Makamba: Mnyika acha Unafiki, sote tumeshindwa Bungeni!

Makamba: Mnyika acha Unafiki, sote tumeshindwa Bungeni!

January Makamba asijifanye kuruka kamba, wananchi tunajua waliosema ndiyoooo ni wabunge wa CCM kwa lengo la kupitisha tozo hiyo iliyoletwa na serikali ya CCM.Tunajua kwamba katika kitabu cha ripoti ya CAG imeanishwa kwamba 27% ya kodi serikali inawasamehe wawekezaji na makampuni yanayoingiza faida lakini wanapoishiwa fedha wanakimbilia kutukamua wananchi.
 
In fact nadhani hii thread badala ya kusomeka:

[h=2]"Mnyika acha Unafiki, sote tumeshindwa Bungeni"[/h]
ilitakiwa kusomeka:
[h=2]"Mnyika acha Unafiki, CHADEMA mmeshindwa Bungeni"[/h]
Kwa kweli katika hili CHADEMA wakubali walichemka kuwatetea wananchi; usiniulize kwa nini.
 
Mnyika anapenda sifa za kizamani sana ndio maana alichemka chuo kijana mzima hana degree

The same ilitokea kwenye fao la kujitoa alianza hivi hivi nje ya bunge na hoja ikarudi bungeni though mbunge wa CCM alitoa hoja lakini move ilianzia uraiani, sio kwamba anapenda sifa bali anatekeleza majukumu yake kwa kuhamasisha wananchi kuliona hili
 
Mnyika anapenda sifa za kizamani sana ndio maana alichemka chuo kijana mzima hana degree
[MENTION]
PHP:
[/MENTION]

Acha kukurupuka wewe ulikuwa umelala? ccm kazi yao nikusema ndiooooo! hata kama hawajaelewa kilichoko kwenye makaratasi mtakuja kusema ndiooo hata siku mnaulizwa mpigwe kitanzi nyinyi vichwa vyenu sijui vikoje, kama mnyika alichemka hao maprofesa wenu tumefaidika nao vp katika mstakabali wa taifa hili kazi kupiga makofi tu.
 
Wabonge wa CCCM wakiwa Dom ni mitungi, mikasi na ushabiki wa kip_mbavu
 
Mnyika anapenda sifa za kizamani sana ndio maana alichemka chuo kijana mzima hana degree
Hizi ndiyo akili za Ki CCM! Hivi Tanzania ina vijana wanagapi wenye degree? Kwa kauli hii huoni kama umewadhalilisha vijana wote ambao hawana degree? Lakini siyo kosa lako, maana avatar yako inaonyesha wazi kwamba wewe ni msukule.
 
John Mnyika ;kaweka namba yangu ya simu ya mkononi ili watu wanipigie na kutukana. Nadhani ni siasa isiyo ya kistaarabu. Hadi sasa nimepata messages zaidi ya 600. Sio sahihi kabisa. Wabunge WOTE tulishindwa kupitisha maamuzi yenye maslahi kwa mtu wa kipato cha chini. Harakati za mitandaoni haziondoi ukweli huo. Vilevile, kodi hii imepitishwa tarehe 29 Juni 2013. Kwa Mbunge ambaye alikuwa na wajibu wa kulipinga siku hiyo na kulisemea kuanzia tarehe 30 Juni 2013 kuamka leo na kutapatapa mitandaoni ni unafiki mkubwa na ni siasa za kuangalia upepo unapovuma na ni unafiki mkubwa. Namheshimu Zitto Kabwe kwasababu alitoa kauli immediately ya kusema anaona aibu kuwa sehemu ya Bunge hili na kwamba wawakilishi wa wananchi wamewaangusha wananchi. Mwenzake John Mnyika anajitoa fahamu na kufanya harakati kupitia press releases.
Suluhisho hapa sio kulumbana wala kutupiana lawama. Suluhisho ni kurudi Bungeni na kubadilisha pale tulipokosea. Sio kutafuta umaarufu mitandaoni. Kunapotokea kosa, tunasahihisha haraka then we move on. Siasa sio kwenye kila jambo.

SOURCE JANUARY MAKAMBA FACEBOOK PROFILE .past 1min
 
Mnapokuwa bungeni wabunge wa CCm huwa mnajitoa roho linabaki kasha tu la mwili! aibu kabisa!!
 
