Majibu ya Prof Mwandosya kwa Zitto

Majibu ya Prof Mwandosya kwa Zitto

Majibu ya Mwandosya ni ya kishikaji hayana uzito kabisa kwa kiongozi alokuwa madarakani akisimamia vyombo hivyo. Ukimsoma kwa makini utaelewa kwamba anaruka majukumu kwa kisingizia mfumo wa Ubinafsishaji.

Jambo moja ambalo hakulielewa ama kulielezea vizuri ni upinzani baina ya ACT na CCM kisera katika Ubinafsishaji ambao ulipelekea kuharibika kabisa kwa mashirika hayo. Hivyo anaposema kimfumo mashirika hayo yalionekana mzigo kwa taifa kwa kugharamiwa na kwamba serikali haikuwa na uwezo huo! lakini laa ajabu ni kwamba hata baada ya kubinafsishwa chini yake, mashirika hayo yameigharmu serikali mara dufu ya gharama za uendeshaji. Chukulia IPTL imetugharimu kiasi gani. Haya Ubinafsishaji wa TTCL inaitupiamlawama PCRC lakinimaamuzi ya kubinafsishwa kupitishwa na serikali yake.

Jambo jingine anazungumzia PCRC kama chombo huru wakati anasema tena kilikuwa chini ya Rais, ni Uhuru upi anaozungumzia hapa. Hivi kweli Mwandosya anataka tuamini kwamba yeye hakufanya kosa lolote isipokuwa ni mfumo na sera za chama chake ila tuyatazame mazuri yake ya vyombo alivyoanzisha kama TCRA, SUMATRA, TCAA na EWURA ambavyo hakuonyesha mafanikio yake ila uanzilishi wa vyombo hivyo.

Swala la ATC na TRC kusema kweli ni aibu hata kulizungumzia kwa sababu mashirika haya yalikuwepo toka enzi ya Nyerere na yakifanya kazi kama alivyojielezea. Kama ameacha shirika la ndege lina Boeng 2 na fokker 2 ambazo zimenunuliwa toka mwaka 1975, anajaribu kujenga hoja gani hapo? ya kwamba yeye aliweza kuzitunza ndege hizo ama kazi yake ilikuwa kuliendeleza shirika hilo pamoja na Reli yalokufa vibaya vibaya. Au lengo lake ni kutuonyesha kwamba kosa sio lake ila la watawala walokuwa juu yake...
Mkuu Mkandara, hawa jamaa ni wahuni tu. Walikuwa na sababu gani kuuza benki (NBC), Kiwanda cha sigara, Kampuni ya pombe TBL...mashirika yaliyokuwa yakijiendesha kwa tija! Hapa prof. anaimba wimbo wa kipumbavu na kushangiliwa la watu wanaomchukia Zito.
 
CCM pitisheni basi wagombea kama hawa basi, maana ili nchi kupata viongozi bora inatakiwa vyama kwanza vipitishe viongozi wenye uafadhali na kwa CCM mwandosya ni mmoja wao!
 
Kama wengi tulivyosikia jana, kuna tuhuma hizi hapa chini ambazo zilitolewa jana na Zitto Kabwe na kuandikwa na vyombo vingi vya habari leo.

HOJA YA ZITTO

Zittokabwe
: Prof. Mark Mwandosya aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wakati wa uongozi wa Rais Benjamin Mkapa. Mashirika yote ya Umma , takribani, katika Wizara hii yaliyobinafsishwa zoezi la ubinafsishaji liligubikwa na tuhuma za ufisadi na hata kuchukuliwa upya na Serikali.

Shirika la Ndege la Taifa lilibinafsishwa chini ya Mwandosya na likafa. Kitengo cha makontena katika Bandari ya Dar Es Salaam kilibinafsishwa kipindi hiki na kuleta maneno mengi sana. Mchakato wa kubinafsisha Shirika la Reli pia ulianza kipindi hiki. Ubinafsishaji ulioleta maneno mengi zaidi ulikuwa ni wa Kampuni ya simu ( TTCL) kwa MSI detecon na Celtel International.

