"Is not natural...The problems of Africa are not natural, but African's problems are natural (therefore the later will have causation effects to the earlier)" (tafsiri isiyo rasmi) Matatizo ya Afrika si ya asili lakini matatizo ya waafrika ni ya asili, kwa hali hiyo uasili wa matatizo ya waafrika yatafanya Afrika iwe na matatizo ya asili.
Nilibishana sana na Professor wangu mmoja Muaustralia alipotoa statement hii darasani yapata miaka takribani 7 iliyopita. Ila leo nitamuandikia email kumuomba radhi na kumkubalia.
Kama mtu aitwaye Professor tena Professor mwenye research interests zinazohusiana na resources ametoa sababu hizi, basi Afrika hususan Tanzania itakuwa tuna tatizo kubwa sana kwenye medula oblangata zetu!!!!!. Dunia nzima Oil na Gas hazina ushindani katika kutafuta mwekezaji. Toka lini ulisikia soko la petrol au gesi limekosekana au limetetereka kutokana na maendeleo ya utandawazi na biashara? Gas na Oil zimo katika kundi la rasilimali zijulikanazo kama "strategic natural resources" kwamba nchi ikiwa nazo inaweza kujidai nazo na kuwa na nguvu ya ziada ya kuingia katika mikataba ya uwekezaji wake. Si uwekezaji katika kilimo cha Pamba huu ambao utasema kesho waweza kusikia bei imeshuka kwasababu ya uwepo wa fibre clothe! Atakuwa ni Professor wa ajabu sana kama hajui kwamba sekta hizi hazina haja ya kushindania kuwahi, ni sekta zinazopingana na ile "earlier the better" zenyewe "the earlier the loser, the late the winner".
Pia anaposema Sheria/sera ya mwaka 1960 inaweza ku-affect na kuwa justifiable policy kwa mwaka 2013, zaidi ya nusu karne, huyu atakuwa alilewa wakati anatoa hizi sababu au? Kweli Professor unatetea sera inayohusiana na masuala ya biashara ya mwaka 1960??, wakati leo Sera za Biashara pekee ni lazima zifanyiwe review kila baada ya miaka 2-6.
Kuhusu, sababu ya tatu ndio kabisa kama hali ingeruhusu ingetosha kumvua hata U-profesa wake. Ni nchi gani duniani iliyoendelea bila kuwa na wawekezaji wa ndani? Ipi hebu Profesa atutajie moja tu. Kwa kweli ni hatari,
Nadhani, TPSF ikiwa pamoja na Dr. Mengi, wasiishie kulalamika kwenye media pekee, kama Muhongo amekataa kukutana nao, mteule wa Muhongo ni Mhe. Rais, waombe kukutana na Mheshimiwa Rais na wamueleze kusudio na madhumuni yao juu ya hoja wanayoisimamia kuhusu Gesi na Mafuta. Tanzania ikipoteza kupata maslahi mazuri kupitia Gesi, ijiandae kwa endless civil riots huko usoni. Hiki kizazi cha leo hakitakubali kutembea barabarani huku wageni na wachache wakiwarushia maji machafu ya mvua kupitia mabenzi yao. Whats wrong with African Leaders?