Majina ya wauza Madawa ya Kulevya: Kikwete anayo!

Mlalahoi

JF-Expert Member
Aug 31, 2006
2,182
885
Vigogo dawa za kulevya watajwa

Written by Mwananchi
Monday, 18 September 2006

*Majina yao yapelekwa kwa Rais Kikwete
*Ni orodha ndefu ya majina ya watu 58
*Wamo wafanyabishara, wanasiasa, viongozi wa dini
*Mbinu wanazotumia nazo zaanikwa hadharani

WITO wa Rais Jakaya Kikwete wa kutaka wananchi wajitokeze kutaja majina ya wahalifu nchini, umepata mwitikio mpya, safari hii watu kadhaa wakijitokeza kutaja majina ya vigogo wanaoongoza kwa biashara ya dawa za kulevya nchini.

Majina hayo yako katika barua iliyoandikwa na wananchi 15 kwenda kwa Rais Kikwete, ambamo wanadai kwamba walikuwa wakitumiwa na vigogo hao kufanya biashara
hiyo, lakini sasa wameamua kuachana nayo. Barua hiyo iliandikwa Septemba 8, mwaka huu na wahusika wanadai wamekwisha kuiwasilisha Ikulu.

Kwa mujibu wa barua hiyo, majina 58 yameorodheshwa yakiwa katika makundi matatu makubwa, la kwanza likiwa ni waagizaji wakubwa wa dawa hizo; la pili ni
wafadhili ambao majina yao hutumika kusafirisha dawa hizo; na la tatu ni wauzaji walioko Dar es Salaam, Tanga, Mwanza, Mbeya na Zanzibar.

Katika orodha ya waandishi wa barua hiyo wanaodai kusukumwa na uzalendo na uchungu kwa nchi yao, yamo majina ya wafanyabiashara maarufu nchini na wanasiasa,
wakuu wa taasisi nyeti, baadhi ya viongozi wa dini na maafisa wa juu serikalini.

Kundi la kwanza lina majina 12, miongoni mwao ni wafanyabiashara maarufu katika miji ya Dar es Salaam, Morogoro, Zanzibar, Arusha na Bagamoyo na baadhi ya
viongozi wa dini wa madhehebu fulani.

Kundi hili linadaiwa kuwa linaingiza dawa za kulevya kwa njia mbalimbali zikiwamo, kutumia mipira ya kondomu, majokofu, vifaa vya hospitali, meli na
marobota ya mitumba.

Katika kundi la pili kuna watu 19, miongoni mwao wamo wanasiasa wakubwa nchini wakiongoza kundi hili, kutoka taasisi ya fedha nchini na wafanyabiashara maarufu wa
Dar es Salaam na Zanzibar.

Kundi la tatu lina majina 27, ambao si ya watu wenye majina makubwa, lakini ndio wanaotumika kusambaza mitaani kwa watumiaji wa dawa za kulevya.


Mbali ya kushiriki katika kusambaza dawa za kulevya, kundi hili pia lina baadhi ya majina ya watu waliotajwa kushiriki katika kuingiza silaha nzito
zinazotumika kwa ajili ya ujambazi kutoka nchi jirani.

Ufukwe wa Pwani ya Bahari ya Hindi eneo la Muhoro wilayani Rufiji inaelezwa kuwa linatumika kuingizia silaha hizo kutoka nchi jirani pamoja na dawa za
kulevya chini ya ufadhili wa mmoja wa wanasiasa nchini.

Uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere unatajwa kuwa unatumiwa na watu hawa kuingiza dawa hizo nchini kutokea nchi za nje, huku baadhi ya maafisa wa polisi
watatu wakitajwa kuwa ndio wanaotoa ulinzi kwa watu wanaopitisha dawa hizo.

Nyumba ya afisa wa juu mstaafu katika idara nyeti iliyopo jijini Dar es Salaam inatajwa kuwa inatumika katika kuhifadhi vijana wanaoingiza dawa za kulevya
nchini, huku nyumba ya mfanyabiashara mmoja iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam ikitajwa kuwa ndiyo inayotumika kama kituo cha kutolea pipi tumboni kwa vijana wanaotumika kuingiza dawa hizo kutoka nje ya nchi.

