Mkuu naona hunielewi, tunataka mtu anayesimamia hayo mambo kwa ukali na sio kwa jazba. Ukisimamia jambo kwa ukali utapata ufanisi, ila ukisimamia jambo kwa jazba utaambulia mafanikio duni. Hofu, kujipendekeza nk sio vigezo vya utendaji bora. Ukitaka kujua kwamba unafiki na woga umeingia nchini angalia sasa hivi imekuwa fashion, kila kiongozi akiongea lazima amtaje Magufuli mara nyingi kuliko hata ujumbe anaotaka ufike kwa umma. Umewahi kumsikia Makonda akihutubia? Umewahi kumuona Ndugai jinsi anavyojichekesha anapokuwa mbele ya rais?
Sasa hivi hata kama rais akija na wazo bovu kila mmoja anayemzunguka analiunga mkono ili aonekane yuko sawa na mawazo ya rais. Kila kiongozi anajifanya kuiga swaga za Magufuli hata kama hakukuhitajika lugha za kukaripia. Huo ni ujinga wa hali ya juu. Mfano mrahisi juzi kwenye uchaguzi wa ccm kumchagua mwenyekiti, Magufuli alichaguliwa wa 100%. Haijapita muda Nyalandu anatoka ccm anasema watu hawana uwezo wa kukosoa na demokrasia inaminywa, je alimpaje kura, ni kweli alipata kura kiasi hicho? Hiyo ni ishara anaongoza watu waliojaa hofu na hofu hiyo anataka ienee nchi nzima.