Huyu Sospeter Muhongo anaelewa yote uliyoeleza, tena kwa makini kabisa, tatizo ni kuwa ameingia kwenye mtego ule ule ambao hakuna mwanaCCM amewahi kuukwepa. Nao ni mtego wa RUSHWA na 10%. Huyu jamaa ameishakamatishwa hela na huenda iko kwenye account yake mpya huko Uswisi na kaamua kujitoa ufaham. Nani hafahamu jinsi Mizengo Pinda alivyokuwa muungwana kabla ya kuwa waziri mkuu?? Lakini kwa sasa amelewa na kuvimbiwa hela za rushwa kiasi cha kuamrishwa wananchi ''tupigwe''. Ndio yanayomkuta Prof Muhongo kwa sasa, amevimbiwa rushwa na kuona watanzania hadhi yetu ni juice na soda licha ya kuwa Mungu katuleta kwenye nchi yenye neema ya gesi.....
Kama wageni wanapewa hakuna ubaya kuwapa vipaumbele wazawa.
Huyu Mengi anaibuka na kupotea kama samaki majini. Mara yuko na Manji, mara yuko na Polisi, leo yuko na Mhongo. kazi kweli kweli, mbona kuna matajiri wengi tu hapa nchini hawajaulizwa sana kauli ya Waziri, au anajiona yeye ndiyo tajiri mzawa kuliko wengine?
Watu someni between line maelezo yake amesema hoja ya wazawa kushiriki ktk gas ilijadiliwa ktk kikao na aliyeitolea maelezo kwa waandishi wa habari ni Simbeye. Hoja yake ni kwa nn aonekane yeye ndio anayedai? Pili kwa nn serikali ing'ang'anie kugawa vitalu bila kuwepo Sera? Jibu wanawahi 10% kabla ya 2015. Kwani hatujui namna wawekezaji wa nje wanavyowapa pesa viongozi wetu? pesa za USwiss zimeishia wapi?
Unapokumbana na marumbano yanayofikia kiwango cha kukosa hekima na busara kwa wadau wa kisiasa na kiuchumi kwenye maswala yao ya kisiasa na kibiashara inabidi uyajongee marumbano yao kwa umakini mkubwa sana huku ukiwa umefungua milango ya fikra na mawazo yako ili pia uchafu wote katika marumbano yao ufike kwenye chujio ndani ya akili ili ukipate kiini cha marumbano yao.
Prof. Muhongo hawezi akawa maraika katika marumbano haya, vivyo hivyo Dr. Mengi na hasa ikichukuliwa kuwa marumbano yao yanakuwa based on personal character and reputation. Inaonekana kama kuna kitu kimejificha na hawawezi kukisema kwa sababu wanafahamu kama hakina maslahi kwa wananchi walalahoi otherwise, kama kingekuwa na maslahi wangekuwa wameisha kisema mapema sana.
Hitimisho la marumbano yao litatokea tu pale watakapo kisema wazi au kwa faragha kwenye inner circle zao kile kinachowafanya kurumbana personally.
Tutegemee kuona na kusikia mengi.
Wewe si mzalendo, Tumia akili yako na si makamasi
Ujinga wa MaCCM ambao umepelekea nchi yetu kuwa maskini hadi leo unatokana na imani yao kuwa maendeleo yataletwa na wazungu tu. Lakini hapa Muhongo kufanya U-turn kwenye msimamo wake wa awali najua ni kutokana na presha kutoka juu yake. Ikumbukwe kuwa watu wanaotajwa kuwekewa fedha kwenye akaunti Uswisi na makampuni ya uchimbaji gesi ni mtoto wa Rais wetu ndugu Riziwani Kikwete. Hii ina maana kuwa hata Muhongo ana msukumo wa rushwa kubwa aliyopewa na wazungu na kwa ubinafsi anadharau watanzania wenzake.