Vile vile, katika kundi hili mwanamke mmoja anayefanya kazi katika taasisi moja ya fedha anatajwa kuwa anashiriki katika kuhujumu uchumi wa nchi kwa
kusafirisha kwenda nje fedha nyingi za kigeni akitumiwa na mfanyabiashara mmoja maarufu wa dawa za kulevya nchini.

Mipaka ya Tunduma mkoani Mbeya, Horohoro mkoani Kilimanjaro na Namanga mkoani Arusha, nayo imetajwa kuwa inatumika kupitisha dawa za kulevya kwa kutumia
mabasi na magari mengine. Kuna kampuni mbili za mabasi nchini zinazotajwa kuongoza kutumika katika usafirishaji.

Barua hiyo ya kurasa 10, pia inamtaja mwanamke mmoja ambaye anatumika kupitisha dawa za kulevya uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere kuwa ni sugu; aliwahi
kuhukumiwa kifungo cha miaka 35 jela kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya, lakini hivi sasa yupo mitaani kifungo chake akitumikia mtu mwingine.

Alipoulizwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Utawala Bora), Philip Marmo, alisema hajapata barua hiyo na kwamba atalizungumzia
baada ya kuipata.

Naye Waziri wa Usalama wa Raia, Bakari Mwapachu, alisema hana taarifa za kuwako kwa barua hiyo. Hata hivyo, alisema kuna tume ya dawa za kulevya iliyopo
chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ndiyo inayoshughulikia zaidi suala hilo.

Alisema Jeshi la Polisi linafanya kazi za kukamata watu wanaojihusisha na dawa hizo na kwamba mikakati mingine ya kupambana na watumiaji inafanywa na tume
hiyo.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Rais Kikwete aliagiza Jeshi la Polisi liongezewe uwezo wa kupambana na uhalifu, ikiwa ni pamoja na kuwahamisha vituo vya kazi askari
waliokaa kituo kimoja kwa muda mrefu.

Pia alilitaka Jeshi hilo lijisafishwe lenyewe kutokana na madai kwamba polisi wanahusika na baadhi ya matukio ya uhalifu nchini.


Rais alitoa wito kwa wananchi wenye taarifa zozote za uhalifu, na wanaojua waliko majambazi wazipeleke taarifa hizo kwake kama wanaogopa kuzipeleka polisi.


Katika kuitikia wito huo, wananchi kadhaa waliandika barua iliyooroshesha majina ya polisi 20, wakiwamo baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa na kuikabidhi kwa Waziri wa Usalama wa Rais, Bakari Mwapachu.

Tangu wakati huo, mabadiliko makubwa yameshuhudiwa yakifanywa kwenye jeshi hilo, hata hivyo hii ni mara ya kwanza kwa watu kujitolea kuandika barua yenye
majina na maelezo ya kina kama hii kuhusu biashara ya kulevya na kuipeleka kwa Rais.
 
Halafu Kulikoni na This Day yakitaja majina ya watuhumiwa watu wanaanza kusema magazeti ya Mengi yanatetea maslahi yake.Hiyo ni "scoop" ya Mwananchi lakini haitoi clues za kutosha kuhusu watuhumiwa.

Halafu kuna mtu alikuwa anasema magazeti yetu hususan non-CCM/Government owned (including Mwananchi) haya-address important social issues.Sijui hii nayo sio important?

Leaving that aside,tarehe kama hii mwezi Desemba bado tutakuwa hatujajua wahusika wamechukuliwa hatua gani,sio kwa vile waandishi wameficha majina yao bali waliopatiwa listi wameikalia.Hatuwezi kuwalaumu kwa vile kiongozi mkuu wa nchi naye ana orodha ya wala rushwa lakini ameikalia ilhali anadai yuko serious na mapambano dhidi ya rushwa.Mbona mambo!?
 
Mzee Es
Hili ndilo tatizo la watanzania, ni wazuri kusema au kuteta lakini kwa matendo ni zero kabisa.

