Amani iwe nayi wakuu,
Kweli mfa maji haachi kutapatapa.Tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani chini ya uongozi mahiri wa Dkt. John Pombe Magufuli, CHADEMA wamekuwa wa kutapatapa tu. Wamekuwa wafa maji, hawana tofauti na Kuku aliyekatwa shingo.
Jambo moja lililowapumaza ni imani kwamba kasi aliyoingia nayo Rais John Pombe Magufuli ilikuwa nguvu za soda. Baada ya kudhihirika pasipo na shaka kwamba dhamira ya Rais ni ya kweli wamebaki kudonoa donoa vijimambo, vimatukio, kutumia wahuni wahuni tu kuwasemea ilimradi tu waonekane wanapambana na Rais John Pombe Magufuli.
Hili ni jambo baya sana kwa mustakabali wa chama. Ni jambo baya kwa sababu chama hakipo kupambana na Rais bali kupamabana na matatizo ya wananachi. CHADEMA hilo wameliweka pembeni. Wananchi hawatasita kuwaadhibu.
Serikali ya awamu ya tano na Chama tawala CCM wamekwepa mishale yote hii ya CHADEMA na wananchi wamewaelewa.
1: Rais John Pombe Magufuli ameingia kwa nguvu za soda
2. Hujuma za kupandisha bei ya bidhaa kama unga, Sukari n.k
3. Kauli za CHADEMA kuwa Rais Magufuli anatekeleza sera za chama chao
4. Kauli ya Lowassa kuwa Wafanyabiashara wa Kariakoo waliokiunga mkono CHADEMA uchaguzi wa 2015 wanaonewa na Rais John Pombe Magufuli. (maana yake Lowassa angeingia madarakani asingehangaika na ukusanyaji kodi)
5. Kauli za CHADEMA kuwa Rais John Pombe Magufuli ni dikteta
6. Porojo kwamba mahusiano ya Tanzania na nchi za nje yatadorora kwa sababu Rais John Pombe Magufuli hasafiri nje ya nchi. Hakuna kipindi Tanzania inazungumzwa kwa mazuri nchi za nje kama awamu hii ya tano. Wameumbuka
7. Kauli kwamba Rais Magufuli ni rafiki wa Rais Kagame wa Uganda na Yoweri Mseveni wa Uganda kwa porojo kwamba ni madikteta. Wamesahau kwamba enzi la Jakaya Kikwete walipiga porojo hizo hizo kwamba Jakaya Kikwete na Kagame hawaelewani na kwamba uchumi wa Rwanda uko juu.
8. Jitihada zao za hivi karibuni za kutaka kuichonganisha Serikali ya Tanzania na ya Kenya, kuwachonganisha Rais John Pombe Magufuli na Uhuru Kenyatta.
Uchaguzi wabaya hawa wa Taifa letu pendwa wametumia nguvu nyingi sana kwenye matukio ya Uchaguzi wa Kenya, matukio ya kupigwa mnada Ngo'mbe na kuteketezwa kwa vifarangkwa mujibu wa sheria zetu baada ya kuingizwa kinyume cha sheria nchini mwetu kutaka kutuchonganisha majirani zetu.
Swali la kujiuliza ni je, mahusiano yetu kuwa.mabaya baina yetu na majirani zetu kunawasaidiaje CHADEMA kushika dola? Kunasaidiaje upatikanaji wa maji, madawa, umeme na huduma.zingine jamii? Au CHADEMA
wanadhani wakenya watawapigia kura?
Matuko ya Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa na Mbunge wa Arusha mjini kwenda Studio za KTN TV ya kenya kuanza kumshambulia Rais Magufuli na Serikali yao. Hili sijui tunaliitaje, ni kukosa uzalendo? Ni uasi? Ni ushamba?
9. Porojo za kwamba Serikali inanunua Ndege, inajenga reli badala ya kuwanunulia wananchi unga, sukari n.k
CHADEMA acheni kutapata, Serikali hii imeamua kuijenga Tanzania mpya, hamtaweza kuidhoofisha kamwe. Rais Uhuru Kenyatta ametoa ruhusa ya kufanyakazi na kuishi huko. Nendeni.