Majibu ya Prof Mwandosya kwa Zitto

Majibu ya Prof Mwandosya kwa Zitto

Wewe una akili sana,
Nakumbuka Mwandosya aliongea tena akasema kuhusu nawewe kupata gawiwo.Kwa mazngira yaliyopo wala usiongelee chochote wakati wa majimuisho Bwana mdogo maana tulushajua ukweli ukowapi....

Lengo lilikuwa ni kusema kuwa ilionesha Zitto alipata chochote kitu kwenye issue za escrow lakin,kwa kaz aliyokuwa kaifanya kulikiluwa mazngira ya kushindwa kuipata hio hela..
Pamoja na akina Ngereja kumtaka Zitto.aseme nayete gawiwo alilopata Mwandosya alimuomba Zitto asilitolee maelezo...

Lakin leo Zitto anamchokonoa mzee wawatu ili tu Lowasa wake aonekane msafi...


Zitto mnafiki mkubwa sana


Hela za ufisadi za Lowassa na genge lake zinawatoa watu ufahamu kabisa. Wakati mwingine unabaki unajiuliza ni huyu huyu au mwingine ?
 
Mbavu zangu leo pro-Chadema wanatetea majibu ya mwana CCM mpaka povu linawatoka.
Ndio maana nilimwabia JokaKuu kwamba Chadema hawakupiga mahesabu vizuri, hawa jamaa ni kama upepo wanageuka wakati wowote hawaaminiki..Halafu basi sababu ya utetezi wao inaweza kuwa ya kijinga kabisa!
 
Last edited by a moderator:
Zitto aliomba majibu kapewa.

Uungwana ni kuwasiliana na aliyetoa majibu one on one na kusafisha hali ya hewa. Then kutolea tamko kama amekubali maelezo au anadhani Prof. amepindisha mambo.

kosa sio kufanya kosaa,bali kulirudia

mimi nadhani swala la ufisadi kuthibitisha ni ngumu sana inahitaji uchunguzi wa kina hata hivyo ubinafsishaji hauna tatizo ishu iliyopo je ulifanywa kwa umakini na weledi,tija kwa maslahi mapana ya taifa jibu siyo kwa hiyo nadhani mwandosya and the all officials failed on this tuache unafiki wa kusifia tu watu
 
mimi nadhani swala la ufisadi kuthibitisha ni ngumu sana inahitaji uchunguzi wa kina hata hivyo ubinafsishaji hauna tatizo ishu iliyopo je ulifanywa kwa umakini na weledi,tija kwa maslahi mapana ya taifa jibu siyo kwa hiyo nadhani mwandosya and the all officials failed on this tuache unafiki wa kusifia tu watu
Ubinafsishaji haukuwa kosa. makosa ni utekelezaji wake na ndio tumepigia makelele miaka yote, leo watu wamegeuka kwa sababu aloyasema haya ni Zitto..
 
Kama wengi tulivyosikia jana, kuna tuhuma hizi hapa chini ambazo zilitolewa jana na Zitto Kabwe na kuandikwa na vyombo vingi vya habari leo.

HOJA YA ZITTO

Zittokabwe
: Prof. Mark Mwandosya aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wakati wa uongozi wa Rais Benjamin Mkapa. Mashirika yote ya Umma , takribani, katika Wizara hii yaliyobinafsishwa zoezi la ubinafsishaji liligubikwa na tuhuma za ufisadi na hata kuchukuliwa upya na Serikali.

Shirika la Ndege la Taifa lilibinafsishwa chini ya Mwandosya na likafa. Kitengo cha makontena katika Bandari ya Dar Es Salaam kilibinafsishwa kipindi hiki na kuleta maneno mengi sana. Mchakato wa kubinafsisha Shirika la Reli pia ulianza kipindi hiki. Ubinafsishaji ulioleta maneno mengi zaidi ulikuwa ni wa Kampuni ya simu ( TTCL) kwa MSI detecon na Celtel International.

