Majibu ya Prof Mwandosya kwa Zitto

Majibu ya Prof Mwandosya kwa Zitto

Hapa naona Blah Blah Blah....., nyingi tu..., Mwisho wa siku baada ya maelezo marefu ni kweli Ubinafsishaji ulitendeka ila anachosema it was for a good cause, kwahio kama ni uongo amesingiziwa ni kwenye mtoto wake kusomeshwa na alikuta mpango wa TTCL umeshaanza yeye alimalizia tu...

Cha kujiuliza ni Je, ni kweli kubinafshisha makampuni kwa waliobinafsishwa was a right call ?
 
Sure mkuu zitto nguvu yake kubwa ni uchawi kwahiyo siyo rahisi kushindana na watu wanaotumia akili kubwa kama huyu mzee,

Kiukweli zitto afanye tu zile kazi za usiku na wachawi wenzake haya mambo ya kutumia akili hovyo kabisa.

duuuuu hapa patam had ndakindak mnamsuta kibaraka wenu yuda
 
Huyu yuda hapo anaswali la nyongeza kweli? Kazi yake kukalili mambo
 
Kama wengi tulivyosikia jana, kuna tuhuma hizi hapa chini ambazo zilitolewa jana na Zitto Kabwe na kuandikwa na vyombo vingi vya habari leo.

HOJA YA ZITTO

Zittokabwe
: Prof. Mark Mwandosya aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wakati wa uongozi wa Rais Benjamin Mkapa. Mashirika yote ya Umma , takribani, katika Wizara hii yaliyobinafsishwa zoezi la ubinafsishaji liligubikwa na tuhuma za ufisadi na hata kuchukuliwa upya na Serikali.

Shirika la Ndege la Taifa lilibinafsishwa chini ya Mwandosya na likafa. Kitengo cha makontena katika Bandari ya Dar Es Salaam kilibinafsishwa kipindi hiki na kuleta maneno mengi sana. Mchakato wa kubinafsisha Shirika la Reli pia ulianza kipindi hiki. Ubinafsishaji ulioleta maneno mengi zaidi ulikuwa ni wa Kampuni ya simu ( TTCL) kwa MSI detecon na Celtel International.

Prof. Mwandosya binafsi alipata tuhuma na mtoto wake kusomeshwa na watu waliouziwa kampuni hii kwa bei ya chee. Masuala haya yaliandikwa na vyombo vya habari miaka ya kati ya 2001 na 2005. Prof. Hana budi kufafanua haya mbele ya umma ili kujiridhisha na uwezo wake wa kupambana na rushwa na ufisadi.


MAJIBU YA PROF MWANDOSYA

Zitto, Salaam.

Hongera pia kwa kuwa kiongozi wa ACT na hongera kwa kazi kubwa unayoifanya kueneza itikadi ya Chama chako. Ni jambo zuri katika kukuza demokrasia ya nchi yetu na hasa kukuza uzalendo. Siku zote nimekuelezea kama kijana ambaye hakika utakuwa tegemeo la Taifa letu, na hili nimekuambia mara nyingi. Nimeona vema nifafanue yale ambayo umeyataja katika post yako.

Niliyatolea maelezo ya kina miaka mingi iliyopita lakini nadhani utafiti sio moja ya maeneo tuliyo na nguvu nayo kwa hiyo umeyafukua bila kuyafanyia utafiti au kutaka upate ufafanuzi kutoka kwa mhusika.

Nianze na hili la ubinafsishaji kwa ujumla wake. Inawezekana ulikuwa badi shule, pamoja na nia njema ya kuanzisha mashirika ya umma, hatimaye yalikuja kuwa mzigo mkubwa kwa hazina yetu, maana yake kwa wananchi. Asilimia kubwa yalitegemea ruzuku ya serikali na baadhi yalikuwa mufilisi. Teknolojia ilikuwa imebadilika sana na ili kuyafungua ingeigharimu serikali na umma wa Tanzania kiasi kikubwa sana. Uchumi wa nchi wakati ule usingeweza kubeba mzigo huo. Ndipo Chama, wakati ule kiliporidhia Serikali ibakie na shughuli zake za msingi za Utawala, Ulinzi na Usalama, na Usimamizi wa ujumla wa uchumi.


