Majina ya ‘majiin’

Majina ya ‘majiin’

Kwa mfano tukisema kwamba hao majini ni waislamu na ndiyo maana wana hayo majina ya kiarabu,Je kabla ya uislamu kabla ya uislamu walikuwa wana imani gani na kutumia majina ya wapi? Maana hao viumbe wapo kitambo sana tu.
 
Kuna dada mmoja alipandisha maruhani basi hilo jini likatambulisha linaitwa Jackson wa Pili limetumwa kumnyonya damu kiti wake
 
Kiu halisia, umewahi kujiuliza pia kwanini majini yawapate wadada pekee? Kuitafakari utagundua ni tatizo la kisaikolojia tu kwa wanawake, si vitu halisi. Fikiria kila anayesema kamuona jini, atakwambia amevaa kanzu nyeupe na ana miguu mirefu sana. Swali, ina maana kila jini vazi lake ni kanzu nyeupe? Nje ya hapo nani kawahi kumuona jini kwa maana ya Kiumbe nje ya binadamu? Ukifatilia hata aya zinazotaja majini kwenye vitabu vya dini utagundua majini si kiumbe nje ya ubinadamu. Yaani si kiumbe chenye sifa nje ya sifa za ubinadamu na ndio maana hakuna rais, waziri mkuu, mbunge au kiongozi yeyote yule wa majini. Maana yake ni kwamba, majini ni sifa nyingine ya binadamu wenye 'hadhi' fulani ya juu miongoni mwa wanadamu ndio maana ikasemwa, 'Sikuwaumba majini na watu ili wapate kuniabudu', maana yake 'Sikuwaumba watu wa hadhi ya juu na hadhi ya kawaida (Matajiri na Masikini, wazuri au wabaya n.k) ili waniabudu'. Ukiutazama ulimwengu unaweza kuona tofauti iliyopo nikisema hivyo. Tazama, mawe, upepo, miti, na viumbe vidogovidogo kama sisimizi, chawa, utitiri n.k vyote vipo katika ibada (abudu). Bakteria mbalimbali ni majini pia. Bakteria wapo wazuri wenye faida na pia wapo wabaya na wenye kuleta madhara mbalimbali mwilini na nje ya mwili wa mwanadamu na viumbe. Imani juu ya uwepo wa majini inashikwa sana na sisi Waislamu wa maeneo ya pwani ambako wengi hatuna maarifa hasa ya dini na kuelewa maana ya maneno yaliyomo ndani ya vitabu vya dini. Waweza kujiuliza pia kwanini majini hayajatajwa kwenye vitabu vingine vya dini kama Zaburi, Injili, na vingine kwa jina hilo hilo la jini? Ingawa wengine wanafananisha na pepo lakini kiuhalisia jini ni sifa nyingine mbali na pepo. Havihusiani katu.

Pamoja na kuwepo kwa usanii mwingi siku hiz kwenye makanisa mbali mbali lakini ninaamini kuwa yapo majiin/ mapepo na wengine wakiita mashetani

Ninaamini hivyo kwasababu nikiwa mdogo, kulikuwa na 'dada' zangu waliokuwa wanasumbuliwa na hayo 'mapepo' na hivyo nilijiridhisha kuwa hakukuwa na 'usanii' pale.

Nimeeleza hayo kwasababu nina swali limenitatiza kwamba wakati wa maombezi kwa hao 'dada' zangu kuna wakati muombaji alikuwa anaongea na hayo 'mapepo' na kuuliza majina yao. (Kwa wenye imani ya kikristo wananielewa hapa) mara zoote ckuwahi kuckia wakijitambulisha kwa majina ya 'kikristo' kama vile Thomas, peter, jeska , mary n.k badala yake nilisikia majina ya 'kiislam' kama juma, Asha, Sharif, n.k. wakati waliokuwa wakiombewa ni wakristo.

Kwahiyo swali langu kwako JF MEMBER je wewe uliwahi kuskia majina yenye nasaba na 'ukristo' kutoka kwa ''mapepo?"

Pia kwa wale wasio amini ikiwa mungu yupo wanazungumza nini kuhusu haya "mapepo"
 
dini ya uislamu ukisoma sana kuna steji unaweza kuijua dunia sana kuliko wakristo .
wakristo wazungu wametuficha vingi ili tusielewe kama wao ndo maana kuna siri nyingi.
majini yapo ya kila aina na elimu yake ni kubwa sana walio bahatika kupata.
 
mwenye kujua jinsi ya kuyapata yale mapepo mazuri mazuri anipe contacts. Tafsida imezingatiwa 😛
 
Hauko sawa umepotea kabisa kuhusi majini na Jambo kama huna elimu nalo usilitungie unachokijua....Majin ni viumbe viliishi muda mrefu hapa duniani kabla ya wanadamu wakafanya uasi na wakamwaga Damu walipigana vita sana na kuuwana Mungu akawaaangamiza wengi na wengine wakatupwa Nje ya rehma zake ila mmoja wa majin aliyekuwa mchamungu sana ndio alichukuliwa na kupelekwa Pepon na kupewa mamlaks ya kuwa mkuu mbingu ya kwanza naye ni Iblis.Quran inasema Iblis ni Jinn sio malaika. Malaika wameumbwa hawana Option ya kumuasi Mungu option hiyo tunayo sisi Wanadamu na Majinn sio malaika na wanyama ndio maana Iblis aliweza kuasi sababu ni Jinn na ameubwa kwa moto kama majin wengine malaika wameumbwa kwa Nuru ya Mungu.

