Major General Abdala natepe afariki

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
947
69
Wapendwa wana JF habari za msiba huu zimetangazwa sasa na Mzee pius Msekwa. Mazishi yatakuwa kesho jioni unguja kwao.
RIP mzee wetu, Bwana amekupenda zaidi
 
nimesikia hivi punde kupitia TBC1 kuwa mzee Abdallah Said Natepe amefariki kwa diabetes katika hospitali ya Lugalo jijini Dsm.

namkumbuka mzee Natepe kama miongoni mwa wakongwe katika siasa za Tanzania ambaye nilimsoma katika somo la siasa nikiwa shule ya msingi.

huku tukiomboleza msiba wa mzee Natepe, huwa najiuliza CCM hii ambayo imetekwa na mafisadi mbele ya macho ya wazee kama Natepe ambao wakati wanapambana, mafisadi ambao wengi wao ni umri wa baba zetu walikuwa shule...itakuwaje pindi wazee wote hao watakapokuwa wamekwisha...maana walau hawa walikuwa wana japo kaujeri ka kuwaambia mafisadi, "hatukudai uhuru ili mfanye haya mnayofanya leo"....itakuwaje wakati huo.....

kwangu ni kiza kinene vinginevyo zimwi hili life mapema iwezekanavyo...AMINA na IWE
 
RIP mzee Natepe.

Katusalimie Mwalimu Nyerere mwambie tumeona cha moto kwa kufuata uzuri wa sura, ni afadhali tungekwenda kunywa nae chai tukamalizana, kuposa isingewezekana.
 
Huyu mzee inawezekana alisononeka na afya yake kuzorota alipoona kuwa Amani ameamua kuyasaliti mapinduzi kwa kuwakumbatia mahasimu wao CUF!! RIP mzee wa mapinduzi.
 
RIP mzee Natepe.

Katusalimie Mwalimu Nyerere mwambie tumeona cha moto kwa kufuata uzuri wa sura, ni afadhali tungekwenda kunywa nae chai tukamalizana, kuposa isingewezekana.
kwi kwi kwi........rais beautiful!!!.........wabongo watu wa ajabu sana wanachagua sura
 
[size=+0]kila roho itaonja uchungu wa mauti!!! Kumbe a.natepe bado alikuwa yuko hai mimi nilifikiria kuwa alikuwa ameshafariki miaka mingi!! Mungu amrehemu na amsamehe makosa yake ya kuwa mshiriki mkubwa wa mapinduzi ya umwagaji damu mkubwa uliofanyika visiwani mwaka 1964![/size]
[size=+0][/size]
[size=+0]wengine ambao bado wako hai na ni miongoni mwa wale washiriki wa mapinduzi na washauri watubie madhambi yao kabla mauti hayajawachukuwa! Miongoni mwao ni mzee aboud jumbe, mzee hassan nassor moyo na wenzao.[/size]
 
we will always remember you,a good neighbour at upanga,who always took the odd time out to lecture us on many aspects of the zanzibar revolution.
 
R.I.P. Mzee Natepe, tunakukumbuka pale ulipochukua hatua kujiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani mwaka 1983 kwa uzembe wa wasaidizi wako, viongozi wa leo hawakubali kuwajibika.
 
Wewe Kadogoo unafikiri ni wakati muafaka wa kumhukumu mtu wakati kama huu unazungumza utafikiri hujui kufa wewe! Mungu ndiye atakayemhukumu kila mmoja wetu. Nadhani ilikuwa ni busara zaidi kuwapa pole wafiwa na kuomba mungu awape faraja. Kumbuka naye ni binadamu kuna waliompenda kama baba yao,kaka yao,babu yao,mjomba wao etc. sasa tujaribu kuwa waungwana kidogo leo kwa mwenzio kesho kwako.. POLENI SANA WAFIWA MUNGU AZIDI KUWATIA NGUVU NI MAPENZI YA MUNGU.
 
mungu ampokee na amuweke pahala pema peponi


kwa kweli tunasikitika sana kwa kuondokewa na shujaa wetu, nguzo yetu na marejeo yetu ya umoja kwa wazanzibari na watanzania kwa umoja


mzee hakuwa na hiyana pale alipokuwa akihitajika kutoa busara zake ushauri wake kwenye serikali zote mbili na hata ndani ya chama


hata huo umoja na hali ya amani ambayo leo tunajisifia kule zanzibar mzee wetu hakuwa nyuma kuwachochea wahusika wafikie makubaliano yaliopo


simanzi na majonzi kwenye mioyo yetu zimetawala, ila hatupingi maamuru ya mungu, sisi tulikupenda na tunakupenda ila yeye anakupenda zaidi jina la mungu litukuzwe
 
RIP MZEE!
Umetumika kwa kiasi cha kutosha, na kazi yako kwa jamii haitasahaulika!
Amen.
 
Back
Top Bottom