Prof. Mwandosya binafsi alipata tuhuma na mtoto wake kusomeshwa na watu waliouziwa kampuni hii kwa bei ya chee. Masuala haya yaliandikwa na vyombo vya habari miaka ya kati ya 2001 na 2005. Prof. Hana budi kufafanua haya mbele ya umma ili kujiridhisha na uwezo wake wa kupambana na rushwa na ufisadi.


MAJIBU YA PROF MWANDOSYA

Zitto, Salaam.

Hongera pia kwa kuwa kiongozi wa ACT na hongera kwa kazi kubwa unayoifanya kueneza itikadi ya Chama chako. Ni jambo zuri katika kukuza demokrasia ya nchi yetu na hasa kukuza uzalendo. Siku zote nimekuelezea kama kijana ambaye hakika utakuwa tegemeo la Taifa letu, na hili nimekuambia mara nyingi. Nimeona vema nifafanue yale ambayo umeyataja katika post yako.

Niliyatolea maelezo ya kina miaka mingi iliyopita lakini nadhani utafiti sio moja ya maeneo tuliyo na nguvu nayo kwa hiyo umeyafukua bila kuyafanyia utafiti au kutaka upate ufafanuzi kutoka kwa mhusika.

Nianze na hili la ubinafsishaji kwa ujumla wake. Inawezekana ulikuwa badi shule, pamoja na nia njema ya kuanzisha mashirika ya umma, hatimaye yalikuja kuwa mzigo mkubwa kwa hazina yetu, maana yake kwa wananchi. Asilimia kubwa yalitegemea ruzuku ya serikali na baadhi yalikuwa mufilisi. Teknolojia ilikuwa imebadilika sana na ili kuyafungua ingeigharimu serikali na umma wa Tanzania kiasi kikubwa sana. Uchumi wa nchi wakati ule usingeweza kubeba mzigo huo. Ndipo Chama, wakati ule kiliporidhia Serikali ibakie na shughuli zake za msingi za Utawala, Ulinzi na Usalama, na Usimamizi wa ujumla wa uchumi.


Maamuzi yafuatayo yakachukuliwa:

Kwa upande wa shughuli za serikali zenye sura ya kibiashara, idara husika zikageuzwa kuwa wakala wa serikali, zikifanya kazi kwa uhuru zaidi chini ya Bodi zao. Kuhusu mashirika na kampuni za umma ilikubalika zirekebishwe na hatimaye zibinafsishwe. Ndipo kilipoundwa chombo maalum kisheria kilichokuwa na mamlaka kamili ya kubinafsisha
Mashirika ya umma.

Chombo hiki, Parastatal Sector Reform Commission (PSRC) kilikuwa chombo huru kikiwa chini ya Ofisi ya Rais, Mipango. Kiliwekwa hapo kwa sababu mamlaka yake yalikuwa Mtambuka, na vyombo husika vilikuwa kwenye sekta mbalimbali. Kwa hiyo sekta husika na Wizara husika, pamoja na kuitwa PSRC wakatii wa majadiliano yaliyohusu mashirika yake, hazikuwa na mamlaka ya kisheria kuhusu ubinafsishaji. Ni vema hili likaeleweka.


Pamoja na hayo, nirudie ufafanuzi kuhusu ubinafsishaji wa TTCL, nafanya hivyo kutokana na dhana ya uwajibikaji wa pamoja, ikumbukwe kwamba maamuzi ya ubinafsishaji wa TTCL yalifikiwa na PSRC mwaka mmoja kabla Waziri Mwandosya hajaingia siasa! Hata hivyo suala kubwa ni mabadiliko ya teknolojia tu. TTCL ilikuwa imejikita zaidi kimfumo na kiteknolojia katika teknolojia ya analogue na land lines.Mfumo wate,kiutawala na kiteknolojia ulikuwa katika msingi huo. Teknolojia ya simu za mkononi, na ushindani uliojitokeza ndio hasa changamoto kubwa ya TTCL.

