Makamu wa Rais Dkt. Mpango usibane sana matumizi, Maisha yatakuwa magumu zaidi

Unajua uchumi ni halisi ingawa wachumi wengi hujificha kwenye kichaka cha theory

Hivi kama wafanyakazi tukisema mshahara ni njiwa/kidichu na haukidhi hata mahitaji ya lazima sasa walitaka tuseme unatosha??

Kama mishahara haijaongezwa takribani past five years hivi tunawaonea hawa???

Waache siasa na matrilioni mawili wanayoyahitaji kila mwezi bila kustimulate biashara kwa kuongeza kipato kwa wafanyakazi tunafikaje??

Maana hata hizo nchi za uchumi wa kati wafanyakazi wa serikali vipato vyao sio kama hivi. Salary ireflect nasi huo ukati wa uchumi sasa

Maana majina ndio yanashamiri tu mara uchumi utasikia mchumi DARAJA la kwanza mara sijui nini waongeze mishahara na waajiri watu tuanze kulipa kodi hizo mpya za viwanja
 
Kha! kha!, khaaa!!,Ina maana Samia asipowasikiliza watu naye atafariki??
Hayo ni ya Mungu sasa , Sisi tunaamin Mungu ndo anatutaftia kilicho Bora, siyo anachotaka mtu kisa yeye ana power ..... watanzania sio watu wa fujo , ukiwatisha kutumia nguvu wanatulia Ila Yupo aliyewaweka atawasikiliza Kwa njia nyingine.

Sikia hiki kisa kidog...... Kama we ni mkristo nakupa kisa, mfalme Suleiman alifanya maisha ya Waisrael yakawa magumu mno , Kodi kibao

Mwanae alipotawala watu wakamwambia tupunguzie mzigo wa kodi, akaomba ushauri Kwa wazee wa nchi wakamwambia hawa watu wasikilize usijifanye mgumu , akatoka hapo akaenda Kwa vijana aliokua nao ujanani akawaomba ushauri wakamwambia we ndio mfalme usiruhusu raia yyte kukuchezea , ...jamaa akachukua ushauri wa vijana akaacha wa wazee, akawajibu kunya wananchi ....Aisee kilichofuata ni historia.....

Hivyo watawala wakiendelea na mitazamo yao wenyewe bila kujali uhalisia wa maisha ya wananchi kisa wao wanatembelea viyoyozi , lolote laweza kutokea kwenye nchi hii ya amani.

Mipango ya Mungu haina makosa , Madikteta huonekana Wana Nia njema na nchi Yao Ila sauti za wananchi ndo zenye nguvu ya kuleta matokeo na sio dola.
 
Hayo ni ya Mungu sasa , Sisi tunaamin Mungu ndo anatutaftia kilicho Bora, siyo anachotaka mtu kisa yeye ana power ..... watanzania sio watu wa fujo , ukiwatisha kutumia nguvu wanatulia Ila Yupo aliyewaweka atawasikiliza Kwa njia nyingine .....
Sikia hiki kisa kidog...... Kama we ni mkristo nakupa kisa, mfalme Suleiman alifanya maisha ya Waisrael yakawa magumu mno , Kodi kibao ... Mwanae alipotawala watu wakamwambia tupunguzie mzigo wa kodi, akaomba ushauri Kwa wazee wa nchi wakamwambia hawa watu wasikilize usijifanye mgumu , akatoka hapo akaenda Kwa vijana aliokua nao ujanani akawaomba ushauri wakamwambia we ndio mfalme usiruhusu raia yyte kukuchezea , ...jamaa akachukua ushauri wa vijana akaacha wa wazee, akawajibu kunya wananchi ....Aisee kilichofuata ni historia.....