Prof. Mwandosya binafsi alipata tuhuma na mtoto wake kusomeshwa na watu waliouziwa kampuni hii kwa bei ya chee. Masuala haya yaliandikwa na vyombo vya habari miaka ya kati ya 2001 na 2005. Prof. Hana budi kufafanua haya mbele ya umma ili kujiridhisha na uwezo wake wa kupambana na rushwa na ufisadi.

MAJIBU YA PROF MWANDOSYA

Zitto, Salaam.

Hongera pia kwa kuwa kiongozi wa ACT na hongera kwa kazi kubwa unayoifanya kueneza itikadi ya Chama chako. Ni jambo zuri katika kukuza demokrasia ya nchi yetu na hasa kukuza uzalendo. Siku zote nimekuelezea kama kijana ambaye hakika utakuwa tegemeo la Taifa letu, na hili nimekuambia mara nyingi. Nimeona vema nifafanue yale ambayo umeyataja katika post yako.

Niliyatolea maelezo ya kina miaka mingi iliyopita lakini nadhani utafiti sio moja ya maeneo tuliyo na nguvu nayo kwa hiyo umeyafukua bila kuyafanyia utafiti au kutaka upate ufafanuzi kutoka kwa mhusika.

Nianze na hili la ubinafsishaji kwa ujumla wake. Inawezekana ulikuwa badi shule, pamoja na nia njema ya kuanzisha mashirika ya umma, hatimaye yalikuja kuwa mzigo mkubwa kwa hazina yetu, maana yake kwa wananchi. Asilimia kubwa yalitegemea ruzuku ya serikali na baadhi yalikuwa mufilisi. Teknolojia ilikuwa imebadilika sana na ili kuyafungua ingeigharimu serikali na umma wa Tanzania kiasi kikubwa sana. Uchumi wa nchi wakati ule usingeweza kubeba mzigo huo. Ndipo Chama, wakati ule kiliporidhia Serikali ibakie na shughuli zake za msingi za Utawala, Ulinzi na Usalama, na Usimamizi wa ujumla wa uchumi.

Maamuzi yafuatayo yakachukuliwa:

Kwa upande wa shughuli za serikali zenye sura ya kibiashara, idara husika zikageuzwa kuwa wakala wa serikali, zikifanya kazi kwa uhuru zaidi chini ya Bodi zao. Kuhusu mashirika na kampuni za umma ilikubalika zirekebishwe na hatimaye zibinafsishwe. Ndipo kilipoundwa chombo maalum kisheria kilichokuwa na mamlaka kamili ya kubinafsisha
Mashirika ya umma.

Chombo hiki, Parastatal Sector Reform Commission (PSRC) kilikuwa chombo huru kikiwa chini ya Ofisi ya Rais, Mipango. Kiliwekwa hapo kwa sababu mamlaka yake yalikuwa Mtambuka, na vyombo husika vilikuwa kwenye sekta mbalimbali. Kwa hiyo sekta husika na Wizara husika, pamoja na kuitwa PSRC wakatii wa majadiliano yaliyohusu mashirika yake, hazikuwa na mamlaka ya kisheria kuhusu ubinafsishaji. Ni vema hili likaeleweka.

Pamoja na hayo, nirudie ufafanuzi kuhusu ubinafsishaji wa TTCL, nafanya hivyo kutokana na dhana ya uwajibikaji wa pamoja, ikumbukwe kwamba maamuzi ya ubinafsishaji wa TTCL yalifikiwa na PSRC mwaka mmoja kabla Waziri Mwandosya hajaingia siasa! Hata hivyo suala kubwa ni mabadiliko ya teknolojia tu. TTCL ilikuwa imejikita zaidi kimfumo na kiteknolojia katika teknolojia ya analogue na land lines.Mfumo wate,kiutawala na kiteknolojia ulikuwa katika msingi huo. Teknolojia ya simu za mkononi, na ushindani uliojitokeza ndio hasa changamoto kubwa ya TTCL.

