Matumizi ya umeme Tanga, Arusha yapaa, Tanesco yasaini mkataba kuyakabili

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,847
21,487
Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limetia saini ya makubaliano ya uendelezaji na ujenzi wa njia za umeme na Kampuni za Gridworks ya Uingereza na Larsen & Tourbo ya India.

Mkataba huo unahusisha utekelezaji wa miundombinu hiyo kutoka Chalinze kupitia Segera mpaka Tanga, na kutoka Chalinze, Segera, Same na Kisongo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Maharage Chande amesema hatua hiyo ni kufuatia kuongezeka kwa matumizi ya umeme katika mikoa ya Tanga na Arusha kwa sababu ya viwanda na shughuli za uchumi kuongezeka hivyo kusababisha njia za kupitisha umeme kuzidiwa.

"Kwa kipindi cha muda mrefu tumechelewa kutekelezeka miradi kama hii kwa kukosa fedha lakini kwa mara ya kwanza tunasaini makubaliano na sekta binafsi kuendeleza sekta hii," amesema Chande.
Chande ameongeza shirika la Larsen & Tourbo (L&T) litaendeleza na kujenga njia hizo kisha Tanesco litalipa kidogo kidogo kurejesha gharama za ujenzi zilizotumika.

"Wakijenga tutaharakisha maendeleo kwa wananchi wa Tanga na Arusha badala ya kusubiri mpaka kibubu chetu kijae huku maendeleo yanachelewa," amesema.

Aidha amesema pande zote mbili zitaketi kupanga gharama za mradi huo na kukubaliana na pia ipo nafasi ya Tanesco kuchukua na kuendesha mradi huo endapo fedha zikipatikana.

"Tunatarajia mradi huu kutumia miezi 30 mpaka kukamilika kwake, miezi 12 kwa ajili ya Utayarishaji na miezi 18 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi," amesema.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Gridworks, Simon Hodson, amesema uwekezaji katika usafirishaji wa nishati ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na upatikanaji wake barani Afrika.

"Miundombinu ya usafirishaji umeme inahitaji mtaji ili kuongeza uwezo wake na kusaidia upatikanaji wa kiwango cha kutosha katika maeneo husika ili kukuza uchumi," amesema Hodson.

Naye Makamu wa Rais wa L&T, Rahul Sikka, amesema mradi huo ni fursa kwao Kwani utachukua jukumu muhimu katika kuimarisha upatikanaji wa nishati na kutegemewa nchini Tanzania.

"Mradi huu utaimarisha mtandao wa usambazaji umeme unaounganisha maeneo muhimu ya nchi, kutengeneza njia ya kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya umeme, kuchochea ukuaji wa uchumi, kuunda fursa kwa biashara zaidi kustawi, na kuboresha hali ya jumla ya maisha kwa jamii za wenyeji," amesema Sikka.
 
Iendelee wapi? Wametumwa na nani kuingia makubaliano haya?

Nakala yake tutaiweka hapa soon.
Yaani nyie ni wapumbavu wa Hali ya Juu,hayo makubaliano Yana shida gani Sasa? Kwani hiyo ni njia ya kusafirisha umeme ya kwanza kuingia? Kuna njia kibao zinatakiwa kuingia kusafirisha umeme.

Kiufupi wewe nyumbu hueleweki yaani shida Yako ni nini?
 
Wewe ndiye pumba , ni utafiti upi ulionyesha matumizi ya umeme Tanga, Arusha yapaa?
 
Nenda Tanesco. Wewe nani hata uoneshwe utafiti?

Yaani viwanda vinavyochipua kwa kasi hii Tanzania unauliza utafiti? Umeme unavyosambazwa kwa kasi mpaka vijijini unauliza utafiti?

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
No wonder hata Niagara falls na Hydro Electric Power Generations za Dunia nzima zikija Tanzania gharama haitashuka....; Ishuke vipi wakati tunatafuta watu wa kugawana nao faida, ili wachache wajipatie faida ?

Hii nchi yanayotokea ni Stranger than Fiction.....
 
