Makamba: Viongozi CHADEMA wana akili ndogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba: Viongozi CHADEMA wana akili ndogo

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtu wa Pwani, Aug 31, 2010.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  hili hasa ndilo waliokuwa wanastahiki kuambiwa hawa jamaa zetu kwa muda mrefu.

  sasa ni juuu yao kumeza au kutema.

  Makamba: Viongozi Chadema wana akili ndogo

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kujibu tuhuma zilizotolewa na makada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam.

  Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, amewachambua makada wa Chadema mmoja baada ya mwingine akiwemo Mabere Marando na John Shibuda.


  Makamba amesema, tuhuma zilizotolewa na Chadema ni matusi hivyo hawezi kuvumilia.


  Alisema, makada wote walioitukana CCM katika mkutano huo wa Chadema wapo katika kundi la watu wenye uelewa mdogo (Simple Mind People).


  Kundi hilo ni miongoni mwa makundi matatu ya watu wenye uelewa na hivyo Makamba ana maana kwamba, viongozi wa Chadema wana akili ndogo.


  "Kikwete (mgombea urais wa CCM, Jakaya), yupo kundi la kwanza la watu wenye akili kubwa si la tatu wala la pili (wenye akili za kawaida), ndiyo maana mpaka sasa amezunguka Mwanza, Kagera, Kigoma, Rukwa na Mbeya, anachofanya anaelezea Ilani ya chama, tumefanya nini tangu 2005 na tutafanya nini, si kuzungumza watu," alisema Makamba.


  Aidha CCM imeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kutosubiri barua ya malalamiko wakati chama kinapokiuka mwongozo wa maadili kwa vyama vya siasa, ichukue hatua kukiwajibisha chama kinachokiuka makubaliano hayo.


  Makamba ambaye alikuwa akizungumza kwa ucheshi huku akitumia neno ‘hapo vipi?' alisema amelazimika kulizungumza hilo kwa kuwa yeye binafsi hawezi kuvumilia kuona kiongozi wao akitukanwa.


  "Hata kama ingekuwa ni wewe, unaona baba au mama yako anatukanwa, ungevumilia? Hakuna anayeweza kufanya hivyo na kama yupo dunia itamshangaa, kuna uvumilivu wa kisiasa unaokulazimu uvumilie chama kinapoguswa lakini si huu," aling'aka Makamba.


  Alitaja uvumilivu huo wa kisiasa kuwa ni kuvumilia pale chama pinzani kinapokukosoa katika masuala ya elimu, kilimo, huduma za jamii lakini si katika kejeli na matusi kwa kuwa yanakwenda kinyume na mwongozo wa maadili ya vyama vya siasa ambao kila chama kinapaswa kuufuata.


  Makamba akisoma baadhi ya makatazo ya mwongozo huo alisema chama chochote hakitakiwi kufanya fujo, vurugu, kutumia lugha ya matusi, kashfa, kejeli, udhalilishaji au vitisho katika kampeni na kuongeza kuwa kinyume cha makatazo hayo, ndicho walichokifanya makada hao.


  Akimchambua kada John Shibuda, alisema, "eti (Shibuda) anasema CCM ni kama tairi bovu, sasa tujiulize, hivi tairi bovu ni nani kati yetu na yeye, Maswa (Jimbo alilokuwa akiliongoza kwa tiketi ya CCM) waligundua hili mapema, wakambwaga katika kura za maoni.


  "Kwanza baada ya kuona maji marefu, alikacha kugombea urais na kumsifia Kikwete kuwa ana maadili, anafaa tena akachangia Sh 200,000, leo anasema CCM gari bovu, kaishiwa hoja," alisema.


  Kuhusu Marando alisema, "anapaswa amshukuru Kikwete, ninajua wenye kesi ya EPA si wakosaji bado ni watuhumiwa mpaka mwisho wa kesi, lakini hivi serikali ikamate watu hata kama ni tuhuma na wewe unawatetea, unatetea mafisadi?"


  Katibu huyo wa CCM alihoji kwa kuwa Dk Willibrod Slaa alishindwa kiapo cha kanisani cha upadri, hawezi kutunza kiapo cha kuongoza nchi.


  Amesema, hajali hata yeye (Makamba) akiwekwa katika kundi la wenye akili ndogo baada ya waandishi kuhoji kwa nini naye anazungumzia majina ya watu.


  source: HabariLeo | Makamba:Viongozi Chadema wana akili ndogo
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,421
  Likes Received: 22,335
  Trophy Points: 280
  Afadhali viongozi wa CHADEMA wenye akili ndogo kuliko yeye (Makamba) asiye na akili kabisa, kiasi kwamba hata mwanawe Januari alikiri kuwa babaye ni mropokaji.
   
 3. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Makamba ni mwehu
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Naona kuna haja ya kuweka ukomo wa umri katika SIASA
   
 5. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hata mtoto wake anajuakuwa baba yake hamnazo. Haina haja ya kujadili saana alichoongea.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Aug 31, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Makamba ajue na watu watafungulia juu ya wale walioshindwa viapo vyao vya ndoa! Na sijui kama hayo maadili waliyosaini yanawafunga wapinzani tu au na CCM kwa sababu sasa hivi ina maana yote twende tu. Chadema na wasilaze damu, CCM nao wasilaze damu na CUF nao wachangie.. now we into true politics..
   
 7. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni siasa tu hizi jamani, kanyaga twende!
   
 8. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #8
  Aug 31, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  jibuni hoja msilete vioja
   
 9. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #9
  Aug 31, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mmoja wa waganga wa kienyeji wa CCM. Ukichunguza sana utakuta ndiye mwenye tunguri za kwao huyo. Aliona amtoe mwnaye yule hakimu asijetia aibu.
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  Aug 31, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ingeanzia kwa Makamba kwanza.
   
 11. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Mhhhhh :confused2:
   
 12. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #12
  Aug 31, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mwehu tu hata hajielewi.
   
 13. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #13
  Aug 31, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye red labda niulize kwenye nini hasa au kwenye BONGO FLEVA?
   
 14. telele

  telele Member

  #14
  Aug 31, 2010
  Joined: Jun 4, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa ajili ya kuweka rekodi sahihi:

  MAKAMBA aliwahi kuweka rekodi ya kuwa mkuu wa mkoa wa kwanza Tanzania (wakati huo akiwa mkuu wa Mkoa wa Morogoro) kufeli masomo yake ya diploma akiwa mwaka wa kwanza tuu katika chuo cha maendeleo Mzumbe Morogoro (kabla hakijawa chuo kikuu).

  Japokuwa alijitahidi kutumia madaraka yake ya ukuu wa Mkoa kuwashinikiza walimu wasimfelishe, lakini kutokana na ukilaza wake alishindwa kubebeka na hivyo ali disko mwaka wa kwanza tu.

  Tutafakari, yeye na hao wenzake anaowasema nani mwenye akili.
   
 15. Oluoch

  Oluoch Senior Member

  #15
  Aug 31, 2010
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Makamba anachachawa na makomandoo. Dr.Slaa yupo juu na huo ni ukweli usiopingika. Inaonekana anaipenda CHADEMA,kama vipi anakaribishwa kwa wateule wa bwana!!
   
 16. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #16
  Aug 31, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Achaneni na hili debe tupu!
   
 17. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #17
  Aug 31, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Makamba anadai baba yake (mgonjwa wa kifafa) katukanwa kwa kuambiwa ukweli kuwa alihusika kuchora ramani ya kupora fedha za EPA, jambo ambalo limetolew ushahidi wa kimaandishi. Lakini hapo hapo nawaita viongozi wa Chadema wenye akili ndogo hivi ni nani mtukanaji hapo?Kwa wale wasiomjua huyu chizi fresh ni kuwa tangu azaliwe hajawahi kupata nafasi ya uongozi kwa kuchaguliwa, yeye siu zote amepata nafasi kwa kuteuliwa na wakubwa na hii inatokana na tabia yake ya kujipendekeza kwa wakubwa na kuwalamba miguu kama anavyofanya kwa Kikwete. Sifa yake nyingine ni ushirikina, hata nafasi ya ukatibu mkuu aliyonayo sasa inatokana na ushirika wake na Kikwete katika nyanja za nguvu za giza,alimpeleka kwa mganga maarufu huko Bumbuli wakati wa mchakato wa kutafuta mgombea wa urais kupitia CCM mwaka 2005.
   
 18. Mwanamosi

  Mwanamosi Member

  #18
  Aug 31, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi kampeni zinakoelekea nadhani watu wanaweza kushangazwa na mambo yanayoweza kutokea...nadhani iko haja ya watu kufanya kampeni kwa kufuata taratibu na makubaliano waliyosaini kuyafuata...hizi siasa za kuongelea watu nadhani zisipewe nafasi.kila chama kitangaze sera na sio nani kafanya nini nasi tusishabikie hizi biashara za kuongeleana kwenye kampeni kwani hapa tutapoteza muda na malengo ya kampeni ambayo ni kutangaza sera kwa kuinadi ilani yako ya uchaguzi na kumnadi mgombea husika atayetekeleza ilani hiyo....nahisi watu wengi wanapenda kusikia nani kafanya nini na sio nani atafanya nini...hao kina Makamba wako kazini na ni wajibu wao kuongea kwa niaba ya vyama vyao...ni wajibu wetu kuwafanya wakae kwenye mstari kwa kunadi sera na kutowapa nafasi ya kuzungumzia nani kafanya nini...ushabiki utatufanya tupoteze sifa ya great thinkers kwa kuwa tutaburuzwa na heka heka za kampeni(ofcourse hazikosekani,lazima ziwepo) na kupoteza umakini wetu tutakapokuwa mstari wa mbele kushabikia mambo binafsi yanayosemwa kwenye kampeni na kuacha kufuatilia sera na ilani za vyama ambazo ninaamini ndizo zinatufanya tuchague huyu badala ya yule. tujadili hoja na tuachane na kushambuliana kwa matusi na kejeli kwani kama mchezo huo utakuwa ndio order of the day basi nadhani mwenye matusi,kashfa na maneno makali ndio atashinda hata kama hana sera wala ilani inayotekelezeka.
   
 19. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #19
  Aug 31, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,206
  Trophy Points: 280
  'Viongozi wa Chadema wana akili ndogo wa CCM wana akili kubwa', mawazo ya kitoto kabisa sikutegemea yatolewe na mtu mzima kama Makamba, ni sawa na watoto kutambiana pipi yako ndogo ya kwangu kubwa, it is another nonsense from Makamba.
   
 20. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #20
  Aug 31, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wenye akili ndogo ni viongozi wa CCM ambao wanajua wazi kwamba waliiba fedha za EPA lakini wanajaribu na kujitahidi kukana! Pia walileta hilo karatasi na vyama kuweka sahihi kwa makusudi mazima ya kutaka kuzuia vyama vingine visizungumzie wizi wao. Aibu sana kwa kweli kwa watu wazima kuamua kuwafanya wananchi wanaowaongoza ni wajinga!
   
Loading...