Hata hivyo mabadiliko makubwa na maendeleo makubwa katika TEHAMA yamepelekea Tanzania kuwa mbali na kuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingi za Afrika. Katika mawasiliano Tanzania imekuwa 'Mecca' na wengi wamekuja kujifunza tumewezaje kufanikiwa. Namshukuru Rabuka kwa kuniwezesha kutoa mchango wangu katika maendeleo ya sekta hii. Na ili kuhakikisha kwamba mlaji au mtumiaji wa huduma za kiuchumi hahujumiwa na wakati huo huo mtoa huduma au mwekezaji ana uhakika wa kufaidika na kuweza kutoa huduma endelevu,ndipo vilipoanzishwa vyombo vya udhibiti wa huduma za kiuchumi, Regulatory Bodies. Nimebahatika kuwa Waziri pekee mwanzilishi na msimamizi wa TCRA, SUMATRA,TCAA, na EWURA.

Nimeelezea kuhusu mfumo wa ubinafsishaji hivyo basi ninachoweza kufafanua ni kwamba nilipomaliza muda wangu kama Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, niliacha Shirika la Reli likisafirisha tani laki tisa za shehena kwa mwaka, safari za abiria kwenda Tabora kutoka Dar zilikuwa kila siku, na ATC ilikuwa na ndege mbili aina ya Boeing 737 na mbili aina ya Fokker Friendship.

Tuhuma za mtoto wa Profesa kulipiwa na kampuni moja ya simu hazina chembe yoyote ya ukweli Bwana Zitto. Mtoto ambaye alifuzu uhandisi wa mawasiliano ya simu aliomba kazi ya muda na akapewa.
Kampuni husika ilikanusha tuhuma hizo ambazo zilitolewa wakati wa mchakato wa kugombea uteuzi katika CCM kwa nafasi ya kuwa mgombea wa Urais mwaka 2005. Sasa zinafufuliwa tena na Bwana Zitto wakati wa mchakato huo huo mwaka 2015! Inaeleweka.

Namalizia kama nilivyoanza, Zitto ni mwanasiasa ninayemheshimu sana. Mara nyingi naye amenitambua kama mwanasiasa wa kuigwa (role model). Lakini katika siasa tunasema saa 24 ni kipindi kirefu sana, na huwa tunabadilika!
Ushauri wangu kwake ni kwamba siku zote kabla hujahukumu sikiliza upande wa pili, kwa kilatini hii ni dhana muhimu inayojulikana kama AUDI ALTERAM PARTEM.

Pili ni vema ukazingatia zaidi mambo chanya ya msimamo na itikadi ya ACT. Lakini katika kushauri hivyo natambua kwamba " Akili ni nywele, kila mtu ana zake"


Ramadhan Kareem. Wakatabahu,

Mwandosya
.
Ni kwa nini zitto kabwe hatumsikii akizungumzia wizi na ufisadi uliofanywa wakati LOWASA akiwa waziri mkuu? au kwa vile ndiye mdhamini mkubwa wa chama chake cha ACT? KAMA KWELI ZITTO NI MZARENDO ATOKE HADHALANI AMSHUTUMU LOWASA KWA KASHFA YARICHMOND. AU UNAOGOPA UKIMSEMA atasitisha zile mil ....za kueneza chama? na kupunguza nguvu ya upinzani?
 
Haja jibu tuhuma zinazomkabili ila ameleta bla bla za kiprofessor
 
Sure mkuu zitto nguvu yake kubwa ni uchawi kwahiyo siyo rahisi kushindana na watu wanaotumia akili kubwa kama huyu mzee,

Kiukweli zitto afanye tu zile kazi za usiku na wachawi wenzake haya mambo ya kutumia akili hovyo kabisa.

Hlo nalo neno.
 
Kama mnakubaliana na majibu ya Prof Mwandosya, basi endeleeni kuipigia kura CCM endelee kuwatawala huo ndio ukweli.

CCM kweli wana watu makini.