Hata hivyo mabadiliko makubwa na maendeleo makubwa katika TEHAMA yamepelekea Tanzania kuwa mbali na kuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingi za Afrika. Katika mawasiliano Tanzania imekuwa 'Mecca' na wengi wamekuja kujifunza tumewezaje kufanikiwa. Namshukuru Rabuka kwa kuniwezesha kutoa mchango wangu katika maendeleo ya sekta hii. Na ili kuhakikisha kwamba mlaji au mtumiaji wa huduma za kiuchumi hahujumiwa na wakati huo huo mtoa huduma au mwekezaji ana uhakika wa kufaidika na kuweza kutoa huduma endelevu,ndipo vilipoanzishwa vyombo vya udhibiti wa huduma za kiuchumi, Regulatory Bodies. Nimebahatika kuwa Waziri pekee mwanzilishi na msimamizi wa TCRA, SUMATRA,TCAA, na EWURA.

Nimeelezea kuhusu mfumo wa ubinafsishaji hivyo basi ninachoweza kufafanua ni kwamba nilipomaliza muda wangu kama Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, niliacha Shirika la Reli likisafirisha tani laki tisa za shehena kwa mwaka, safari za abiria kwenda Tabora kutoka Dar zilikuwa kila siku, na ATC ilikuwa na ndege mbili aina ya Boeing 737 na mbili aina ya Fokker Friendship.

Tuhuma za mtoto wa Profesa kulipiwa na kampuni moja ya simu hazina chembe yoyote ya ukweli Bwana Zitto. Mtoto ambaye alifuzu uhandisi wa mawasiliano ya simu aliomba kazi ya muda na akapewa.
Kampuni husika ilikanusha tuhuma hizo ambazo zilitolewa wakati wa mchakato wa kugombea uteuzi katika CCM kwa nafasi ya kuwa mgombea wa Urais mwaka 2005. Sasa zinafufuliwa tena na Bwana Zitto wakati wa mchakato huo huo mwaka 2015! Inaeleweka.

Namalizia kama nilivyoanza, Zitto ni mwanasiasa ninayemheshimu sana. Mara nyingi naye amenitambua kama mwanasiasa wa kuigwa (role model). Lakini katika siasa tunasema saa 24 ni kipindi kirefu sana, na huwa tunabadilika!
Ushauri wangu kwake ni kwamba siku zote kabla hujahukumu sikiliza upande wa pili, kwa kilatini hii ni dhana muhimu inayojulikana kama AUDI ALTERAM PARTEM.

Pili ni vema ukazingatia zaidi mambo chanya ya msimamo na itikadi ya ACT. Lakini katika kushauri hivyo natambua kwamba " Akili ni nywele, kila mtu ana zake"

Ramadhan Kareem. Wakatabahu,

Mwandosya
.
Zitto anaonekana kikaragosi anayetumiwa kumchafua Prof kwa mambo ambayo ni uongo uliotungwa.

Uongo huo ulitumgwa na wana mtandao mwaka 2005 na kusambazwa magazetini.
Kwamba 10 years later Zito bado hajaelewa kuwa ameingizwa mkenge ineleza sana juu ha umakini na intelligence yake.
Aidha Zitto anatumiwa, kama tuhuma zinavyosikika, na mgombea mmoja wa urais aliyekuwa kundi la mtandao.
Huyo mgombea ndio anasemekana ana fadhili ACT.
 
Hivi unamjua au unajisemea?
Waambie wapambe wake akina MADODI, wamlete hadharani, watu wakamue jipu

Usikwepe, ulilolisema hapa halihusiani na Madodi hivyo ata hukuwa na sababu ya kumtaja.

Jibu swali dogo tu hili kama kweli wewe sio mtunzi wa hadithi,otherwise tusipende kuchafua watu kwa uongo.

Wakati unasema hajajibu lolote lakini nawe hujauliza lolote.

Ni kampuni ipi aliyokuwa nayo Mwandosya na Prof Luhanga?ilikuwa inajishughulisha na nini na ilipewa tender wapi?

Ni wapi ambako alifanya huo ukabila wake?sijawahi kabisa kulisikia hili kwenye utendaji wake.

Ngoja nikusaidie kidogo, hivi katika taasisi ambazo Prof Mwandosya alizianzisha akiwa waziri,yaan EWURA, SUMATRA, TCRA, na TCAA, je kuna Mkurugenzi Mkuu yeyote aliyeteuliwa wa kabila lake kwenye mashirika hayo?je vip kuna wenyeviti wa bodi wa kabila lake aliowateua?Yombayomba acha utunzi wa hadithi.
 