Maamuzi yafuatayo yakachukuliwa:

Kwa upande wa shughuli za serikali zenye sura ya kibiashara, idara husika zikageuzwa kuwa wakala wa serikali, zikifanya kazi kwa uhuru zaidi chini ya Bodi zao. Kuhusu mashirika na kampuni za umma ilikubalika zirekebishwe na hatimaye zibinafsishwe. Ndipo kilipoundwa chombo maalum kisheria kilichokuwa na mamlaka kamili ya kubinafsisha
Mashirika ya umma.

Chombo hiki, Parastatal Sector Reform Commission (PSRC) kilikuwa chombo huru kikiwa chini ya Ofisi ya Rais, Mipango. Kiliwekwa hapo kwa sababu mamlaka yake yalikuwa Mtambuka, na vyombo husika vilikuwa kwenye sekta mbalimbali. Kwa hiyo sekta husika na Wizara husika, pamoja na kuitwa PSRC wakatii wa majadiliano yaliyohusu mashirika yake, hazikuwa na mamlaka ya kisheria kuhusu ubinafsishaji. Ni vema hili likaeleweka.


Pamoja na hayo, nirudie ufafanuzi kuhusu ubinafsishaji wa TTCL, nafanya hivyo kutokana na dhana ya uwajibikaji wa pamoja, ikumbukwe kwamba maamuzi ya ubinafsishaji wa TTCL yalifikiwa na PSRC mwaka mmoja kabla Waziri Mwandosya hajaingia siasa! Hata hivyo suala kubwa ni mabadiliko ya teknolojia tu. TTCL ilikuwa imejikita zaidi kimfumo na kiteknolojia katika teknolojia ya analogue na land lines.Mfumo wate,kiutawala na kiteknolojia ulikuwa katika msingi huo. Teknolojia ya simu za mkononi, na ushindani uliojitokeza ndio hasa changamoto kubwa ya TTCL.

Hata hivyo mabadiliko makubwa na maendeleo makubwa katika TEHAMA yamepelekea Tanzania kuwa mbali na kuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingi za Afrika. Katika mawasiliano Tanzania imekuwa 'Mecca' na wengi wamekuja kujifunza tumewezaje kufanikiwa. Namshukuru Rabuka kwa kuniwezesha kutoa mchango wangu katika maendeleo ya sekta hii. Na ili kuhakikisha kwamba mlaji au mtumiaji wa huduma za kiuchumi hahujumiwa na wakati huo huo mtoa huduma au mwekezaji ana uhakika wa kufaidika na kuweza kutoa huduma endelevu,ndipo vilipoanzishwa vyombo vya udhibiti wa huduma za kiuchumi, Regulatory Bodies. Nimebahatika kuwa Waziri pekee mwanzilishi na msimamizi wa TCRA, SUMATRA,TCAA, na EWURA.

Nimeelezea kuhusu mfumo wa ubinafsishaji hivyo basi ninachoweza kufafanua ni kwamba nilipomaliza muda wangu kama Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, niliacha Shirika la Reli likisafirisha tani laki tisa za shehena kwa mwaka, safari za abiria kwenda Tabora kutoka Dar zilikuwa kila siku, na ATC ilikuwa na ndege mbili aina ya Boeing 737 na mbili aina ya Fokker Friendship.

Tuhuma za mtoto wa Profesa kulipiwa na kampuni moja ya simu hazina chembe yoyote ya ukweli Bwana Zitto. Mtoto ambaye alifuzu uhandisi wa mawasiliano ya simu aliomba kazi ya muda na akapewa.
Kampuni husika ilikanusha tuhuma hizo ambazo zilitolewa wakati wa mchakato wa kugombea uteuzi katika CCM kwa nafasi ya kuwa mgombea wa Urais mwaka 2005. Sasa zinafufuliwa tena na Bwana Zitto wakati wa mchakato huo huo mwaka 2015! Inaeleweka.