Kumbuka RA ni mwanahisa wa Mwananchi Communication kwa hiyo itakuwa ni ndoto kutaja majina ya wahusika hasa kama kuna majina ya baadhi ya wanamtandao.
Mimi nataka kuona JK akitoa hizo list za majina anayopelekewa na aliyokiri kuwa anafahamu mwenyewe. hata kama hana uhakika na kama kweli wanahusika basi itakuwa ni wakati mwafaka kwa wahusika kujitokeza kukataa au kukubali shutuma.

tuna safari ndefu.
 
Majina ya vigogo ninayo-JK

03 Oct 2006
By Mwandishi Wetu


Rais Jakaya Kikwete, amekiri kupokea majina ya vigogo wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kwamba majina hayo yanafanyiwa kazi na watendaji wake.

Rais Kikwete aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na taifa kupitia kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam.

Alikuwa akijibu swali kutoka mmoja wa wahariri aliyetaka kujua iwapo amepokea waraka wenye majina ya vigogo wanaodaiwa kujihusisha na dawa za kulevya.

Bila kufafanua, Rais Kikwete alijibu, “waraka nimeupata na nimewapa wahusika na wanaufanyia kazi.” Inadaiwa kwamba, katika waraka huo ulioandikwa na kikundi kimoja cha wananchi, kimetaja majina ya vigogo zaidi ya 100 wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya ama kuingiza nchini dawa za kulevya au kuwa mawakala wa dawa hizo au wauzaji.

Kwa mujibu wa waraka huo, baadhi ya wafanyabiashara waliotajwa ni wa kutoka mikoa ya Tanga, Mbeya, Dodoma, Kigoma, Arusha, Iringa, Manyara, Kilimanjaro, Dar es Salaam na Zanzibar wamedaiwa kuhusika na biashara hiyo.

Aidha, katika waraka huo, umetaja baadhi ya hoteli Jijini Dar es Salaam, kutumiwa kama vituo maalum vya kukutanisha wafanyabiashara wa dawa hizo, kwa ukanda wa Nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Kazi ya kuandaa taarifa hiyo yenye kurasa 12, ilifanywa na Shirika moja linalopigania haki na Usawa na Mazingira katika Jamii la Jijini Dar es Salaam.

Imeelezwa kwamba, taarifa hiyo ya siri, ilikabidhiwa kwa Rais Kikwete kupitia kwa Waziri wa Usalama wa Raia, Bw. Bakari Mwapachu.

Katika taarifa hiyo, yamo baadhi ya majina ya wabunge, wafanyabiashara maarufu, maofisa wa idara nyeti za serikali kama vile Mamlaka ya Mapato Nchini, Benki Kuu (BoT) na maofisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi, pamoja na watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini.

Viwanja vilivyotajwa kwenye waraka huo ni Dar es Salaam, Kilimanjaro (KIA), Zanzibar (Karume Aiport), Tanga, Arusha na Mbeya.

Mbali na viwanja vya ndege, waraka huo umetaja wafanyabiashara hao kuzitumia Bandari za Dar es Salaam, Tanga, Zanzibar na fukwe za Bagamoyo kuingiza shehena kubwa za dawa hizo.

Taarifa hiyo pia imetaja majina na namba za magari ya watu yanayotumika kusafirisha dawa hizo na kusambaza kwa walengwa jijini Dar es Salaam.

Pia majina ya kampuni za ndege zinazotumiwa na watuhumiwa hao kuingiza dawa, huku wengine wakitumia mikataba ya usafirishaji wa vifaa vya hospitali pamoja na matairi ya magari.

* SOURCE: Nipashe
 
Kama JK kapewa majina na bado hajachukua hatua za haraka hata kuacha waitwe na kuhojiwa hadi sasa ina maana anawapa muda waondoke na watakao kamatwa utakuwa ni ujinga wake . Kama ndiyo hilo basi naamini kweli JK he is not serious na naamini wengi wao ama ni wafadhili wa CCM ama washikaji watakuwemo.Sasa ni bora JK ukaacha habari za vita dhidi ya madawa ya kulevya .Maoni yangu haya

2006-10-14 09:34:59
Na Waandishi wetu



Baadhi ya vigogo wanaodaiwa kuwa ni ’mafia’ wa biashara ya dawa za kulevya nchini ambao majina yao yalikabidhiwa kwa Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni, wamedaiwa kuanza kuikimbia nchi na kwenda nchi jirani na Asia kwa hofu ya kushughulikiwa na Serikali ya Awamu ya Nne, imefahamika.

