi kuelimisha watu ambao wanashangilia bila kuwa na uelewa wa sera zinazoandikwa kwa kiingereza
 
Huko tushatoka kwenye utawala wa jiwe aliyetutaka tuishi maisha ya shetani
 
Wanabodi, uteuzi wa Dkt Mpango kuwa Makamu wa Rais ni kudhibiti matumizi ya serikali na mambo mengine ya uchumi...
Mimi napinga hoja yako ya kwanza kwamba mabenki yanaikopesha serikali fedha.

Hiyo inakuwa serikali inafanya biashara na mabenki njia ambayo si sahihi.

Serikali yoyote ile huiagiza benki kuu pekee ama kuchapa fedha zaidi kwenda kwenye mzunguko au kudhibiti mfumuko wa bei na kuangalia kiwango cha riba.

Suala hapa ni kuruhusu biashara zishamiri huku biashara hizo zikilipa kodi stahiki.

Kila mlipa kodi ana wajibu huo wa kulipa kodi iwe kodi ya mapato, kidi ya maendeleo, kodi ya kiwanja, na kodi zingine zilizopo.

Hakuna njia ingine ya ya kupata fedha kwenye mzunguko na hata hiyo FDI nao hutakiwa kulipa kodi ya corporational tax ambayo 0wao hawataki kufanya hivyo.

Makampuni makubwa duniani kama Amzon wamekumbwa na dhoruba ya kiasi kikubwa cha kodi ambazo wamekuwa wakidaiwa na serikali za nchi kadhaa duniani.

Kodi ni wajibu .
 
Mambo ya uchumi hayako static, ni dynamic so serikali iende na biti sio linapigwa rege yenyewe inacheza sebene.
 
Kwa vyovyote vile wakifanya maisha magumu tutakula nao sahani moja , make wananchi hatutaelewa na pia unafaidika nini kufanya vitu ambavyo jamii unayoiongoza haikuelewi ? Unapata faida gani ?! Au huwa wanafurahia kuona raia wanalalamika ?? Wanajiskia furaha Sana huenda
Kwani wakati Magufuli alipokuwa hai si watu tulilalamika tena kwa kusaidiwa na Wabunge, tena Wabunge wa chama tawala, lakini nani aliyesikia malalamiko yetu?. Kwa hiyo hata kama tutalalamika kama wao hawajaamua kubadili mtizamo haitasaidia.
 
Je athari zake ni zipi Kwa kubana matumizi wakati mlaji na mtumiaji mkubwa wa pesa ni Serikali?

Ninavyoelewa mimi DR. Mpango kwenye hotuba yake emphasis haikuwa kwenye kubana matumizi ya serikali bali kuthibiti matumizi mabaya ya fedha za Serikali. Kuthibiti matumizi sio CONTRACTIONARY POLICY bali PRUDENT PUBLIC EXPENDITURE POLICY. Serikali inapeleka fedha nyingi kwenye Halmashauri lakini matumizi yake ni mabaya sana ,hayaridhishi . Hiyo ni moja ya sababu ya kumuondoa Jaffo TAMISEMI, alishindwa kuthibiti matumizi mabaya ya fedha kwenye halmashauri.

Rais Samia ingefaa kama angewauliza hao wachumi wake ; KAMA MISHAHARA WANAYOWALIPA WAFANYAKZI SERIKALINI KAMA NI LIVING WAGE? JE HIYO NDIO SABABU ILIYOFANYA MSIONGEZE MISHAHARA TOKA MAGUFULI AINGIE MADARAKANI? Mpango should be able to explain this anomaly.
 
Kwani wakati Magufuli alipokuwa hai si watu tulilalamika tena kwa kusaidiwa na Wabunge,tena Wabunge wa chama tawala,lkn nani aliyesikia malalamiko yetu?.Kwa hiyo hata km tutalalamika km wao hawajaamua kubadili mtizamo haitasaidia.
We huoni kilichotokea, vilio vyetu visiposikiwa na watawala, aliyetuweka duniani atasikia.
 
Ninavyoelewa mimi DR. Mpango kwenye hotuba yake emphasis haikuwa kwenye kubana matumizi ya serikali bali kuthibiti matumizi mabaya ya fedha za Serikali. Kuthibiti matumizi sio CONTRACTIONARY POLICY bali PRUDENT PUBLIC EXPENDITURE POLICY. Serikali inapeleka fedha nyingi kwenye Halmashauri lakini matumizi yake ni mabaya sana ,hayaridhishi . Hiyo ni moja ya sababu ya kumuondoa Jaffo TAMISEMI, alishindwa kuthibiti matumizi mabaya ya fedha kwenye halmashauri.