HUNA AKILI KWELI NA NADHANI HUFUATILIE MAMBO YA BUNGE..NA KUMBUKA BUNGENI CDM NA CCM WENGI NI WAPI .NA KINA NANI WANASEMAGA NDIOOOOOOOOOOOOO....NAUNGA HOJA 100%MKONO,THEN WANAANZA KULALAMIKA.CCM NDO MMETUFIKISHA HAPA TULIPO..NA BADO MTAAONA MENGI MPAKA HATA MAHARAGE MTASHINDWA KUNUNUA.

Everything that can be counted does not necessarily count; everything that counts cannot necessarily be counted.
Albert Einstein
 
Majibu ya makamba haya hapa:

January Y. Makamba

John Mnyika kaweka namba yangu ya simu ya mkononi ili watu wanipigie na kutukana. Nadhani ni siasa isiyo ya kistaarabu. Hadi sasa nimepata messages zaidi ya 600. Sio sahihi kabisa.

Wabunge WOTE tulishindwa kupitisha maamuzi yenye maslahi kwa mtu wa kipato cha chini. Harakati za mitandaoni haziondoi ukweli huo. Vilevile, kodi hii imepitishwa tarehe 29 Juni 2013. Kwa Mbunge ambaye alikuwa na wajibu wa kulipinga siku hiyo na kulisemea kuanzia tarehe 30 Juni 2013 kuamka leo na kutapatapa mitandaoni ni unafiki mkubwa na ni siasa za kuangalia upepo unapovuma na ni unafiki mkubwa. Namheshimu Zitto Kabwe kwasababu alitoa kauli immediately ya kusema anaona aibu kuwa sehemu ya Bunge hili na kwamba wawakilishi wa wananchi wamewaangusha wananchi. Mwenzake John Mnyika anajitoa fahamu na kufanya harakati kupitia press releases.

Suluhisho hapa sio kulumbana wala kutupiana lawama. Suluhisho ni kurudi Bungeni na kubadilisha pale tulipokosea. Sio kutafuta umaarufu mitandaoni. Kunapotokea kosa, tunasahihisha haraka then we move on. Siasa sio kwenye kila jambo.
 
Mnyika anapenda sifa za kizamani sana ndio maana alichemka chuo kijana mzima hana degree

Kwani vijana wote watanzania wana degree? Hata hivyo sidhani km degree inamata! Mwigulu ana degree lakini inamsaidia kutoa matusi tu ambayo hayasaidii taifa hili
 
Wana-JF nao ni vigeu geu kama wana-siasa....ndo upuuzi wa kuburuzwa na wanasiasa huu!! Mbunge Ally Kessy aliposhuka nondo kule bungeni kuhusu wananchi kulipa kodi; humu watu wakamshangilia huku wakimvika mashada ya maua! Wakatokea wengine wakasema Ally Kessy hakustahili kabisa kuwepo kwenye chama cha magamba!!Leo mnatandikwa kodi ya book book kwa mwezi; mnakuja tena hapa mnatupigia kelele! Tuache unafiki.....

By the way, naungana na January...wabunge walikuwapo na wakapitisha, waache unafiki wao hapa wa kujifanya wanapinga! Hawa akina Mnyika nao ni wale wale tu....Mnyika ninayemfahamu mimi kama kitu anakipinga kwa ukweli, lazima ataitisha Press Conference! And for this, am convinced kwamba wiki ijayo haitaisha kabla Mnyika hajaitisha Press Conference kuzungumzia kodi ya Laini za simu.....seuze wiki ijayo, hiyo jtatu sijui kama itafika!!!!!!
 
Hata upinzani wakisema hapana nyie ccm mnapitidha kwa ndio ya kishindo. Msiwatupie lawama upinzani kwani kwenye kipitisha sauti zao zinazimwa.
 
Makamba nambie kuhusu hii, mnaunga mkono hoja ndiooo! Mnatumia wingi wenu? Mmeumbuka nyie mnatia aibu
 
In fact nadhani hii thread badala ya kusomeka:

"Mnyika acha Unafiki, sote tumeshindwa Bungeni"


ilitakiwa kusomeka:
"Mnyika acha Unafiki, CHADEMA mmeshindwa Bungeni"


Kwa kweli katika hili CHADEMA wakubali walichemka kuwatetea wananchi; usiniulize kwa nini.
Naungana na wewe, hawa jamaa kama kitu hawakitaki, pamoja na uchache wao bunge linatikisika....full miongozo, full kutoana bungeni na ikibidi, wenyewe wanasepa......lakini hili la kadi za simu kimyaaaa; hata kama walipinga, si kwa staili ile iliyozoeleka; ni kupinga ili mradi tu lakini hawakuwa determined!
 