Wewe na Zitto walewale..watu wanaandika vitu vya msingi wewe unaandika porojo..lini utaanza kuandika mambo ya maana
 
Ni kwa nini zitto kabwe hatumsikii akizungumzia wizi na ufisadi uliofanywa wakati LOWASA akiwa waziri mkuu? au kwa vile ndiye mdhamini mkubwa wa chama chake cha ACT? KAMA KWELI ZITTO NI MZARENDO ATOKE HADHALANI AMSHUTUMU LOWASA KWA KASHFA YARICHMOND. AU UNAOGOPA UKIMSEMA atasitisha zile mil ....za kueneza chama? na kupunguza nguvu ya upinzani?
Wewe umewahi kumsikia kiongozi gani wa Upinzani akimshutumu Lowassa kwa Kashfa ya Ufisadi moja kwa moja katika mihadhara? ukiacha Mwakyembe, Makongoro Nyerere, Nape na Wasira! Tuseme ukweli nani alowahi kumtaja Lowassa wazi wazi toka list ya Mafisadi..Ya Richomnd, Chadema wote wamebadilika wanaamini hilo ni deal la JK au leo mmebadilika..
 
mimi nadhani swala la ufisadi kuthibitisha ni ngumu sana inahitaji uchunguzi wa kina hata hivyo ubinafsishaji hauna tatizo ishu iliyopo je ulifanywa kwa umakini na weledi,tija kwa maslahi mapana ya taifa jibu siyo kwa hiyo nadhani mwandosya and the all officials failed on this tuache unafiki wa kusifia tu watu

Hili ni swali gumu sana,Nakumbuka Mzee Mwinyi aliwahi kusema nchi alivyoikuta ilikuwa kama Mzee mwenye basi mbovu lililoegeshwa juu ya mawe, hivyo Mzee huyo anakuwa na machaguo mawili, moja kila siku asubuhi akitoka kupiga mswaki awe wanaliangalia gari lile lililo juu ya mawe au amtafute mtu mwenye pesa alitengeneze gari hilo,aliendeshe na kisha Mzee yule walau apate gawio.

Hivyo swala la ubinafsishaji ulikuwa uamuzi makini na sahihi kwa mazingira yetu, sasa kama kuna ufisadi ulipitia kwenye uwekezaji huo hatuwezi kuulaumu uamuzi wa ubinafsishaji bali tuwapate watu hao waliofanya ufisadi na kuvunja taratibu hizo kama wapo, na hili Sumaye husema kila siku na ninamuunga mkono pia.

Tuna tatizo kidogo tu cha kigugumizi cha kuchukua hatua, walioshiriki kuiba/kufisadi kupitia uamuzi huo sahihi wanaweza kupatikana tukitaka.
 
Hajajibu lolote, kuna maswali mengi saana, hivi mlio karibu naye mnaonaje mkimshauri, aitishe press conference ili watu wawe huru kuja kumuuliza? kuna tuhuma pia akiwa katibu mkuu wa Nishati, alikuwa akitumia vibaya wadhifa wake, wakupeleka tenda kwa kijikampuni alichokuwa akimiliki yeye na Prof Luhanga.

Kingine, anatakiwa atoe ufafanuzi kuhusu kutuhumiwa kuwa ni MKABILA saana, huwezi kupata kitu kwake mpaka uwe MWANAFYALE/NYAKAFYALE.

Tuhuma kuhusu mwanae, hajaweza kuzijibu, hivi wapi duniani mwanafuzi wa MSc anaweza kupangishiwa kuishi Hotel ya nyota 5? tena na kampuni ambayo imenunua kampuni iko chini ya wizara inaongozwa na baba yake?

Kuna mengi, mimi naomba mumlete hadharani.

Hapa tuache siasa za uchama, huyu tutakuja kulia, si msafi hata kidogo. Handsome boy, ni mchafu saana
Kingine, hivi kweli ana uchungu na NCHI hii? kama amekaa analipwa mshahara bila kazi yeyote, huu si hujumu uchumi? Watu wanakosa huduma za afya, yeye analipiwa kwenda kusoma magazeti offisini, leo eti niachieni niongoze nchi?
 
