Majibu ya Reginald Mengi juu ya Gesi kwa Profesa Muhongo

Majibu ya Reginald Mengi juu ya Gesi kwa Profesa Muhongo

Nchi yetu inakila kitu na ni vyema kuwaheshimu wazawa hawa ndio nadhani wenye uchungu na Tanzania kuliko kuwapa kipaumbele wageni tu.
Nyie tena? Si mwenzio alisema kama una uchungu ukazae! "Lusinde - Arumeru"!
 
m nimekerwa na huyu profesa feki mwenye dharau kiasi naogopa kumtaja bure nkapigwa ban mana nna hasira naye vibaya..,
 
muhongo ana nyodo sana mzee huyu.,lakini serikali ina historia ya kuwanyima biashara wazawa hasa wale wasioendekeza rushwa za 10%(rejea kempinski kati ya mengi na masilingi).
hivi kile kiwanja alichokuwa ajenge ipp house kesha jenga? na kipo?
Hivi NIco na Tol zinaendeleaje?
mkitaka mambo ya uzawa inabidi turudi kwenye sera za Nyerere aliye ona kwa wakati ule hakuna mtanzania anayeweza kumiliki viwanda na migodi akaanzisha Stamico, ndc na kadhalika, ili huyu mtanzania akiwa tayari basi wanaweza uziwa shares, mpaka sasa hivi sijamuona mtanzania anayeweza hicho zaidi ya pa kodi, epa, madawa ya kulevya, na ku inflate prices.
 
haya mkuu hayo madini yameshatoka huko chini mashimo ya kutosha! umeona faida yake kwa watanzania? ndo maana watu tunalilia sera ya vitu kama hivi ili kila mtanzania aweze kuona kile kinachopatikana kutoka kwenye hizi natural resources!
ukinisoma vizuri kwenye hiyo hiyo quote, na mimi ndo ninacholilia.
nalilia kuwa na viongozi waadilifu ambao watasaidia nchi.
Unafikiri hao waliopo hawajui la kufanya ili nchi iwe pazuri? wanajua ila wametawaliwa na ubinafsi.
hata tuwe na sera gani, kama hatutakuwa na viongozi waadilifu basi tutaishia hapa hapa.
 
Mengi na wewe unaingia kwenye siasa nini, mbona kila siku malumbano na wanasiasa.

Nadhani umeshindwa kuona mantiki ya huyu Mzee! Prof Muhongo ni sawa kabisa na mbumbu wengi nchini ambao wakimwona mzungu wanaamini anajua kila kitu, na wako tayari wampe kila kitu hata kama itaamaanisha wao walale na njaa! Nenda mawirani uone ni nani anapewa kandarasi/consultancy tenders- ni watoto mafailia wa kizungu! Wakifika nchini wanatuajiri sisi na kutafanyiza kazi kwa ujira mdogo sana na tunachekelea.

Kwenye hizi biashara za madini ndio usiseme kabisa. Onyo: Unapofanya biashara na kampuni kubwa kama British Gas au StartOil - makampuni yaliyobobea katika biashara hio, waliofilisi wajanja wa Nigeria tena wasomi wakina Obi na kuwaua wale vichwa nazi (Kero-Saro Wiwa) ambao walijitolea kuwaonyesha wanigeria njia ya kunufaika na raslimali asili- ni lazima uwe mwangalifu. Kuwa na sera na sheria kabla ya kuanza nao biashara ni kinga kubwa. Muhongo alilifahamu hili hadi majuzi alipokolezwa na kuununua umbumbu ule ule - uliotufanya tukauza nchi zetu kwa wakoloni kwa shanga!

Muhongo- please stay away from us and stop raising fingers at our beloved nationalist Reginald Mengi!
 
ndo maana huwa napenda kusisitiza mara kwa mara, tuwaache wataalamu wawe wataalamu.... siyo lazima kila mtaalamu awe mwanasiasa.... tunaua maendeleo ya nchi....
Prof. Muhongo anaheshimika sana ndani na nje ya nchi katika maswala hayo hayo ya madini na gesi, sasa hivi anaonekana ni wale wale tu (kasoro tarehe).
Uongozi ni zaidi ya kuwa mtaalamu wa kitu fulani....
Nikiangalia hili swala kwa angle nyingine ninaona inawezekana wananchi hawamuelewi Prof. Muhongo kutokana kuzoea utendaji wa chini sana wa kisiasa kutoka kwa wanasiasa wengine waliopita na waliopo ambao hauna malengo na ufanisi wa kutosha.