Majibu ya Mwandosya ni ya kishikaji hayana uzito kabisa kwa kiongozi alokuwa madarakani akisimamia vyombo hivyo. Ukimsoma kwa makini utaelewa kwamba anaruka majukumu kwa kisingizia mfumo wa Ubinafsishaji.

Jambo moja ambalo hakulielewa ama kulielezea vizuri ni upinzani baina ya ACT na CCM kisera katika Ubinafsishaji ambao ulipelekea kuharibika kabisa kwa mashirika hayo. Hivyo anaposema kimfumo mashirika hayo yalionekana mzigo kwa taifa kwa kugharamiwa na kwamba serikali haikuwa na uwezo huo! lakini laa ajabu ni kwamba hata baada ya kubinafsishwa chini yake, mashirika hayo yameigharmu serikali mara dufu ya gharama za uendeshaji. Chukulia IPTL imetugharimu kiasi gani. Haya Ubinafsishaji wa TTCL inaitupiamlawama PCRC lakinimaamuzi ya kubinafsishwa kupitishwa na serikali yake.

Jambo jingine anazungumzia PCRC kama chombo huru wakati anasema tena kilikuwa chini ya Rais, ni Uhuru upi anaozungumzia hapa. Hivi kweli Mwandosya anataka tuamini kwamba yeye hakufanya kosa lolote isipokuwa ni mfumo na sera za chama chake ila tuyatazame mazuri yake ya vyombo alivyoanzisha kama TCRA, SUMATRA, TCAA na EWURA ambavyo hakuonyesha mafanikio yake ila uanzilishi wa vyombo hivyo.

Swala la ATC na TRC kusema kweli ni aibu hata kulizungumzia kwa sababu mashirika haya yalikuwepo toka enzi ya Nyerere na yakifanya kazi kama alivyojielezea. Kama ameacha shirika la ndege lina Boeng 2 na fokker 2 ambazo zimenunuliwa toka mwaka 1975, anajaribu kujenga hoja gani hapo? ya kwamba yeye aliweza kuzitunza ndege hizo ama kazi yake ilikuwa kuliendeleza shirika hilo pamoja na Reli yalokufa vibaya vibaya. Au lengo lake ni kutuonyesha kwamba kosa sio lake ila la watawala walokuwa juu yake...
Ni ajabu na masikitiko makubwa katika jukwaa la siasa (na sio Chit Chat) watu wanashangilia delivery ya majibu na jinsi ya kujibu na vijembe na sio kilichopo kwenye majibu...

Hata kama aliyeuliza ni Mnafiki na hafai na Mwongo na ametumwa..., who cares kama alichouliza kinahitaji majibu stahiki ?, Kweli kwa mtaji huu bado tuna safari ndefu ambayo huenda hata vitukuu vyetu hawatafika endapo hatutabadilika. Kwa mtazamo wangu Prof na maelezo marefu ila hakuna majibu yenye substance..
 
Tanzania hamna upinzani tunajidanganya huyu Prof Mwandosya leo amekuwa shujaa wa Chadema.
 
Wewe umewahi kumsikia kiongozi gani wa Upinzani akimshutumu Lowassa kwa Kashfa ya Ufisadi moja kwa moja katika mihadhara? ukiacha Mwakyembe, Makongoro Nyerere, Nape na Wasira! Tuseme ukweli nani alowahi kumtaja Lowassa wazi wazi toka list ya Mafisadi..Ya Richomnd, Chadema wote wamebadilika wanaamini hilo ni deal la JK au leo mmebadilika..

Wewe nae acha porojo,Mbona wote wanamtaja tu?.Tuanzie Arusha jirani mbona G.Lema alimtaja nakuwaambia wananchi kwamba kumzomea fisadi ni baraka kwa Mungu?.Au umeingia kwenye mambo haya jana?
 
Zitto unazidi kujishushia heshima kila siku malipo hapa duniani dhambi ya usaliti itazidi kumtafuna maisha yake yote bora aache siasa kila anapogusa ni moto tuu.
 