Zitto Ulikua hayajui hayo hapo mwanzo? ulikua wap kuyasema? Acha kutumika kisiasa
 
Spika wa Bunge Ana Makinda aliwahi sema bungeni kuwa kuna vijana walikuwa wanakuja vizuri sana kisiasa sijui wamepatwa na nn!! Njaa mbaya sana ukijumuisha na ukosefu wa uzalendo na uadilifu ndio ninachokiona kuwa kikwazo kikubwa kwa vijana waingiao kwenye siasa. Na hawa tusipokuwa makini wanaweza hata sababisha political unrest. Tuwaogope kama ukoma kuwa support watu kama akina zito wanaobadilika badilika zaidi ya kinyonga
 
unamtukana mtu kiproffessor ,wanajua matusi ya kiproffessor tu ndio watagundua wengine wataona kasifiwa

Safi sana professor

Kumbe ndio maana proffessor anaheshimika na kina membe .Hii kitu imenifanya nimkubali katika wagombea wote wa CCM ni kichwa ,anakupa vielelezo huku anakutukana bila neno la tusi aisee jamaa ni big brain, mnaosema mnaakili kuliko watu wengine jifunzeni kwa prof na huwa haongei sana short and clear

Profesa katiririka vizuri.Ameonyesha ukongwe wa hali ya juu katika siasa.

Majibu mengine hata swali la nyongeza hulioni!

Zito kakimbia na umbea! Kwamba alisikia 2005 ilizungumzwa, yeye leo kakumbushia japo majibu sahihi yalishatolewa zamanii!!!

Zitto na yeye si alifanya field kwa Fisadi Nimrod Mkono? Au anatafuta namna ya kuandikwa na Kibanda?

Msumari WA Moto kwa --------- WA act mwandiga

Amejibu kiprofessor, zitto mtoto mdogo sana...kwa sasa amebaki kua msaliti wa watu nchi hii...

Mkitaka kujua undani wa Zitto, waulizeni CDM. Msaliti na msaka tonge full stop. Mwandosya huyo huyo ndio kiasi fulani alimnsuru na hoja za Kibajaji wakati wa mjadala wa ESCROW bungeni. Akalia machozi huku akiunganisha na kifo cha mama yake mzazi. May be Kibajaji had a point lakini tulimpuuza.

Mwisho wa Zitto utakuwa kama wa Lyatonga. Lakini wa kwake utakuja mapema zaidi. Lyatonga anaweza kuwa amefifia kisiasa na jambo la kawaida lakini si rahisi kumtuhumu kuwa corrupt kama inavyotokea kwa Zitto.

Teh Teh leo Bavicha wameungana na Mwana CCM na wamemkubali mwana CCM...! Teh Teh siasa hizi! Bavicha muda mwingine hawana tofauti kundi la nzige..
 
Ni kwa nini zitto kabwe hatumsikii akizungumzia wizi na ufisadi uliofanywa wakati LOWASA akiwa waziri mkuu? au kwa vile ndiye mdhamini mkubwa wa chama chake cha ACT? KAMA KWELI ZITTO NI MZARENDO ATOKE HADHALANI AMSHUTUMU LOWASA KWA KASHFA YARICHMOND. AU UNAOGOPA UKIMSEMA atasitisha zile mil ....za kueneza chama? na kupunguza nguvu ya upinzani?

sio kila jambo la kuongea mengine yamewazidi uwezo
 
thibitisheni bwana mbona mnakuwa na double standard tuhuma ni tuhuma tu

Akiingia Rais msafi asiye fisadi mwenye ujasiri na kupambana na ufisadi, hayo yako peupe tu. Kwa wakati huu kesi ya nyani kumpelekea ngedere itakuwa kupoteza muda.
 
Upo vizuri sana kiongozi na ukweli huo haupo mbali ingawa dogo ni mbishi sana

kweli yupo zitto na mengi hautasikia wanamgusa lowasa bali wanatumia vyombo vyao vya habari kuwachafua wengine.

Huo ndo ukomavu wa kisiasa. Nadhani zzk kayapata majibu aliyoyakusudia.

zito hacha kutumika na wazee ambao kwenye siasa ndo wameishagota wewe bado una muda mwingi wanakualibia kwa tamaa zako za kijinga,

Masaa 24 kwa mwanasiasa ni mengi,____Zitto si Zitto tena.

Akili ni nywele, kila mtu ana, zake_____Zitto hana zake pekee, amechukua za akina Laigwanan

Kinacho nifurahisha kwenye huu uzi ni jinsi Bavicha wanavyo mfagilia Prof kutoka CCM! Teh Teh CCM haina mpinzani!
 
Back
Top Bottom