Makamba: Mnyika acha Unafiki, sote tumeshindwa Bungeni!

Makamba: Mnyika acha Unafiki, sote tumeshindwa Bungeni!

Dr. Mgimwa alisema kwamba kodi hiyo ya Sh 1,000 haikupendekezwa na Serikali, bali ilipendekezwa na Bunge kupitia Kamati ya Bunge ambayo ilitaka wananchi wakatwe Sh 1,450.

Baada ya mapendekezo, Mgimwa alisema Serikali ilifanya uchambuzi na kuamua kupunguza hadi Sh 1,000. Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, jana alisema msimamo wa Serikali ndio wake pia.

Kauli ya Mgimwa inajibu malalamiko ya baadhi ya kampuni,wabunge na vyama vya siasa, kwamba ongezeko hilo linaongeza ugumu wa maisha kwa wananchi.

Hivi karibuni kampuni za simu na Mbunge wa Ubungo,John Mnyika (Chadema), walilalamikia kodi hiyo kwamba inaongeza gharama za maisha kwa wananchi.

Mbali na Mnyika,hata CCM kupitia taarifa ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ilitaka kodi hiyo iondolewe na Serikali itafute vyanzo vingine vya mapato.

Pia Chama cha Watoa Huduma za Mitandao ya Intaneti Tanzania (TISPA), walilalamikia sheria mpya ya kodi na ushuru wa bidhaa katika intaneti,kwamba itachangia ongezeko la gharama za huduma ya intaneti kwa watumiaji wa kawaida.

Source: Habari Leo
 
Wana-JF nao ni vigeu geu kama wana-siasa....ndo upuuzi wa kuburuzwa na wanasiasa huu!! Mbunge Ally Kessy aliposhuka nondo kule bungeni kuhusu wananchi kulipa kodi; humu watu wakamshangilia huku wakimvika mashada ya maua! Wakatokea wengine wakasema Ally Kessy hakustahili kabisa kuwepo kwenye chama cha magamba!!Leo mnatandikwa kodi ya book book kwa mwezi; mnakuja tena hapa mnatupigia kelele! Tuache unafiki.....

By the way, naungana na January...wabunge walikuwapo na wakapitisha, waache unafiki wao hapa wa kujifanya wanapinga! Hawa akina Mnyika nao ni wale wale tu....Mnyika ninayemfahamu mimi kama kitu anakipinga kwa ukweli, lazima ataitisha Press Conference! And for this, am convinced kwamba wiki ijayo haitaisha kabla Mnyika hajaitisha Press Conference kuzungumzia kodi ya Laini za simu.....seuze wiki ijayo, hiyo jtatu sijui kama itafika!!!!!!

NasDaz una taarifa chama chako kina pinga hii kodi?
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: Pai
Kufuatia kauli za Serikali magazetini kuhusu mimi na kodi ya umiliki wa kadi za simu; nijibu tu kwa ujumla kwamba SITAACHA. Badala yake naomba kuwapatia namba zao: Makamba 0767783996 na Mgimwa 0754/0684765644, tunachohitaji ni kauli ya Serikali kuwa kodi imesitishwa na itaondolewa na sio siasa chafu.

Kwa mliotaka msimamo wangu juu ya kauli ilinukuliwa jana tarehe 18 Julai 2013 na Gazeti la Majira kwamba Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba kwamba; “Mnyika anaangalia upepo unakoelekea, akiona watu wanalalamika ndipo anaongea namsihi aache kufanya siasa katika jambo hili”, naomba kutumia mtandao huu kutoa majibu ya ujumla kwa maswali na masuala yote kama ifuatavyo:

Nieleze kwamba sitaacha kufanya siasa kwenye jambo hili mpaka kodi hiyo itakapofutwa kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kubaki na fedha walau kidogo kwa maendeleo.

Sitaacha kufanya siasa kwa sababu ndio kazi yangu ambayo wananchi walinichagua kuifanya ya kuwawakilisha na kuisimamia Serikali ambayo yeye Makamba ni sehemu yake. Sitaacha kufanya siasa kwa sababu Mwalimu Nyerere alisema ili nchi yetu iendelee inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.