Labda pia no nonsense approach yake ambayo wananchi wengi hawakuidhoea kuisikia na kuiona kutoka kwa wanasiasa wengine waliopita na waliopo wanaiona kama ni dharau na kejeri.

Mimi nadhani pia wanasiasa kutokuwa wawazi sana katika utendaji wao wa kila siku unasababisha manung'uniko mengi kutoka kwa wananchi ambapo mengine yanaweza yakawa yanasababishwa na ukosefu wa information kwenye eneo la kitendaji wanalolilalamikia.

Inawezekana wananchi pia hawajitadhimini na kujiweka katika mazingira ya mabadiliko kifikra na kimtazamo.

Kuna connection inakosekana kati ya wanansiasa na wananchi.
 
Mengi aspoangalia atajipiga risasi mguuni, mie subirini hivi hivi.

With 3k+ sq km?
 
Mengi na wewe unaingia kwenye siasa nini, mbona kila siku malumbano na wanasiasa.
Ndugu zangu watanzania tumelogwa?

Mbona unazungumza kama wale watu wanaosema "mimi sitaki siasa" lakini wakati huo huo analalamika kijijini kwake hana maji, barabara mbovu, shule hazina madawati, askari wanawaonea watu, wawekezaji wanachukua ardhi kiholela, na mambo chungu nzima yanayohusu maisha yake ya kila siku. Wakati huo huo anamlaumu diwani, mbunge, na rais wake.

Kifupi ni kwamba hatuwezi kuzungumzia maisha yetu ya kila siku bila kuyahusisha na siasa. Siasa ni viongozi ni watendaji wote ambao aidha wanatusababishia kero au kutuondolea kero. Kwa hali hiyo Mengi kama walivyo wanaharakati wengine amepiga kengele kwamba wazalendo wasiachwe kwenye swala Zima la rasilimali zetu.

Leo hii Watanzania wote wanalia jinsi wanavyotengwa katika umiliki wa rasilimali zao ziwe kwenye ardhi, madini nk. Hakuna sera bayana zinazompa upendeleo Mtanzania. Na kwa makusudi sera hazitayarishwi kwa kuwa Watanzania wakipewa upendeleo hawataweza kutoa rushwa kama inayotolewa na wawekezaji wa nje. Inawezekana ikawa ni kweli itakua taabu kwa mzalendo kuendesha kitalu cha gesi. Lakini si uwape angalau viwili vitatu uone kama wataweza? Vipi unawajudge kabla? Hata kama watavilangua kama waziri anavyohofu bado watakua na hisa kwa huyo mwekezaji wa nje atakae nunua.

Na hilo si ndilo tunalotaka kwamba ikiwezekana penye kila mwekezaji wa nje pawe na mtanzania mwenye hisa? Sasa roho ya korosho imetoka wapi tena? Kumhusisha Mengi na siasa za Chadema wapi na wapi? Kwani ni uongo waziri Muhongo alipochukua tu madaraka alilaani sana mikataba mibovu na iliahidi kutorudia makosa kama ya wenzake waliomtangulia? Kwani ni uongo aliahidi hatagawa vitalu kabla hajaandaa sera ya madini? AKANUSHE. Why the sudden U turn?

Watanzania tuwe wamoja kwenye maswala ya kutetea rasilimali zetu na kupewa kipaumbele. Tusiwe ndumila kuwili. Tusiache viongozi na watendaji wakatuchimbia kaburi. Katika kufanya hivyo tusiache fikra za mimi ni ccm mimi ni chadema zikatutawala.
 
muhongo ana nyodo sana mzee huyu.,lakini serikali ina historia ya kuwanyima biashara wazawa hasa wale wasioendekeza rushwa za 10%(rejea kempinski kati ya mengi na masilingi).

Nimeandika sana humu hili ila mods wenye ugonjwa na kila kitu changu wapo busy kutoa kila thread....Hili gubu kw angozi nyeusi ndilo linatupeleka Congo...maCCm yenyewe yakiwepo 10% yanakuwa loosers mara tuu 10%ikikata.

Wazawa wenye rangi nyingine hata wakizaliwa interior singida, igunga, kilosa, kimamba, sumbawanga...ma CCM watajichekesha na kuwapa deal..
 
Du muhogo kweli ana wivu wa kike.au ana nanihii mbili?au uprofesa wake kama wa waganga wa kienyeji?
 
Kwanini Muhongo hajifunzi uhaini wa uchumi alioufanya Mkapa kwa madini yetu kunyonywa na wa-SA? Kweli ukitaka jua rangi halisi ya mtu mpe MADARAKA au FEDHA. Anashusha hadhi ya level ya uProfessor wake.
 
Kwenye hili Mengi amechemka anatumia Tpsf kuwasilisha mahitaji yake.
 
katika mambulula we ndo wa kwanza badala uunge mkono gesi ye2 isiende kwa wageni we una mpond R.mengi...alaf ujaxom hp juu alivy jb hajawai kushikilia vitalu vya madini

mkuu hili ni jibu jepesi kwa swali gumu,mengi ajibu kwa kina juu ya vitalu vya madini.hamna jkibu hapo kwa wenye akili.
 
Mengi na wewe unaingia kwenye siasa nini, mbona kila siku malumbano na wanasiasa.

aisee umchnag karata kabla ya kuzisoma nini?hembu ziweke vizuri....Wanasiasa ndio wapo obsessed na mengi...wengine wanatumiwa na wapinzani wa mengi haswa wenye asili ya kiasia kwani akina mfuruki hawana muda wala nia ya kupiga vita wabongo wenzao.

Siku zote CCM hawapo at easy na Mengi..mengi akiingia ktk rushwa kelele zao zitaisha...wanamzushia mara Natumia media zake vibaya....,mara kaua Nico, mara anakwepa kodi, mara yupo upinzani, mara sijui anapiga vita uislam, mara sijui hafai yanga, etc......mara ana ukabila...ni vi zoezi vidogo vya CCM.

mengi kashikilia Vitalu?mengi anachimba Tanzanite na kui process hadi mwisho kabla y akuiza nje, hauzi km wahuni wanaopeleka raw nje.....kwa taarifa yao Mengi hayauzi madini hovyo anayaweka tuu kwa ajili ya future wakati madini yatakuwa yamepungua km si kuisha..Akianza kuuza nadhano mohongo na statistics za forbes zitabadilika...ghafla ndio hawa wanasiasa na wasomi wetu wasio na akili watakapofungua mdomo .....
 
Hao wazungu ni proxy tu. Wenye vitalu ni wanasiasa na wenye nchi. Wanafloat stocks, share na bonds nchi za nje na mabenki makubwa ya kimataifa kwa kupitia hivyo hivyo vitalu wanapata fedha ya uchimbaji wanapata faida wanarudisha cha watu wanatulia huku wakila kuku kwa mrija. Vingine utasikia vya akina Obama na Bush. Its good business na ndio maana watu wanapigana vikumbo aliyeshika mpini ndio mwenye jeuri, aliyeshika makali anatafuta public sympathy. Lakini njia za utafutaji ni zilezile
 
Dk Mengi, achana na huyu Muhongo. Bila shaka haelewi nini maanaya kuwawezesha wazawa, maana hata hao wawekezaji wanaokuja nchini huja bila hata seenti, hukopa hukonje na wakati mwingine umuhumu nchini. Watanzania wasingependa uendelee kulumbana na hawa mabwanyenye wetu, wana matatizo makubwa. Tungependa iwepo ofauti kati yako na Pof Mhongo. Hilo waachie Watanzania.


Duniani kuna watu wawili tu waliobarikiwa na waliolaaniwa. Na wote utawajua kwa fikra na matendo yao hata nchi vilevile. na jambp baya kuliko lote ni mtu yule asiyewaheshimu wazazi, mzazi wetu ni tanzania na mali zake basi kuishi kudumu kwetu kuna walakini. Basi tuna tofauti gani na wapumbavu watapanyao mali ya urithi kwa sifa za Bar. TAFAKARI.
 
Historia nayoifahamu ni kwamba kiongozi wa unaposhindana na wawekezaji wa sampuli ya mzee Mengi inabidi ujiandae ...Muhongo inabidi amuulize Masilingi na Masha mziki wa watu kama hawa wanapoamua kukushughulikia unakuwaje . Namwonea huruma sana prof Muhongo kwa stement zake tokea Mtwara saga
 
Back
Top Bottom