Hivyo watawala wakiendelea na mitazamo yao wenyewe bila kujali uhalisia wa maisha ya wananchi kisa wao wanatembelea viyoyozi , lolote laweza kutokea kwenye nchi hii ya amani ...... Mipango ya Mungu haina makosa , Madikteta huonekana Wana Nia njema na nchi Yao Ila sauti za wananchi ndo zenye nguvu ya kuleta matokeo na sio dola ....
Sawa mkuu
 
Anataka trilions 2 kwa mwezi kutoka TRA, yajayo yanafurahisha, mtaita maji mma...kama unasuruali zilizobana usizitupe zitakufaa
Watatumia akili badala ya nguvu kama mama alivyoshauri. Kinyume na hapo watafeli.
 
Kwani Bank ya Maendeleo Africa sio Bank??? Exim Bank sio Bank??? Mbona serikali inakopa huk

Mkuu kwa ufupi huwezi kuitenganisha Benki kuu na Mabenki ya biashara

Ndio maana kila Benki ya biashara inahitajika kuwa na reserve ya pesa Benki kuu

Kuna muda pesa zinakuwa nyingi mikononi mwa watu kupitia mabenki na kuna muda pesa Zinakuwa nyingi serikalini kupitia Benki kuu

Hapa kinachohitajika ni kufanya mlinganyo yaani Balance

Kwa miaka mitano mizani imeegemea upande mmoja wa serikali, Serikali imekusanya kila kitu mfukoni mwetu
Mkuu, unaposema fedha kuwa nyingi mifukoni mwa watu wamaanisha watu wa aina gani?

Kama ni wafanyakazi au wafanyabiashara si wameajiriwa?

Subira yavuta kheri kwani kila jambo lina wakti wake.

Hakuna serikali inayodhamiria kuumiza wanachih wake bila sababu.

Miradi mikubwa ikikamilka kwa wakti ulopangwa fedha itarudi mifukoni.

Ila bado walipa kodi wanakwepa kulipa kodi.

jambo ambalo si kheri ni kwa vyombo vya serikali kama halmashauri kukusanya kodi halafu kuweka fedha zote za mapato kwenye mabenki ya biashara.

Ukifanya hivyo unakuwa unazuia mzunguko wa fedha kwenda kuboresha miundombinu kama barabara na mashule ambapo wahandisi wa barabara na walimu mashuleni wanahitaji mishahara kwa wakti.

Ndpo maana sasa hivi hakuna kelele za kucheleweshwa mishahara na shuile nyingi zimejengwa au kukarabatiwa na watoto wetu wanasoma bure hadi kidato cha nne.

Hivyo balance ipo hapo nini kipewe kipaumbele na kipi kingojee.

Hata hivyo bado tuna nafasi ya kuona serikali ikikamilisha miradi na mipango yote ilowekwa kwa wakti kisha tuje na hukumu hapo 2025.
 
Mkuu kama wewe ni mchumi toa hoja una uwezo gani wa kuelewa uchumi

Mimi sio mtaalamu sana lakini nimetumia lugha rahisi kuelimisha watu ambao wanashangilia bila kuwa na uelewa wa sera zinazoandikwa kwa kiingereza
Makamu wa Rais hana mamlaka ya kusimamia wala kipanga matumizi ya fedha, yeye ni msaidizi wa kawaida kama alivyokuwa mama Suluhu.
 
Hizo austerity policies zinakuwa implemented kuwabana wengine, wao mifuko yao haiwezi kukutwa na ukata hata kwa bahati mbaya na kichaka wanachotumia ni kuwapigania wanyonge na kumuenzi mkuu wa malaika.....
 