Wewe ndiye pumba , ni utafiti upi ulionyesha matumizi ya umeme Tanga, Arusha yapaa?
Una akili timamu wewe? Walioko Tanesco na wewe mpuuzi nani ana takwimu za mzigo na uhitaji wa Umeme Kanda ya kaskazini? Kwani hujui Kwamba Serikali ilizindua mradi wa densification yaani kuongeza ujazilozi kwenye njia za umeme Kwa sababu maeneo mengi Yanapata umeme mdogo Kwa sababu ya ufinyu wa njia za Sasa?

Kwa hiyo uchumi unarudi kinyume nyume au? Hivi nyie kima mna shida gani vichwani mwenu?
Screenshot_20230531-152146.jpg
Screenshot_20230531-152014.jpg
 
Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limetia saini ya makubaliano ya uendelezaji na ujenzi wa njia za umeme na Kampuni za Gridworks ya Uingereza na Larsen & Tourbo ya India.

Mkataba huo unahusisha utekelezaji wa miundombinu hiyo kutoka Chalinze kupitia Segera mpaka Tanga, na kutoka Chalinze, Segera, Same na Kisongo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Maharage Chande amesema hatua hiyo ni kufuatia kuongezeka kwa matumizi ya umeme katika mikoa ya Tanga na Arusha kwa sababu ya viwanda na shughuli za uchumi kuongezeka hivyo kusababisha njia za kupitisha umeme kuzidiwa.

"Kwa kipindi cha muda mrefu tumechelewa kutekelezeka miradi kama hii kwa kukosa fedha lakini kwa mara ya kwanza tunasaini makubaliano na sekta binafsi kuendeleza sekta hii," amesema Chande.
Chande ameongeza shirika la Larsen & Tourbo (L&T) litaendeleza na kujenga njia hizo kisha Tanesco litalipa kidogo kidogo kurejesha gharama za ujenzi zilizotumika.

"Wakijenga tutaharakisha maendeleo kwa wananchi wa Tanga na Arusha badala ya kusubiri mpaka kibubu chetu kijae huku maendeleo yanachelewa," amesema.

Aidha amesema pande zote mbili zitaketi kupanga gharama za mradi huo na kukubaliana na pia ipo nafasi ya Tanesco kuchukua na kuendesha mradi huo endapo fedha zikipatikana.

"Tunatarajia mradi huu kutumia miezi 30 mpaka kukamilika kwake, miezi 12 kwa ajili ya Utayarishaji na miezi 18 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi," amesema.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Gridworks, Simon Hodson, amesema uwekezaji katika usafirishaji wa nishati ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na upatikanaji wake barani Afrika.

"Miundombinu ya usafirishaji umeme inahitaji mtaji ili kuongeza uwezo wake na kusaidia upatikanaji wa kiwango cha kutosha katika maeneo husika ili kukuza uchumi," amesema Hodson.

Naye Makamu wa Rais wa L&T, Rahul Sikka, amesema mradi huo ni fursa kwao Kwani utachukua jukumu muhimu katika kuimarisha upatikanaji wa nishati na kutegemewa nchini Tanzania.

"Mradi huu utaimarisha mtandao wa usambazaji umeme unaounganisha maeneo muhimu ya nchi, kutengeneza njia ya kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya umeme, kuchochea ukuaji wa uchumi, kuunda fursa kwa biashara zaidi kustawi, na kuboresha hali ya jumla ya maisha kwa jamii za wenyeji," amesema Sikka.

Mnapigwa, msiseme si kuwaambia
 
Una akili timamu wewe? Walioko Tanesco na wewe mpuuzi nani ana takwimu za mzigo na uhitaji wa Umeme Kanda ya kaskazini? Kwani hujui Kwamba Serikali ilizindua mradi wa densification yaani kuongeza ujazilozi kwenye njia za umeme Kwa sababu maeneo mengi Yanapata umeme mdogo Kwa sababu ya ufinyu wa njia za Sasa?

Kwa hiyo uchumi unarudi kinyume nyume au? Hivi nyie kima mna shida gani vichwani mwenu?View attachment 2700629View attachment 2700630
Kwa makabrasha hujambo!!
 
Back
Top Bottom