Nimeyapenda sana majibu ya Prof Mwandosya, bila kujali kama yapo sahihi au lah!
Yaani mpangilio tu metulia sana, pia madongo aliyompiga Zitto yameenda shule.
 
TTCL ilikuwa imejikita zaidi kimfumo na kiteknolojia katika teknolojia ya analogue na land lines.Mfumo wate,kiutawala na kiteknolojia ulikuwa katika msingi huo. Teknolojia ya simu za mkononi, na ushindani uliojitokeza ndio hasa changamoto kubwa ya TTCL.

na ATC ilikuwa na ndege mbili aina ya Boeing 737 na mbili aina ya Fokker Friendship?

Pamoja na kumheshimu sana Prof hayo mambo mawili ndio yananitia wasiwasi na uwezo wa watawala wetu. Hakueleza changamoto zilishughulikiwa vipi kuhakikisha kuwa TTCL inaendelea kushindana na hasa kwa kuwa soko lilikuwapo na ilikuwa na monopoly kwa upande wa masafa na miundombinu. BT ya UK bado anaendelea kuishi kwa sababu ya hiyo monopoly ya miundombinu ila kawekewa viwango vya ubora vinavyotakiwa kufikiwa ili kuendelea na monopoly. Ki ukweli wanaweza tu kubadili muendeshaji na siyo umiliki wa mitambo! Sioni kama hiyo kweli ilikuwa sababu ya kuiua TTCL. Tatizo letu huwa tunakuwa na nia nzuri bila upeo wa utekelezaji.

Kuhusu ATC ni aibu hizo ndege kutaja kuwa ndio alizoacha na akiamini mrithi wake angeendeleza ATC. Labda aseme hata yeye alikabidhiwa ikiwa taabani and nothing could have been done. Ndege hizo tatu kwa gharama ipi ya uendeshaji? Ingekuwa vizuri, kama alivyosema kuhusu collective responsibility, akakubali udhaifu uliokuwapo na kutuambia kama Rais mtarajiwa ni nini hasa tatizo na atafanya nini kutatua changamoto hizo na siyo kuonyesha kuwa warithi wake ndio waliharibu mambo.
 
zzk, anataka kushindana na mwalimu wake! duh professor kamuonesha kuwa si level zake!
 
MAJIBU YA PROF MWANDOSYA

[/SIZE]Zitto, S

Nianze na hili la ubinafsishaji kwa ujumla wake. Inawezekana ulikuwa badi shule, pamoja na nia njema ya kuanzisha mashirika ya umma, hatimaye yalikuja kuwa mzigo mkubwa kwa hazina yetu, maana yake kwa wananchi. Asilimia kubwa yalitegemea ruzuku ya serikali na baadhi yalikuwa mufilisi. Teknolojia ilikuwa imebadilika sana na ili kuyafungua ingeigharimu serikali na umma wa Tanzania kiasi kikubwa sana. Uchumi wa nchi wakati ule usingeweza kubeba mzigo huo. Ndipo Chama, wakati ule kiliporidhia Serikali ibakie na shughuli zake za msingi za Utawala, Ulinzi na Usalama, na Usimamizi wa ujumla wa uchumi.

MAELEZO HAYO HAPO JUU KWA MWENYE akilli timamu yanatosha kwamba Mwandosya ni kiongozi mwepesi kushindwa, kwa kauli hiyo ya kuogopa ushindani ni ishara kwamba hata viwanda karibu vyote vimekufa kwa sababu ya uoga wa wanaCCM. Pia kwa maelezo hayo ya Mwandosya kuogopa risk, watanzania wasitegemee kufufuliwa kwa viwanda Mwandosya akiwa kocha wa CCM.

Basi Watanzania, tuelewe kwamba mafanikio ya China na kuwa taifa kubwa kiuchumi duniani imetokana na uwezo wa Deng Xiaoping ambaye alilibadili taifa hilo kwa kuboresha mashirika ya umma, kufungua viwanda vipya na kwenda sambamba na mapinduzi ya teknolojia duniani. SASA tuna Mwandosya na wanaCCM wenzake wanaona teknolojia ni adui wa kumkimbia na kutelekeza mashirika ya serikali badala ya kuwa rafiki wa kumkimbilia.

