Makala ya Mwanakijiji: Serikali ya TZ na double standard kwenye "utawala wa sheria"

Umenena mkuu, point yako naizingatia

Hili ndilo suala la msingi. Ni kutokujibu hoja zao na hasa huyu FaizaFoxy sijui. Walikuwepo kina Kishogo hapa walikuwa wanasumbua kweli lakini tulipoamua kutokujibu hoja zao, walikimbia wenyewe au labda ndio huyu FF amerudi kwa jina lingine? Dawa ni kutochangia post zao!!!

Tiba
 
1) Fair Enough

2) Kuna uhusiano upi kesi ya madai na kesi ya kuvuruga amani? moja ni criminal case na moja ni civil case. Hapo amechemsha ana "compare" oranges na apples.

3) Sawa na namba mbili hapo juu.

4) Kesi tofauti kabisa na kama unaona wapo na sheria hazijachukuliwa unangoja nini kuwashitaki? Ulikatazwa?

5) EPA, looo! soma hapa: KESI YA EPA: Maranda, Farijala wafungwa miaka 5

6) Kesi za manunuzi maarufu hizi hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-kesi-dhidi-ya-balozi-mahalu-na-wenzake.html na hii hapa: Shahidi amlipua Dk. Msabaha kesi ya Bosi wa Richmond na pitia TAKUKURU ukaone zingine kibao,si zote zinazotangazwa.

7) Macho ya kengeza? hivi mtu mzima unatolea mfano kilema cha mtu kama vile ameomba? huu ni upunguwani wa hali ya juu, kuna nyuzi mwanakijiji alianza kumkebehi aliye na matatizo ya akili humu humu JF leo anatolea mfano kwa macho kengeza kama yule mwenye nayo kapenda hivyo au kajiumba mwenyewe? Hata Mwenyekiti wa chama kimoja cha siasa hapa nchini ni kengeza lakini ni lini akatolewa mfano kwa kilema chake? Au anataka kumdhalilisha?

Hao aliowataja wote ni pumba tu na chuki binafsi. Kutaja majina bila kuonesha makosa yao ndio nini?


Nasikia harufu ya chooni.........
 
Solution ni kutovunja sheria,ila ukivunja sheria kwa kutegemea mtu fulani mbona walimwacha utakuwa mvivu wa kufikiri.
 
Chief Mkwawa umenena na umesikika, tungekuwa na machifu kama wewe wawili watatu humu, mambo yangekuwa swaaafi. Jee, unajuwa kuwa babu yake Kikwete alikuwa Chief wa ukweli?

heeh! huyu FF yupo obsessed ama?? mbona hasomeki...sasa nimeelewa kwanini watu wame-doubt uwezo wake wa kufikiri.

JF ina sections nyingi jamani ,kuna jukwaa la mapenzi,nk ; hili umeingia la siasa na sio eneo la taarab wewe mama.
 
Solution ni kutovunja sheria,ila ukivunja sheria kwa kutegemea mtu fulani mbona walimwacha utakuwa mvivu wa kufikiri.

solution ni mahakama na polisi zijue kutafsiri sheria na kuzifuata,ili tusizungumzie swala la double standard. Mwenye akili timamu hawezi kuvunja sheria kusudi pasipo sababu ya msingi,ila tafsiri potofu/mabavu ya dola yakitumika basi atawekwa ndani.
 
Solution ni kutotafsiri vibaya sheria za nchi au kuzipndisha na kutegemea utaachiwa kwa kuwa labda...baba alimnunulia suti kiongozi fulani ili aende umoja wa mataifa.Mbona waliomchangia kirilo japhet hawana chochote leo hii?

What about my uncle Seth Benjamin?.....Did he die for these capitalists?
 
Solution ni kutovunja sheria,ila ukivunja sheria kwa kutegemea mtu fulani mbona walimwacha utakuwa mvivu wa kufikiri.

A typical texbook wish-wash, Kobello.

Ukiachilia mbali upuuzi wa wa kupindisha facts uliofanywa na mahakama ya Arusha uliopelekea kukamatwa kwa Mbowe, maneno yaliyokuwa yakitolewa na sympathisers mbalimbali (nimtaje Prof Lipumba??) kuhusu double standard kwenye mambo ya sheria ni wazi yalichangia sana kuwapiga pressure dogs (govt) na hata wakatumia mil 50 kumpeleka Mbowe mahakamani haraka, ambako aliishia kuachiwa bila hata ya kutamka neno!

See??

So, unaweza ukaondoa precedences za kiugandamizaji kwa kuwa-provoke wakandamizaji wajitazame kwenye kioo ambako wataona taswira zao zilizotapakaa kinyesi kuzidi hasidi wao ambaye kumbe amemwagikiwa na mkojo tu!!
Na hii ni lugha ambayo ni wapigania ukombozi tu ndiyo wataielewa....si opportunists wanaosubiri favours za akina JK!
 
