Makamba yu njiani kujiuzuru?

Dr Dr Dr (Fitna, Majungu, Unazi) Makamba yu njiani kujiuzuru

taarifa zilizonifikia hivi punde kuna ushawishi mkubwa kutoka NEC juu ya Makamba kutoendelea na wadhifa wake wa Ukatibu Mkuu! Mkutano wa NEC ulio mbioni kufanyika huenda utamtema kutokana na vuguvugu kubwa la kumtaka aachie ngazi haswa kuhusiana na sakata la Arusha! Tega sikio kuskia zaidi​

Baada ya kuchakachua kura wakishirikiana na NEC wakati umefika wa kumchakachua Makamba......................lakini hawataishia hapo mwishowe raia tutahakikisha haki inatendeka na JK anaachia ngazi na kumpisha Dr. Slaa...........................
 
mh wamweke tambwe ili chama kife kabisaaaaaaaaaaaaa


.
Mkuu nakuunga mkono.
Nafasi hiyo akabidhiwe jemadari Tambwe Hiza, anaimudu baraaabara kwani ni mchapakazi mahiriri na machachari mwenye uwezo wa kipekee wa kuugeuza uongo hadi ukawa ukweli usio na shaka ndani mwake.
.
 
Atajiuzulu wapi wakati anafurahia sherehe ya Mapinduzi kwa kuchekelea??? Lini Watu Wa CCM wanafukuzana??
Hawawezi kumtoa huyu Mzee na ni hatari kwa CCM na wanajua...


Acheni Uongo Huyu Hapa Kwenye Sherehe Za Mapinduzi Z'Bar akichekelea na furaha Tele...

makamba%25282%2529.JPG


Si kila anayecheka kafurahi.
 
Nahisi team itapungua. Maana ktk safu ya ushambuliaji kulikuwa na winga wa kushoto Makamba, mzee wa propaganda kulia na huyu beki Maria Chatanda alikuwa fullback right lakina akawa ana force kuja kushambulia badala ya kumpasia Makamba.
 
Baada ya NEC na CC kufanikiwa kumchakachua Makamba ambaye sasa wanamwita ni mropokaji na kusahau fadhila nyingi za kifisadi alizowafanyia na kusababisha hadhi yake binafsi kushuka.......................nimepata tetesi Kinana ndiye anayetajwa mara nyingi kuwa ndiyo chaguo la JK na ya kuwa yupo mstari wa mbele kumrithi Babu yetu huyo...............Makamba...............

Kiona mbali changu kinanipasha ya kuwa........................................

Tatizo la CCM ni kumtafuta mchawi na kumtupia lawama ya kwanini JK alibwagwa na Dr. Slaa na ya kuwa sasa wananchi sasa wengi hawajitambulishi kuwa na miliki yoyote ya chama hicho tawala........... ............................lakini ukweli ni kuwa ufisadi ndani ya baraza la mawaziri ndilo litasababisha Chadema wakabidhiwe nchi hivi karibuni......................................................
 
Kati ya Mropokaji na Fisadi yupi anastahili kuwa Katibu Mkuu? Wanaruka mkojo na kuangukia mavi!
 
hapa umenena mkuu huyu jamaa abakie azidi kuharibu maana amesaidia sana wapinzani kuwa na nguvu.

kwa kuwa huyu jamaa hajui chochote zaidi ya porojo ni bora sana kuliko kuja mwingine ambaye anaweza kuanza kukisuka sisiem kikasimama tena.

kwa sasa sisiem inahemea kwenye mashine ya dharura ni vyema huyu ambaye hajui kitu aendelee ili upinzani uzidi kug'ara na kuwapiga chini 2015

Mkwere anamuita mzee wa kazi so kwake ni heroe wa kundi lile. acha awamalize wajifunze. walimtoa mangula wa watu bila kupata mtu mbadala mwenye busara.
 
Huyo nae ni fisadi mbaya, tena alipiga wakati watu wengi hatujaamka. Pia ni mjeshi nadhani, sasa pata picha kama Kinana akiwa km.

Rais/ mwenyekiti wa ccm, katibu mkuu ccm na naibu wake wote wajeshi.
 
