Makamba yu njiani kujiuzuru?

Makamba yu njiani kujiuzuru?

mh kwel jaman ..bt kwenye chanzo chako ulichotoa kinasema anatarajia kujiuzulu
 
Kuna tetesi ambayo itathibitishwa muda siyo mrefu nadhani ndani ya wiki kwamba FISADI Yusuf Makamba amesalimu amri na kuamua kujiuzulu wadhifa wa ukatibu mkuu wa CCM. Chanzo Bofya Hapa

hii blog tunategemea itakuwa ni ya watu makini kama wana-JF

vinginevyo asipojiuzulu itakula kwenu wamiliki wa blog hii.
 
Kuna tetesi ambayo itathibitishwa muda siyo mrefu nadhani ndani ya wiki kwamba FISADI Yusuf Makamba amesalimu amri na kuamua kujiuzulu wadhifa wa ukatibu mkuu wa CCM. Chanzo Bofya Hapa

Umeweka sehemu si yake maana unaongelea TETESI na si BREAKING NEWS please wahusika iwekeni sawa hii.

ingawa si habari njema maana tulitaka huyu KILAZA aendelee hadi 2015 ili iwe rahisi kwa SISIEM kula MWELEKA WA MWAKA. ANY WAY LETS WAIT AND SEE
 
WanaJF,
Kwa mtizamo wangu kama kuna nguvu inayosaidia sana wapinzani katika kuing'oa ccm madarakani basi nguvu hiyo inatoka kwa katibu mkuu wa ccm bw. Makamba. Sasa kuna tetesi kwamba makamba anataka kujiuzuru. Kwa kweli itakuwa ni pigo sana kwa wapinzani kwani huyu mzee uropokaji wake unawasaidia sana wapinzani.
 
Breaking news? Tetesi? Au udaku? Sielewi elewi bado.
 
mh.lets be serious we dont depend on tetesi wana jf,give us tha real thing....
 
CCM yote ilishachafuka, yeyote atakayepewa nafasi ya Katibu Mkuu lazima ataishia kuwa kama Makamba tu.

Uliona Chiligati alivyolikoroga wakati alipokuwa akitetea KAGODA? Pia alijikanyaga sana kwenye sakata la Bashe. Ukweli ulipoanza kuwekwa wazi, aliruka kimanga na kuanza kukimbia waandishi wa habari.

CCM ya leo ina ombwe kubwa kwenye uongozi na ndio maana kila mtu anajisemea la kwake. Tatizo ni kwamba viongozi wengi wa CCM hawajui msimamo wa Mwenyekiti wao wa CCM.

Kikwete hajiamini, siku zote amekuwa ni mtu wa kupima upepo kwanza ili aje kutoa tamko mwishoni wakati wasaidizi wake walishalikoroga tayari.

Mifano michache ni swala la Katiba, waziri wa sheria na mwanasheria mkuu walitoa misimamo/maoni yao kuhusu katiba, JK siku zote alikuwa kimya, baada ya kuona upepo ni mbaya ndipo akaja na kauli kwamba mwaka huu ni mwaka wa katiba mpya.

Mauji yalipotokea Arusha, alikuwa kimya, ameishia kusema kwamba amesikitishwa sana, bila kuonyesha kosa lilikuwa wapi na inabidi lishughulikiwe kwa njia zipi ili lisitokee tena. Baada ya Membe kubanwa na mabalozi, akakiri Polisi walitumia nguvu zaidi na kwamba serikali itatoa tamko rasmi.

Kiongozi anayesubiri kupima upepo ni mbaya sana kwa kuwa huwezi jua anafikiria nini au msimamo wake uko wapi au anaamini nini. Ni sawa na bendera fuata upepo.
 
kwani sakata la richmond na EPA alianzisha yeye? Acha ushabiki
 
Atajiuzulu wapi wakati anafurahia sherehe ya Mapinduzi kwa kuchekelea??? Lini Watu Wa CCM wanafukuzana??
Hawawezi kumtoa huyu Mzee na ni hatari kwa CCM na wanajua...
makamba%25282%2529.JPG
 
Ndio baadhi ya watu wanavyoamini, eti kiongozi bora, huwa hana msimamo unaoeleweka. Yaani hatabiriki! Hii falsafa wengi wanaojaribu kuiiga inawashinda, kwani wanachanganya, kutotabirika na kukosa mwelekeo. Viongozi waovu ndo huwa hawana mwelekeo na mara nyingi hawatabiriki. Kama umesoma vizuri historia ya jinsi hitler alivyoingia madarakani, kutotabirika kwake ndo ilikuwa silaha yake kuu. Hata alipoingia madarakani, alijaribu kujionesha kuwa kiongozi bora huku chini chini akiendelea na kampeni zake za kuangamiza watu.

Msimamo wa Kikwete katika masuala mengi ya kitaifa umekuwa ni wa kutatanisha kwani usafi wake unatiliwa shaka. Kwa hiyo hata suala ambalo linaonekana wazi ni chafu; huwezi kujua Kikwete yuko upande gani! Ndo maana watendaji wake mara nyingi wamekuwa wakijikuta katika mapambano ya wao kwa wao bila kujua ni yupi hasa yuko upande wa Bwana mkubwa. Kifupi ana sifa zote za viongozi waliokuja kuwa viongozi wa hatari kabisa duniani.