Nimalizie tu, kwa uelewa mdogo na ushabiki wa wanaJF kwa majibu ya Mwandosya na kuyachukulia kijumla jumla bila kushirikisha ubongo, to find if there is any substance in his counterargument, then we are doomed as a nation and overal we lack human potential for the future of this nation.
 
Unajua huyu zitto nikilaza swala alilo mshambulia prof mwandosya nikuto kufikili vizur mbona hakumtaja lowassa ambae ushahidi upo au kwasababu anazamini chama
 
Kama wengi tulivyosikia jana, kuna tuhuma hizi hapa chini ambazo zilitolewa jana na Zitto Kabwe na kuandikwa na vyombo vingi vya habari leo.

HOJA YA ZITTO

Zittokabwe : Prof. Mark Mwandosya aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wakati wa uongozi wa Rais Benjamin Mkapa. Mashirika yote ya Umma , takribani, katika Wizara hii yaliyobinafsishwa zoezi la ubinafsishaji liligubikwa na tuhuma za ufisadi na hata kuchukuliwa upya na Serikali.

Shirika la Ndege la Taifa lilibinafsishwa chini ya Mwandosya na likafa. Kitengo cha makontena katika Bandari ya Dar Es Salaam kilibinafsishwa kipindi hiki na kuleta maneno mengi sana. Mchakato wa kubinafsisha Shirika la Reli pia ulianza kipindi hiki. Ubinafsishaji ulioleta maneno mengi zaidi ulikuwa ni wa Kampuni ya simu ( TTCL) kwa MSI detecon na Celtel International.

Prof. Mwandosya binafsi alipata tuhuma na mtoto wake kusomeshwa na watu waliouziwa kampuni hii kwa bei ya chee. Masuala haya yaliandikwa na vyombo vya habari miaka ya kati ya 2001 na 2005. Prof. Hana budi kufafanua haya mbele ya umma ili kujiridhisha na uwezo wake wa kupambana na rushwa na ufisadi.

MAJIBU YA PROF MWANDOSYA

Zitto, Salaam.

Hongera pia kwa kuwa kiongozi wa ACT na hongera kwa kazi kubwa unayoifanya kueneza itikadi ya Chama chako. Ni jambo zuri katika kukuza demokrasia ya nchi yetu na hasa kukuza uzalendo. Siku zote nimekuelezea kama kijana ambaye hakika utakuwa tegemeo la Taifa letu, na hili nimekuambia mara nyingi. Nimeona vema nifafanue yale ambayo umeyataja katika post yako.

Niliyatolea maelezo ya kina miaka mingi iliyopita lakini nadhani utafiti sio moja ya maeneo tuliyo na nguvu nayo kwa hiyo umeyafukua bila kuyafanyia utafiti au kutaka upate ufafanuzi kutoka kwa mhusika.

Nianze na hili la ubinafsishaji kwa ujumla wake. Inawezekana ulikuwa badi shule, pamoja na nia njema ya kuanzisha mashirika ya umma, hatimaye yalikuja kuwa mzigo mkubwa kwa hazina yetu, maana yake kwa wananchi. Asilimia kubwa yalitegemea ruzuku ya serikali na baadhi yalikuwa mufilisi. Teknolojia ilikuwa imebadilika sana na ili kuyafungua ingeigharimu serikali na umma wa Tanzania kiasi kikubwa sana. Uchumi wa nchi wakati ule usingeweza kubeba mzigo huo. Ndipo Chama, wakati ule kiliporidhia Serikali ibakie na shughuli zake za msingi za Utawala, Ulinzi na Usalama, na Usimamizi wa ujumla wa uchumi.

Maamuzi yafuatayo yakachukuliwa:

Kwa upande wa shughuli za serikali zenye sura ya kibiashara, idara husika zikageuzwa kuwa wakala wa serikali, zikifanya kazi kwa uhuru zaidi chini ya Bodi zao. Kuhusu mashirika na kampuni za umma ilikubalika zirekebishwe na hatimaye zibinafsishwe. Ndipo kilipoundwa chombo maalum kisheria kilichokuwa na mamlaka kamili ya kubinafsisha Mashirika ya umma.