Namalizia kama nilivyoanza, Zitto ni mwanasiasa ninayemheshimu sana. Mara nyingi naye amenitambua kama mwanasiasa wa kuigwa (role model). Lakini katika siasa tunasema saa 24 ni kipindi kirefu sana, na huwa tunabadilika!
Ushauri wangu kwake ni kwamba siku zote kabla hujahukumu sikiliza upande wa pili, kwa kilatini hii ni dhana muhimu inayojulikana kama AUDI ALTERAM PARTEM.

Pili ni vema ukazingatia zaidi mambo chanya ya msimamo na itikadi ya ACT. Lakini katika kushauri hivyo natambua kwamba " Akili ni nywele, kila mtu ana zake"


Ramadhan Kareem. Wakatabahu,

Mwandosya
.
Majibu ya Mwandosya ni ya kishikaji hayana uzito kabisa kwa kiongozi alokuwa madarakani akisimamia vyombo hivyo. Ukimsoma kwa makini utaelewa kwamba anaruka majukumu kwa kisingizia mfumo wa Ubinafsishaji.

Jambo moja ambalo hakulielewa ama kulielezea vizuri ni upinzani baina ya ACT na CCM kisera katika Ubinafsishaji ambao ulipelekea kuharibika kabisa kwa mashirika hayo. Hivyo anaposema kimfumo mashirika hayo yalionekana mzigo kwa taifa kwa kugharamiwa na kwamba serikali haikuwa na uwezo huo! lakini laa ajabu ni kwamba hata baada ya kubinafsishwa chini yake, mashirika hayo yameigharmu serikali mara dufu ya gharama za uendeshaji. Chukulia IPTL imetugharimu kiasi gani. Haya Ubinafsishaji wa TTCL inaitupiamlawama PCRC lakinimaamuzi ya kubinafsishwa kupitishwa na serikali yake.

Jambo jingine anazungumzia PCRC kama chombo huru wakati anasema tena kilikuwa chini ya Rais, ni Uhuru upi anaozungumzia hapa. Hivi kweli Mwandosya anataka tuamini kwamba yeye hakufanya kosa lolote isipokuwa ni mfumo na sera za chama chake ila tuyatazame mazuri yake ya vyombo alivyoanzisha kama TCRA, SUMATRA, TCAA na EWURA ambavyo hakuonyesha mafanikio yake ila uanzilishi wa vyombo hivyo.

Swala la ATC na TRC kusema kweli ni aibu hata kulizungumzia kwa sababu mashirika haya yalikuwepo toka enzi ya Nyerere na yakifanya kazi kama alivyojielezea. Kama ameacha shirika la ndege lina Boeng 2 na fokker 2 ambazo zimenunuliwa toka mwaka 1975, anajaribu kujenga hoja gani hapo? ya kwamba yeye aliweza kuzitunza ndege hizo ama kazi yake ilikuwa kuliendeleza shirika hilo pamoja na Reli yalokufa vibaya vibaya. Au lengo lake ni kutuonyesha kwamba kosa sio lake ila la watawala walokuwa juu yake...
 
Masaa 24 kwa mwanasiasa ni mengi,____Zitto si Zitto tena.

Akili ni nywele, kila mtu ana, zake_____Zitto hana zake pekee, amechukua za akina Laigwanan

Watu wengine wa ajabu! Kila anayemshambulia Zitto yeye anamuunga mkono...doesnt matter anaongelea nini!
 
Majibu ya Mwandosya ni ya kishikaji hayana uzito kabisa kwa kiongozi alokuwa madarakani akisimamia vyombo hivyo. Ukimsoma kwa makini utalelewa kwamba anaruka majukumu kwa kisingizia cha mfumo wa Utaifishaji.

