Majina saba ya askari walio uwawa Sudan

Majina saba ya askari walio uwawa Sudan

Mungu awafariji wafiwa, wazazi, ndugu na watoto wao!!!
 
Una uhakika gani kwamba walikuwa hawafungi.. ?? How shamefull we will look infront of ALLAH For judging people of the sins which he had already forgiven them for

Kwani kufunga kuna uhusiano gani na kusamehewa dhambi?
 
Tunawaomba Al shabab waje Mtwara watusaidie, hawa askari wetu kumbe kuonea wanawake tu hawawezi kupigana na wanaume wa vita, ndo maana siku hizi wanatumika kama polisisiem. Kule sio comoro, mara wengine hawajui hata kuogelea wanakufa maji
 
Kuna msemo wa kiswahili usemao, "Pilipili usioila inakuwashia nini?"... Hii vita ya somalia inamanufaa gani kwetu sisi mpaka tujipeleke na kuishia kuuliwa kama kuku? Ni kipi hasa tunachokitafuta huko, sifa?

Kinachotupasa ni kulinda mipaka yetu basi.... Haya mambo mengine ya kutafuta sifa hayafai....
 
This is a sad news; nawapa pole familia za marehemu wote, JWTZ na Watanzania wenzangu kwa pigo hili. Moyo wangu ulishtuka kwani nina dadangu ambaye yuko huko kwa kazi hii. Mungu azilaze pema roho za marehemu na kuwafariji familia.


Ipi tofauti ya mwanajeshi anayeua "muasi" na muasi anayeua mwanajeshi? Is it morals au upande hawa binadamu wawili hawa waliochagua?
 
Naomba niulize, hivi majeshi ya Rwanda ynayo apo pale Darfur???

Inawezekana lakini kwa uhakika ni Somalia, yeye Rwanda ana vikosi vingi huko.
Kwa sasa hiii ni biashara na UN hawa Peacekeeper wanalipwa in Doller na Serikali pia wanavuna
 
kwani kufunga kuna uhusiano gani na kusamehewa dhambi?


mada nyingine hiyo.. Ila sisi waislam mafundisho yetu yanasema huu ni mwezi wa toba na utasamehewa makosa yote ukifanya toba ilhali swaum yako ipo sawa... ( hutamani, unatoa misaada kama unauwezo,, etcl)

namshangaa huyo jamaa aliyesema hao wenye majina ya kiislam hawakutakiwa wawe hapo walitakiwa wawe kwenye mfungo...

Hivyo ndivyo waislam tunavyoamini .. Sikulazimishi uamini hivo

kulinda amani ni moja ya ibada , na basi kama amefariki akiwa anafanya ibada kwa nia nzuri malipo yao ni makubwa tu!!....


 
wapumzike mahali walipoandaliwa kwa jinsi walivyojiandaa wakiwa duniani......kwetu sisi tuwaombee amani ya roho zao na hukumu huko waendako iwe sawa na matendo yao..Amina
 
kuna msemo wa kiswahili usemao, "pilipili usioila inakuwashia nini?"... Hii vita ya somalia inamanufaa gani kwetu sisi mpaka tujipeleke na kuishia kuuliwa kama kuku? Ni kipi hasa tunachokitafuta huko, sifa?

Kinachotupasa ni kulinda mipaka yetu basi.... Haya mambo mengine ya kutafuta sifa hayafai....


hatuna jeshi somalia...

Tanzania kama member wa un , lazima ajitolee na yeye kulinda amani...

Wanajeshi hawakwenda kupigana , walipelekwa kulinda amani ....
 
Mauaji haya ni sababu tosha sisi kama Watanzania kuongeza mshikamano wetu. R.I.P Makamanda wetu.
 
Sio sahihi kusema wameifia tanzania. Sema wamefia haki, usawa na amani. Kupata justification ya kusema wameifia tanzania kwangu ni ngumu.
una uhakika gani kuwa walikuwa wanapigani a haki usawa na amani? kwani si juzi tu tumesikia rais akitaka nchi wahusika zifabye mazungumzo? una fikiri kama ni wanyang'anyi wanaweza mazungumzo?
ila kagame alisema "i will hit him at right time and right place"
 
hatuna jeshi somalia...

Tanzania kama member wa un , lazima ajitolee na yeye kulinda amani...

Wanajeshi hawakwenda kupigana , walipelekwa kulinda amani ....

Subiri nikuelimishe bwana mdogo.

(1) Unapozungumzia swala la jeshi kwenda kulinda amani maana yake ni kwamba hili eneo au hapo mahali pana machafuko ya vita, kwa hiyo ni LAZIMA jeshi lipelekwe kwenda kutuliza hayo machafuko ya kivita....

(2) Pia, kutokana na mahali hapo kuwa na vita ndio maana wanajeshi wanatakiwa wabebe silaha, tena nzito za kivita kwa ajili ya kuakikisha hilo eneo linakua na amani...

(3) Hizo silaha wanazobeba sio UREMBO, ni silaha wananzotakiwa kuzitumia pindi adui anapokua anataka kuleta za kuleta....

(4) Kwa hilo, huko somalia ni vitani na wanajeshi wetu wapo vitani... Hilo unatakiwa ufahamu...

Sasa swali la kujiuliza, Jeshi letu limeenda vitani kwa manufaa ya nani hasa, UN?? Kwa taarifa yako hizo vita za namna hiyo zinaigharimu sana taifa letu, kuanzania Human Capital, Financing, Equipment etc...

Pia, inakupasa utambua hatuna sababu ya msingi ya kupigana vita sasa... Je, tumepakana na Somalia? Wacha kila mtu atatue matatizo yake na sio kujifanya kimbelembele...
 
Jamani natumaini kunawatu kutoka Juu, kunaswala la mausiano yetu na nchi majirani na zinazooonyesha chuki juu yetu. isije kuwa ni intelligent setup iliyofanya na maadui zetu kutuonyesha kwamba wanaweza kufya chochote wakitakacho. tufanye uchunguzi wa kina kwa Vijana wetu. Mungu alaze rohoo za marehemu mhala pema peponi.

Yes, unapoahidiwa kuhujumiwa na jirani yako na asikuambie atakuhujumu vipi, kisha ukajikuta umehujumiwa, hauwezi kupuuza maneno yake hata siku moja. Kinachonipa mashaka zaidi, the man who said '' I will hit you'' majeshi yake yapo Darfur kwa muda mrefu sana na kuna wakati, Kamanda wa vikosi vya UN Darfur alitoka kwa 'I will hit you''. Uchunguzi ufanyike itabainika who is behind the incident. Anaweza asifanye yeye kama yeye ila aka-conspire na waasi kwa kuwapa fedha na wakatekeleza unyama huo. Ni mapema mno kusema hivyo, lakini madamu tuliambiwa tutapigwa muda muafaka utakapofika na tusijue ni nani katupiga na katupiga wapi, basi tujizatiti. Makamanda wetu R.I.P na wale mliosalia tupo pamoja fanyeni kazi yenu kwa ueledi, ushupavu, kujiamini, na tumjue adui yetu kwani ADUI HANA RANGI
 
Back
Top Bottom