Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,845
Unaweza ukawa na akili lakini usiwe na maarifa.. Makinika... Kumbuka maandishi hayafutiki... Hata unapofuta ama kuhariri maudhui yako hapa JF.. Original version hubaki huko kwenye sever
Tendo la kwanza ndio huwa halisi.. Baada ya hapo uhariri wowote mbele ya sheria huitwa bandia... Yaani sio halisi... Hata ukipiga picha umeshika msokoto mmoja wa bangi na kuirusha mtandaoni... Lakini baadae ukahariri na kuweka sigara ili kuficha uhalisia.. Hilo ni kosa la jinai kisheria na unapaswa kushitakiwa kwa kuharibu ushahidi (tumia neno kuhariri)
Idd baada ya kufanya lile kosa alililoshtakiwa nalo.. Nadhani kuna watu walimshika MASIKIO yake makubwa kwamba afute haraka la sivyo anajiweka matatani... Kwa mwendokasi wa super sonic (sio ya COVID-19) aidha alifuta kabisa ama alihariri maudhui husika ili asalimike kuingia matatani.
Haikufua dafu... Awali ni awali tuu... hakuna awali mbovu... Awali ndio halisi.. Kafuta/kahariri lakini macho kuona yalikuwa yameshachota kila kitu... Alikolalia yeye wenzake ndio wameakia.
Hii kesi ya Idd hata kama ina mapungufu kisheria na kijamii lakini ina funzo kubwa la kutufunza sote hasa linapokuja swala la ushahidi na vidhibiti... Unaweza kuandika na kufuta... Lakini kumbuka umefuta ama umehariri kwenye kifaa CHAKO lakini sio kwenye sever... Siku wakikuhitaji watakupata tuu
Jr