Majibu ya Reginald Mengi juu ya Gesi kwa Profesa Muhongo

Majibu ya Reginald Mengi juu ya Gesi kwa Profesa Muhongo

damu ya wanamtwara itatutafuna sana..lazima tutubu..hapa naona vita ya maslahi..tpsf kwa nini hamkwenda mtwara kutetea wananchi? uzalendo!!!?
 
Muhongo anajua watanzania wamemdharau kwa kuongea utumbo ndo maana anamshambulia Mengi persônal. Unajua hawa watu maskini wakishaanza kushika hela za rushwa wanakuwa matatizo sana. Mwanzoni alijifanya kuja na sera ya kwamba yeye sio mwanasiasa ni mtendaji zaidi kumbe ni mpuuzi kuliko waziri yeyote wa jk.

Huyu Muhongo alipoanza alikuja na mkwara wa kwenda kula ugali na samaki kwa mama ntilie kule Arusha
huku anaponda vyakula vya kizungu. Cha kushangaza sasa anawashadadia hata wazungu wenyewe. Hao wazungu watakaokuja kuwekeza huku hawatakuja na hela zao. Deposit iliyopo hapo pamoja na government securities ndio zitatumika kuchukua mikopo kwenye mabenki makubwa na watafanya biashara, kitu ambacho hata wabongo wanaweza kukifanya. Huwezi kukata tamaa kujifunza kutembea eti kwa kuwa unatambaa. Tambaa kwanza then taratibu utatembea na mwishowe kukimbia.

Zamani watanzania walikuwa wanachimba dhahabu kwa kutumia sululu na majembe, leo hii kuna watanzania wana migodi yao ya dhahabu na wanatumia zana kama za wazungu. Kuna dogo mmoja Geita aliibuka na mtambo wa kuprocess mchanga walioacha watu wanaotumia zana duni saizi ana hela za kutisha.
 
Nchi yetu inakila kitu na ni vyema kuwaheshimu wazawa hawa ndio nadhani wenye uchungu na Tanzania kuliko kuwapa kipaumbele wageni tu.

Hebu soma tahariri ya gazeti la Raia Mwema (jana11 Sept, 2013) uone wajanja walivyonaswa na mtego wa Muhongo. Tahariri hiyo inawaita wawekezaji watanzania wazalendo uchwara! Mhariri alinasa baada ya kupewa tangazo nusu ukurasa na Wizara ya Nishati na Madini na lipo kwenye toleo hilo hilo.
 
hawa maprofesa na dr's wa ccm hawanaga msaada wowote kwa taifa hili.alivyoanza kazi huyu muhongo alikuwa mzuri sana sasa hivi ameshasimikwa kwenye ukoo wa panya (MAKOKOI ) tayari ameshasahau taaluma yake
 
Watu tunakaa kimya tu kwa sababu hatujazishika documents mikononi.
 
Tunahitaji maelezo ya kina pia kwenye hii hoja ya Mengi kumiliki vitalu 59 vya madini bila kuviendeleza. Je ni kweli anamiliki hivyo vitalu kama ujumbe wa simu unavyodai? Je alivipataje au alipewa katika mazingira gani? Je ulikuwa ni mchakato huru wenye kushirikisha wazawa wengi? Je amekuwa navyo kwa muda gani tangu amilikishwe hivyo vitalu na ana mpango gani wa kuviendeleza? Kama hafanyi udalali na hivyo vitalu vya madini kama anavyodai je anavifanyia nini bila kuviendeleza? Haoni anawanyima fursa wachimbaji wengine hasa wazawa wadogo wadogo kufanya uwekezaji kwenye hayo maeneo?