Hadi sasa, inaaminika kuwa, takriban vinara 17 kati ya 74 ambao majina yao yaliwasilishwa kwa Rais Kikwete, tayari ’wamelala mbele’ kwa nyakati tofauti na kwenda nchi jirani za Kenya na Uganda na baadhi yao India.

Habari ambazo Nipashe imezipata, zimeeleza kuwa, kundi hilo linalowahusisha wafanyabiashara maarufu nchini, wengi wao wakiwa ni wakazi wa jijini Dar es Salaam, Arusha, Mbeya na Dodoma, wameamua kuikimbia nchi kutokana na kuingiwa woga baada ya majina yao kuanikwa mbele ya Rais Kikwete.

Chanzo chetu cha habari kimedokeza kuwa, kinara wa genge hilo, anayemiliki makampuni kadhaa jijini Dar es Salaam, aliondoka nchini wiki mbili zilizopita kwenda nchini India.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, mara baada ya Rais Kikwete kukiri kupokea majina ya vinara wa biashara hiyo ya ’unga’ mbele ya Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya habari, waliingiwa na kiwewe.

Imedaiwa kwamba, Oktoba 8, mwaka huu, kundi hilo lilikutana katika hoteli mbili maarufu jijini Dar es Salaam, ambazo ni za washirika wao, ajenda kuu ikiwa ni kupanga mikakati ya jinsi ya kudhoofisha juhudi za Rais Kikwete za kukabiliana na biashara hiyo haramu.

Awali, ilidaiwa kuwa, vinara hao walitaka kufanyia kikao hicho cha siri katika hoteli moja ambayo pia ni ya mshirika wao, lakini aliamua kuwatolea nje dakika za mwisho.

”Mpaka sasa, wanazidi kujipanga na kutafakari namna na kumwingia Rais na njia wanayokusudia kuitumia, ni kumweleza wanataka kutoa misaada mingi kwa jamii inayohitaji,” kilisema chanzo hicho.

Aidha, imedaiwa kuwa, taarifa za kukabidhiwa Rais Kikwete orodha ya vinara wa biashara ya unga, pia imesaidia meli moja iliyokuwa na shehena ya dawa hizo, kushindwa kupakua ’mzigo’ huo katika bandari ya Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa habari hizo, baada ya meli hiyo kushindwa kuteremsha dawa hizo, sasa imebadilisha mwelekeo kwenda Kusini mwa Afrika.

Imeelezwa kuwa, taarifa za kuanikwa kwa majina hayo na meli hiyo kushindwa kutia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam, kumechangia kuwepo kwa uhaba mkubwa wa dawa za kulevya nchini hususan jijini Dar es Salaam.

”Hivi sasa watumiaji wa dawa hizo, wanahaha kuzitafuta?imekuwa kama bidhaa adimu, wale waliokubuhu wanalazimika ’kubwia’ majivu yaliyochanganywa na poda ili mradi watimize dhamira yao,” alisema na kutahadharisha kuwa, hiyo ni hatari kwani wanaweza kupata saratani ya ini.

Mtoa habari huyo alisema kama serikali haitayafanyia kazi haraka majina ya watuhumiwa hao, huenda Rais Kikwete akajikuta anabaki na majina yao tu baada ya watuhumiwa wote kuikimbia nchi.

Mwezi uliopita, ilidaiwa kuwa, Rais Kikwete alikabidhiwa taarifa ya siri yenye kurasa tisa.

Taarifa hiyo alikabidhiwa kupitia kwa Waziri wa Usalama wa Raia, Bw. Bakari Mwapachu.

Alipozungumza na wananchi kupitia kwa Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari, Rais Kikwete alikiri kupokea taarifa hiyo na kwamba inafanyiwa kazi na vyombo husika.


