MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 836
Habari zenu wakuu.
Leo nina dukuduku ambalo nataka kulitoa. Sijui kama wenzangu linawatatiza pia. Hivi jamani makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana kazi gani haswa?
Nauliza hivi kutokana na ninayoyaona kwahiyo kama sipo sahihi nitarekebishwa. Kila nikiona kwenye vyombo vya habari namuona makamu wa rais aidha anazindua kitu au ni mgeni rasmi sehemu au anafanya ziara sehemu. Yani amekuwa "mzee wa kukata utepe". Ninachosema ni hivi huyu mtu tunaemuita makamu wa rais tunamlipa na kumhudumia kwa ajili ya kuhudhuria sherehe tu? Kwa nchi masikini kama yetu why do we need a ceremonial leader?
Najua watu wataanza kusema oh ni kwa ajili ya ku-accomodate muungano. Siamini hiyo ni sababu. Kwa maana tunaweza kabisa kufuta nafasi ya makamo wa rais na tukasema rais akitoka upande mmoja wa muungano basi waziri mkuu atoke upande mwingine. Kwanini tupoteze rasilimali za nchi kwa ajili ya kuwa na mtu asiye na shughuli za maana ambazo hata rais na waziri mkuu wanaweza waka gawana na kufanya?
Sina nia ya kumshushia heshima makamu wa raisi wala nafasi ya umakamu wa rais ila ninachosema sasa ifike wakati aidha tumpe makamu wa rais kazi za maana za kufanya au tukifute hiki cheo. Kwa ufahamu wangu, Makamu wa Rais ni msaidizi wa rais kwa maana rais ndiyo anaamua ampe kazi zipi makamu wake. Sasa ni kwamba rais hamuamini makamu wake kumpa kazi zozote za maana?
Jamani hili ndilo dukuduku langu.
========

Jibu lake ni rahisi tu. Hizi ndizo kazi zake kwa mujibu wa kifungu cha 47 katiba ya JMT. Kama kuna kazi nyingine atakuwa anafanya zaidi ya hizi hapa basi hasitahili kulipwa kwani hakuajiriwa kwa zaidi ya hizi hapa.
47.-(1) Kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atakuwa ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano kwa jumla, na hususan-
(a) atamsaidia Rais katika kufuatilia utekelezaji wa siku hata siku za Mambo ya Muungano;
(b) atafanya kazi zote atakazoagizwa na Rais;
(c) atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi.
(2) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 37(5), Makamu wa Rais atapatikana kwa kuchaguliwa katika uchaguzi ule ule kwa pamoja na Rais, baada ya kupendekezwa na chama chake wakati ule ule anapopendekezwa mgombea kiti cha Rais na watapigiwa kura kwa pamoja. Mgombea kiti cha Rais akichaguliwa basi na Mahakmu wa Rais atakuwa amechaguliwa.
(3) Mtu atateuliwa kugombea kiti cha Makamu wa Rais kwa kufuata kanuni kwamba endapo Rais wa Jamhuri ya Muungano atatoka sehemu moja ya Muungano, basi Makamu wa Rais atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(4) Mtu hatateuliwa kugombea au kushika kiti cha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa sheria ya Uraia;
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;
(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi;
(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya uchaguzi hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.
(5) Chama chochote hakitazuiwa kumpendekeza mtu yeyote kuwa mgombea kiti cha Makamu wa Rais kwa sababu tu kwamba mtu huyo kwa wakati huo ameshika kiti cha Rais wa Zanzibar au kiti cha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.
(6) Makamu wa Rais hatakuwa kwa wakati huo huo Mbunge, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, wala Rais wa Zanzibar.
(7) Endapo mtu ambaye ni Waziri Mkuu, au Rais wa Zanzibar anateuliwa au kuchaguliwa kuwa Makamu wa Rais ataacha kiti cha Waziri Mkuu, au cha Rais wa Zanzibar, kadri itakavyokuwa.
(8) Makamu wa Rais atatekeleza madaraka yake chini ya uongozi na usimamizi wa Rais, na ataongoza na kuwajibika kwa Rais kuhusu mambo au shughuli zozote atakazokabidhiwa na Rais.