M-mbabe
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 13,203
- 23,020
Nimesoma makala moja ya Mzee Mwanakijiji (MMK) kwenye gazeti la Mwanahalisi la leo (uk wa 9).
Anaongelea juu ya recent arrest ya Mbowe na suala zima la "utawala wa sheria" hapa nchini......
Kupitia makala hii, MMK anaainisha jinsi serikali yetu hii inavyojichanganya katika matumizi ya hii kitu inayoitwa "utawala wa sheria". Anasema ni dhahiri serikali yetu huwa inachagua ni wakati gani itumike na wakati gani isitumike - double standard!
Hapa nitaweka highlights za baadhi tu ya yale aliyoyaandika (vikolezo vingi ni maneno yangu mwenyewe lakini maudhui ni ya MMK). Na kwa vile tayari iko kwenye public media sidhani kama ninahitaji idhini yake kuibandika hapa.
1/ Mbowe amekamatwa kwa kupuuzia amri ya mahakama. Serikali ime-act swiftly kupitia polisi kwa kuzingatia misingi ya "utawala wa sheria". Fair enough.
2/ Mfanyabiashara Valambia alifungua kesi ya madai dhidi ya serikali ya tshs bilioni 56, lakini pamoja na mahakama hii hii inayowadhalilisha akina Mbowe kutoa ruling more than 10 times all in favour of Valambia, bado hajalipwa hadi leo - miaka 14 hebu imagine! MMK anauliza "utawala wa sheria uko wapi hapa?".
3/ Balali (note: sijatumia marehemu kwa sababu zilizo wazi), kwa nafasi yake ya ugavana alikuwa summoned na mahakama kwa kugoma kumlipa Valambia. Balali hakwenda mahakamani... lakini cha ajabu wala hakukamatwa!!
MMK anaendelea kuuliza, na mimi naafiki, "utawala wa sheria uko wapi?"
4/ Baada ya kubainika kuwa kwenye ununuzi wa rada serikali ilikuwa ripped off by a staggering Tsh 21 billion, huku waliotafuna huo mshiko (directly or indirectly) wanajulikana, kila mtu alitegemea kuwa serikali inayojinadi kuzingatia "utawala ya sheria" ingechukua hatua za haraka za kuwafikisha wahusika hao kunakostahili....lakini wapi bwana.....hadi leo jamaa wanadunda mtaani kwa raha zao huku wakitukuzwa "waheshimiwa"!!
MMK ana-conclude hii point kwa kusema "...lakini katika suala la Mbowe wanasema 'hakuna aliye juu ya sheria'".
5/ MMK hajaisahau ile infamous Kagoda story na yale mahela ya EPA/BoT.
Anasema... "tulipoanza kupiga kelele wakati ule, kauli za viongozi zilikuwa 'tukiwakamata Kagoda nchi italipuka' na wengine wakadai eti 'Kagoda haikamatiki'".
Katika hili MMK anachagiza zaidi... "je, suala la kutokuwa juu ya sheria ni Chadema tu?".
6/ MMK pia ameongelea juu ya ripoti ya CAG inavyoonyesha jinsi "sheria mbalimbali zinavyovurugwa kwa maslahi ya watu binafsii". Ametoa mfano wa sheria ya manunuzi (PPRA) na sheria ya fedha haramu (money laundering).... anabainisha kuwa hakuna "kamata kamata" ya watendaji waliohusika kupoteza mabilioni ya umma!
Kwenye hili MMK anachagiza.... "haki haitakiwi kuwa na macho".
7/ MMK anatoa mlinganisho...."ingawa ukiangalia kwa jicho la kengeza utaona kuwa kukamatwa kwa Mbowe na wenzake kunaweza kuwa sawa, katika mizani ya haki makosa wanayodaiwa kuyafanya hayawezi kulinganishwa na makosa ya watu kama Benjamin Mkapa, Robert Mboma, Andrew Chenge, Rostam Aziz, Daud Balali na wengine".
Hii mimi nimeipenda zaidi..
Kwa uchache, hayo ndiyo aliyoyaandika Mwanakijiji (shukurani kwake) kwenye gazeti la Mwanahalisi hii leo 8 Juni 2011.