Ambacho sitafanya ni siasa chafu kama hizo ambazo Makamba amefanya za kusema uongo, kwa kuwa naamini anafahamu kabisa kwamba sijaanza kuongea kuhusu suala hili baada ya malalamiko ya wananchi bali jambo hili nilianza kulishughulikia bungeni mara baada ya Waziri wa Fedha kuwasilisha jedwali la marekebisho la kuanzisha kodi lukuki za simu ikiwemo hii. Katika mchango wangu bungeni, nieleza kwamba muswada huo wa sheria ya fedha kwa kupandisha kodi kwenye mafuta na simu ni ‘muswada wa majanga ya kuwaongezea mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi.


Aidha, sikuishia kusema tu kwa niaba ya wananchi bali nilichukua hatua kwa mujibu wa kanuni za Bunge nami kuwasilisha jedwali la marekebisho ya kupinga kodi ya umiliki wa kadi za simu pamoja na kodi nyingine zote zenye kuongeza mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi sio kwenye sekta ya mawasiliano bali pia kwenye sekta zingine ikiwemo sekta ndogo (sub sector) nyeti ya mafuta.

Mlioniuliza kwa SMS katika simu na kwenye mitandao ya kijamii sasa ni wakati wa Makamba kuhojiwa kwa njia hizo hizo (Simu yake ya Mkononi ni 0767783996) kwa kuwa yeye ni sehemu ya Serikali na Serikali ndiyo ambayo iliingiza suala hili kwa mara ya kwanza ndani ya ukumbi wa Bunge kupitia hotuba ya Bajeti Serikali na ikalirudia kuliingiza kupitia jedwali la marekebisho ya Sheria ya Serikali; ni wakina nani hasa kwa majina ndani ya Serikali na Bunge walioingiza kodi hii? Na ni wakina nani hasa waliopigia kura ya ndio kuipitisha?

Aidha, amenukuliwa na gazeti la Mwananchi la leo tarehe 19 Julai 2013 akieleza kwamba hakubaliani na suala hili na kupita kwake ilikuwa na kuzidiwa nguvu. Hivyo, ataje kwa majina hayo waliozidi nguvu serikali kinyume na matakwa yake. Amenukuliwa akisema pia kwamba anajua kuwa suala hili haliwezi kutekelezwa na kwamba ni lazima litabadilishwa kwa kuangalia eneo lingine la kutoza kodi. Ni vizuri akahojiwa, ikiwa huo ni msimamo wa Serikali; mwenye mamlaka ya kusitisha kodi hiyo ni nani na kwanini hajitokezi kutoa agizo la kusitisha wakati maandalizi yakiendelea ya kupeleka muswada bungeni wa kuifuta kabisa kodi hiyo katika mkutano ujao?

Wakati Naibu Waziri akisema hayo, Waziri wa Fedha Dk William Mgimwa katika Serikali hiyo hiyo yeye ametoa kauli tofauti siku hii hii ya leo ambapo kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania amewataka watumiaji wa mitandao ya simu nchini na watanzania kwa ujumla kuwa na subira kuhusu tozo ya sh 1000 kwa mwezi kwa kila laini ya simu za kiganjani.

Na kwa kuwa amesema kwamba Serikali inaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau, natoa mwito kwa wananchi kumtumia maoni kupitia namba zake za simu za mkononi 0754/0684-765644. Aidha, ni vizuri aeleze subira hiyo ivutwe mpaka lini? Na ni wakina nani hasa kwa majina waliomfanya akaingiza kodi hiyo katika kitabu cha Hotuba yake aliyosoma bungeni kuhusu bajeti ya Serikali na wakina na hasa kwa majina waliomfanya arejeshe kodi hiyo ya kadi za simu kwenye jedwali la marekebisho ya muswada wa sheria ya fedha alilowasilisha bungeni.

Nasisiza kuwa kauli za ujumla za Serikali bila kuwataja kwa majina wahusika ni za kujivua mzigo wa lawama baada ya malalamiko ya wananchi kuhusu kodi hii na nyinginezo kwa kuhamisha mzigo huo kwa wabunge. Ni muhimu badala ya kutoa kauli za ujumla za kulaumu wabunge, Rais ama kiongozi mwingine mwenye mamlaka ajitokeze kusitisha kutozwa kwa kodi hiyo na kuanzisha mchakato wa muswada wa kufuta kodi hiyo kuwasilishwa katika mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza tarehe 27 Agosti 2013.