jambo moja ambalo hakulielewa ama kulielezea vizuri ni upinzani baina ya ACT na CCM katika Utaifishaji ambao ulipelekea kuharibika kabisa kwa mashirika hayo. Hivyo anaposema kimfumo mashirika hayo yalionekana mzigo kwa taifa kwa kugharamiwa na kwamba serikali haikuwa na uwezo huo! lakini laa ajabu ni kwamba hata bnaada ya kubinafsishwa mashirika hayo yameigharmu serikali mara dufu ya gharama za uendeshaji. Chukulia IPTL imetugharimu kiasi gani. Haya Ubinafsishaji wa TTCL inaitupiamlawama PCRC lakinimaamuzi ya kubinafsishwa kupitishwa na serikali yake.
jambo jingie anazungumzia PCRC kama chombo huru wakati anasema tena kikiwa chini ya Rais hni Uhuru upi anaozungumzia hapa. Hivi kweli Mwandosya anataka tuamini kwamba yeye hakufanyakosa lolote isipokuwa tuyatazame mazuri yake ya vyombo kama TCRA, SUMATRA, TCAA na EWURA vyombo ambavyo hakuonyesha mafanikio yake ila uanzilishi wa vyombo hivyo.

Swala la ATC na TRC kusema kweli ni aibu hata kulizungumzia kwa sababu mashirka haya yalikuwwepo toka enzi ya Nyerere na yakifanya kazi kama alivyojielezea. kaa ameacha shirika la ndege lina Boeng 2 na fokker ambazo zimenunuliwa toka mwaka 1975, anajaribu kujenga hoja gani hapo? ya kwamba yeye aliweza kuzitunza ndege hizo ama kazi yake ilikuwa kuliendeleza shirika hilo pamoja na Reli yalokufa vibaya vibaya.. Au lengo lake ni kutuonyesha kwamba kosa sio lake ila la watawala walokuwa juu yake...
Mkuu, hivi una akili timamu kweli?
 
Profesa katiririka vizuri.Ameonyesha ukongwe wa hali ya juu katika siasa.
Umekiri kwa nafsi yako CCM ni kiboko mtu kama huyu ni muhimu sana bora aje kuwa rais wetu.
 
Chadema dawa yao ndogo tu ukiwapa majibu murua inatosha, teh teh teh
 
Mkitaka kujua undani wa Zitto, waulizeni CDM. Msaliti na msaka tonge full stop. Mwandosya huyo huyo ndio kiasi fulani alimnsuru na hoja za Kibajaji wakati wa mjadala wa ESCROW bungeni. Akalia machozi huku akiunganisha na kifo cha mama yake mzazi. May be Kibajaji had a point lakini tulimpuuza.

Mwisho wa Zitto utakuwa kama wa Lyatonga. Lakini wa kwake utakuja mapema zaidi. Lyatonga anaweza kuwa amefifia kisiasa na jambo la kawaida lakini si rahisi kumtuhumu kuwa corrupt kama inavyotokea kwa Zitto.

Wewe una akili sana,
Nakumbuka Mwandosya aliongea tena akasema kuhusu nawewe kupata gawiwo.Kwa mazngira yaliyopo wala usiongelee chochote wakati wa majimuisho Bwana mdogo maana tulushajua ukweli ukowapi....

Lengo lilikuwa ni kusema kuwa ilionesha Zitto alipata chochote kitu kwenye issue za escrow lakin,kwa kaz aliyokuwa kaifanya kulikiluwa mazngira ya kushindwa kuipata hio hela..
Pamoja na akina Ngereja kumtaka Zitto.aseme nayete gawiwo alilopata Mwandosya alimuomba Zitto asilitolee maelezo...

Lakin leo Zitto anamchokonoa mzee wawatu ili tu Lowasa wake aonekane msafi...


Zitto mnafiki mkubwa sana
 
Mkuu, hivi una akili timamu kweli?
Akili timamu sina, ila nilichokielewa kwa upunguani wangu miye ni kwamba. Zitto kama MJAMAA kachukulia swala la Mwandosya kuonyesha ubovu wa sera za CCM na kwamba yeye kama mgombea Urais haya ndio mapungufu yake na ya chama. Sasa Mwandosya kwa vile yeye ni mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, na ili asiharibu record yake kaonyesha makosa mengi ni ya kisera na sio yeye kumbe anajenga hoja ya Zitto wakati anajisafisha..
 
Back
Top Bottom