Elections 2010 Makamba: Viongozi CHADEMA wana akili ndogo

Makamba angekuwa na akili, asinge ruhusu mgonjwa kugombea,kama mgonjwa ndo huyo bora, thithiem si michosho?
 
Hizi kampeni zinakoelekea nadhani watu wanaweza kushangazwa na mambo yanayoweza kutokea...nadhani iko haja ya watu kufanya kampeni kwa kufuata taratibu na makubaliano waliyosaini kuyafuata...hizi siasa za kuongelea watu nadhani zisipewe nafasi.kila chama kitangaze sera na sio nani kafanya nini nasi tusishabikie hizi biashara za kuongeleana kwenye kampeni kwani hapa tutapoteza muda na malengo ya kampeni ambayo ni kutangaza sera kwa kuinadi ilani yako ya uchaguzi na kumnadi mgombea husika atayetekeleza ilani hiyo....nahisi watu wengi wanapenda kusikia nani kafanya nini na sio nani atafanya nini...hao kina Makamba wako kazini na ni wajibu wao kuongea kwa niaba ya vyama vyao...ni wajibu wetu kuwafanya wakae kwenye mstari kwa kunadi sera na kutowapa nafasi ya kuzungumzia nani kafanya nini...ushabiki utatufanya tupoteze sifa ya great thinkers kwa kuwa tutaburuzwa na heka heka za kampeni(ofcourse hazikosekani,lazima ziwepo) na kupoteza umakini wetu tutakapokuwa mstari wa mbele kushabikia mambo binafsi yanayosemwa kwenye kampeni na kuacha kufuatilia sera na ilani za vyama ambazo ninaamini ndizo zinatufanya tuchague huyu badala ya yule. tujadili hoja na tuachane na kushambuliana kwa matusi na kejeli kwani kama mchezo huo utakuwa ndio order of the day basi nadhani mwenye matusi,kashfa na maneno makali ndio atashinda hata kama hana sera wala ilani inayotekelezeka.
Kama ni sera tumeimbiwa kila mara. Kama kuna ushahidi wa rekodi mbaya lazima zitajwe ili watu wachague watu wasio na rekodi chafu. Mfano kama kweli kuna ushahidi kuwa 2005 pesa ziliibwa serikalini ili kufanyiwa kampeni, lazima tujue ili tusije chagua wezi. HIVO HISTORIA INATAKIWA ILI TUFANYE MAAMUZI SAHIHI.
Sio busara kukaa kimya wakati madudu yamefanywa na watawala, eti watu wanyamaze.
 
hakuna wala haja ya kuumiza kichwa na makamba... nadhani yeye ndio mwenye matatizo na chanzo cha matatizo mengi humu nchini kwa ku-vuvuzela chochote kilicho mbele yake

zama zake ziliisha miaka hiyo sijui kwanini bado anakula ruzuku ya watanzania
 
Hahahah well hili linafurahisha haswa. Makamba kweli aachwe abaki kuwa Makamba. <simple mind people
 
Hebu jibuni hizo hoja jamani, stop cherry picking hoja ambazo ziko upande wenu tu. Halafu mkiambiwa mna akili ndogo mnalalamika. Ukiangalia kwa undani majority ya posts za Chademanistas humu ndani zina ufinyu wa mawazo.

Selemani hakai mbali na thread za Makamba.
Muda si mrefu utamwona kwenye thread za Mbowe.....ha ha ha ha
 
huyu si ndio alisema rais kadanganywa suala la uraia wa Bashe...sasa mwenye akili ndogo nani?yeye na huyo rais wake au nani?? Makamba pleaseeeeeee funga hilo domo lako unatutia hasira bure hapa
 
Heheheheeee...you couldn't stay out of this one, could you?

NN,

he he he he ... Selemani ametoka kifungoni leo. Kwa jitihada zake, amejishindia hii toka kwa timu Kikwete:

CD.JPG
 
Hebu jibuni hizo hoja jamani, stop cherry picking hoja ambazo ziko upande wenu tu. Halafu mkiambiwa mna akili ndogo mnalalamika. Ukiangalia kwa undani majority ya posts za Chademanistas humu ndani zina ufinyu wa mawazo.

Hahahahahahahah

DSC_5826.JPG
 
kwa ajili ya kuweka rekodi sahihi. MAKAMBA aliwahi kuweka rekodi ya kuwa mkuu wa mkoa wa kwanza tanzania (wakati huo akiwa mkuu wa Mkoa wa Morogoro) kufeli masomo yake ya diploma akiwa mwaka wa kwanza tuu katika chuo cha maendeleo Mzumbe Morogoro (kabla hakijawa chuo kikuu). Japokuwa alijitahidi kutumia madaraka yake ya ukuu wa Mkoa kuwashiniza walimu wasimfelishe, lakini kutokana na ukilaza wake alishindwa kubebeka na hivyo ali disko mwaka wa kwanza tu.
tutafakali, yeye na hao wenzake anaowasema nani mwenye akili.

Mwambieni Makamba awahi Airport kumpokea Mkwewe aliyempeleka Amerika kujifungua kwa sababu tu Tanzania hakuna huduma nzuri za Afya na kutaka mjukuu wake apate Uraia wa Marekani.......Wale watanzania wa kule Bumbuli wakiachwa wanajifungua nyumbani bila huduma nzuri za Afya.Hawa ndio viongozi tunaowataka Tanzania!
 
