Mashetani aka Majini aka Mapepo yapo yameumbwa na Mungu kama tulivyoumbwa sisi Binaadamu.
Mungu kaumba MALAIKA, MAJINI na BINAADAMU ili wamuabudu tu, na sio chengine, na viumbe wasiomuabudu Mungu amewaekea adhabu kali
Marehemu Bibi yangu alikuwa hajui kusoma wala kuandika,lakini pale Shetani aka pepo anapokuwa amepanda kichwani kwake alikuwa anaweza kuongea kiarabu fasaha kabisa..
Marehemu Baba alikuwa ana uwezo wa kumwita jini wa Bibi, alipokuwa anamwita familia nzima inatakiwa wepo, Alikuwa ni jini wa famili, chakula chake kulikuwa, Asali, muwa, manda
Yule juni alikuwa anatusalimia kwa kutuzungusha shingo, kutunyoosha mkono huku Akisema "zein, zein", baba alikuwa anamwita jini wa Bibi pale anapokuwa anataka msaada wa kitu fulani..
Jini wa Bibi alikuwa na Uwezo mkubwa Sana, jina lake lilikuwa sio la kiarabu bali ni la kiswahili wa pwani, siku moja nilimsikia akisema wapi anatoka na yeye ni nani
Nilimsikia akisema yeye ni Mkuu wa Majini katoka sehemu fulani Pemba, vile vile alikuwa anawakilisha sehemu kubwa ya ufukwe wa Afrika Mashariki yaani, Mambasa, Unguja, Pemba, Kilwa..
Sitaki kutaja jina la huyu jini, kwakweli alikuwa na Uwezo wa ajabu Sana, uwezo wakuona na kutabiri, mambo mengi sana Alikuwa na Uwezo wa kuwaadhibu Majini wengine nk..
Haya mambo yapo, nimeyashuhudia mwenyewe, hivi viumbe vimeumbwa na Mungu,..
Yale tunayoyaona Makanisani ni "usanii", "utapeli",..huwezi kumtoa jini kwa kumpiga kelele, Majini wana vyakula vyao, wana njia zao za kuwaita na wana njia zao za kuwatoa,nimeyaona haya nikiwa na umri mdogo mpaka umri wa kumaliza Chuo
Tunatakiwa tujue kuwa hivi viumbe, ni kama sisi Binaadamu, wako wabaya na Wazuri, wako wanaomcha Mungu na wanaomuasi Mungu, lakini Wengi wao ni wa ha Mungu, wanaishi maisha marefu kuliko binaadamu