Baada ya anguko hilo kikapita kipindi ndio akaumbwa Mtu . na hata malaika walipo ambiwa na Mungu kuwa nataka niumbe kiongoz wa dunia wakamwambia sisi tunakutukuza kwanini uumbe kiumbe kingine kitakachoenda kufanya uharibifu na kumwaga damu, Mungu akawajibu hakika mimi nayajua msiyo yajua.

Hivyo basi majin yanazaliana yapo kwa jamii na koo na iman tofauti na tamadun kama tulivyo sisi wanadamu ili kimewekwa kizuiz kati yao na sisi wao wanatuona lakin sisi hatuwaoni na hawana mamlaka juu yetu ila ukiwa na elimu na ulimwengu wao ndio utawaendesha wewe na elimu hiyo ipo miaka mingi nyuma tangu kina seleman huko waliwatumia na kabla ya huko...so kwenye majin wapo wauslam,wakristo,wachawi,wasio amin Mungu,washenz,wezi au wazizi na wapole na waganga wapo ni kama sisi tu.

kimaumbile hawawez kuhusiana na sisi ila wakutumiwa au wakawavamia watu kutoka na hitilafu za mtu yule kuna mtu kauliza kwaninj wanawake wengu ndio wana mapepo,wanawake wapo wazi sana kimaumbile na la pili ni wachafu sababu wanafuga minywele ile wiki nzima haoshi kichwa na kichwa cha mwanadamu kupaka maji kwenye utosi ni kinga kubwa sana dhid ya viumbe vingi ndio maana Waislam tunaosha kichwa mara tano kwa kwa siku,lakin pia mwanamke anapojifungua ndani ya siku 40/anakuwa sio msafi hivyo rahisi kuvamiwa au wakati wa kubleed hivyo anatakiwa ajitunze na udhu dhikiri na pia zipo aya za kuwafukuza au kujikinga nao...ila ukweli majin ni viumbe na wapo na watahukumiwa kama wanadamu...Jinn ni kiumbe tofauti na binadamu..kasome Quran surat Jinn utapata habari zao au Surat Rahman
 
Pamoja na kuwepo kwa usanii mwingi siku hiz kwenye makanisa mbali mbali lakini ninaamini kuwa yapo majiin/ mapepo na wengine wakiita mashetani

Ninaamini hivyo kwasababu nikiwa mdogo, kulikuwa na 'dada' zangu waliokuwa wanasumbuliwa na hayo 'mapepo' na hivyo nilijiridhisha kuwa hakukuwa na 'usanii' pale.

Nimeeleza hayo kwasababu nina swali limenitatiza kwamba wakati wa maombezi kwa hao 'dada' zangu kuna wakati muombaji alikuwa anaongea na hayo 'mapepo' na kuuliza majina yao. (Kwa wenye imani ya kikristo wananielewa hapa) mara zoote ckuwahi kuckia wakijitambulisha kwa majina ya 'kikristo' kama vile Thomas, peter, jeska , mary n.k badala yake nilisikia majina ya 'kiislam' kama juma, Asha, Sharif, n.k. wakati waliokuwa wakiombewa ni wakristo.

Kwahiyo swali langu kwako JF MEMBER je wewe uliwahi kuskia majina yenye nasaba na 'ukristo' kutoka kwa ''mapepo?"

Pia kwa wale wasio amini ikiwa mungu yupo wanazungumza nini kuhusu haya "mapepo"
Jini sharif,maimuna,subian,dah kuna kapointi hapa ila subiri waje wenye majina yao
 
Mashetani aka Majini aka Mapepo yapo yameumbwa na Mungu kama tulivyoumbwa sisi Binaadamu.

Mungu kaumba MALAIKA, MAJINI na BINAADAMU ili wamuabudu tu, na sio chengine, na viumbe wasiomuabudu Mungu amewaekea adhabu kali

Marehemu Bibi yangu alikuwa hajui kusoma wala kuandika,lakini pale Shetani aka pepo anapokuwa amepanda kichwani kwake alikuwa anaweza kuongea kiarabu fasaha kabisa..