Who cares nan anakuwa KM wa sisiem. They are all screwed upstairs. Don't expect kitu kipya. Upuuzi ule ule kwemda mbele. Au mumemsahau wakat wa campaign? Alikuwa tofauti na makamba?
 
taarifa zilizonifikia hivi punde kuna ushawishi mkubwa kutoka NEC juu ya Makamba kutoendelea na wadhifa wake wa Ukatibu Mkuu! Mkutano wa NEC ulio mbioni kufanyika huenda utamtema kutokana na vuguvugu kubwa la kumtaka aachie ngazi haswa kuhusiana na sakata la Arusha! Tega sikio kuskia zaidi

Hiyo ni tetesi na wala sio news alert wala breaking news. Lakini hata hivyo sitegemei kama ataendelea na wadhifa huo kutokana na ukilaza wake.
 
makamba amefanya kazi nzuri sana pamoja na mwenyekiti wake tuwaombee wamalizie muda wao!
 
taarifa zilizonifikia hivi punde kuna ushawishi mkubwa kutoka NEC juu ya Makamba kutoendelea na wadhifa wake wa Ukatibu Mkuu! Mkutano wa NEC ulio mbioni kufanyika huenda utamtema kutokana na vuguvugu kubwa la kumtaka aachie ngazi haswa kuhusiana na sakata la Arusha! Tega sikio kuskia zaidi

TAARIFA ZAELEZA HALI YA HEWA NDANI CCM SI SHWARI HATA KIDOGO

Kwenye suala la Kikwete kugawa 'nyama' ya taifa kwa maana ya Uwaziri, kuna madai Mzee Makamba alikuwa na uhakika asilimia 99 % mtoto wake kuwa bosi wa sura ya Tanzania huko nje.

Sasa mara alipogundua kwamba hata unaibu tu hakuweza kulipwa kama shukrani wa 'kazi zetu zile' kufaulisha uchaguzi kimazingaombwe basi watu walioko jirani naye wanasema mzee roho yake imegeuka nyeusiiii zaidi ya mkaa kwa uongozi wa juu wa chama chake.


Tangu hapo, tafsiri ya matendo na kauli haribifu za Mzee wetu mcheshi sana huyu, watu wanasema Makamba kaamua kuendesha vita vya chini kwa chini kwa ukaidi dhidi ya mwenyekiti wake kwa mtazamo wa 'Maadam Umemwaga Ugali wa mwanangu mpendwa Januari basi na mimi nimalizie kabisa kiaina kutia mchanga mboga yote'.


Kwa bahati mbaya sana maswahiba waliokashirishwa na baraza jipya la JK, ambao nao wameamua kumhujumu bosi wao kwa msingi kwamba wenzao hawakuwekeza zaidi kupatikana ushindi wa CCM 2010, idadi yao inaongezeka kwa kazi ajabu na kukidhoofisha kabisa chama hicho achilia mbali wanamtandao 'waliohadaika' awamu ya kwanza ya Mhe Kikwete.


Ugomvi wa vikundi mbali mbali navyo vimechachamali vita vya sauti kibao zisizoweza kupikwa chungu kimoja. Marupurupu ya CCM kupungua kwa zaidi ya milioni 400 nayo ni vita kali kwani posho mbalimbali kauka kau kadri asasi za kiraia zinavyotia kofuli kila mwanya wa CCM kujitengenezea fedha za bwerere na anasa kubwa iliozoeleka huko nyuma.

Hasira za vikundi vilivyokomolewa kwenye uteuzi kugombea kwa tiketi ya CCM na viti maalum navyo ni kupe ya ndani kwandani.

Kwa ujumla maadui wa CCM ndani kwa ndani ni wa hatari zaidi kuliko wengine tunavyodhani huku CCM Uadilifu siku hizi wakiwa wamebakia tu wasikilizaji na kupiga kura kwenye vikao kwa sababu CCM Rostam Aziz imewaweka kando katika mambo mengi sana tangu kipindi sasa.

Kwa hayo machache kwa leo nadiriki kusema kwamba kabla hata adhabu za 'Nguvu ya Umma' haiyafikia hata 1/8 ya mpango mzima kwa hasira za kuchakachua uchaguzi wetu mkuu na kujibidisha kuibia walipakodi kila kona, kisu cha mwisho shingoni mwa CCM kitasukumwa na mtu wa ndani tena si kipindi kirefu.

Uongozi wa juu mle tangu ujifedheheshe kupita kiwango mbele ya jamii ya Tanzania kwa ujumla na waliokuwa wanachama wa chama hicho ambao mpaka sasa wamechagua kujiweka pembeni na aibu za kila kukicha, taarifa za waandamizi zasema UTII UMESHUKA sana tena sana tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom