Majibu ya Kikwete na BBC: Tumevuna tulichokipanda

Ndugu zangu, Kuna mengine yamenipita hapa kati. Leo nimesikiliza mahojiano ya mwandishi wa BBC na Rais Jakaya Kikwete kuhusu tatizo la upatikanaji wa umeme Tanzania. Nimefuatilia pia maoni ya Watanzania mtandaoni juu ya majibu ya Kikwete. Tafsiri yangu; uongozi wa nchi ni kitu kigumu sana. Wengi wamemshambulia Kikwete kwa majibu yake kiasi wengine wamediriki kuandika; kuwa hatuna Rais. Tunafanya makosa sana kutoa hukumu zenye kusukumwa na hisia hasi. Nimesikiliza mara mbili majibu ya Rais. Sikuona mahala pa kumshutumu Rais isipokuwa nimesikitishwa na maswali ya mwandishi wa BBC ambayo kwa Kikwete ilikuwa kama penalti alizokuwa akipigiwa mikononi na yeye kuzidaka huku akitabasamu. Tusisahau, kuwa Kikwete ni mwanasiasa mahiri. Mwandishi anayekutana na Kikwete ni vema akajiandaa vilivyo juu ya namna ya kumbana Kikwete ndani ya majibu yake. Afanye hivyo ili kupata maswali mapya na hivyo basi habari mpya kutokana na majibu ya Rais. Niseme tu, mahojiano yale ya Kikwete na BBC hayakutoa maswali mapya wala kuja na habari mpya. Na huo si udhaifu wa Kikwete bali mwandishi wa BBC aliyemhoji Kikwete. Si tumemwona? Kikwete aliweza kucheza anavyotaka kwenye mahojiano yale. Na umahiri wake ulijidhihirisha pale alipogeuza sura ya mahojiano yale na Kikwete kuchukua nafasi ya mwandishi kwa kumbana mwandishi na husuan juu ya maarifa ya mwandishi katika eneo husika; ” Wakati mwingine na nyinyi mjifunze hayo mambo ya kitaalamu kulikoni kuuliza tu hivi hivi. Unajua ungekuwa na wewe unauliza kwa hoja - “unajua kwamba hiki kitu hiki ingekuwa umeme wa jua miezi miwili tu upo” - tungeweza kufanya hivyo.” Kikwete anamwambia mwandishi wa BBC. Katika mahojiano yale Kikwete alikwenda na takwimu zake mfukoni. Kama moja ya mbinu katika sanaa ya mawasiliano ili kufikisha ujumbe, mara tatu ndani ya mahojiano yale Kikwete alizungumzia MW 600 zilizozalishwa tangu uhuru na MW 145 zilizozalishwa tangu 2009, na MW 160 zitakazozalishwa ifikapo Desemba mwaka huu. Jumla zitakuwa MW 305 tangu 2009. Na hapo ndipo kwenye hoja ya msingi ya Kikwete. Ana haki kuwashangaa wasioona jitihada zake. Na Kikwete hakosi majibu ukimwuliza juu ya umeme wa jua, upepo na mvuke. Ana hoja anaposema kuwa umeme huo pia unahitaji mipango na kuwa huwezi kupata umeme wa jua kesho kwa vile jua linawaka. Kama msikilizaji ningependa mwandishi ambane Kikwete kwenye maeneo ya ufisadi kwenye mikataba ikiwamo yenye kuhusiana na nishati ya umeme. Hakika, kama tungedhibiti ufisadi kwenye mikataba, basi, ni imani ya wengi kuwa tungejenga uwezo wa kuzalisha MW nyingi zaidi za umeme na kwa kasi kabisa, kulifanya tatizo la umeme kuwa ni historia. Tungeweza pia kupunguza gharama za mtumiaji wa umeme. Tuna tatizo pia la baadhi ya wanasiasa kujiingiza katika kuwekeza kwenye eneo la nishati ya umeme. Wachague kati ya uongozi na uwekezaji. Kiongozi huwezi kuwa na hisa kwenye kampuni binafsi ya kuzalisha umeme na wakati huo huo ukalinda maslahi ya umma badala ya kampuni yako. Vinginevyo, kwa waliokuwa na utayari wa kuelewa, mahojiano yale ya BBC na Kikwete yamempa nafasi Kikwete ya kujenga hoja ya msingi juu ya nini alichofanikiwa kufanya tangu aingie madarakani katika jitihada za kutatua tatizo la umeme nchini. Nawasilisha. Maggid, Sweden, Jumanne, Julai 26,2011MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
Natamani ungekuwa karibu nikutane maanake sasa hv itakuwa ban kwa jinsi navyofikiria kukutukana.Nikuulize swali moja angalau nikuache,vp bado unaandika makala kwenye gazeti la rai?
 
Natamani ungekuwa karibu nikutane maanake sasa hv itakuwa ban kwa jinsi navyofikiria kukutukana.Nikuulize swali moja angalau nikuache,vp bado unaandika makala kwenye gazeti la rai?

Mkuu mtukane tu lkn ban ije kwangu...au nikutakanie? FU.CK HIM...
 
Majid, heshima mbele!
Hivi hayo majibu ndio umeme umewaka? Watu wanataka umeme na hii mipango na visingizio sio vipya bali tumekuwa tukivisikia kila mara maji yanapokauka. Hata hizo MW300 alizosema katengeneza bado hazijawaka!
 
Mkuu mtukane tu lkn ban ije kwangu...au nikutakanie? FU.CK HIM...
Afadhali umenisaidia,ujue kuna watu wana akili magamba kiasi kwamba huwa natamani kuwachapa bakora.Kuna wa2 wanaleta mzaha kwenye mambo makubwa yasiyotakiwa kufanyiwa mzaha.Kuna wa2 wanaonekana kuwa na ustarab kumbe hawana akili.Huyu jamaa sidhani kama hajui kwamba suala la umeme si suala la masihara kama anavyofanya huyu aliyewah kuitwa na halima mdee kuwa rais wao.MAGGID naomba utuombe radhi tafadhari kwa kebehi ulizoonyesha au ndio mwendelezo wa akina salva reyemamu na akina prince bagenda,eti jk tumain lililorejea shame on u!
 
Majjid unajua unajidhalilisha sana na hizi tafsiri zako uchwara! Kama huna hoja ni lazima utafsiri au umetumwa? ninakubaliana na hao wadau waliokutupia matusi - tena wangetuma yale ya nguoni.
 
JF bana wananiachaga hoi wakati mwingine.... badala ya kujadili ishu at hand, wanajadili mleta ishu..... kweli ukiwa ni mwenyechuki hata zuri la umchukiaye hulioni!
 
Siyo mungu anayeleta mvua,ni binadamu.
Umeme wa jua ni muhimu kwa small scale/households na serikali ingefacilitate upatikanaji wake kupitia ruzuku,taxexemptions,na ununuaji wa umeme kutokas kwa wenye solar,umeme wa solar unaweza kufeed grid na wananchi wakapata fedha.Serikali inaweza kuchochea uwekezaji wa solar majumbani.
Kuhusu mtera,serikali inazembea sana kuhusu conservation of rufiji basin,mkuu angemuuliza prez kama anajua record ya mvua na evaporation ya maji kwenye great ruaha river,au kwenye sources esp. uporoto na catchment areas kwa miaka ishirini iliyopita halafu afanye comparison na water levels za mtera.
Je anaonaje kuhusu hiyo discrepancy? Does it suggest that lack of rainfall is the issue?
 
umepanda ndege uko ulaya huko unakuja hapa kumtetea Kikwete? NJOO TUPIGWE NWOTE NA MGAO HAPA NDIO UANZE KUMTETEA huyo mpanda ndege mwenzako
Umeshasema nilichokusudia kusema. Ahsante sana. Mjengwa ni mwandishi mnafiki kama walivyo waandishi wengi hapa nchini.
 

