John Mnyika ;kaweka namba yangu ya simu ya mkononi ili watu wanipigie na kutukana. Nadhani ni siasa isiyo ya kistaarabu. Hadi sasa nimepata messages zaidi ya 600. Sio sahihi kabisa. Wabunge WOTE tulishindwa kupitisha maamuzi yenye maslahi kwa mtu wa kipato cha chini. Harakati za mitandaoni haziondoi ukweli huo. Vilevile, kodi hii imepitishwa tarehe 29 Juni 2013. Kwa Mbunge ambaye alikuwa na wajibu wa kulipinga siku hiyo na kulisemea kuanzia tarehe 30 Juni 2013 kuamka leo na kutapatapa mitandaoni ni unafiki mkubwa na ni siasa za kuangalia upepo unapovuma na ni unafiki mkubwa. Namheshimu
Zitto Kabwe kwasababu alitoa kauli immediately ya kusema anaona aibu kuwa sehemu ya Bunge hili na kwamba wawakilishi wa wananchi wamewaangusha wananchi. Mwenzake John Mnyika anajitoa fahamu na kufanya harakati kupitia press releases.
Suluhisho hapa sio kulumbana wala kutupiana lawama. Suluhisho ni kurudi Bungeni na kubadilisha pale tulipokosea. Sio kutafuta umaarufu mitandaoni. Kunapotokea kosa, tunasahihisha haraka then we move on. Siasa sio kwenye kila jambo.
SOURCE JANUARY MAKAMBA FACEBOOK PROFILE .past 1min
Kwa hili naomba nimtetee Mnyika. Nilikuwepo wakati muswada wa fedha ulipowasilishwa, kujadiliwa na kupitishwa na Bunge.
Kwanza, kipengele cha hii kodi ya laini za simu kilikuwepo kwenye hotuba ya Waziri wa Fedha. Lakini wakati anaisoma hotuba hiyo, alipofikia kwenye kipengele hicho akaliambia bunge kuwa kimeondolkewa, hakipo.
Lakini hilo halikuwazuia baadhi ya wabunge kulizungumzia wakati wakiijadili bajeti. Na nilichokibaini katika michango ya wabunge walionyesha kuwa serikali imekuwa haitozi kodi kwa kiasi cha kutosha kutoka kwenye makampuni ya simu. Nadhani Waziri wa Fedha (Serikali) ikadhani kuwa hata kule kuondoa kodi ya laini za simu ilikuwa ni kosa.
Hivyo, alipokuja kusoma muswada wa fedha, Waziri wa Fedha akakirudisha kile kifungu cha kodi ya laini za simu. Katika mjadala wa muswada huo kulikuwa na baadhi ya wabunge, Mnyika akiwa mmoja wao, walipinga sana kuletwa kwa kifungu hicho na argument yao ilikuwa ni kuwa ni kodi hii itawaumiza wananchi wa kipato cha chini.
Nakumbuka Mnyika pia aliwasilisha jedwali la mabadiliko akipendekeza kuondolewa kwa kifungu hicho na kupendekeza serikali itapataje fedha za kufidia pengo litakalotokana na kuondolewa kwa kifungu hicho.
Lakini, licha ya jitihada hizo na michango ya baadhi ya wabunge, mtindo wa kutumia wingi wa wabunge wa CCM, kipengele hiki kilipita.
Nilifahamu tangu pale kuwa mjadala kuhusiana na suala hili utaendelea mpaka nje ya Bunge na serikali (na CCM) watakuwa katika hali mbaya.
Nadhani wanachokifanya serikali hivi sasa ni kutafuta namna ya kujinasua katika kosa hilo walilolifanya kwa sababu CCM inafahamu fika kuwa mwakani ni mwaka wa uchaguzi wa serikali za mitaa na hili ni moja ya mambo ambayo yatawaharibia sana kwenye kampeni zao vijijini.
Hivyo, Makamba asimlaumu Mnyika kwamba hakulisemea suala hili. Mnyika alilisemea tena kwa nguvu na weledi mkubwa, isipokuwa wingi wa wabunge wa CCM ndio ulizima sauti yake.
Makamba, mmelikoroga, tafuteni namna ya kulinywa bila kutafuta mbuzi wa kafara