Majina ya ‘majiin’

Majina ya ‘majiin’

Ahhh Upo SAHIHI KWA IMANI YAKO.
LAKINI KWA IMANI YANGU HAUPO SAHIHI
Nani mapepo, nani Majini, unajichanganya Mkuu

Mungu kaumba, Malaika, Majini na Binaadamu pamoja na Wanyama..

Pepo, Ruhani ni miongoni mwa Majini sema wao wameokoka, ni wacha Mungu.
 
Sasa hivi wewe unafuga Mangapi muheshimiwa? Vipi huyo wa bibi nani kabaki nae
Bibi amefarilki zamani sana, lakini kwavile yule Jini, Bibi alirithi kwa Wazazi wake na yeye inabidi arithiwe na mtu mwengine

Jini ndie anaamua arithiwe na nani, bahati mbaya amekwenda kwa mtu mwengine sio mimi..

Jamaa aliemrithi huyo Jini yeye sio kama Bibi, yeye amejua kumtumia kwani jamaa ni Tajiri sana na anaendelea kutajirika..
 
Kuhusu kuwatoa majibu kanisani,si utapeli...

I did that myself,mara nyingi sana,tena kwa uwezo wa kukushika tu..na hilo dude chafu likatoka.
Unatumia uwezo wa Yesu au shetani, maana hilo jina lenyewe unalojiita "Zeus" ni Mkuu wa pepo. Unaombeaje kanisani huku mwenyewe unatukuza mapepo?
 
Tatizo kuna dini moja inakemea majini nyingine inawatambua majina kama masela wao a.k.a wana ambao hawastahili kutengwa.
Pamoja na kuwepo kwa usanii mwingi siku hiz kwenye makanisa mbali mbali lakini ninaamini kuwa yapo majiin/ mapepo na wengine wakiita mashetani

Ninaamini hivyo kwasababu nikiwa mdogo, kulikuwa na 'dada' zangu waliokuwa wanasumbuliwa na hayo 'mapepo' na hivyo nilijiridhisha kuwa hakukuwa na 'usanii' pale.

Nimeeleza hayo kwasababu nina swali limenitatiza kwamba wakati wa maombezi kwa hao 'dada' zangu kuna wakati muombaji alikuwa anaongea na hayo 'mapepo' na kuuliza majina yao. (Kwa wenye imani ya kikristo wananielewa hapa) mara zoote ckuwahi kuckia wakijitambulisha kwa majina ya 'kikristo' kama vile Thomas, peter, jeska , mary n.k badala yake nilisikia majina ya 'kiislam' kama juma, Asha, Sharif, n.k. wakati waliokuwa wakiombewa ni wakristo.

Kwahiyo swali langu kwako JF MEMBER je wewe uliwahi kuskia majina yenye nasaba na 'ukristo' kutoka kwa ''mapepo?"

Pia kwa wale wasio amini ikiwa mungu yupo wanazungumza nini kuhusu haya "mapepo"
 