Mwambieni Makamba awahi Airport kumpokea Mkwewe aliyempeleka Amerika kujifungua kwa sababu tu Tanzania hakuna huduma nzuri za Afya na kutaka mjukuu wake apate Uraia wa Marekani.......Wale watanzania wa kule Bumbuli wakiachwa wanajifungua nyumbani bila huduma nzuri za Afya.Hawa ndio viongozi tunaowataka Tanzania!

Ouuuch....no you didn't!!!

Selemani what say you on this one?
 
Kwani Sele alikuwa kifungoni?

Halafu hizi totoz unazitoa wapi bana? Loh!!!!!!

Hizi totoz ziko kwenye kampeni ya Kikwete. Inabidi uingie CCM tu mazee maana huko mambo yake sio mchezo ---- sifa zote kwa muumba wa mbingu na nchi.

Hapa natafuta picha ya Njoki (sijui kama nimekosea jina).

Najua tu Rev Masa atakuwa nayo maana nasikia Njoki alikwenda fanya maombi kwa mzee wa southern gospel
 
Makamba acha kukurupuka, eti

  • mwenye akili ndogo yuko tayari kushiriki katika mdahalo lakini mwenye akili nyingi yuko mbioni anatafuta namna ya kukwepa !
  • mwenye akili ndogo haogopi kufanya mtihani huku mwenye akili nyingi anaingia mitini akipanga namna ya kuiba mtihani !
  • mwenye akili ndogo anayo maelezo umasikini wetu unasababishwa na nini, mwenye akili nyingi hajui kwa nini tu masikini !
  • mwenye akili ndogo anao mkakati wa kuondokana na uchafu katika jamii, mwenye akili nyingi haoni hata hatari ya kuishi na uchafu !
  • mwenye akili ndogo haogopi kupambana na mafisadi, mwenye akili nyingi hana mpango wowote wa kulinusuru taifa kutoka kwenye makucha yao !
Ooh masikini Makamba hata huwezi kutambua kati ya hawa yupi hana hata chembe ya akili. Hakuna kibaya kama utumwa wa akili na Makamba hapa katia fora !
Ninavyojua kwenye kampeni hutaji tu sifa zako kwa nini uchaguliwe, unataja pia mapungufu ya mpinzani wako kwa nini asichaguliwe. Hivyo kutaja mapungufu ya CCM na mgombea wake ni kampeni halali kabisa na haikwepeki labda Tanzania kampeni ina maana tofauti kabisa na kwingineko duniani. Kinachogomba hapa ni kuwa kuna jitihada za kufagia chini ya kitanda uchafu wa CCM wa miaka karibu hamsini na hili bila shaka iwe Chadema au CUF hawawezi kulikubali.
 
Hizi totoz ziko kwenye kampeni ya Kikwete. Inabidi uingie CCM tu mazee maana huko mambo yake sio mchezo ---- sifa zote kwa muumba wa mbingu na nchi.

Hapa natafuta picha ya Njoki (sijui kama nimekosea jina).

Najua tu Rev Masa atakuwa nayo maana nasikia Njoki alikwenda fanya maombi kwa mzee wa southern gospel


Una maana Dokii?

dokii2.JPG
 
point hapa wenye kuzungumzia watu baada ya issue hili ndilo linapelekea simple mind kama za akina hawa

Yaani na ww sijuhi nduguye makamba wote hamnazo ,umeleta hii habari ukazani makamba anaongea point kumbe anaharisha maskini kijitu cha pwaniii!!!!!!!!!!!! Yaani ume leta hiyo habari kusaidia kuonyesha pumba za mtoa pumba maarufu afrika mashariki na kati ambazo atukuzisikia wengine
 
Yaani na ww sijuhi nduguye makamba wote hamnazo ,umeleta hii habari ukazani makamba anaongea point kumbe anaharisha maskini kijitu cha pwaniii!!!!!!!!!!!! Yaani ume leta hiyo habari kusaidia kuonyesha pumba za mtoa pumba maarufu afrika mashariki na kati ambazo atukuzisikia wengine
Mutu,
Halafu ukiangalia hii mitu ya pwani haijaonekana hapa tangu uchaguzi iliyopita. Ndio wameingia kama nzige.
 
Kwa ajili ya kuweka rekodi sahihi:

MAKAMBA aliwahi kuweka rekodi ya kuwa mkuu wa mkoa wa kwanza Tanzania (wakati huo akiwa mkuu wa Mkoa wa Morogoro) kufeli masomo yake ya diploma akiwa mwaka wa kwanza tuu katika chuo cha maendeleo Mzumbe Morogoro (kabla hakijawa chuo kikuu).

Japokuwa alijitahidi kutumia madaraka yake ya ukuu wa Mkoa kuwashinikiza walimu wasimfelishe, lakini kutokana na ukilaza wake alishindwa kubebeka na hivyo ali disko mwaka wa kwanza tu.

Tutafakari, yeye na hao wenzake anaowasema nani mwenye akili.

Hapa ndiyo mnaniacha hoi nyie watu hicho chama. Makamba ni bonge la Professor ukifananisha na mgombea mwenza wa Slaa. Mmefikiria hilo? Kwa namna yoyote ile haiwezekani kabisa Slaa akapata Urais wa nchi hii kwa sababu hiyo kituko yenu.
 
Mutu,
Halafu ukiangalia hii mitu ya pwani haijaonekana hapa tangu uchaguzi iliyopita. Ndio wameingia kama nzige.

Easy mzee wangu Jasusi,

Najua inakera lakini ndio hivyo tu hakuna cha kuwazuia. Wanaonesha vile kampeni ya Kikwete ilivyoishiwa sera na kila kitu. Kuwepo kwao hapa kunaifunua vyema sana kampeni ya Kikwete.

Me likes it ....lol
 
Back
Top Bottom