Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,184
- 671
hili hasa ndilo waliokuwa wanastahiki kuambiwa hawa jamaa zetu kwa muda mrefu.
sasa ni juuu yao kumeza au kutema.
Makamba: Viongozi Chadema wana akili ndogo
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kujibu tuhuma zilizotolewa na makada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, amewachambua makada wa Chadema mmoja baada ya mwingine akiwemo Mabere Marando na John Shibuda.
Makamba amesema, tuhuma zilizotolewa na Chadema ni matusi hivyo hawezi kuvumilia.
Alisema, makada wote walioitukana CCM katika mkutano huo wa Chadema wapo katika kundi la watu wenye uelewa mdogo (Simple Mind People).
Kundi hilo ni miongoni mwa makundi matatu ya watu wenye uelewa na hivyo Makamba ana maana kwamba, viongozi wa Chadema wana akili ndogo.
"Kikwete (mgombea urais wa CCM, Jakaya), yupo kundi la kwanza la watu wenye akili kubwa si la tatu wala la pili (wenye akili za kawaida), ndiyo maana mpaka sasa amezunguka Mwanza, Kagera, Kigoma, Rukwa na Mbeya, anachofanya anaelezea Ilani ya chama, tumefanya nini tangu 2005 na tutafanya nini, si kuzungumza watu," alisema Makamba.
Aidha CCM imeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kutosubiri barua ya malalamiko wakati chama kinapokiuka mwongozo wa maadili kwa vyama vya siasa, ichukue hatua kukiwajibisha chama kinachokiuka makubaliano hayo.
Makamba ambaye alikuwa akizungumza kwa ucheshi huku akitumia neno ‘hapo vipi?' alisema amelazimika kulizungumza hilo kwa kuwa yeye binafsi hawezi kuvumilia kuona kiongozi wao akitukanwa.
"Hata kama ingekuwa ni wewe, unaona baba au mama yako anatukanwa, ungevumilia? Hakuna anayeweza kufanya hivyo na kama yupo dunia itamshangaa, kuna uvumilivu wa kisiasa unaokulazimu uvumilie chama kinapoguswa lakini si huu," aling'aka Makamba.
Alitaja uvumilivu huo wa kisiasa kuwa ni kuvumilia pale chama pinzani kinapokukosoa katika masuala ya elimu, kilimo, huduma za jamii lakini si katika kejeli na matusi kwa kuwa yanakwenda kinyume na mwongozo wa maadili ya vyama vya siasa ambao kila chama kinapaswa kuufuata.
Makamba akisoma baadhi ya makatazo ya mwongozo huo alisema chama chochote hakitakiwi kufanya fujo, vurugu, kutumia lugha ya matusi, kashfa, kejeli, udhalilishaji au vitisho katika kampeni na kuongeza kuwa kinyume cha makatazo hayo, ndicho walichokifanya makada hao.
Akimchambua kada John Shibuda, alisema, "eti (Shibuda) anasema CCM ni kama tairi bovu, sasa tujiulize, hivi tairi bovu ni nani kati yetu na yeye, Maswa (Jimbo alilokuwa akiliongoza kwa tiketi ya CCM) waligundua hili mapema, wakambwaga katika kura za maoni.
"Kwanza baada ya kuona maji marefu, alikacha kugombea urais na kumsifia Kikwete kuwa ana maadili, anafaa tena akachangia Sh 200,000, leo anasema CCM gari bovu, kaishiwa hoja," alisema.
Kuhusu Marando alisema, "anapaswa amshukuru Kikwete, ninajua wenye kesi ya EPA si wakosaji bado ni watuhumiwa mpaka mwisho wa kesi, lakini hivi serikali ikamate watu hata kama ni tuhuma na wewe unawatetea, unatetea mafisadi?"
Katibu huyo wa CCM alihoji kwa kuwa Dk Willibrod Slaa alishindwa kiapo cha kanisani cha upadri, hawezi kutunza kiapo cha kuongoza nchi.
Amesema, hajali hata yeye (Makamba) akiwekwa katika kundi la wenye akili ndogo baada ya waandishi kuhoji kwa nini naye anazungumzia majina ya watu.
source: HabariLeo | Makamba:Viongozi Chadema wana akili ndogo