Hili suala la kodi mmmmh ngozi nyeusi ukimbembeleza ataishia kukuahidi tu na kukuona mjinga kwa chenga nyingi mwisho wa siku halipi kodi wala nini na biashara anafanya. Ukitumia nguvu napo lawama kibao mara watumie akili sijui haki. Ukibana matumizi ufanye maendeleo watu oooh bora watu wale bata. Watu wakila bata utasikia ooooh mafisadi watu wanalipana mishahara mikubwa hospitalini hamna madawa miundo mbinu mibovu mtoto wa raisi anakula bata tu dubai kwa hela za walipa kodi mara mkurugenzi flani ni fisadi. Jamani wananchi mnataka nini.
Nchi ngumu hii
 
Wanabodi, uteuzi wa Dkt. Mpango kuwa Makamu wa Rais ni kudhibiti matumizi ya serikali na mambo mengine ya uchumi

Hii kauli ya kudhibiti matumizi imesemwa na Rais Mama Samia mwenyewe kwanini amemchagua Dkt Mpango, Lengo kudhibiti matumizi ya serikali na baadhi ya sera za uchumi.

Makamu wa Rais Dkt Mpango nae amekazia kauli hiyo Kuwa watadhibiti matumizi yaani watapunguza matumizi ya serikali

Mimi sio mchumi(Economist) wala mtaalamu wa mambo ya Fedha(Finance).

Kuna njia kuu mbili tu za kuongoza Uchumi duniani kote ambao una vipengele baadhi vinatekelezwa na Benki kuu za nchi husika

1. Management of Public expenditure yaani matumizi jumla ya serikali kuyatanua au kuyaongeza ( Expansionary public expenditure policy) au kuyabana /kupunguza ( Contraction public expenditure policy).

2. Monetary policy Management, Hii mara nyingi inatekelezwa na Benki kuu za nchi husika ni sera inayohusu udhibiti wa Bei za bidhaa(Price stability) , Riba ya mabenk kukopa na kukopeshwa(Bank rate) , Mfumuko wa bei (Inflation).

Makamu wa Rais Dkt Mpango Philip ni muumini wa Contraction public expenditure yaani kubana matumizi ya serikali, Kumbuka ukibana matumizi ya serikali hakuna mzunguko wa pesa kwenye Uchumi, Hii sera imetekelezwa kwa miaka 5 chini ya Dkt Mpango kama Waziri wa Fedha, Na Ataendele nayo kama Makamu wa Rais kwa miaka mitano kwa maongezi yake mwenyewe Kuwa watadhibiti matumizi ya serikali.

Je athari zake ni zipi Kwa kubana matumizi wakati mlaji na mtumiaji mkubwa wa pesa ni Serikali?

Mosi, Sekta ya Fedha itatoa riba ndogo kwa watu walioweka pesa kwenye mabenki kwani Mabenki yakitaka kuikopesha serikali, Serikali itakopa kwa riba ndogo kwa kujiona ina pesa, Hivyo ni ngumu kwa Benk kukusanya pesa yaani deposit mobilisation kwani riba kwa wawekaji (Depositors))inakatisha tamaa.

Pili, Benki zitashindwa kukopesha na hata zikitaka kukopesha masharti yatakupa magumu sana kwa wakopaji kwani mzunguko wa pesa ni mgumu sana hivyo hakuna wa kupeleka pesa Benki za biashara.

Miaka mitano ya Hayati JPM kubana matumizi na Kutekeleza miradi ya serikali mzunguko wa pesa kwenye Uchumi Ulikuwa mgumu sana, Ni muda muafaka wa Makamu wa Rais kubadili mitazamo wa sera toka kubana matumizi ( contraction policy) na kuruhusu matumizi ( Expansionary policy) ili Kuongeza pesa au ujazo kwenye uchumi.

Tushindane kwa hoja linapofika suala la utaalamu tunaweka siasa pembeni na kujadili uhalisia.

Kila mtu ana kitu anachokiamini Katika taaluma yake, Mimi ni muumini wa sera za kuwafanya watu wale bata na kuwa na Furaha huku kwa mbali ukidhibiti Mfumuko wa bei.
Lakini kazi za uchumi sio za VP.Labda awamu hii imeamua hivyo.Ikiwa wote watashughulikia uchumi nani atakayesimamia masuala ya mazingira,Tabia Nchi(Global Warm/Climate)?Hili suala linachukuliwa kwa mzaha sana kama wanavyolishughulikia suala la ugonjwa Wa corona.Yote ni Majanga.Kifupi climate change isipodhibitiwa nchi yetu inaweza kuathirika na mambo mengi kama vile Ardhi yetu ikageuka Jangwa,mafuriko,ukame,joto kali sana n.k Sasa tukifika huko uchumi lazima utadondoka!!!
 