Ndugu zangu,



Kuna mengine yamenipita hapa kati. Leo nimesikiliza mahojiano ya mwandishi wa BBC na Rais Jakaya Kikwete kuhusu tatizo la upatikanaji wa umeme Tanzania.



Nimefuatilia pia maoni ya Watanzania mtandaoni juu ya majibu ya Kikwete. Tafsiri yangu; uongozi wa nchi ni kitu kigumu sana. Wengi wamemshambulia Kikwete kwa majibu yake kiasi wengine wamediriki kuandika; kuwa hatuna Rais.



Tunafanya makosa sana kutoa hukumu zenye kusukumwa na hisia hasi. Nimesikiliza mara mbili majibu ya Rais. Sikuona mahala pa kumshutumu Rais isipokuwa nimesikitishwa na maswali ya mwandishi wa BBC ambayo kwa Kikwete ilikuwa kama penalti alizokuwa akipigiwa mikononi na yeye kuzidaka huku akitabasamu.


Tusisahau, kuwa Kikwete ni mwanasiasa mahiri. Mwandishi anayekutana na Kikwete ni vema akajiandaa vilivyo juu ya namna ya kumbana Kikwete ndani ya majibu yake. Afanye hivyo ili kupata maswali mapya na hivyo basi habari mpya kutokana na majibu ya Rais.


Niseme tu, mahojiano yale ya Kikwete na BBC hayakutoa maswali mapya wala kuja na habari mpya. Na huo si udhaifu wa Kikwete bali mwandishi wa BBC aliyemhoji Kikwete.



Si tumemwona? Kikwete aliweza kucheza anavyotaka kwenye mahojiano yale. Na umahiri wake ulijidhihirisha pale alipogeuza sura ya mahojiano yale na Kikwete kuchukua nafasi ya mwandishi kwa kumbana mwandishi na husuan juu ya maarifa ya mwandishi katika eneo husika;



” Wakati mwingine na nyinyi mjifunze hayo mambo ya kitaalamu kulikoni kuuliza tu hivi hivi. Unajua ungekuwa na wewe unauliza kwa hoja - “unajua kwamba hiki kitu hiki ingekuwa umeme wa jua miezi miwili tu upo” - tungeweza kufanya hivyo.” Kikwete anamwambia mwandishi wa BBC.

Katika mahojiano yale Kikwete alikwenda na takwimu zake mfukoni. Kama moja ya mbinu katika sanaa ya mawasiliano ili kufikisha ujumbe, mara tatu ndani ya mahojiano yale Kikwete alizungumzia MW 600 zilizozalishwa tangu uhuru na MW 145 zilizozalishwa tangu 2009, na MW 160 zitakazozalishwa ifikapo Desemba mwaka huu. Jumla zitakuwa MW 305 tangu 2009. Na hapo ndipo kwenye hoja ya msingi ya Kikwete. Ana haki kuwashangaa wasioona jitihada zake.


Na Kikwete hakosi majibu ukimwuliza juu ya umeme wa jua, upepo na mvuke. Ana hoja anaposema kuwa umeme huo pia unahitaji mipango na kuwa huwezi kupata umeme wa jua kesho kwa vile jua linawaka.



Kama msikilizaji ningependa mwandishi ambane Kikwete kwenye maeneo ya ufisadi kwenye mikataba ikiwamo yenye kuhusiana na nishati ya umeme. Hakika, kama tungedhibiti ufisadi kwenye mikataba, basi, ni imani ya wengi kuwa tungejenga uwezo wa kuzalisha MW nyingi zaidi za umeme na kwa kasi kabisa, kulifanya tatizo la umeme kuwa ni historia. Tungeweza pia kupunguza gharama za mtumiaji wa umeme.


