Kila nafsi itaonja mauti. Imeandikwa. Pumzikeni kwa amani, Makamanda. Mmeifia nchi. Tanzani. Kifo cha kishujaa. Mungu ibariki Tanzani.
Tanzania inapigana na Sudani ?
Kila nafsi itaonja mauti. Imeandikwa. Pumzikeni kwa amani, Makamanda. Mmeifia nchi. Tanzani. Kifo cha kishujaa. Mungu ibariki Tanzani.
Inawezekana lakini kwa uhakika ni Somalia, yeye Rwanda ana vikosi vingi huko.
Kwa sasa hiii ni biashara na UN hawa Peacekeeper wanalipwa in Doller na Serikali pia wanavuna
.....ni kweli mkuu, hayo ni "mashaka yangu tu".....
Hayo maneno uliyoandika hapo chini ni upumbavu na kukosa akili kuliko pitiliza.
Rest in peace askari wetu. Mmekufa kishujaa
![]()
Vifo hivi viwakumbushe wanajeshi wetu kwamba watanzania wote ni ndugu na kwamba sote ni mavumbi na mavumbini ni lazima tutarudi. Mateso wanayoyafanya wanajeshi kwa raia wa Mtwara ni ya kinyama!!! Si ya kiutu hata kidogo!!! Ni bahati mbaya kwamba jeshi letu linatumiwa vibaya na wanasiasa!!! Mungu aturehemu sote na roho za wanajeshi hawa zipumzike kwa amani!!
Subiri nikuelimishe bwana mdogo.
(1) Unapozungumzia swala la jeshi kwenda kulinda amani maana yake ni kwamba hili eneo au hapo mahali pana machafuko ya vita, kwa hiyo ni LAZIMA jeshi lipelekwe kwenda kutuliza hayo machafuko ya kivita....
hapa unazungumzia Peace Enforcement ..Peace Enforcement is actually getting in the middle and using military force creating peace through harsh military action against anyone who threatens the other side. Its a stronger guns blazing approach of if you don't stay peaceful we'll blast you to pieces.(2) Pia, kutokana na mahali hapo kuwa na vita ndio maana wanajeshi wanatakiwa wabebe silaha, tena nzito za kivita kwa ajili ya kuakikisha hilo eneo linakua na amani...
(3) Hizo silaha wanazobeba sio UREMBO, ni silaha wananzotakiwa kuzitumia pindi adui anapokua anataka kuleta za kuleta....
(4) Kwa hilo, huko somalia ni vitani na wanajeshi wetu wapo vitani... Hilo unatakiwa ufahamu...
Sasa swali la kujiuliza, Jeshi letu limeenda vitani kwa manufaa ya nani hasa, UN??
Kwa taarifa yako hizo vita za namna hiyo zinaigharimu sana taifa letu, kuanzania Human Capital, Financing, Equipment etc...
Pia, inakupasa utambua hatuna sababu ya msingi ya kupigana vita sasa... Wacha kila mtu atatue matatizo yake na sio kujifanya kimbelembele...
Je, tumepakana na Somalia?
Wacha kila mtu atatue matatizo yake na sio kujifanya kimbelembele...
Hivi mkuu wameifia Tanzania ama Sudan?Naomba kueleweshwa kwenye hili.Kuuliza si ujinga mkuu wangu.
Mkuu mbona unajibu kwa haraka haraka hivyo?si tunaeleweshana mkuu?
Ninavyoelewa hao ni mchango wa Tanzania UN,kwahiyo mission yao inaratibiwa na UN.
Sisi kama Tanzania hatuna mission ya kusapoti upande wowote huko Darfur Sudan.
Labda tuseme wameifia freedom and justice,lakini si Tanzania,unless uniambie walikuwa wakiipigania Tanzania,mipaka yake ama interests zake.
Na ndiyo maana wengine tunataka kuona wanafamilia wao wanakuwa taken care of kwasababu nasikia kuna malipo ambayo wakubwa wanayakinga.
Tanzania inapigana na Sudani ?
usitafsiri vitu directly mkuu.
Kumbe nini maana ya kuifia nchi ? Labda kama ingesemwa kuifia Afrika au dunia, maana wametumwa kwa ajili ya kuweka amani katika Bara la Afrika kwa ujumla na sio sio kuifia Tanzania. Ni kweli kwamba ni wanajeshi wa Tanzania, laikini hawako huko kwa maslahi binafisi ya Tanzania, bali ya Afrika na dunia nzima kwa ujumla.
![]()
Vifo hivi viwakumbushe wanajeshi wetu kwamba watanzania wote ni ndugu na kwamba sote ni mavumbi na mavumbini ni lazima tutarudi. Mateso wanayoyafanya wanajeshi kwa raia wa Mtwara ni ya kinyama!!! Si ya kiutu hata kidogo!!! Ni bahati mbaya kwamba jeshi letu linatumiwa vibaya na wanasiasa!!! Mungu aturehemu sote na roho za wanajeshi hawa zipumzike kwa amani!!