Majina ya ‘majiin’

Majina ya ‘majiin’

Hakuna kitu kinatokea tokea hewani kila kitu kinasababu zake. Umeandika lakini sijajua kama hizo sentensi zako umezielewa

1. Hao mbwa wanapewa majina ya kikiristo sababu wanaishi na wakristo lakini mbwa siyo wakristo lakini wanauhusiano na wanakristo yaani wanaishi na watu wakristo.
2. Tukirudi kwenye mada, inaonesha majini wanaabudu kwenye dini ya kiarabu ndiyo maana lugha, majina na mavazi yanaendana na jamii ya kiarabu
3. Dini ya Kiarabu inasema "Mungu kaumba majini. Wapo majini wanaomubudu Allah, na wapo wasiomuabudu na pia kuna majini azuri na wabaya. Kwa wakristo ndiyo wanakubali kuwa Mungu kawaumba majini lakini hakuna jini linalomuabudu Mungu kwasababu ni malaika walioasi pamoja na shetani. Kiufupi hakuna jini mzuri au mbaya wote ni wabaya. Kwa sentensi yenu bado kuna uwalakini.
Chief uliwahi kusikia jina linalojitambulisha kwa jina kama joseph, Aloyce au martha?

Bila kujali kuwa huyo aliyeingiwa na huyo 'pepo' ni mkristo, muislam au mpagani
 
Isikusumbue ndugu,ni sawa tu na kukuta mbwa kapewa jina kama, Maurice, john nk.
Haimaanishi kuwa hao mbwa nao ni wakristo ni majina tu.
Hainisumbui boss bali ni kaz ya akili siwezi kuizuia. Je uliwahi kuckia jini linaitwa isack?
 
Mashetani aka Majini aka Mapepo yapo yameumbwa na Mungu kama tulivyoumbwa sisi Binaadamu.

Mungu kaumba MALAIKA, MAJINI na BINAADAMU ili wamuabudu tu, na sio chengine, na viumbe wasiomuabudu Mungu amewaekea adhabu kali

Marehemu Bibi yangu alikuwa hajui kusoma wala kuandika,lakini pale Shetani aka pepo anapokuwa amepanda kichwani kwake alikuwa anaweza kuongea kiarabu fasaha kabisa..

Marehemu Baba alikuwa ana uwezo wa kumwita jini wa Bibi, alipokuwa anamwita familia nzima inatakiwa wepo, Alikuwa ni jini wa famili, chakula chake kulikuwa, Asali, muwa, manda

Yule juni alikuwa anatusalimia kwa kutuzungusha shingo, kutunyoosha mkono huku Akisema "zein, zein", baba alikuwa anamwita jini wa Bibi pale anapokuwa anataka msaada wa kitu fulani..

Jini wa Bibi alikuwa na Uwezo mkubwa Sana, jina lake lilikuwa sio la kiarabu bali ni la kiswahili wa pwani, siku moja nilimsikia akisema wapi anatoka na yeye ni nani

Nilimsikia akisema yeye ni Mkuu wa Majini katoka sehemu fulani Pemba, vile vile alikuwa anawakilisha sehemu kubwa ya ufukwe wa Afrika Mashariki yaani, Mambasa, Unguja, Pemba, Kilwa..

Sitaki kutaja jina la huyu jini, kwakweli alikuwa na Uwezo wa ajabu Sana, uwezo wakuona na kutabiri, mambo mengi sana Alikuwa na Uwezo wa kuwaadhibu Majini wengine nk..

Haya mambo yapo, nimeyashuhudia mwenyewe, hivi viumbe vimeumbwa na Mungu,..

Yale tunayoyaona Makanisani ni "usanii", "utapeli",..huwezi kumtoa jini kwa kumpiga kelele, Majini wana vyakula vyao, wana njia zao za kuwaita na wana njia zao za kuwatoa,nimeyaona haya nikiwa na umri mdogo mpaka umri wa kumaliza Chuo

Tunatakiwa tujue kuwa hivi viumbe, ni kama sisi Binaadamu, wako wabaya na Wazuri, wako wanaomcha Mungu na wanaomuasi Mungu, lakini Wengi wao ni wa ha Mungu, wanaishi maisha marefu kuliko binaadamu
Mara nyingine shetani hujifanya malaika wa nuru
 
Siamini mambo ya Waganga, kwani ni wasanii, matapeli..

Siku moja nilikutana Bibi mmoja alikuwa na miaka kama 89,alikuwa mkristo, katika mazungumzo yetu aliniambia Kuwa mtoto wake wa kiume anaemtegea kapata wazimu amekuwa kuchaa

Nilimuuliza sasa amechukua hatua gani, kumsuru na huo ugonjwa, alilonijibu nilishangaa, sikuweza kuamini..

Aliniambia kampeleka kwa Sheikh kusomewa, nikamuliza Je mtoto wake alipata nafuu Akanijibu ndio, tena sana..

Nikamuuliza kwanini asimpeleke kwa Mchungaji wakati yeye ni Mkristo?! Akanijibu baba angu wewe acha tu!

Nilichanganyikiwa, nilishindwa kumfahamu yule Bibi.. Labda wadau mnaweza kunieleza kwanini imekuwa vile kwa huyu Bibi
Kuitwa Mkiristo ni kawaida sana kazi ipo kuwa na imani ya kweli isiyo changanyika, huyo mbibi ni mlozi aka mchawi
 
Kwa Mujibu wa kitabu cha Kurani Mungu hakuumba binaadamu peke yake, kaumba Malaika, Majini, Binaadamu, Wanyama na viumbe vyengine..

Nabii Suleiman(Solomon) Mungu alimpa uwezo wa kuongea na Majini pamoja na Wanyama..

Hivi viumbe vipo lakini havipo KISIASA, vina uwezo lakini tumeamriwa tusiviabudu..
Suleiman wa quran ni tofauti sana na wa biblia
 
Kuitwa Mkiristo ni kawaida sana kazi ipo kuwa na imani ya kweli isiyo changanyika, huyo mbibi ni mlozi aka mchawi
Hapana yule Bibi alikuwa sio mchawi, Ukristo ni dini ya Kubuni, hakuna Hata sehemu moja katika Biblia Yesu kasema aabudiwe, au dini (gospel) anayoihubiri iitwe Kristo

Kristo neno La Kigiririki lenye maana "Aliepakwa Mafuta", Biblia vile vile ni neno la Kigiriki lenye maana Maktaba au mkusanyiko wa Vitabu
 
Hakika Quran haikuwacha kitu hata dawa na kinga hupatikana kwenye Quran. Masheikh wengi hutumia surat za Quran mfano suratul kursi ina kinga kubwa sana. Sasa sijui upande wa wakristo wao inakuwaje


Nangatukaa
TUNATUMIA JINA LA YESU
 
Aahah Laiti Ungejua!
Watu wanapambana na Lucifer na Yezebeli.
Sembuse Jini???
Sawa, lakini ukweli ni huo, huwezi kumtoa au kumfukuza kiumbe chenye uwezo kuliko Binaadamu, kiumbe kilichomsaliti Mungu, kwa kumpiga kelele, "kwa jina la Yesu, toka, toka...." inabidi ujiongeze kidogo
 
Sawa lakini je unaijua tofauti baina ya majini na masheitani?
Labda kwa kukuweka sawa nahitaji tofauti hapo kwanza
Majini ni viumbe vilivyoumbwa na Mungu, viumbe hivi havionekani, vinaishi duniani, vinaishi katika jamii tafauti,pamoja na Binaadamu, vina makabila tafauti, vina Miji yao nk

kwa ufupi Hawa viumbe ni sawa na Binaadamu, wanaishi katika mfumo kama tunavyoishi Binaadamu, wako Majini wazuri na wabaya, Gini akiwa kaasi, akiwa Muovu huitwa SHETANI..

MASHETANI ndio wanatumiwa na baadhi ya Binaadamu kufanya mambo Maovu..
 
Nakubali majini yana majina yao...zebaq,jupta,subiani,makata,pruto,na kuna jini kikongwe kabisa anaishi ktk MBAAZI anaitwa qdaz.
 
Aahah Laiti Ungejua!
Watu wanapambana na Lucifer na Yezebeli.
Sembuse Jini???
Kuna siku kwenye tv nilikuwa namuangalia nabii mmoja anatowa watu mapepo basi akaja kijana ndio ana jini na anasema ni Lucifer,ila kilichonifurahisha zaidi ni kiingereza chake huyo Lucifer maana alikuwa anaongea kiingereza ila kilikuwa cha kutafuta maneno. Nikaona huyu Lucifer anatakiwa akapigwe msasa na Ras simba.
 
Back
Top Bottom