Makamba: Mnyika acha Unafiki, sote tumeshindwa Bungeni!

Makamba: Mnyika acha Unafiki, sote tumeshindwa Bungeni!

Mnyika wewe ni jembe na kazi zako unatimiza kwa kufuatilia ILA kuna watu ambao wamepewa madaraka kwa sababu fulani tu na kutokana na udhaifu wao ni waoga mno wanapoambiwa ukweli au wanapokumbushwa wajibu wao na hii inatokana na udhaifu wao au kuogopa kujulikana kwa ubabaishaji wao! Keep it up Mnyika tupo nawe daima.
 
Makamba anachokifanya hapa ni upumbavu kwa sababu, Tanzania yote inafahamu ni kwa namna gani chini ya makinda na ndungai bunge la Tanzania limehodhiwa na ccm.

Bunge linaendeshwa kibauguzi kila mtu akiona. ccm wameruhusiwa kututkana na kutumia kila aina ya kinachowezekana kuhakikiksha wapinzani wanakuwa kama watoto wa kambo. Nani asiyejua makinda na ndugai wamekuwa msitahir wa mbele kuhakikisha hakuna hoja inayosimamiwa na upinzani inapita.

Kama Makamba ama ccm wangelikuwa na nia ya kusaidia wananchi, wao kwa kuwa bunge ni la kwao na lolote wanalolitaka wao linapita chini ya mama yao makinda, ndio walitakiwa wapitishe hiyo hoja. Mnyika na wapinzani wote nani angewasilikliza?

Sasa yameharibika, mnaanza upumbavu wa kusema hata mnyika alikuwa bungeni na alitakiwa naye apitishe hoja. Hiyo heshima kwa wapinzani kama ingelikuwa ndani ya moyo wa ccm, bunge la makinda na serikali yao, tanzania leo tungekuwa mbali sana.

Makamba, usimlaumu Mnyika kwa kusema ukweli. Lawama zako ziende kwa raisi Kikwete anayeabudu anayeendekeza matabaka nchini bia kuonyesha ufahamu na kujali mgawanyo wa majukumu ya kofia zake za uongozi wa ccm na serikali. Yote kayaweka ccm.

Lawama ilaumu ccm kwa kuadvocate mfumo gandamizi, nyanyasi kwa watetea wananchi na huku mfumo huo ukiwa butu kwa mahtaji ya taifa, na kukumbatia interest zenu na mafisadi.

Mtaumbuka na huu ni mwanzo.....

Bunge mdictate huku kila mtu akiona. Udhalilishaji unaofanywa kwa vyama vya upinzani asiyeujua ni yule asiyfahamu kiswahili tu. Hoja za wapinzania hata kama ziko nzuri namna gani, mnafanya kampeni za kuzikataa kwamba haziwezekani na kuwazomea. Mkiona nguvu ya umma inazikubali, mnazidandia na kuzitekeleza bila utaalamu wala nia, na kwa ujumla mnazitekeleza kinafiki.

Sasa leo ni nain atakaye kubali kwamba mkirudi bungeni mtafanya jema ikiwa kila siku mmekuwa mkiwatukana watetezi wa wananchi?

Makamba haya yanyweni wenyewe. Sis tunajua ukweli. Bungeni mmepafanya pango la wanyang'anyi sehemu ya kunyonga haki za watanzania.

Mnyika, songa mbele!, makamba na magamba yao shame on you!!!!!!!!!!.



Kauli ya MNYIKA:

John-Mnyika-on-kodi-za-simu-July-19-2013.png



Kauli ya MAKAMBA:

January-Makamba-on-Mnyika-acha-unafiki-July-19-20131.png




MAJIBU YA MNYIKA KWA MATUSI YA MAKAMBA.

Kufuatia kauli za Serikali magazetini kuhusu mimi na kodi ya umiliki wa kadi za simu; nijibu tu kwa ujumla kwamba SITAACHA. Badala yake naomba kuwapatia namba zao: Makamba 0767783996 na Mgimwa 0754/0684765644, tunachohitaji ni kauli ya Serikali kuwa kodi imesitishwa na itaondolewa na sio siasa chafu.

Kwa mliotaka msimamo wangu juu ya kauli ilinukuliwa jana tarehe 18 Julai 2013 na Gazeti la Majira kwamba Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba kwamba "Mnyika anaangalia upepo unakoelekea, akiona watu wanalalamika ndipo anaongea namsihi aache kufanya siasa katika jambo hili", naomba kutumia mtandao huu kutoa majibu ya ujumla kwa maswali na masuala yote kama ifuatavyo:
Nieleze kwamba sitaacha kufanya siasa kwenye jambo hili mpaka kodi hiyo itakapofutwa kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kubaki na fedha walau kidogo kwa maendeleo.

Sitaacha kufanya siasa kwa sababu ndio kazi yangu ambayo wananchi walinichagua kuifanya ya kuwawakilisha na kuisimamia Serikali ambayo yeye Makamba ni sehemu yake. Sitaacha kufanya siasa kwa sababu Mwalimu Nyerere alisema ili nchi yetu iendelee inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.