Majina ya wahusika yasipotajwa au mamlaka zinazohusika zisipotoa kauli katika mkutano wa hadhara nitakaoshiriki jumapili tarehe 21 Julai 2013 katika Uwanja wa Sahara kata ya Mabibo kuanzia saa 8 Mchana mpaka saa 11 Jioni nitatoa mrejesho kuhusu yaliyojiri katika mkutano uliopita wa Bunge na kueleza hatua zaidi zinazopaswa kuchukuliwa kuwezesha majina ya wabunge hao kutajwa hadharani na hatua za kuondoa kodi hiyo kuchukuliwa.

Uongozi bora na uraia mwema wenye uwajibikaji ni chimbuko na chachu ya ukuaji endelevu wa uchumi wa nchi na ustawi wa maisha ya wananchi. Twende kazi.

John Mnyika (Mb)

19 Julai 2013
John Mnyika at 2:15 AM
Share
HAYA NDIYO MAJIBU YA MH JOHN MNYIKA KUPITIA UKRASA WAKE WA TWITTER
 
Dr. Mgimwa alisema kwamba kodi hiyo ya Sh 1,000 haikupendekezwa na Serikali, bali ilipendekezwa na Bunge kupitia Kamati ya Bunge ambayo ilitaka wananchi wakatwe Sh 1,450.

Baada ya mapendekezo, Mgimwa alisema Serikali ilifanya uchambuzi na kuamua kupunguza hadi Sh 1,000. Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, jana alisema msimamo wa Serikali ndio wake pia.

Kauli ya Mgimwa inajibu malalamiko ya baadhi ya kampuni,wabunge na vyama vya siasa, kwamba ongezeko hilo linaongeza ugumu wa maisha kwa wananchi.

Hivi karibuni kampuni za simu na Mbunge wa Ubungo,John Mnyika (Chadema), walilalamikia kodi hiyo kwamba inaongeza gharama za maisha kwa wananchi.

Mbali na Mnyika,hata CCM kupitia taarifa ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ilitaka kodi hiyo iondolewe na Serikali itafute vyanzo vingine vya mapato.

Pia Chama cha Watoa Huduma za Mitandao ya Intaneti Tanzania (TISPA), walilalamikia sheria mpya ya kodi na ushuru wa bidhaa katika intaneti,kwamba itachangia ongezeko la gharama za huduma ya intaneti kwa watumiaji wa kawaida.

Source: Habari Leo

cc zomba, NasDaz
 
Last edited by a moderator:
ahaa wa@@@@@ wameacha kututete huko bungeni wanakuja huku mtandaon ili tujue nini watuchefue huyo mnyika pamo ja na makamba wote wako bungeni nawalikuwa na uwezo wotee kwa pamoja kutetea maslai ya wananch wao kutafuta sifa za kijinga

Duh kweli akili kumkichwa.Wapinzani ndo watetezi wa kweli wa wananchi mnyika na wenzake wamekuwa mstari wa mbele kupinga kodi na tozo kandamizi ila CCm kwa wingi,kiburi na jeuri wamekuwa wakipitisha.Ukimfananisha Makamba na Mnyika tutashindwa kuelewa uwezo wako kiakili.Wao CCm walipitisha ilo ili wapate pesaa ya kuhonga wapiga kura na kuwasaidia outgoing mafisadi wewe unakaa kumlaumu mnyika.Kura za Ndiyoooo walipiga wapinzani?Mbona unachangia Jf kwa uwezo mdogo kama unachangia kwenye blog ya michuzi?
 
Tuanza kutazama watu wafuatao,
1.Jacob Zuma ana degree?(Anaongoza nchi yenye technolojia ya hali juu na watu wenye elimu kubwa kuliko yako)
2.Melez Zenawi alikuwa na degree?Linganisha maendeleo yao na yako
3.Paul Kagame ana degree?(Nchi hiyo kiteknolojia inalingana na ya dokta wako?)
4.Bill Gates ana degree?(Unamlinganishaje na Profesa Muhongo na Dokta Mgimwa?)
5.Ongeza listi yako.....
6. ..........
Listi ya wanaccm
1. Deo Sanga kamaliza darasa la saba?
2. Steven Ngonyani kamaliza darasa la nne?
3. John Komba kamaliza darasa la 12?