Nadhani ningekuwa mwalimu wanafunzi wangepata kazi sana ya kuelewa; when people speak of "the rule of law" ina maana siyo katika kukamatwa au kukamata mtu na kumfikisha mahakamani bali inahusina na kusimamia sheria zisivunjwe kabla hazijavunjwa.

Kwa maneno mengine, utawala wa sheria unamtaka aliyeapa kwa kushika Katiba anashikilia kiapo chake, unamtaka Polisi kutimiza wajibu wake kwa kuangalia sheria; unamtaka Hakimu kufanya kazi yake kwa kuzingatia sheria na unawataka wananchi (bila kujali nafasi na hadhi zao katika jamii) kuzingatia sheria. Kilichotokea kwenye suala la Mbowe ambacho kimetukera wengine ni kuwa "utawala wa sheria" katika hili umeenda mipaka na kuna uwezekano kuna watu wamevunja sheria wakati wanajaribu kuzingatia sheria. Utawala wa sheria ni kutawala kwa sheria.

Sasa kama kuna mtu anasema "Kagoda hawakamatiki" au anasema "Tukiwakamata nchi italipuka" mtu huyo huyo hawezi kuja na kumkamata mwingine bila kujali kama kwa kufanya hivyo nchi inaweza kulipuka! Hivi kati ya kumkamata Mbowe na wale wa EPA au Meremeta ni lipi linaonesha uwezo wa kuilipua nchi?
 
Mkuu Mwanakijiji udumu past 90s ili uendelee kufundisha akina KENGE'NDE et al. Ni ajabu sana kushabikia hukumu ya akina Farjallah na nduguye waliokwapua "vijisenti" lakini Malegese aliyekwapua TZS 13.5billions hana kesi Kisutu. Kagoda, Meremeta, Tangold etc hawakamatiki. Chenge alifoji Insurance Cover wala DCI hajamkamata kwa forgery ambapo adhabu yake Shall be not less than 7years. Chenge ndiye mzee wa maadili CCM. Naomba Kenge'nde na watu wenye akili finyu kama yeye wakapimwe akili either Milembe kama wapo Bongo au hospitali za jirani huko Mamtoni/Ughaibuni
 
Samahani nemekosea jina. I meant, KERENGE'NDE et al.Chenge aligonga bajaji ikaua watu wawili wakati haina Insurance ndipo akaback date ili kuonyesha ilikuwa na bima wakati ajali inatokea maeneo ya Oysterbay. Mahakama iliridhia kuwa feki ambapo angekuwa Freeman Mbowe au Dr. Slaa wangekuwa wanaozea jela sasa hivi ninavyoandika post hii. Asalaam Aleikum Super Kereng'ende. Think twice before you talk or write in future
 
Utawala wa sheria unaangaliwa kwa 'limited definition' ingawa maana halisi ni pana sana. Tunadhani utawala wa sheria ni kumkamata mtu au kumfikisha mahakamani. Tunasahau kuwa taratibu zinazosimamia shughuli zetu kila siku ni sehemu ya utawala wa sheria kama tulivyokubaliana katika sheria, taratibu na katiba yetu.

Mtu mwenye ushawishi ndani ya jamii kama mh Mengi kudai mbele ya vyombo vya habari kuwa mwanae alibambikiwa madawa ya kulevya na watendaji wa serikali, ilibidi serikali ifuate utawala wa sheria kuthibitisha au kukanusha madai hayo ikifuatiwa na hatua stahiki.
Leo hatujui ukweli wa suala hilo na sijui mimi mwananchi wa kawaida nitaiamini vipi serikali yangu kama ina utwala wa sheria, si kwa suala la mengi bali nitakapojikuta katika mazingira kama hayo.

Mh Mwakyembe alitoa madai mazito ya kuuawa, na alitaja hata waliohusika. Mhe Spika Sitta wakati huo naye alitoa madai kama hayo.
Kwa kufuata utawala wa sheria madai ya wazito kama haya yasingeachwa tu bila majibu. Mwananchi wa kawaida ata aimini utawala wa sheria upi uliofumbia macho madai mazito kama haya.
Mh. Sumaye aliwahi kutuhumiwa kuhodhi mali za wanavijiji. Kwa utawala wa sheria aliyemteua (Mkapa) hakupaswa kumtolea maelezo, pengine tume huru ingetoa majibu mazuri zaidi, hadi leo wanavijiji wamebaki wakiamini ni dhuluma.

Vithlani aliyetuibia mabilioni ya fedha na inajulikana alipo na serikali haitaki kumfuata huyo utawala wa sheria haumgusi, lakini unamgusa Mbowe aliyeshindwa kutokea mahakamani.