Ambacho sitafanya ni siasa chafu kama hizo ambazo Makamba amefanya za kusema uongo, kwa kuwa naamini anafahamu kabisa kwamba sijaanza kuongea kuhusu suala hili baada ya malalamiko ya wananchi bali jambo hili nilianza kulishughulikia bungeni mara baada ya Waziri wa Fedha kuwasilisha jedwali la marekebisho la kuanzisha kodi lukuki za simu ikiwemo hii. Katika mchango wangu bungeni, nieleza kwamba muswada huo wa sheria ya fedha kwa kupandisha kodi kwenye mafuta na simu ni ‘muswada wa majanga ya kuwaongezea mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi.

Aidha, sikuishia kusema tu kwa niaba ya wananchi bali nilichukua hatua kwa mujibu wa kanuni za Bunge nami kuwasilisha jedwali la marekebisho ya kupinga kodi ya umiliki wa kadi za simu pamoja na kodi nyingine zote zenye kuongeza mzigo wa gharama za maisha kwa wananchi sio kwenye sekta ya mawasiliano bali pia kwenye sekta zingine ikiwemo sekta ndogo (sub sector) nyeti ya mafuta.

Mlioniuliza kwa SMS katika simu na kwenye mitandao ya kijamii sasa ni wakati wa Makamba kuhojiwa kwa njia hizo hizo (Simu yake ya Mkononi ni 0767783996) kwa kuwa yeye ni sehemu ya Serikali na Serikali ndiyo ambayo iliingiza suala hili kwa mara ya kwanza ndani ya ukumbi wa Bunge kupitia hotuba ya Bajeti Serikali na ikalirudia kuliingiza kupitia jedwali la marekebisho ya Sheria ya Serikali; ni wakina nani hasa kwa majina ndani ya Serikali na Bunge walioingiza kodi hii? Na ni wakina nani hasa waliopigia kura ya ndio kuipitisha?

Aidha, amenukuliwa na gazeti la Mwananchi la leo tarehe 19 Julai 2013 akieleza kwamba hakubaliani na suala hili na kupita kwake ilikuwa na kuzidiwa nguvu. Hivyo, ataje kwa majina hayo waliozidi nguvu serikali kinyume na matakwa yake. Amenukuliwa akisema pia kwamba anajua kuwa suala hili haliwezi kutekelezwa na kwamba ni lazima litabadilishwa kwa kuangalia eneo lingine la kutoza kodi. Ni vizuri akahojiwa, ikiwa huo ni msimamo wa Serikali; mwenye mamlaka ya kusitisha kodi hiyo ni nani na kwanini hajitokezi kutoa agizo la kusitisha wakati maandalizi yakiendelea ya kupeleka muswada bungeni wa kuifuta kabisa kodi hiyo katika mkutano ujao?

Wakati Naibu Waziri akisema hayo, Waziri wa Fedha Dk William Mgimwa katika Serikali hiyo hiyo yeye ametoa kauli tofauti siku hii hii ya leo ambapo kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania amewataka watumiaji wa mitandao ya simu nchini na watanzania kwa ujumla kuwa na subira kuhusu tozo ya sh 1000 kwa mwezi kwa kila laini ya simu za kiganjani.

Na kwa kuwa amesema kwamba Serikali inaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau, natoa mwito kwa wananchi kumtumia maoni kupitia namba zake za simu za mkononi 0754/0684-765644.
Aidha, ni vizuri aeleze subira hiyo ivutwe mpaka lini? Na ni wakina nani hasa kwa majina waliomfanya akaingiza kodi hiyo katika kitabu cha Hotuba yake aliyosoma bungeni kuhusu bajeti ya Serikali na wakina na hasa kwa majina waliomfanya arejeshe kodi hiyo ya kadi za simu kwenye jedwali la marekebisho ya muswada wa sheria ya fedha alilowasilisha bungeni.

Nasisiza kuwa kauli za ujumla za Serikali bila kuwataja kwa majina wahusika ni za kujivua mzigo wa lawama baada ya malalamiko ya wananchi kuhusu kodi hii na nyinginezo kwa kuhamisha mzigo huo kwa wabunge. Ni muhimu badala ya kutoa kauli za ujumla za kulaumu wabunge, Rais ama kiongozi mwingine mwenye mamlaka ajitokeze kusitisha kutozwa kwa kodi hiyo na kuanzisha mchakato wa muswada wa kufuta kodi hiyo kuwasilishwa katika mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza tarehe 27 Agosti 2013.

Majina ya wahusika yasipotajwa au mamlaka zinazohusika zisipotoa kauli katika mkutano wa hadhara nitakaoshiriki jumapili tarehe 21 Julai 2013 katika Uwanja wa Sahara kata ya Mabibo kuanzia saa 8 Mchana mpaka saa 11 Jioni nitatoa mrejesho kuhusu yaliyojiri katika mkutano uliopita wa Bunge na kueleza hatua zaidi zinazopaswa kuchukuliwa kuwezesha majina ya wabunge hao kutajwa hadharani na hatua za kuondoa kodi hiyo kuchukuliwa.

Uongozi bora na uraia mwema wenye uwajibikaji ni chimbuko na chachu ya ukuaji endelevu wa uchumi wa nchi na ustawi wa maisha ya wananchi. Twende kazi.
John Mnyika (Mb)
19 Julai 2013



 
Back
Top Bottom