Hoja kuwa suala la vitalu madini halihusiani na hoja ya vitalu vya gesi ni hoja dhaifu mno kuzuia watu wasihoji nia ya Mengi na genge lake la kuanzisha huu mdahalo wa vitalu vya gesi. Kinachoangaliwa hapa ni malengo ya kupata vitalu ni nini hasa. Ikiwa ni kweli itathibitishwa kuwa tayari Mengi ana vitalu 59 "vyenye ukubwa wa mita za mraba 3,752.37 (sq km)" (hii nimeikopi kama ilivyo kwenye thread kwani sielewi hasa mwandishi alikuwa na maana gani) basi hatakuwa na uhalali (moral authority) wa kuongelea vitalu ya gesi mpaka hapo atakapojibu maswali hayo hapo juu.

Mkuu hapa bado hujaweka vizuri ulichopost..mita za mraba au (Sq Km) bado hizi ni tungo tata hapa.. Maana kama ni mita za mraba mbona hata mimi ninazo nyingi tu na Profesa wenu wa madini na gesi hajanitaja hapa
 

Profesa Muhongo asipingane na ushauri huu mzuri.
Nimalizie kwa kuwahakikishia Watanzania kwamba mashambulizi binafsi dhidi yangu yenye nia mbaya ya kunishushia heshima hayatakaa yafanikiwe.
Wenu,

Dk. Reginald A. Mengi

Mkuu; hii document imeshiba. BIG UP. Ila tusidanganyane na maneno ya "serikali sikivu" au "CCM sikivu"; hakuna mzuri mwenye dhamira njema na nchi. Huyo Prof ni MUONGO period.
 
Changamoto ambayo Tanzania inakabiliana nayo kwa sasa ni kwamba IMEKOSA WATU.......
USINIULIZE WATU GANI
 
Kwa ujumla Prof Muhongo ni waziri ambaye bado hajaeleweka anafanya nini.. Nakumbuka alivyoingia nikajua kwanza ni waziri mtaalamu wa eneo husika.. Nilitarajia atafuta madudu yote aliyoyaacha Ngeleja. Lakini inavyoonekana pamoja na uprofesa wake pesa zimempoteza kwenye muelekeo. Amebakia kupiga kelele za uwongo (siasa zaidi) na dharau kubwa kwa wafanyabiashara wa Tanzania.
 
Tatizo kubwa hawa wazawa wanaopewa wanafanya udalali kwa wenye pesa wa nje. bora tu kuwekeana mikataba na watu wa nje ambao kazi zao zinaonekana

Mikataba yenye kuipatia serkali 3%????
 
Kama wageni wanapewa hakuna ubaya kuwapa vipaumbele wazawa.

Kwa mara ya kwanza umeongea point..Endelea hivi..Hata kwa wale wa kipato cha chini..wanyonge..nk
 
Word...!

Mmoja ni msomi sana na ana cheo tena kwa kufuatwa na mkulu akaombwa...alafu mwingine ni msomi na ni tajiri.
Kila mmoja namuona mwenzake mpuuzi na si lolote kwake...ila binafsi namshangaa Prof. Muhongo kwa jinsi "alivyobadilika" ghafla kutoka kwenye misimamo yake.

swali la msingi ni nini "kimemlainisha"?
Mimi huwa sishangai binadamu anapobadilika bali huwa namshangaa na kumuona wa ajabu binadamu asiyebadilika.

Ningeshangaa sana kumuona Prof. Muhongo wa wakati ule mitaani mpaka sasa hajabadilika.

Kila nikiona mabadiliko ya kiutendaji kwa binadamu huwa ninamkumbuka mwalimu wangu wa shule ya msingi ambaye yeye alikuwa anawateua wale wanafunzi watukutu na wafanya fujo darasani kuwa ni ma-monitor wa darasa ili wafahamu ugumu wa kazi na vile vile mwalimu aondokane na adha ya kupambana nao. Kilichokuwa kinatokea ni wao kubadilika kwa haraka sana mpaka wanafunzi wengine lilikuwa wanapata wasiwasi na mabadiliko yao ya kutoka utukutu na furugu darasani mpaka kuwa zaidi ya watu wanyeyekevu darasani.