Kwa nini usifanye jaribio? Jini ana uwezo much far kuliko binadamu, hilo halina ubishi. Lakini aliye ndani ya Yesu, ni mrithi pamoja na Kristo, amekuwa adopted na hivyo kufanyika mwana wa Mungu, mzaliwa wa pili baada ya Kristo. Yaani situation inakuwa hivi, Yesu anakuwa ni First Born, halafu aliye ndani ya Yesu anakuwa Second Born, yaani wanakuwa sawa tu kama wewe na wadogo zako au kaka zako uliozaliwa nao tumbo moja ulio nao hapo nyumbani kwenu. Kinachotakiwa tu kwa yule ambaye amekuwa adopted, inabidi AAMURU (na si kuomba) kwa Jina la Yesu, ili pepo atoke. Humwombi pepo atoke ila unamwamuru. Sasa inapokuja kwenye kuamuru, hapo ndiyo inaingia hadi hulka yetu sisi ya kibinadamu (ambayo si kosa, japo haichangii au haina uhusiano na pepo kutoka au kutokutoka), kwamba tuna kawaida ya kutoa amri kwa sauti yenye mkwara na ya juu sana, wakati kwa Jina la Yesu, kinachotakiwa ni maneno yenye amri tu hata kama utayatoa kwa sauti ya kawaida na ya upole, pepo lazima ang'oke. Wakati Yesu anaulaani mtini kwa kutokuwa na matunda, aliongea kwa sauti ya kawaida tu, hata namna alivyokuwa anaamuru mapepo yatoke, alikuwa anongea maneno ya amri na kwa sauti ya kawaida tu.
Ni kwamba ukishakuwa adopted na kufanyika mwana wa Mungu, nguvu yote ya Mungu inarithishwa kwako, na unakuwa na uwezo wa kuitumia to an unlimited extent, na kama ukiona kuna vitu bado vinaleta mgogoro pamoja na kuwa uko adopted, jua kuna mahali Mungu anapenda kukuweka uwe sawasawa, ili uwe CHOMBO CHAKE KIPYA, KIKALI CHA KUPULIA. Vinginevyo labda uwe haujasimama kisawasawa na Mungu, uko mguu ndani mguu nje, na hivyo huna uwezo wa kutumia mamlaka zake kwa ukamilifu kama unavyotakiwa, amekunyima uwezo unaostahili kuwa nao.
Muhimu tu ni kuwa huwezi ukamu-invoke Yesu ili utoe pepo. Wana wa Skewa kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume, walikuwa wanafanya kitu hiki. Siku moja wakiwa wanajaribu kumtoa pepo, pepo aliwakatalia na akawazidi nguvu na kuwapiga vibaya sana. Wana wa Skewa hawakuwa ndani ya Yesu, hawakuwa na adoption na hivyo walikuwa wanafanya exorcism sawa tu kama vile anavyoweza kufanya Mganga wa Kienyeji. Hakuna nguvu iliyo juu ya Mungu, lakini pia ieleweke wazi kuwa hakuna binadamu aliye nje ya Mungu mwenye nguvu kumzidi Shetani, bado ana upako wa muda aliopewa na Mungu, hakunyang'anywa, ila upako wake uliwekewa tu kikomo.
"Jinni ana uwezo much far kuliko binadam"

Chief! Unao ushahidi wa hiyo sentensi hapo juu?
 
Tatizo kuna dini moja inakemea majini nyingine inawatambua majina kama masela wao a.k.a wana ambao hawastahili kutengwa.
Dini gani hiyo inayowakubali Majini?
Kuna dini badala ya Kumwabudu Mungu sehemu zao za Ibada zimekuwa viringe vya kuunga Mashetani
 
Majini yote ni ya kiislamu au majina ya kiislamu au kiarabu maana piga ua hakuna jini Mathew
 
Mashetani aka Majini aka Mapepo yapo yameumbwa na Mungu kama tulivyoumbwa sisi Binaadamu.

Mungu kaumba MALAIKA, MAJINI na BINAADAMU ili wamuabudu tu, na sio chengine, na viumbe wasiomuabudu Mungu amewaekea adhabu kali

Marehemu Bibi yangu alikuwa hajui kusoma wala kuandika,lakini pale Shetani aka pepo anapokuwa amepanda kichwani kwake alikuwa anaweza kuongea kiarabu fasaha kabisa..

Marehemu Baba alikuwa ana uwezo wa kumwita jini wa Bibi, alipokuwa anamwita familia nzima inatakiwa wepo, Alikuwa ni jini wa famili, chakula chake kulikuwa, Asali, muwa, manda

Yule juni alikuwa anatusalimia kwa kutuzungusha shingo, kutunyoosha mkono huku Akisema "zein, zein", baba alikuwa anamwita jini wa Bibi pale anapokuwa anataka msaada wa kitu fulani..

Jini wa Bibi alikuwa na Uwezo mkubwa Sana, jina lake lilikuwa sio la kiarabu bali ni la kiswahili wa pwani, siku moja nilimsikia akisema wapi anatoka na yeye ni nani

Nilimsikia akisema yeye ni Mkuu wa Majini katoka sehemu fulani Pemba, vile vile alikuwa anawakilisha sehemu kubwa ya ufukwe wa Afrika Mashariki yaani, Mambasa, Unguja, Pemba, Kilwa..

Sitaki kutaja jina la huyu jini, kwakweli alikuwa na Uwezo wa ajabu Sana, uwezo wakuona na kutabiri, mambo mengi sana Alikuwa na Uwezo wa kuwaadhibu Majini wengine nk..

Haya mambo yapo, nimeyashuhudia mwenyewe, hivi viumbe vimeumbwa na Mungu,..

Yale tunayoyaona Makanisani ni "usanii", "utapeli",..huwezi kumtoa jini kwa kumpiga kelele, Majini wana vyakula vyao, wana njia zao za kuwaita na wana njia zao za kuwatoa,nimeyaona haya nikiwa na umri mdogo mpaka umri wa kumaliza Chuo

Tunatakiwa tujue kuwa hivi viumbe, ni kama sisi Binaadamu, wako wabaya na Wazuri, wako wanaomcha Mungu na wanaomuasi Mungu, lakini Wengi wao ni wa ha Mungu, wanaishi maisha marefu kuliko binaadamu
Wewe ndo msanii kwa kuamini mashetani, Hakika jehannamu inakusubiri usipotubu
 
Hakuna tofauti baina ya mashetani, majini, na mapepo.
Mungu haabudiwi na na mashetani wala Majini halikadhalika mapepo enyi watu wa dini acheki kujidangaya maana jehannamu ipo ikiwa hamtatubu..
 
Tatizo kuna dini moja inakemea majini nyingine inawatambua majina kama masela wao a.k.a wana ambao hawastahili kutengwa.
Hapana mkuu tatizo linaanzia mbali,ukiangalia sifa za majini kwa inavyoelezwa kwenye dini moja ni tofauti na dini nyengine.

Huku tunaambiwa malaika waliyoasi ndio majini na kwa hivyo wana asili yao ni malaika kwahiyo hawazaliani hawana jinsia ila kwengine tunaambiwa malaika ni viumbe vilivyoumbwa na Mungu(na sio malaika waasi) na wana jinsia hivyo wanazaliana.

Sasa sijui kwanini iwe majini ndio malaika waovu?
 
Unatumia uwezo wa Yesu au shetani, maana hilo jina lenyewe unalojiita "Zeus" ni Mkuu wa pepo. Unaombeaje kanisani huku mwenyewe unatukuza mapepo?
Mkuu na wewe ni nabiidaniel??

Tusipende kuhukumu nakujiona safi kuliko mwingine.
 
Usichokijua ni sawa na usiku wa kiza kinene. Fungua kamusi zote za Kiarabu halafu angalia maana ya neno Jinn (Kamusi kubwa za Kiarabu mojawapo ni Akrane). Neno jinn lina maana nyingi mojawapo ni, nyoka wakaao milimani, vijidudu vidogo vikaavyo kwenye takataka au bakteria, watu wakubwa kama viongozi wasiionekana mara kwa mara, n.k. Vyote , hivyo vimeitwa majinni. Hata aya inayozungumzia Majinni inaelezea kisa cha wafanyabiashara wa Kiyahudi wa kabila la Nasibin waliokutana na Mtume s.a.w akiwa anatoka Taif na akazungumza nao kuhusu Islam na kuwasomea aya zake.
Kweli usichikijua ni usiku wa giza. nyie wafuasi wa Ahmadiyya mnanishangaza sana. Jinni Tangu lini ikawa na maana ya mtu mwenye hadhi kubwa? Sasa kwanini basi hujasem hio aya (Sikuwaumba majini na binaadamu...) inazungumzia nyoka, bakteria au takataka? Wapi imetumika kumaanisha watu wakubwa wakubwa wasioonekana sana? Kaaaaazi kweli kweli!
 
Back
Top Bottom