Wapeni vitalu wawekezaji wazawa ili washindwe wenyewe, wakishindwa wapeni hao wazungu wa CCM lakini hakuna kitakachopotea. Hata maendeleo yaliyoko Marekani yameletwa na matajiri wa kimarekani. Faida ya kuwekeza kwa matajiri wazawa fedha zao wanaweka kwenye benki za ndani na sisi walalahoi tunakopa. Barick Gold, Geita Gold Mine faida zao zinaenda ulaya na marekani inarudi hela ya mishahara tu na operations. CCM Fungukeni akili na kuanza kuifikiria hii nchi. Ted Turner, Bill Gates, Oprah Winfrey, Michael Dell wote wametajirikia hapo hapo marekani na sasa ni investors wakubwa sana. Bakhresa, Mengi, Christopher Gachuma ni wawekezaji wa kitanzania, wana ajili watanzania katika sekta nyingi, wapeni fursa na huko kwenye madini na gesi. Moise Katumbi Chapwe ni mkongomani anamiliki migodi kibao kule kwao Katanga, ana hela nyingi ambazo wacongoman wenzake wanazifaidi. Harry Openheimer ni msouth Afrika ametajirika kwenye migodi na nchi yake inanufaika na uwekezaji wake. Kwa nini nyie maCCM hamjifunzi huko?? Mbona sasa kuna watanzania wanawekeza kwenye umeme na juzi tumeambiwa IPTL imenunuliwa na watanzania. Nyie maCCM mmeishachukua rushwa ndio maana mnajifanya hamna akili.
Nilipoona Muhongo amevaa manguo ya kijani wakati wa ziara ya Kikwete Mwanza, nikajua tayari huyu mzee ameishanunuliwa na wazungu kwa hiyo anaficha rushwa alizochukua kwenye hayo manguo ya kijani
yenye laana.
Kama wageni wanapewa hakuna ubaya kuwapa vipaumbele wazawa.
Mimi naona amejibu vizuri tu. Hoja ilikuwa ni kuhusu gesi. Hata kama RM ana vitalu vya madini na hajaviendeleza, hilo ni la RM binafsi na haiwezi kufanya wazawa/watanzania wote tuwekwe kwenye kapu moja. Halizuii TPSF kutoa maoni yake kuhusu gesi kuhakikisha wazawa wananufaika na maliasili yao. Hilo la vitalu, pia haliondo ukweli kuwa hatuna sera ya gesi lakini waziri amebadilisha muelekeo na hataki kusubiri tena! Kwamba watanzania tunaweza 'juisi na maji' tu kwa hakika ni matusi na dharau kubwa kutoka kwa "msomi" huyu. Sijui alikuwa anamrushia kombora RM au hata Bakhresa...! Ngoja tuone sinema itakapoishia!Mkuu, swali hilo amejibu kisanii sana na ametumia muda mwingi kuelezea asiyoulizwa. haya chini ndiyo majibu yake
Kuingizwa kwa vitalu vya madini katika hoja ya gesi
Huo ni upotoshwaji wenye lengo la kututoa kwenye hoja ya msingi ya rasilimali yetu ya gesi. Sijawahi kufanya udalali kwenye vitalu vya madini. Huu ni uongo wa hali ya juu.
Mengi ni mjanja sana alisemaje kuhusu kuhamia digital alisema kama serikali haita rudisha analogue system watafunga vituo vyao sasa ana usemi upi mtoto wa mjini huyo na tapeli
Muhongo anakupotosha mengi aliongea kwa niaba ya wenzake katika kikao rasmi(Tanzania pravate sector foundation)yeye ni mwenyekiti na wapo wafanya biashara wengi tu ktk umoja huo na wala sio kama yeye binafsi>Mfuatilie muhongo vizuri jamaa ana nyodo sana
mkuu binafsi siungani na wewe kwa kiasi fulani hofu yangu ni mitaji ya watanzania mfano benki za tz hakuna benki ambayo inaweza kutoa mkopo wa kutosha kuwekeza kwenye gesi kwani ni mikubwa sana sasa niambie wazawa wataenda kukopa kwa nani.
Kama wageni wanapewa hakuna ubaya kuwapa vipaumbele wazawa.