Wanabodi, uteuzi wa Dkt. Mpango kuwa Makamu wa Rais ni kudhibiti matumizi ya serikali na mambo mengine ya uchumi

Hii kauli ya kudhibiti matumizi imesemwa na Rais Mama Samia mwenyewe kwanini amemchagua Dkt Mpango, Lengo kudhibiti matumizi ya serikali na baadhi ya sera za uchumi.

Makamu wa Rais Dkt Mpango nae amekazia kauli hiyo Kuwa watadhibiti matumizi yaani watapunguza matumizi ya serikali

Mimi sio mchumi(Economist) wala mtaalamu wa mambo ya Fedha(Finance).

Kuna njia kuu mbili tu za kuongoza Uchumi duniani kote ambao una vipengele baadhi vinatekelezwa na Benki kuu za nchi husika

1. Management of Public expenditure yaani matumizi jumla ya serikali kuyatanua au kuyaongeza ( Expansionary public expenditure policy) au kuyabana /kupunguza ( Contraction public expenditure policy).

2. Monetary policy Management, Hii mara nyingi inatekelezwa na Benki kuu za nchi husika ni sera inayohusu udhibiti wa Bei za bidhaa(Price stability) , Riba ya mabenk kukopa na kukopeshwa(Bank rate) , Mfumuko wa bei (Inflation).

Makamu wa Rais Dkt Mpango Philip ni muumini wa Contraction public expenditure yaani kubana matumizi ya serikali, Kumbuka ukibana matumizi ya serikali hakuna mzunguko wa pesa kwenye Uchumi, Hii sera imetekelezwa kwa miaka 5 chini ya Dkt Mpango kama Waziri wa Fedha, Na Ataendele nayo kama Makamu wa Rais kwa miaka mitano kwa maongezi yake mwenyewe Kuwa watadhibiti matumizi ya serikali.

Je athari zake ni zipi Kwa kubana matumizi wakati mlaji na mtumiaji mkubwa wa pesa ni Serikali?

Mosi, Sekta ya Fedha itatoa riba ndogo kwa watu walioweka pesa kwenye mabenki kwani Mabenki yakitaka kuikopesha serikali, Serikali itakopa kwa riba ndogo kwa kujiona ina pesa, Hivyo ni ngumu kwa Benk kukusanya pesa yaani deposit mobilisation kwani riba kwa wawekaji (Depositors))inakatisha tamaa.

Pili, Benki zitashindwa kukopesha na hata zikitaka kukopesha masharti yatakupa magumu sana kwa wakopaji kwani mzunguko wa pesa ni mgumu sana hivyo hakuna wa kupeleka pesa Benki za biashara.

Miaka mitano ya Hayati JPM kubana matumizi na Kutekeleza miradi ya serikali mzunguko wa pesa kwenye Uchumi Ulikuwa mgumu sana, Ni muda muafaka wa Makamu wa Rais kubadili mitazamo wa sera toka kubana matumizi ( contraction policy) na kuruhusu matumizi ( Expansionary policy) ili Kuongeza pesa au ujazo kwenye uchumi.

Tushindane kwa hoja linapofika suala la utaalamu tunaweka siasa pembeni na kujadili uhalisia.

Kila mtu ana kitu anachokiamini Katika taaluma yake, Mimi ni muumini wa sera za kuwafanya watu wale bata na kuwa na Furaha huku kwa mbali ukidhibiti Mfumuko wa bei.
Naomba kujua kazi za makamu wa raisi wa Tanzania
 
Back
Top Bottom