Chombo hiki, Parastatal Sector Reform Commission (PSRC) kilikuwa chombo huru kikiwa chini ya Ofisi ya Rais, Mipango. Kiliwekwa hapo kwa sababu mamlaka yake yalikuwa Mtambuka, na vyombo husika vilikuwa kwenye sekta mbalimbali. Kwa hiyo sekta husika na Wizara husika, pamoja na kuitwa PSRC wakatii wa majadiliano yaliyohusu mashirika yake, hazikuwa na mamlaka ya kisheria kuhusu ubinafsishaji. Ni vema hili likaeleweka.

Pamoja na hayo, nirudie ufafanuzi kuhusu ubinafsishaji wa TTCL, nafanya hivyo kutokana na dhana ya uwajibikaji wa pamoja, ikumbukwe kwamba maamuzi ya ubinafsishaji wa TTCL yalifikiwa na PSRC mwaka mmoja kabla Waziri Mwandosya hajaingia siasa! Hata hivyo suala kubwa ni mabadiliko ya teknolojia tu. TTCL ilikuwa imejikita zaidi kimfumo na kiteknolojia katika teknolojia ya analogue na land lines.Mfumo wate,kiutawala na kiteknolojia ulikuwa katika msingi huo. Teknolojia ya simu za mkononi, na ushindani uliojitokeza ndio hasa changamoto kubwa ya TTCL.

Hata hivyo mabadiliko makubwa na maendeleo makubwa katika TEHAMA yamepelekea Tanzania kuwa mbali na kuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingi za Afrika. Katika mawasiliano Tanzania imekuwa 'Mecca' na wengi wamekuja kujifunza tumewezaje kufanikiwa. Namshukuru Rabuka kwa kuniwezesha kutoa mchango wangu katika maendeleo ya sekta hii. Na ili kuhakikisha kwamba mlaji au mtumiaji wa huduma za kiuchumi hahujumiwa na wakati huo huo mtoa huduma au mwekezaji ana uhakika wa kufaidika na kuweza kutoa huduma endelevu,ndipo vilipoanzishwa vyombo vya udhibiti wa huduma za kiuchumi, Regulatory Bodies. Nimebahatika kuwa Waziri pekee mwanzilishi na msimamizi wa TCRA, SUMATRA,TCAA, na EWURA.

Nimeelezea kuhusu mfumo wa ubinafsishaji hivyo basi ninachoweza kufafanua ni kwamba nilipomaliza muda wangu kama Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, niliacha Shirika la Reli likisafirisha tani laki tisa za shehena kwa mwaka, safari za abiria kwenda Tabora kutoka Dar zilikuwa kila siku, na ATC ilikuwa na ndege mbili aina ya Boeing 737 na mbili aina ya Fokker Friendship.

Tuhuma za mtoto wa Profesa kulipiwa na kampuni moja ya simu hazina chembe yoyote ya ukweli Bwana Zitto. Mtoto ambaye alifuzu uhandisi wa mawasiliano ya simu aliomba kazi ya muda na akapewa.Kampuni husika ilikanusha tuhuma hizo ambazo zilitolewa wakati wa mchakato wa kugombea uteuzi katika CCM kwa nafasi ya kuwa mgombea wa Urais mwaka 2005. Sasa zinafufuliwa tena na Bwana Zitto wakati wa mchakato huo huo mwaka 2015! Inaeleweka.

Namalizia kama nilivyoanza, Zitto ni mwanasiasa ninayemheshimu sana. Mara nyingi naye amenitambua kama mwanasiasa wa kuigwa (role model). Lakini katika siasa tunasema saa 24 ni kipindi kirefu sana, na huwa tunabadilika!Ushauri wangu kwake ni kwamba siku zote kabla hujahukumu sikiliza upande wa pili, kwa kilatini hii ni dhana muhimu inayojulikana kama AUDI ALTERAM PARTEM.

Pili ni vema ukazingatia zaidi mambo chanya ya msimamo na itikadi ya ACT. Lakini katika kushauri hivyo natambua kwamba " Akili ni nywele, kila mtu ana zake"

Ramadhan Kareem. Wakatabahu,

Mwandosya.​

chanzo mwanahalisi online
 
Back
Top Bottom