SOURCE: Nipashe
 
Hii issue imejitokeza tena,na inasemekana wengi wa hawa jamaa wamekimbia nchi,majina ya wengine ni quite shocking! Mpaka mtu it gets u thinking kama utajiri wenyewe ndio huo,ambao watu tumekuwa tuki-admire! Bear with me for the shocking revelations...
 
Sasa hata kama Rais akiwa na majina hayo..so what? kwa sababu nadhani hiyo ni kazi ya Polisi au Anti-Drug Agency sasa Rais akianza kuingilia mambo haya nadhani kutakuwa na conflict kuko mbeleni
 
Majina ambayo yanatajwa ni pamoja na:

  • Dewji (Mo'hd Enterprise) mbunge huyu,
  • Yusuf Manji,
  • Mrema (mmliki wa Ngurdoto lodge na Impalla Hotel Arusha),
  • kuna madiwani kama watano wa Dar, mmoja wao akiwa ni Meya wa Ilala na msaidizi wake (majina yamenitoka),
  • mume wake Amina Chifupa (Mpakanjia)... Na hili balaa alilianzisha huyo huyo Amina Chifupa,sasa sijui hakujua kuwa mume wake yumo au vipi, maana yeye ndiye aliyehoji bungeni kuwa hawa watu wanafaamika sasa kwa nini wasikamatwe?
Raisi akalivalia njuga.Wengi wao wamekimbia nchi,na inasemekana hawa walikuwa wanashirikiana sana na polisi,kitengo cha madawa ya kulevya.

Hao Manji na Dewji, inasemekana kuna mzigo wao uliibiwa Tanga juzijuzi hapa na wajanja,na ukauzwa. Kinachosemekana ni kuwa hawa watu wanafanya hii biashara kiujanja sana kiasi cha kwamba kuwashika sio rahisi kabisa kwa kuwa they can justify their means thru the legal businesses, lakini wengi walitajwa na wafanya biashara wa madawa ya kulevya wadogo,ambao wengi wao hutumwa na hawa jamaa..
 
Manji naye kakimbia Nchi ? Je Dewji Mbunge ? haya majina ni kweli kwamba hakuna mkono wa mtandao maana mpaka rais anawapa nafasi ya kujisafisha badala ya kuachia Polisi wafanye kazi zao basi TZ imeisha. Huu ndiyo ukombozi toka kwa Nabii JK tuliokuwa tuna ngojea ?
 
Manji hajakimbia nchi....huyu ni Mohammed Dewji(mbunge) sio yule Dewji wa Simba.Haya majina ni kweli....na wenyewe wanajua kuwa wamo kwenye list
 
Kama hii ndiyo hali halisi sasa JK ana uoga wa nini kuwaacha wachukuliwe hatua ?Kwa nini alijigamba kwamba atawashukia kwa kasi kubwa kama alijua hawezi kuwashukia kwa sababu moja ama nyingine ? Tutakuelewa vipi ndugu rais kwa ukimya wako na kutoa mwanya hawa jamaa wakimbie ?
 
kulaleki!

Yaani mimi wakati wote najiuliza how comes some people in Tz become extremely rich na wanafanya biashara za kawaida kama wengine ambao they don't get that much rich. JK kutoa muda kwa kujisafisha nahisi inatokana na fact kuwa hawa jamaa ndio mafinanciers wa rulling class, if you know what I mean!
 
Kesi zao zisikilizwe hadharani, si faragha
Na Bakari Mnkondo, Dodoma

BAADHI ya wabunge wamepinga mabadiliko ya sheria yatakayotoa nafasi kwa watuhumiwa wa dawa za kulevya, kesi zao kusikilizwa faragha na kuwa kufanya hivyo ni sawa na kuwalinda wahusika.

Mbali na hatua hiyo, wengi walipendekeza kesi za ubakaji na udhalilishaji ndizo zisikilizwe faragha, isipokuwa kesi zinazohusu watu wa jinsia moja ambao watakamatwa wakijamiianaziwe hadharani.

Wabunge waliyasema hayo jana bungeni mjini hapa walipokuwa wakichangia muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali uliowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika.