Degree kam ni kigezo cha kufikiri na maendeleo basi hapa kwetu tungeendelea siku nyingi tu maana taifa hili linaongozwa na mtu mwenye degree nyingi zisizohesabika hadi za.........
Mbona hujasema na mnyika kwamba yuko kidato cha sita,mbowe kidato cha nne,sugu la saba,msigwa kidato cha nne.
 
Hata mimi ndugu mh Mnyika ningeomba kujua kama kabla ya kuandika mswaada Waziri wa Fedha alipita kwa wananchi ili kuomba maoni juu ya tozo hiyo anayoisema ya elfu 1000. Kwa nini wasitafute maoni kabla alafu wanakuja kubwabwaja kuomba maoni ya wananchi wale wale ambao waliwapuuza hapo kabla!! Na isingekuwa kelele za wabunge wa upinzani na kina Nape kwenye CCM wala hilo lisingesikilizwa. Na ajabu waliopitisha kwa wingi ni wabunge wa CCm. Najiuliza wakati mwingine hawa wabunge wa CCM wanaenda mwakilisha nani kama hta maoni ya wananchi wao hawayapati ili watengeze hoja???? Huwezi kumpuuza mwananchi at first site alafu tena eti waja kumuuliza kama anataka kutozwa kodi ama la!! Pathetic!! Sijapenda approach ya serikali yetu kufanya vitu kwa kutojiamini kiasi hiki!!

Anyway ndio Tanzania yetu hiyo inayowafumbia wakwepa kodi na mafisadi yawaonea wananchi wake kuwafanya ndio vyanzo vya mapato mbadala..
Tozo hiyo ilipendekezwa na Bunge lenyewe kupitia kamati ya bajeti inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi mashariki na aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali ya awamu ya tatu Mhe. Andrew Chenge. Na imeelezwa kwamba kamati hiyo ilipendekeza wananchi watozwe shs 1,450. Hivyo baada ya serikali kupokea mapendekezo hayo iliyachambua na kupunguza hadi shs 1,000 kwa line moja ya simu. Sasa suala la serikali kukusanya maoni ya wananchi litatoka wapi tena wakati suala lenyewe limependekezwa na wawakilishi au wasemaji wa wananchi. Wakulaumiwa zaidi ni hawa wabunge wetu (wasemaji kwa niaba ya wananchi). Hivyo huenda wabunge wa kamati hiyo walikusanya maoni ya wananchi ndio maana wakaja na mapendekezo hayo.
 
mnyika mmbea sana huyu kijana na mnafiki siasa za kijambazi zimepitwa na wakati jenga hoja acha uhuni hautakusaidia kitu.
 
NAMSIHI JANUARY MAKAMBA AACHE SIASA KATIKA SUALA LA KODI YA UMILIKI WA KADI ZA SIMU - MNYIKA


Mbunge wa Ubungo, John Mnyika.


​
Kufuatia kauli za Serikali magazetini kuhusu mimi na kodi ya umiliki wa kadi za simu; nijibu tu kwa ujumla kwamba SITAACHA. Badala yake naomba kuwapatia namba zao: Makamba 0767783996 na Mgimwa 0754/0684765644, tunachohitaji ni kauli ya Serikali kuwa kodi imesitishwa na itaondolewa na sio siasa chafu.

Kwa mliotaka msimamo wangu juu ya kauli ilinukuliwa jana tarehe 18 Julai 2013 na Gazeti la Majira kwamba Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba kwamba "Mnyika anaangalia upepo unakoelekea, akiona watu wanalalamika ndipo anaongea namsihi aache kufanya siasa katika jambo hili", naomba kutumia mtandao huu kutoa majibu ya ujumla kwa maswali na masuala yote kama ifuatavyo:

Nieleze kwamba sitaacha kufanya siasa kwenye jambo hili mpaka kodi hiyo itakapofutwa kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kubaki na fedha walau kidogo kwa maendeleo.

Sitaacha kufanya siasa kwa sababu ndio kazi yangu ambayo wananchi walinichagua kuifanya ya kuwawakilisha na kuisimamia Serikali ambayo yeye Makamba ni sehemu yake. Sitaacha kufanya siasa kwa sababu Mwalimu Nyerere alisema ili nchi yetu iendelee inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.