Prof. Muhongo wakati akiwa nje ya utendaji serikali alikuwa kinara wa kubainisha makosa na ufumbuzi wake, na kwa kufanya hivyo, he was pain in the government ass na serikali kwa kutambua hivyo, kwa kupitia uwezo wa Rais kisheria, akapewa wizara hiyo kuisimamia. Matokeo yake ndiyo haya tunayoyajengea hoja. 'Amebadilika'.
 
Kwa ujumla Prof Muhongo ni waziri ambaye bado hajaeleweka anafanya nini.. Nakumbuka alivyoingia nikajua kwanza ni waziri mtaalamu wa eneo husika.. Nilitarajia atafuta madudu yote aliyoyaacha Ngeleja. Lakini inavyoonekana pamoja na uprofesa wake pesa zimempoteza kwenye muelekeo. Amebakia kupiga kelele za uwongo (siasa zaidi) na dharau kubwa kwa wafanyabiashara wa Tanzania.

Ndio maana ukiwafikiria wasomi wa kitanzania na walioshika madaraka, utabaini kwamba hata miongoni mwa marais wanne walioongoza nchi hii, kumbe "Kikwete ni Booonge ya Rais" baada ya Nyerere, Hakuna aliyetarajia huyu Profesa atakuja na majibu ya namna hii. Ndio maana sishangai kila teuzi za Kikwete zinaangukia kwa watu ambao wanaonekana failure, ukweli ni kwamba ndio aina ya watu tulionao. Hata sijui tuifanyeje nchi hii iitwayo Tanzania.
 
wew unalishwa na mengi ndiyo maana unatetea hata uchafu wa mengi.

Sawa hapa tunaongelea frusa ya wazawa kuwekeza,faida yake ni kubwa sana kwani ata faida wakiipata wanazidi kuwekeza tanzania na frusa za kijamii za kiuchumi nazo zinaongezeka,tofauti na wageni ambao wao wanaondoka na faida yote,pia elewa ata hao wawekezaji awana keshi nao pia wanakopa katika mabenki ya kimataifa.Duniani hakuna nchi yenye maendeleo kama wazawa wanamiliki uchumi wao kwa asilimia ndogo.
 
Kiukweli kabisa hii serikali ya ccm inanitia kinyaa na kuhisi kutapika, eti kila hoja ya msingi na yenye mwelekeo wa kusaidia taifa wao wanapinga na kuanza kujitetea kwa hoja nyepesi tena zisizo na maana kwa hiyo mnataka kusema na Mengi nae ni CHADEMA? Sasa kwa staili kama hii wananchi tukiamua kupigania rasilimali zetu tutakwepa kuwa kama misri au tunisia? Bora nife kuliko kuishi na watu hawa wa ccm
 
Huyu Mengi anaibuka na kupotea kama samaki majini. Mara yuko na Manji, mara yuko na Polisi, leo yuko na Mhongo. kazi kweli kweli, mbona kuna matajiri wengi tu hapa nchini hawajaulizwa sana kauli ya Waziri, au anajiona yeye ndiyo tajiri mzawa kuliko wengine?
Hivi unajua Mengi ni nani TPSF?
Au unaropoka tu!!
 
Hebu soma tahariri ya gazeti la Raia Mwema (jana11 Sept, 2013) uone wajanja walivyonaswa na mtego wa Muhongo. Tahariri hiyo inawaita wawekezaji watanzania wazalendo uchwara! Mhariri alinasa baada ya kupewa tangazo nusu ukurasa na Wizara ya Nishati na Madini na lipo kwenye toleo hilo hilo.
As we are heading towards 2015 general election ndio mtawajua Raia Mwema ni watu wa aina gani.

......Hawaminiki wale...wakina Ulimwengu??!!! wale wa siasa chafu za kuchafuana enzi za Habari Cooperation?!!
 
Back
Top Bottom