Marehemu Baba alikuwa ana uwezo wa kumwita jini wa Bibi, alipokuwa anamwita familia nzima inatakiwa wepo, Alikuwa ni jini wa famili, chakula chake kulikuwa, Asali, muwa, manda

Yule juni alikuwa anatusalimia kwa kutuzungusha shingo, kutunyoosha mkono huku Akisema "zein, zein", baba alikuwa anamwita jini wa Bibi pale anapokuwa anataka msaada wa kitu fulani..

Jini wa Bibi alikuwa na Uwezo mkubwa Sana, jina lake lilikuwa sio la kiarabu bali ni la kiswahili wa pwani, siku moja nilimsikia akisema wapi anatoka na yeye ni nani

Nilimsikia akisema yeye ni Mkuu wa Majini katoka sehemu fulani Pemba, vile vile alikuwa anawakilisha sehemu kubwa ya ufukwe wa Afrika Mashariki yaani, Mambasa, Unguja, Pemba, Kilwa..

Sitaki kutaja jina la huyu jini, kwakweli alikuwa na Uwezo wa ajabu Sana, uwezo wakuona na kutabiri, mambo mengi sana Alikuwa na Uwezo wa kuwaadhibu Majini wengine nk..

Haya mambo yapo, nimeyashuhudia mwenyewe, hivi viumbe vimeumbwa na Mungu,..

Yale tunayoyaona Makanisani ni "usanii", "utapeli",..huwezi kumtoa jini kwa kumpiga kelele, Majini wana vyakula vyao, wana njia zao za kuwaita na wana njia zao za kuwatoa,nimeyaona haya nikiwa na umri mdogo mpaka umri wa kumaliza Chuo

Tunatakiwa tujue kuwa hivi viumbe, ni kama sisi Binaadamu, wako wabaya na Wazuri, wako wanaomcha Mungu na wanaomuasi Mungu, lakini Wengi wao ni wa ha Mungu, wanaishi maisha marefu kuliko binaadamu
Huyo ,zein zein nimhuni sana anabadili majina san sindo huyu kwasasa anaitwa eatel, mwehu kabisa
 
Nilichojifuza hapa

MAJINI WOTE NI WAARABU
majin wapo wa kila taifa kila Lugha wapo majin wanaopatikana maeneo flan tu africa hawapo kabisa wapo wanaopatikana africa tu sehem zingine hawapo...kuna elimu kinwa juu ya viumbe hawa muda na sehem hii haitoshi
 
Basi kiti wa Jiwe anaitwa Ernest....

Sema nini amegoma kupanda toka siku ya graduation ya Phd ndo maana English is not richabo
 
majin wapo wa kila taifa kila Lugha wapo majin wanaopatikana maeneo flan tu africa hawapo kabisa wapo wanaopatikana africa tu sehem zingine hawapo...kuna elimu kinwa juu ya viumbe hawa muda na sehem hii haitoshi
Mkuu nasema ni waarabu kwasababu

Mtu akigalagala na kijitupa chini huwa kuna mambo kama matatu

Wengine watasema labda kifafa!!

Wengine watasema labda malaria lmempanda!!

Ataanza kupewa huduma ya kwanza lakini kosa huyu mgonjwa akianza kuongea kiarabu

Huduma zote zitasitishwa jibu litakuwa limeshapatikana kuwa ana MAJINI!!

NA KIPIMO NI KIARABU!!
 
'Sikuwaumba majini na watu ili wapate kuniabudu', maana yake 'Sikuwaumba watu wa hadhi ya juu na hadhi ya kawaida (Matajiri na Masikini, wazuri au wabaya n.k) ili waniabudu'.
Na ndio maana Quran mpaka tutakufa itabaki kwenye Asili yake ya Kiarabu. Ingekuwa inatafsiriwa na kupoteza uhalisia wake ungeweza kuwapotosha wengi sana hapa.

Tangulini Jini maana yake ni mtu mwenye hadhi kubwa.
 
acha tu ndugu yangu jamaa kayumba sana.! nimempa historia ya majinn
 
Nilichojifuza hapa
MAJINI WOTE NI WAARABU
Kuna maelezo ya aina mbili kuhusu majini kutoka kwenye vitabu vya dini,wengine wanasema majini asili yao ni malaika(wale malaika waliyoasi) na wengine wanasema asili yao ni moto na majini ni viumbe(tofauti na malaika na binaadamu) vilivyo na Mungu kwa sababu zile zile walizoumbiwa binaadamu.
 
Malaika alivyoumba nature yake hawez kuasi hana Option hiyo Jinn ni kiumbe kingine,Malaika ni kiumbe kingine na mtu ni kitu kingine...Mtu kaumbwa kwa udongo,Malaika kaumbwa kwa Nuru na Jinni kaumbwa kwa miale ya Moto...Kasomen surat rahman Allha ameelezea uumbaji wa wa hivyo viumbe
 
Back
Top Bottom