Kutoeleweka kwake badala ya kusaidia, kumekuwa ndo mwiba mkubwa kwa serikali yake. Kwa mfano wakati wa sakata la Richmond ilikuwa vigumu kujua alikuwa kwa kina mwakyembe au kwa kina Lowassa. Lakini njia ya muongo ni fupi. Kutotabirika kwa kuigiza huwa muda si mrefu kunagundulika - kwani baada ya Lowassa kulazimika kujiuzulu Kikwete alionekana ku-shake sana (hata kama alifurahi kiasi fulani Lowassa kuondoka, hakupenda alivyoondoka ukizingatia bado ni mshirika wake wa karibu mno na alikuwa akipenda misimamo yake). Ukweli ni kuwa kutoeleweka kwake kulitishia kuisambaratisha serikali yake kipindi kile. Na hadi leo, kutoeleweka kwake kunaiweka sana CCM matatani.

Kuondoka kwa Makamba CCM kunaweza kurudisha imani kwa chama kwa baadhi ya wanachama, lakini tatizo la CCM si Makamba. Tatizo la CCM ni Mwenyekiti wake. Hivyo kuondoka kwa Makamba kunaweza kuonekana suluhisho kwa muda mfupi, lakini songombingo na minyukano ya ndani haitaisha, kwani mwenyekiti Kinyonga (jicho moja linatazama mbele lingine nyuma) bado yupo pale pale na maguvu yote ya Dola yeye ndo bado anayadhibiti.

CCM isipoondoka madarakani na utawala wa Kikwete itakuwa imepona!
 
ni ujinga wa kupindukia aliofanya jk kumchagua makamba kushika nafasi ya utendaji mkuu ktk chama ktk karne hivi.makamba elimu yake ni ndogo saana, anaongea hovyo kama vijana wa mitaani.mie mara zote akiongea nasikia kichefu chefu.inasikitisha sana!.watu wengi wameachana na ccm kwa sababu makamba ameifanya ccm kuwa chama cha kihuni.jk is always not serious about his nominations.anakutana na mtu kwenye party leo kesho anampa cheo.watu wa pwani hovyo kabsa.jamaa ametuaribia nchi.
 
Acheni Uongo Huyu Hapa Kwenye Sherehe Za Mapinduzi Z'Bar akichekelea na furaha Tele...

makamba%25282%2529.JPG
 
Ndio baadhi ya watu wanavyoamini, eti kiongozi bora, huwa hana msimamo unaoeleweka. Yaani hatabiriki! Hii falsafa wengi wanaojaribu kuiiga inawashinda, kwani wanachanganya, kutotabirika na kukosa mwelekeo. Viongozi waovu ndo huwa hawana mwelekeo na mara nyingi hawatabiriki. Kama umesoma vizuri historia ya jinsi hitler alivyoingia madarakani, kutotabirika kwake ndo ilikuwa silaha yake kuu. Hata alipoingia madarakani, alijaribu kujionesha kuwa kiongozi bora huku chini chini akiendelea na kampeni zake za kuangamiza watu. Umesema ukweli mtupu.kikwete ni kigeugeu na hiloo linatosha kuiondoa ccm madarakani.

Msimamo wa Kikwete katika masuala mengi ya kitaifa umekuwa ni wa kutatanisha kwani usafi wake unatiliwa shaka. Kwa hiyo hata suala ambalo linaonekana wazi ni chafu; huwezi kujua Kikwete yuko upande gani! Ndo maana watendaji wake mara nyingi wamekuwa wakijikuta katika mapambano ya wao kwa wao bila kujua ni yupi hasa yuko upande wa Bwana mkubwa. Kifupi ana sifa zote za viongozi waliokuja kuwa viongozi wa hatari kabisa duniani.

Kutoeleweka kwake badala ya kusaidia, kumekuwa ndo mwiba mkubwa kwa serikali yake. Kwa mfano wakati wa sakata la Richmond ilikuwa vigumu kujua alikuwa kwa kina mwakyembe au kwa kina Lowassa. Lakini njia ya muongo ni fupi. Kutotabirika kwa kuigiza huwa muda si mrefu kunagundulika - kwani baada ya Lowassa kulazimika kujiuzulu Kikwete alionekana ku-shake sana (hata kama alifurahi kiasi fulani Lowassa kuondoka, hakupenda alivyoondoka ukizingatia bado ni mshirika wake wa karibu mno na alikuwa akipenda misimamo yake). Ukweli ni kuwa kutoeleweka kwake kulitishia kuisambaratisha serikali yake kipindi kile. Na hadi leo, kutoeleweka kwake kunaiweka sana CCM matatani.

Kuondoka kwa Makamba CCM kunaweza kurudisha imani kwa chama kwa baadhi ya wanachama, lakini tatizo la CCM si Makamba. Tatizo la CCM ni Mwenyekiti wake. Hivyo kuondoka kwa Makamba kunaweza kuonekana suluhisho kwa muda mfupi, lakini songombingo na minyukano ya ndani haitaisha, kwani mwenyekiti Kinyonga (jicho moja linatazama mbele lingine nyuma) bado yupo pale pale na maguvu yote ya Dola yeye ndo bado anayadhibiti.

CCM isipoondoka madarakani na utawala wa Kikwete itakuwa imepona!

Kikwete ni kigeugeu na kwa sifa hiyo ccm mwisho wake u karibu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom