Elections 2010 Makamba: Viongozi CHADEMA wana akili ndogo

Wakuu mbona hatuambiwi ni MATUSI gani ambayo yanazungumziwa? Nakumbuka wakati wa kongamano la Taasisi ya Mwalimu Nyerere baadhi ya viongozi wastaafu wa ngazi ya juu wenye heshima na hadhi kubwa humu nchini walitoa madukuduku yao kuhusu ambavyo hawakubaliani na jinsi ambavyo Serikali inaendesha baadhi ya mambo. Makamba akakurupuka na kudai kwamba viongozi hao wamemtukana Rais! Kwa Mzee Makamba, kutoa dukuduku lako dhidi ya Rais ama kiongozi wa CCM ni kutukana! Ama kweli CCM wamefulia ile mbaya.
 
Hata mtoto wake anajuakuwa baba yake hamnazo. Haina haja ya kujadili saana alichoongea.


hivi huyu Makamba Jeshini alikuwa Kitengo gani?, alipoigana vita yoyote huyu?, mbona anaonekana ana akili za kushikiwa?
 
point hapa wenye kuzungumzia watu baada ya issue hili ndilo linapelekea simple mind kama za akina hawa
 
Wana JF,

Sasa tukianza kuongerea swala la nani anaakili na nani hana akili na nani anaakili za grade one na nani ana za grade two tutakuwa sasa hatuijui siasa ni kubwabwaja tuuu unajua mwenzio akikutwanga kimtindo ndani ya siasa tumia akili kujibu kwa hoja na sio kujibu kwa kuonyesha kuwa wewe nawewe huko kwa grade izo na bahati mbaya grade yako ionekane ndio ya mwisho sasa ndipo hapo utawafanya wananchi wakuone wewe ndio mpuuuzi wa grade isiweza kutamkwa kwa jamiii.

Sasa sijui viongozi hawa na siasa hii hujifunzia wapi propaganda zao na kushindwa kujibwa kwa kutumia hoja.

Yaani katika siasa usipo angalia Umri,alama za nyakati,na unachokiongea kwa wananchi vikipishana tuuu imekula kwako.

Kwa viongozi wetu wa CCM mpigwapo dongo na vyama vingine mwatakiwa nanyi kukaa na kujua mwatakiwa kujibu nini nasio tu kukurupuka nyie ndio mwaiongoza nchi bado mnakuwa na woga wa aajabu kiasi kwamba hata sisi twawashuku uwezo na utendaji kazi wenu ndani ya chama na serikali
 
kwa ajili ya kuweka rekodi sahihi. MAKAMBA aliwahi kuweka rekodi ya kuwa mkuu wa mkoa wa kwanza tanzania (wakati huo akiwa mkuu wa Mkoa wa Morogoro) kufeli masomo yake ya diploma akiwa mwaka wa kwanza tuu katika chuo cha maendeleo Mzumbe Morogoro (kabla hakijawa chuo kikuu). Japokuwa alijitahidi kutumia madaraka yake ya ukuu wa Mkoa kuwashiniza walimu wasimfelishe, lakini kutokana na ukilaza wake alishindwa kubebeka na hivyo ali disko mwaka wa kwanza tu.
tutafakali, yeye na hao wenzake anaowasema nani mwenye akili.

Very interesting.
 
Makamba anachachawa na makomandoo. Dr.Slaa yupo juu na huo ni ukweli usiopingika. Inaonekana anaipenda CHADEMA,kama vipi anakaribishwa kwa wateule wa bwana!!


Please please, hakuna kukaribishwa huyu nungayembe! mtupu namna hiyo ni mzigo usiobebeka akiingia Chadema.
 
Hivi makamba analala usingizi kweli? Naona afya yake kama mtu mwenye kisukari na mwenye msongo wa mawazo...........
Ila Slaa anatisha, ndiyo maana hawalali na amewavuruga vilivyo!
 
hili hasa ndilo waliokuwa wanastahiki kuambiwa hawa jamaa zetu kwa muda mrefu.

sasa ni juuu yao kumeza au kutema.

Makamba:Viongozi Chadema wana akili ndogo

HAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kujibu tuhuma zilizotolewa na makada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, amewachambua makada wa Chadema mmoja baada ya mwingine akiwemo Mabere Marando na John Shibuda.

Makamba amesema, tuhuma zilizotolewa na Chadema ni matusi hivyo hawezi kuvumilia.

Alisema, makada wote walioitukana CCM katika mkutano huo wa Chadema wapo katika kundi la watu wenye uelewa mdogo (Simple Mind People).

Kundi hilo ni miongoni mwa makundi matatu ya watu wenye uelewa na hivyo Makamba ana maana kwamba, viongozi wa Chadema wana akili ndogo.

“Kikwete (mgombea urais wa CCM, Jakaya), yupo kundi la kwanza la watu wenye akili kubwa si la tatu wala la pili (wenye akili za kawaida), ndiyo maana mpaka sasa amezunguka Mwanza, Kagera, Kigoma, Rukwa na Mbeya, anachofanya anaelezea Ilani ya chama, tumefanya nini tangu 2005 na tutafanya nini, si kuzungumza watu,” alisema Makamba.

Aidha CCM imeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kutosubiri barua ya malalamiko wakati chama kinapokiuka mwongozo wa maadili kwa vyama vya siasa, ichukue hatua kukiwajibisha chama kinachokiuka makubaliano hayo.

Makamba ambaye alikuwa akizungumza kwa ucheshi huku akitumia neno ‘hapo vipi?’ alisema amelazimika kulizungumza hilo kwa kuwa yeye binafsi hawezi kuvumilia kuona kiongozi wao akitukanwa.

“Hata kama ingekuwa ni wewe, unaona baba au mama yako anatukanwa, ungevumilia? Hakuna anayeweza kufanya hivyo na kama yupo dunia itamshangaa, kuna uvumilivu wa kisiasa unaokulazimu uvumilie chama kinapoguswa lakini si huu,” aling’aka Makamba.

Alitaja uvumilivu huo wa kisiasa kuwa ni kuvumilia pale chama pinzani kinapokukosoa katika masuala ya elimu, kilimo, huduma za jamii lakini si katika kejeli na matusi kwa kuwa yanakwenda kinyume na mwongozo wa maadili ya vyama vya siasa ambao kila chama kinapaswa kuufuata.

Makamba akisoma baadhi ya makatazo ya mwongozo huo alisema chama chochote hakitakiwi kufanya fujo, vurugu, kutumia lugha ya matusi, kashfa, kejeli, udhalilishaji au vitisho katika kampeni na kuongeza kuwa kinyume cha makatazo hayo, ndicho walichokifanya makada hao.

Akimchambua kada John Shibuda, alisema, “eti (Shibuda) anasema CCM ni kama tairi bovu, sasa tujiulize, hivi tairi bovu ni nani kati yetu na yeye, Maswa (Jimbo alilokuwa akiliongoza kwa tiketi ya CCM) waligundua hili mapema, wakambwaga katika kura za maoni.

“Kwanza baada ya kuona maji marefu, alikacha kugombea urais na kumsifia Kikwete kuwa ana maadili, anafaa tena akachangia Sh 200,000, leo anasema CCM gari bovu, kaishiwa hoja,” alisema.

Kuhusu Marando alisema, “anapaswa amshukuru Kikwete, ninajua wenye kesi ya EPA si wakosaji bado ni watuhumiwa mpaka mwisho wa kesi, lakini hivi serikali ikamate watu hata kama ni tuhuma na wewe unawatetea, unatetea mafisadi?”

Katibu huyo wa CCM alihoji kwa kuwa Dk Willibrod Slaa alishindwa kiapo cha kanisani cha upadri, hawezi kutunza kiapo cha kuongoza nchi. Ouuch!

Amesema, hajali hata yeye (Makamba) akiwekwa katika kundi la wenye akili ndogo baada ya waandishi kuhoji kwa nini naye anazungumzia majina ya watu.

source: HabariLeo | Makamba:Viongozi Chadema wana akili ndogo


Hebu jibuni hizo hoja jamani, stop cherry picking hoja ambazo ziko upande wenu tu. Halafu mkiambiwa mna akili ndogo mnalalamika. Ukiangalia kwa undani majority ya posts za Chademanistas humu ndani zina ufinyu wa mawazo.
 
Afadhali viongozi wa CHADEMA wenye akili ndogo kuliko yeye (Makamba) asiye na akili kabisa, kiasi kwamba hata mwanawe Januari alikiri kuwa babaye ni mropokaji.

Makamba ni mwehu

MAKAMBA si mwehu.. Ni mwendawazimu.:glasses-nerdy:

mmh hapa ni conclude tu kwamba Kichwa cha makamba kitakuwa ni sifuri.......................sasa najiuliza kwa nini ccm bado wanamtumia kama spokesman wao!!!!
 
Hebu jibuni hizo hoja jamani, stop cherry picking hoja ambazo ziko upande wenu tu. And maybe you guys (CHADEMA) need a seasoned and a more effective attack dog.

Heheheheeee...you couldn't stay out of this one, could you?
 
kwa ajili ya kuweka rekodi sahihi. MAKAMBA aliwahi kuweka rekodi ya kuwa mkuu wa mkoa wa kwanza tanzania (wakati huo akiwa mkuu wa Mkoa wa Morogoro) kufeli masomo yake ya diploma akiwa mwaka wa kwanza tuu katika chuo cha maendeleo Mzumbe Morogoro (kabla hakijawa chuo kikuu). Japokuwa alijitahidi kutumia madaraka yake ya ukuu wa Mkoa kuwashiniza walimu wasimfelishe, lakini kutokana na ukilaza wake alishindwa kubebeka na hivyo ali disko mwaka wa kwanza tu.
tutafakali, yeye na hao wenzake anaowasema nani mwenye akili.
Duh hii mbaya sana.
Diploma unapigwa DISCO? shughuli ipo kweli kwenye kichwa cha huyu mtu. Ndo maana ktk kura za maoni alikuwa anasindikizwa na Msekwa. kisha kila aliloongea Makamba, msekwa alilirudia akisema kuweka rekodi sawa. Ina maana Aliyemteua kuwa katibu mkuu hakujua anateua kilaza? ama ndo zile kuteua watu dhaifu ionekane weye ndo unafanyakazi peke yako?
 
Mi nadhani Makamba anasema kitu kama kweli vile, tokea kampeni zianze mimi sijaona wala sijasikia chadema wakinadi sera wanaongea watu tu, nilishangaa mpaka kusikia wanazusha mambo ya uwongo, kueleza mambo bila ya ushahidi na utafiti wowote kama kawaida yao. Chadema wamekuja na mpya uchaguzi huu, wanakurupuka kurupuka tu, mimi siwakumbuki kuwa hivi hapo kabla, niliwajuwa kuwa ni chama makini chenye watu waelewa hawaongei ovyo ovyo bila ya utafiti.

Ajabu juzi namsikia Mbowe anam defend mgombea wake wa STD7 kwa kudai kuwa hata marehemu Mzee Idris Abdul wakyl,(alyekuwa rais wa awamu ya 4 Zanzibar) alikuwa ana elimu ya kiwango hicho, wakati ni uwongo mtupu, Mzee Idris amesoma kwa kiwango cha elimu ya chuo kikuu (alisoma Makerere University, Uganda), hili hata mtoto mdogo Zanzibar analijuwa.
 
hili hasa ndilo waliokuwa wanastahiki kuambiwa hawa jamaa zetu kwa muda mrefu.



Katibu huyo wa CCM alihoji kwa kuwa Dk Willibrod Slaa alishindwa kiapo cha kanisani cha upadri, hawezi kutunza kiapo cha kuongoza nchi.

source: HabariLeo | Makamba:Viongozi Chadema wana akili ndogo

Say what?

Makamba amesema nini? na habari Leo (gazeti la serikali) wameandika nini?

Labda nimuulize Shehe Kikwete:

8D6U9904.JPG
 
Mi nadhani Makamba anasema kitu kama kweli vile, tokea kampeni zianze mimi sijaona wala sijasikia chadema wakinadi sera wanaongea watu tu, nilishangaa mpaka kusikia wanazusha mambo ya uwongo, kueleza mambo bila ya ushahidi na utafiti wowote kama kawaida yao. Chadema wamekuja na mpya uchaguzi huu, wanakurupuka kurupuka tu, mimi siwakumbuki kuwa hivi hapo kabla, niliwajuwa kuwa ni chama makini chenye watu waelewa hawaongei ovyo ovyo bila ya utafiti.

Ajabu juzi namsikia Mbowe anam defend mgombea wake wa STD7 kwa kudai kuwa hata marehemu Mzee Idris Abdul wakyl,(alyekuwa rais wa awamu ya 4 Zanzibar) alikuwa ana elimu ya kiwango hicho, wakati ni uwongo mtupu, Mzee Idris amesoma kwa kiwango cha elimu ya chuo kikuu (alisoma Makerere University, Uganda), hili hata mtoto mdogo Zanzibar analijuwa.

Huyu naye anadanganya watu kuwa ni mwanachama wa CUF. Au ndio ndoa ya CUF na CCM imewekwa hadharani?
 
..ku-disco IDM Mzumbe + nafasi za kuteuliwa tu maishani mwake + kumpa cheo CCM nyumba ndogo yake(Tambwe) + kujikomba kwa epileptic= akili za Makamba (yaani ndoooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooogo)
 
Back
Top Bottom