Ambacho sitafanya ni siasa chafu kama hizo ambazo Makamba amefanya za kusema uongo, kwa kuwa naamini anafahamu kabisa kwamba sijaanza kuongea kuhusu suala hili baada ya malalamiko ya wananchi bali jambo hili nilianza kulishughulikia bungeni mara baada ya Waziri wa Fedha kuwasilisha jedwali la marekebisho la kuanzisha kodi lukuki za simu ikiwemo hii. Katika mchango wangu bungeni, nieleza kwamba muswada huo wa sheria ya fedha kwa kupandisha kodi kwenye mafuta na simu ni ‘muswada wa majanga ya kuwaongezea mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi.

Aidha, sikuishia kusema tu kwa niaba ya wananchi bali nilichukua hatua kwa mujibu wa kanuni za Bunge nami kuwasilisha jedwali la marekebisho ya kupinga kodi ya umiliki wa kadi za simu pamoja na kodi nyingine zote zenye kuongeza mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi sio kwenye sekta ya mawasiliano bali pia kwenye sekta zingine ikiwemo sekta ndogo (sub sector) nyeti ya mafuta.

Mlioniuliza kwa SMS katika simu na kwenye mitandao ya kijamii sasa ni wakati wa Makamba kuhojiwa kwa njia hizo hizo (Simu yake ya Mkononi ni 0767783996) kwa kuwa yeye ni sehemu ya Serikali na Serikali ndiyo ambayo iliingiza suala hili kwa mara ya kwanza ndani ya ukumbi wa Bunge kupitia hotuba ya Bajeti Serikali na ikalirudia kuliingiza kupitia jedwali la marekebisho ya Sheria ya Serikali; ni wakina nani hasa kwa majina ndani ya Serikali na Bunge walioingiza kodi hii? Na ni wakina nani hasa waliopigia kura ya ndio kuipitisha?

Aidha, amenukuliwa na gazeti la Mwananchi la leo tarehe 19 Julai 2013 akieleza kwamba hakubaliani na suala hili na kupita kwake ilikuwa na kuzidiwa nguvu. Hivyo, ataje kwa majina hayo waliozidi nguvu serikali kinyume na matakwa yake. Amenukuliwa akisema pia kwamba anajua kuwa suala hili haliwezi kutekelezwa na kwamba ni lazima litabadilishwa kwa kuangalia eneo lingine la kutoza kodi.

Ni vizuri akahojiwa, ikiwa huo ni msimamo wa Serikali; mwenye mamlaka ya kusitisha kodi hiyo ni nani na kwanini hajitokezi kutoa agizo la kusitisha wakati maandalizi yakiendelea ya kupeleka muswada bungeni wa kuifuta kabisa kodi hiyo katika mkutano ujao?

Wakati Naibu Waziri akisema hayo, Waziri wa Fedha Dk William Mgimwa katika Serikali hiyo hiyo yeye ametoa kauli tofauti siku hii hii ya leo ambapo kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania amewataka watumiaji wa mitandao ya simu nchini na watanzania kwa ujumla kuwa na subira kuhusu tozo ya sh 1000 kwa mwezi kwa kila laini ya simu za kiganjani.

Na kwa kuwa amesema kwamba Serikali inaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau, natoa mwito kwa wananchi kumtumia maoni kupitia namba zake za simu za mkononi 0754/0684-765644.

Aidha, ni vizuri aeleze subira hiyo ivutwe mpaka lini? Na ni wakina nani hasa kwa majina waliomfanya akaingiza kodi hiyo katika kitabu cha Hotuba yake aliyosoma bungeni kuhusu bajeti ya Serikali na wakina na hasa kwa majina waliomfanya arejeshe kodi hiyo ya kadi za simu kwenye jedwali la marekebisho ya muswada wa sheria ya fedha alilowasilisha bungeni.

Nasisiza kuwa kauli za ujumla za Serikali bila kuwataja kwa majina wahusika ni za kujivua mzigo wa lawama baada ya malalamiko ya wananchi kuhusu kodi hii na nyinginezo kwa kuhamisha mzigo huo kwa wabunge. Ni muhimu badala ya kutoa kauli za ujumla za kulaumu wabunge, Rais ama kiongozi mwingine mwenye mamlaka ajitokeze kusitisha kutozwa kwa kodi hiyo na kuanzisha mchakato wa muswada wa kufuta kodi hiyo kuwasilishwa katika mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza tarehe 27 Agosti 2013.