Rais Samia ingefaa kama angewauliza hao wachumi wake ; KAMA MISHAHARA WANAYOWALIPA WAFANYAKZI SERIKALINI KAMA NI LIVING WAGE? JE HIYO NDIO SABABU ILIYOFANYA MSIONGEZE MISHAHARA TOKA MAGUFULI AINGIE MADARAKANI? Mpango should be able to explain this anomaly.
Mkuu Trilioni mbili makusanyo kwa Walipa kodi hawazidi watu miliona nne

Kumbuka zile rekodi za hayati JPM ndio hizo Mama anasema ziliua biashara

Tusubiri tuone
 
Mimi napinga hoja yako ya kwanza kwamba mabenki yanaikopesha serikali fedha.

Hiyo inakuwa serikali inafanya biashara na mabenki njia ambayo si sahihi.

Serikali yoyote ile huiagiza benki kuu pekee ama kuchapa fedha zaidi kwenda kwenye mzunguko au kudhibiti mfumuko wa bei na kuangalia kiwango cha riba.

Suala hapa ni kuruhusu biashara zishamiri huku biashara hizo zikilipa kodi stahiki.

Kila mlipa kodi ana wajibu huo wa kulipa kodi iwe kodi ya mapato, kidi ya maendeleo, kodi ya kiwanja, na kodi zingine zilizopo.

Hakuna njia ingine ya ya kupata fedha kwenye mzunguko na hata hiyo FDI nao hutakiwa kulipa kodi ya corporational tax ambayo 0wao hawataki kufanya hivyo.

Makampuni makubwa duniani kama Amzon wamekumbwa na dhoruba ya kiasi kikubwa cha kodi ambazo wamekuwa wakidaiwa na serikali za nchi kadhaa duniani.

Kodi ni wajibu .
Mkuu kwa ufupi huwezi kuitenganisha Benki kuu na Mabenki ya biashara

Ndio maana kila Benki ya biashara inahitajika kuwa na reserve ya pesa Benki kuu

Kuna muda pesa zinakuwa nyingi mikononi mwa watu kupitia mabenki na kuna muda pesa Zinakuwa nyingi serikalini kupitia Benki kuu

Hapa kinachohitajika ni kufanya mlinganyo yaani Balance

Kwa miaka mitano mizani imeegemea upande mmoja wa serikali, Serikali imekusanya kila kitu mfukoni mwetu
 
Mimi napinga hoja yako ya kwanza kwamba mabenki yanaikopesha serikali fedha.

Hiyo inakuwa serikali inafanya biashara na mabenki njia ambayo si sahihi.

Serikali yoyote ile huiagiza benki kuu pekee ama kuchapa fedha zaidi kwenda kwenye mzunguko au kudhibiti mfumuko wa bei na kuangalia kiwango cha riba.

Suala hapa ni kuruhusu biashara zishamiri huku biashara hizo zikilipa kodi stahiki.

Kila mlipa kodi ana wajibu huo wa kulipa kodi iwe kodi ya mapato, kidi ya maendeleo, kodi ya kiwanja, na kodi zingine zilizopo.

Hakuna njia ingine ya ya kupata fedha kwenye mzunguko na hata hiyo FDI nao hutakiwa kulipa kodi ya corporational tax ambayo 0wao hawataki kufanya hivyo.

Makampuni makubwa duniani kama Amzon wamekumbwa na dhoruba ya kiasi kikubwa cha kodi ambazo wamekuwa wakidaiwa na serikali za nchi kadhaa duniani.

Kodi ni wajibu .
Safi sana mkuuu.
Jamani kulipa kodi ni lazima (Amri) sio jambo lakumbembelezana.
 
Kwani Bank ya Maendeleo Africa sio Bank??? Exim Bank sio Bank??? Mbona serikali inakopa huko???
 
Hofu ya nini? Wamekuambia kuwa kusema Kwao huko kuwa wataendelea Kubana matumizi wamemaanisha wataenda Kufanya Maisha kuwa Magumu hasa Kiuchumi kwa Mtanzania?

Wasiwasi wako huu unatokana na nini Ndugu wakati Lengo ni Kujenga Tanzania ya sasa tuliopo Sisi na ile ya Vizazi vyetu vijavyo?

Kwa miaka Mitano au Sita iliyopita tumekuwa tukiimba Maisha Magumu ila mbona tunakula, tupo tunaishi na wengine bado wanajenga Nyumba zao / Majumba yao, wanafungua Biashara zao na Kufanya Maendeleo?

Maisha yangu kuwa Magumu pengine kwa Kutokujipanga Kwangu Kimaisha haimaanishi kuwa Watanzania wote wana Maisha Magumu.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom