Majina saba ya askari walio uwawa Sudan

Majina saba ya askari walio uwawa Sudan

ni habari iliyonisikitisha sana...........maombi yangu ni kwa wanafamilia na wapendwa wote ambao msiba huu umewagusa kwa karibu sana kwamba mungu awape faraja yake na awafanyie wepesi katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.

kama taifa na jumuiya ya kimataifa ni lazima uchunguzi wenye haja ufanyike kwani hii ni mara ya pili kwa askari wa kulinda amani wa umoja wa mataifa kushambuliwa. Ikumbukwe ilishatokea tena jamhuri ya afrika ya kati.
 
subiri nikuelimishe bwana mdogo.

(1) unapozungumzia swala la jeshi kwenda kulinda amani maana yake ni kwamba hili eneo au hapo mahali pana machafuko ya vita, kwa hiyo ni lazima jeshi lipelekwe kwenda kutuliza hayo machafuko ya kivita....

(2) pia, kutokana na mahali hapo kuwa na vita ndio maana wanajeshi wanatakiwa wabebe silaha, tena nzito za kivita kwa ajili ya kuakikisha hilo eneo linakua na amani...

(3) hizo silaha wanazobeba sio urembo, ni silaha wananzotakiwa kuzitumia pindi adui anapokua anataka kuleta za kuleta....

(4) kwa hilo, huko somalia ni vitani na wanajeshi wetu wapo vitani... Hilo unatakiwa ufahamu...

Sasa swali la kujiuliza, jeshi letu limeenda vitani kwa manufaa ya nani hasa, un?? Kwa taarifa yako hizo vita za namna hiyo zinaigharimu sana taifa letu, kuanzania human capital, financing, equipment etc...

Pia, inakupasa utambua hatuna sababu ya msingi ya kupigana vita sasa... Je, tumepakana na somalia? Wacha kila mtu atatue matatizo yake na sio kujifanya kimbelembele...

nijuzeni jamani.darfur iko wapi?ni vita gani iko huko yaani nani anapigana na nani?kwa nini kuna vita kila mahali katika bara la afrika?majeshi ya un yako kila mahali!!au imeshindwa kusuluhisha hii migogoro?hii migogoro mbona haiishi??kwa mfano eastern drc waafrika wanaua waafrika wenzao bila sababu.hii ni nini?
Wanajf nijuzeni?hapa tanzania wanachadema wanauawa kwa mabomu kwenye mikusanyiko yao bila sababu?ni kwa faida ya nani?

Nawasilisha.
 
Nawapa pole wanafamilia wote kwa msiba mzito
 
Jeshi liache kufanya mambo kisiasa kwanza ndo wataendelea. Hawana uzalendo hata kidogo na wakiendelea hivi tujiandae kuchimba makaburi zaidi ya wanajeshi. Jeshi letu inachokifanya huku mtwara sihitaji hata kuwasikia. Wanasiasa wanaingilia sana shughuli za jeshi na wanajeshi wanajipendekeza kwa wanasiasa ili wapewe ukuu wa mikoa na wilaya. Hii mbaya sana. Kikwete ameongeza maadui zaidi so watanzania kila tulipo tunatafutwa. Kwanini atekwe mtanzania na kwanini wafe watanzania?. Poleni wafiwa. Mia
 
Kuliko kuwa JW kwa Tanzania kwa sasa hata ukifia kazini familia yako inaambulia maneno matupu na watoto wako wanakuwa machokoraa bora kujiunga na walume M23 maana kule mkipiga fungu linakuwa la uhakika
 
kama watanzania hatuna budii kuungana na ndugu za wana familia waliopeteza maisha wakiwa katika kazi ya kulinda amani mungu azilaze roho za mashujaa wetu mahali pema peponi
 
Mungu awapumzishe kwa amani Makamanda hawa waliopoteza uhai na awaponye majeruhi!
Natoa wito kwa vikosi vyetu vyote vilivyokwenda kulinda amani chini ya mwamvuli wa UN au AU (kuongeza umakini, jiepusheni kufanya kazi kwa mazoea, jiepusheni na wamawake wa watu, epukeni ulevi mbwa na anasa za usiku) Pangeni mbinu na nyendo mpya kila siku! Huko ni ugenini raia yeyote atakayejichanganya mkimshuku "ACHEZEE KUBWA" maana waswahili husema 'ukicheka na nyani uatavuna mabua'.Nawatakia kila la kheri na mrejee nyumbani salama.
POLENI MAKAMANDA POLE WATANZANIA WOTE KWA KUPOTEZA WAPIGANAJI WETU.
 
Duh ni habari ya kusikitisha sana Kama Taifa tumepoteza wapiganaji wetu na walinzi wa mipaka yetu. MUNGU AZIWEKE ROHO ZA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI.
 
Hayo maneno uliyoandika hapo chini ni upumbavu na kukosa akili kuliko pitiliza.
Rest in peace askari wetu. Mmekufa kishujaa

Ni mtazamo tu unaweza kuwa na ukweli ndani yake au la. Kwa hiyo kabla ya kupinga jaribu kufuatilia kisemwacho halafu ndio uhitimishe au utoe pendekezo!
 
Kuliko kuwa JW kwa Tanzania kwa sasa hata ukifia kazini familia yako inaambulia maneno matupu na watoto wako wanakuwa machokoraa bora kujiunga na walume M23 maana kule mkipiga fungu linakuwa la uhakika

Jamani hawa ni watanzania wenzetu wamepata ajali kazini. Tuwapeni POLE wote waliofiwa. Hii ni ajali kazini kama za wengine wanaofia migodini au kunaswa na umeme, kuangukiwa na majumba wanayojenga nk.
 
Poleni sana wafiwa na taifa kwa ujumla..
Mungu azilaze rohozao mahala pema peponi AMEN!!
 
Pumzikeni kwa amani makamanda mliokufa. polen ndugu wa marehemu
 
Majina ya askari saba wa Tanzania waliokufa kwenye shambulio la ghafla mjini Darfur yamepatikana.


2.png

Askari hao waliokufa ambao walikuwa kwenye vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa huko nchini Sudan ni :-
1. Sajenti Shaibu Othuman,
2. Koplo Oswald Chaula,
3. Koplo Mohamed Juma,
4. Koplo Mohamed Chikilizo,
5. Pte. Rodney Ndunguru,
6. Pte. Peter Werema,
7. Pte. Fortunatus Msofe.



Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kwenye mtandao ni kwamba askari hao walikwenda kujaribu kumwokoa mwenzao (ambaye hakutajwa) ambaye alisemekana kutekwa na vikosi vya waasi nchini humo.

Wakati wakijiandaa, ghafla walizingirwa na askari hao waasi na kisha kushambuliwa kwa risasi hadi kufa.

Haikufahamika hali ya askari huyo ambaye alidaiwa kutekwa kama bado yu hai ama ni miongoni mwa waliokufa.

Mungu azilaze roho za askari wetu mahali pema peponi, Amina.
Sad day kws TPDF, na RIP kwa hawa vijana wsliojitolea maisha yso kwa ajili ys amani.
Ni vema sasa TPDF kufanya utafiti wa tukio ns kubadili rules of engagement.
 
JWTZ sasa ihakikishe zile POSHO wanazowaminyia wanapokuwa kwenye mission huko nje ya Tanzania wanawapa zote maana wahanga ni familia zao angalau hata hicho kidogo kiwafae wanaopoteza ndugu zao. Kamwe watu wasijenge MAGHOROFA kwa kuwadhulumu hawa jamaa...kamchezo kachafu sana. Poleni sana wanafamilia na watanzania wenzangu Kwa ujumla. RIP makamanda
 
Je askari wetu walio mtwara wameona hiyo,maana wao wanaamin kwamba askari hafi ndo maana wanetesa raia tena aliye mikono mitupu,kama waasi tu wanapiga pigo moja saba chali,serikali haioni ni bora kuboresha mafunzo kwa askari kuliko kuwalipa kwa kupiga raia huko ntwara? Bado kunja wa mpanda ayedhani ataishi milele
 
Back
Top Bottom