Kwa upande mwingine, mauaji kama ya Gongola mboto na Mbagala, Arusha n.k kwanza walitakiwa wasimamizi wa maeneo hayo walitakiwa wakae pembeni, uchunguzi ufanyike na taarifa itolewe, hiyo ndiyo dhana ya utawala wa sheria, lakini je imefanyika?

Kwa kukosa kuonyesha utawala wa sheria kivitendo, ndio maana wananchi wamechoka na sasa wanajichukulia sheria mikononi.
Utawala wa sheria ni msumeno unaokata mbele na nyuma, wa kwetu unakata mbele tu!
 
kobello;2076330]Solution ni kutovunja sheria,ila ukivunja sheria kwa kutegemea mtu fulani mbona walimwacha utakuwa mvivu wa kufikiri
Nakubaliana na wewe kabisa, sasa solution ya yule anayevunja sheria na sheria hazichukuliwi dhidi yake solution yake ni nini?
Tunapokuwa na sheria moja kwa taifa halafu ikatumika au istumike sawa kwa wote solution yake ni nini!!!!
kobello;2076491]Solution ni kutotafsiri vibaya sheria za nchi au kuzipndisha na kutegemea utaachiwa kwa kuwa labda...baba alimnunulia suti kiongozi fulani ili aende umoja wa mataifa.Mbona waliomchangia kirilo japhet hawana chochote leo hii?
What about my uncle Seth Benjamin?.....Did he die for these capitalists nakubaliana nawe, swali ni kuwa kwanini sheria ionekane imepindishwa kwa mtu mmoja au wawili na si watu 10 au 15
Je wewe na mimi tunaweza kupinda sheria! maana hatuna mamlaka hayo sisi ni watumiaji wa sheria ima tunajua au la. Anayeweza kupinda sheria yaweza kuwa serikali, mahakama, au polisi.

Labda nimekuelewa vibaya tafadhali tufafanulie, kwa post zako mbili una imply au refer nini?
Hili ni jukwaa la majadiliano wala huna sababu ya kuwa na hofu ukiongea unajiuma uma.
 
Wakati wa kampeini, Kikwete alipitiliza muda wa mkutano lakini hakukamatwa
 
Nakubaliana na wewe kabisa, sasa solution ya yule anayevunja sheria na sheria hazichukuliwi dhidi yake solution yake ni nini?
Tunapokuwa na sheria moja kwa taifa halafu ikatumika au istumike sawa kwa wote solution yake ni nini!!!!
Je wewe na mimi tunaweza kupinda sheria! maana hatuna mamlaka hayo sisi ni watumiaji wa sheria ima tunajua au la. Anayeweza kupinda sheria yaweza kuwa serikali, mahakama, au polisi.

Labda nimekuelewa vibaya tafadhali tufafanulie, kwa post zako mbili una imply au refer nini?
Hili ni jukwaa la majadiliano wala huna sababu ya kuwa na hofu ukiongea unajiuma uma.
Namaanisha mbowe alivunja sheria na lissu ametafsiri vibaya sheria zinazomlinda mbunge...don't act like you don't know that....these peoiple are too....normal.
Oooh!....nilipos muda kidogo nikakujibu bila kuelewa vizuri swalli lako,
Solution ni kufuata sheria.....siyo kulalamika mpaka kiongozi wenu akikamatwa......mitaani kuna class ya watu inalindwa na polisi,na nyingine inawindwa na polisi,haya yote tunayajua na haikuwahi kuandikwa.
Mnafanya double standard kama ipo kwa viongozi tu,
Hii kitu imekuwepo mitaani kwa miaka mingi tu......
Tufuate sheria....wananchi na serikali!
 
heeh! huyu FF yupo obsessed ama?? mbona hasomeki...sasa nimeelewa kwanini watu wame-doubt uwezo wake wa kufikiri.

JF ina sections nyingi jamani ,kuna jukwaa la mapenzi,nk ; hili umeingia la siasa na sio eneo la taarab wewe mama.

Hujui nnachokiongea kwa kuwa umtoto kwangu kwa weledi, mengine nnayoongea yatakupiga chenga babuwee, kwa sababu tu, upeo wako ni hafifu sana. Unataka kushindana siasa na Mwalim wa siasa? Kamuulize Shivji, Faiza Foxy ni nani atakueleza.

Hicho nilichokiongea mimi kumjibu Chief Mkwawa, wewe bado darsa lako la siasa ni dogo hujafikia huko, kwa kukujuza tu, hiyo inaitwa Diplomatic Politics. Sasa i google uisome halafu utaelewa. Unanchekeshaaa.
 
Nasikia harufu ya chooni.........

Utaisikia sana, unapopewa hoja zikakushinda kujibu lazima ushikwe na tumbo pumzi. Unalijuwa tumbo la pumzi weye? Kama hulijuwi ndio hilo lililo kushika mpaka ukasikia harufu za choo na hujui zinakotokea kumbe kheee, umeyaachia mwenyewe! yatakushinda.
 
Back
Top Bottom