Mnyika anapenda sifa za kizamani sana ndio maana alichemka chuo kijana mzima hana degree

Issue sio degree Jina; Tumewaona Ma-Professors wakishindwa Kuongoza na hawana cha Kufanya. Issue ni Kujua kuchambua mambo, Degree ni nini?? Bila kujua kinachohitajika kwa wakati gani.. Wasomi wenye ma Phd wameweka mfukoni elimu zao na Kufikiria kwa kutumia matumbo. Ondoa mawazo yako mgando huyu Kijana ni KICHWA wether you like or not..Enjoy Oja sio Elimu ya Mtu " Elimu za Vyuo Vya Tanzania njingi ni Feki" wala usijalibu kuturudisha nyuma. The Guy is smart....
 
Kwani si yeye aliesema namba za wabunge wetu zipo kwenye site ya bunge? Sasa kama tumeipata hii namba huko? Huyu jamaa lina wivu halafu ni linafiki halioni hata aibu kuwa naibu waziri wa mawasiliano wizara hiyohiyo iliyobariki hii tozi kweli!!!?
 
AAche UKUDA huyo February lini wamekubaliana na upinzani? Tena walipitisha hoja hii wakati wabunge wa CDM wakiwa Arusha
 
Binafsi niseme tu kuwa, ndugu yangu Januari Yusufu Makamba anamapungufu makubwa katika tafakuri ya mambo mazito,

Yeye ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia ambapo mamlaka ya mawasiliano ipo chini yake,

Yeye ni mbunge wa ccm, ambapo mswada wowote wa serikali kabla ya kupitishwa na Bunge ilikuwa sheria ni lazima WABUNGE wa chama chenye serikali wakutane na kuridhia upitishaji huo, kisha huingia bungeni na kupitisha kwa KAULI moja,

Sasa haiingii akili kijana tunaemtegemea kuwa injini ya maamuzi mema anakuwa na akili nyepesi kiasi hiki, anafanya siasa kwenye mambo yasiyohitaji siasa?

Sasa ndio anataka tuamini kuwa ana maslahi katika makampuni haya ya simu nchini?,

Wabunge wote CCM wamelipitisha hili suala la kodi ya simu kadi bila hata kusita, na kibaya zaidi limepitishwa kipindi kile cha mpito wa Mauaji ya BOMU yaliyofanywa na JESHI la polisi kule ARUSHA ambapo wabunge wote wa CHADEMA walikuwa huko na wale waliorejea hawakupata fursa ya kupitia jambo hili kwa utuvu,

Sasa Januari atueleze wazi kuwa yeye na tumu yake wameshindwa kusimamia wizara hii na wapishe watu wengune,

Watanzania ni werevu na wanatambua kuwa kulipa kodi ni lazima, lakini wanayo haki yakupinga kodi zenye sura ya unyanyasaji na za kifisadi!

Hivi mtanzania anaeishi chini ya mstari wa umasikini (under poverty line) wa shilingi 260 kwa siku, aliyejikakamua kwa miezi sita na kufanikiwa kumiliki simu ya 15,000/= leo umtake alipe 1000 kwa mwezi, gharama ya mda wa maongezi nayo imepanda, gharama ya chakula imepanda, gharama ya matibabu imepanda, gharama ya maji imepanda, nauli imepanda,

Lakini cha ajabu KIPATO cha Mtanzania huyu HAKIJAPANDA, je ataweza mzigo huu????

Januari mtoto wa Makamba fikiria kwanza kabla hujatoa maneno mkuu!

Takwimu za uchumi wa Tanzania kupitia GIN 2000-2010 zinasema kuwa, watanzania 60% wanaishi chini ya mstari wa umasikini, na watanzania 26% ni maikini wa wastani, wakati WATANZANIA 14% ni matajiri wanaoishi maisha ya anasa wakimiliki mahekalu ya kifahari na watoto wao kusoma shule za sifa ya kimataifa,

Sasa jiulize, je Bibi zetu akina Maseto, Mng'anzagala, Chabilibi, Muhuvila, walipe shilingi 1000 sawa na Reginand Mengi, Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete, Edward Lowasa, Freeman Mbowe, Yusufu Manji?????????

Kodi hii ni mzigo kwa Watanzania 60% wanaoishi chini ya mstari wa umasikini!

Serikali isitishe haraka sana kabla watanzania hatujaamua kuisitisha wenyewe!
 
Back
Top Bottom