Majina ya wahusika yasipotajwa au mamlaka zinazohusika zisipotoa kauli katika mkutano wa hadhara nitakaoshiriki jumapili tarehe 21 Julai 2013 katika Uwanja wa Sahara kata ya Mabibo kuanzia saa 8 Mchana mpaka saa 11 Jioni nitatoa mrejesho kuhusu yaliyojiri katika mkutano uliopita wa Bunge na kueleza hatua zaidi zinazopaswa kuchukuliwa kuwezesha majina ya wabunge hao kutajwa hadharani na hatua za kuondoa kodi hiyo kuchukuliwa.

Uongozi bora na uraia mwema wenye uwajibikaji ni chimbuko na chachu ya ukuaji endelevu wa uchumi wa nchi na ustawi wa maisha ya wananchi.

Twende kazi.

John Mnyika (Mb)
19 Julai 2013
 
Hivi hata Myika angetetea bungeni kwa jinsi wabunge wa ccm walivyo wangekubali/ni mara ngapi mnyika amekuwa akitetea hoja muhimu lakini ccm wanaleta mambo ya kijongoo jongoo!
ahaa wa@@@@@ wameacha kututete huko bungeni wanakuja huku mtandaon ili tujue nini watuchefue huyo mnyika pamo ja na makamba wote wako bungeni nawalikuwa na uwezo wotee kwa pamoja kutetea maslai ya wananch wao kutafuta sifa za kijinga
 
Mimi nimesema kuwa na mbunge kama mnyika bora kufuga kuku utakula nyama kwa nini mnyika awe muongo kiasi kile alikuwepo bungeni akachangia eti leo ndiyo kaweka pua juu anapinga si unafiki huo mnona hakupinga bungeni siku ile wabunge wengine hasara tupu.
 
kwa mantiki hiyo mnyika anataka tuamini kuwa yeye ndiye mwenye huruma na watu akawadanganye akina junior wale wa dk slaa lakini hawezi kudanganya watu wazima tunajua uongo na uzandiki wa mnyika ulivyo.
 
Nawe ni afadhali ya kunguru utaweza safisha jiji lililomshinda waziri wa mazingira kwa sasa
 
mnyika mmbea sana huyu kijana na mnafiki siasa za kijambazi zimepitwa na wakati jenga hoja acha uhuni hautakusaidia kitu.

Kijana na kushauri uwe unasoma kwa makini? sidhani kama hata maana ya hoja unaifahamu. nakuonea huruma pengine hata ujui nini kina jadiliwa, tulia chini soma hoja za mnyika hapo juu ameandika vizuri sana.
 
kwa mantiki hiyo mnyika anataka tuamini kuwa yeye ndiye mwenye huruma na watu akawadanganye akina junior wale wa dk slaa lakini hawezi kudanganya watu wazima tunajua uongo na uzandiki wa mnyika ulivyo.

nimeamini sasa hujui kinacho ongelewa hapa au ujui kusoma, hebu tueleze uongo wa mnyika na ukweli wa January.
 
Mbona hujasema na mnyika kwamba yuko kidato cha sita,mbowe kidato cha nne,sugu la saba,msigwa kidato cha nne.

Shirikisha ubongo kwanza.Kama elimu ni kigezo kwanini sasa hawa unaowaita kidato cha sita,nne,la saba wanawatikisa wenye degree kubwa kubwa kina Makame Mbarawa?Elimu waliyoipata inatusaidiaje sisi tusio na elimu?Elimu kubwa kuwaongezea mzigo wananchi?Degree za kuhonga hizo.Mnyika ana elimu na maarifa pia.Uchambuzi wake ndio unaowaamsha wananchi kujua haki zao.Tangu lini kina Juma Nkamia wakajenga hoja za maana?Kila siku kupigana vikumbo tu vya kusifia kina kikwete na salma ili wafikiriwe kuwa mawaziri.Na kuonesha akili kuwa ndogo mnapinga hata waziri kutokuwa mbunge.Unaweza kutuambia kwanini?Huna hoja kaa chumbani kwako wewe.
 
Back
Top Bottom