Akichangia, Dk. Wilbroad Slaa (Karatu-CHADEMA) alisema dawa za kulevya ni tishio hapa nchini na kuwa kesi zinazowahusu wahusika wa dawa hizo zinapaswa kusikilizwa hadharani.

“Kesi za dawa za kulevya si vyema zikasikilizwa faragha. Jamii ya Watanzania haitatuelewa iwapo tunatengeneza mazingira ya kuwalinda na kuwasitiri hivyo wananchi watakata tamaa,” alisema Dk. Slaa, na kuwa sheria yoyote isipowatia hofu wahusika, inawachochea kutenda maovu.

Alisema suala la kupambana na wafanyabiashara wa dawa za kulevya inabidi lifanywe kwa umakini na kwa kasi kwa kuwa wahusika ni watu wengi, wengine wakiwa ni maarufu.

Dk Slaa alitoa mfano kuwa gari lake liliwahi kukamatwa mwaka 1992 likiwa limebeba tani tano za dawa za kulevya na liliachiwa mwaka 1998 na kuwa katika kipindi hicho kontena lililokuwa na dawa hizo lilifumuliwa juu na kilichokuwepo ndani kutoweka, hivyo: “Watanzania wanahitaji kujua wabaya wa taifa.”

Aliongeza kuwa kuwaficha wafanyabiashara wa dawa za kulevya kutawavunja moyo wananchi ambao wamekuwa wakijitokeza kuwataja, na kwamba hivi karibuni walimpa orodha ya wahusika Rais Jakaya Kikwete, ambaye ameahidi kupambana nao.

Kwa upande wake, Fatuma Maghimbi alisema kukataa kesi za wahusika wa dawa za kulevya kusikilizwa hadharani kunadhihirisha biashara hiyo inahusisha ‘vigogo’.

Fatuma alisema mapendekezo ya mabadiliko ya sheria hayatoi nafasi hata kwa vyombo vya habari kuandika na kutangaza kesi za wafanyabiashara wa dawa za kulevya, hivyo jamii itakuwa haina taarifa zozote.

Mbunge huyo, ambaye pia ni waziri kivuli wa Wizara ya Sheria na Katiba, alisema hakuna haja ya kuwaficha wafanyabiashara hao, labda mashahidi na waendesha mashitaka.

Dk. Lucy Nkya (Viti Maalum – CCM) alisema mtandao wa wauzaji wa dawa hizo ni mkubwa hivyo wakiwekwa hadharani, waliobaki wanaweza kutafuta jinsi ya kujihami au kujificha.

Alipendekeza wahusika kesi zao zisikilizwe faragha ili wengine wasijue, wakati jitihada za kuwasaka zikiendelea na kuonya kuwa dawa hizo zina madhara makubwa kwa jamii, lakini wahusika wakubwa bado hawajakamatwa.

Lucy alisema wahusika wengi wa dawa hizo bado wanalindwa kwa kuwa mara nyingi ushahidi dhidi yao uharibiwa kwenye mchakato wa kupelekwa kupimwa kwa mkemia mkuu.

Katika hatua nyingine, Abubakar Khamis Bakari (CUF) alipendekeza kesi za watoto kubakwa na wanawake kudhalilishwa kijinsia ndizo zisikilizwe faragha, lakini za watu wazima wa jinsia moja wanapokamatwa baada ya kuwa wamekubaliana, kesi zao zisikilizwe hadharani kwa kuwa wanakuwa wamevua utu wao na kuwa kama wanyama.

Alisema kufanya hivyo kutawatia woga wengine na itakuwa ni sehemu ya adhabu wakati kesi hiyo ikisikilizwa ili kukomesha vitendo hivyo.

Mwanasheria Mkuu Mwanyika aliwasilisha muswada wa mabadiliko ya sheria mbalimbali, ikiwemo ya kudhibiti biashara haramu ya fedha ambalo ni tatizo kubwa la dunia ya leo na sheria itakayotoa nafasi kwa waziri mhusika kuandaa kanuni za kushughulikia mienendo ya vyama vya siasa nchini.
 
Back
Top Bottom