Tuna tatizo pia la baadhi ya wanasiasa kujiingiza katika kuwekeza kwenye eneo la nishati ya umeme. Wachague kati ya uongozi na uwekezaji. Kiongozi huwezi kuwa na hisa kwenye kampuni binafsi ya kuzalisha umeme na wakati huo huo ukalinda maslahi ya umma badala ya kampuni yako.


Vinginevyo, kwa waliokuwa na utayari wa kuelewa, mahojiano yale ya BBC na Kikwete yamempa nafasi Kikwete ya kujenga hoja ya msingi juu ya nini alichofanikiwa kufanya tangu aingie madarakani katika jitihada za kutatua tatizo la umeme nchini.



Nawasilisha.



Maggid,


Sweden, Jumanne, Julai 26,2011
MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo

Maggid nimerudia kuisoma makala yako mara mbili kama wewe ulivyoirudia mara mbili kusikiliza hayo mahojiano ya Jk na huyo mwandishi wa BBC. Awali ya yote nikuambie tu kwa hili umeteleza katika kulitafsiri /kulifikisha.
Pamoja na kusema JK ni mwanasiasa mahiri kwa kutembea na hizo takwimu mfukoni, nikuulize hizo MW 145 zipo wapi? Kwa kusema hivyo wewe kakufurahisha na takwimu ambazo kiukweli hazipo, watu wanapoteza ajira nenda mahospitalini ukaone hali halisi ndo uje useme hizo takwimu zinatusaidia nini. Unajaribu kufuatilia hata yanaendelea/hali halisi ilivyo kwa Tanesco? Kiukweli TANESCO wamekata tamaa!


Hata kama mwandishi angemuuliza hayo maswali ya ufisadi tusingetegemea jibu jipya zaidi ya yale tuliyozoea kuyasikia kuwa serikali ipo mbioni, tanafanya jitihada kuiongezea meno PCCB, toka nimeingia mimi madarakani nimepeleka kesi nyingi za ufisidi mahakamani na story kama hizo. Au wewe ungetegemea upate jipya kutokana na swali la aina hiyo? Lakini niungane pia na mchangiaji mmoja hapo juu, kuwa kwa serikali makini ingeweza kuchukua hatua za haraka toka huo mwaka 2006, story za makaa ya mawe yaliishia wapi? Si mpaka hii juzi ndo tumeanza kuisikia tena baada ya kuona hali ya umeme nchini imeanza kuwa tete. Tunapofanya mambo haya kwa zima moto matokeo yake ndo masuala ya ufisadi yanatokea ndani yake.

Nikuulize ndugu yangu, hivi hawa viongozi wetu si huwa wanakuja huku Ulaya hivi huwa hawajifunzi kutokana na wanayoyaona huku?

Twende shule tukatafute ukweli na sio kuleta SIHASA kwa suala ambalo linaumiza ndugu zetu huko nyumbani , uchumi wa nchi unayumba. Halafu tunakuja na hoja nyepesi namna hii.


 
Kama hukuona tatizo kwenye speechi yake basi kuna tatizo somewhere. Binafsi sikupenda kusikiliza hadi mwisho kwa maudhi aliyonipa kwa kuongea kwa jazba na hasira. Kwanza swali aliloulizwa ilimzidi uwezo raisi aidha kwasababu ya utendaji mbovu wa serikali yake au kwa nia ya kujilinda kwa kushushuliwa na waziri kivuli wa nishati na madini kutoka Chadema. Hawezi kutujibu kihuni kuwa serikali haina uwezo wa kujaza mabwawa, katika karne hii ya 21 huwezi kutegemea mambo kufanyika kwa kudra za mwenyezi mungu, mvua si kitu reliable, na tatizo la umeme ni la siku nyingi. Tulitegemea raisi atuambia kuwa nitawaleta wataalumu wa kuzalisha mitambo ya nyuklia kwa ajili ya nishati ya umeme, maana kila siku tumekuwa tukiimba Tanzania kuna Uranium sasa kwanini tusitumie neema hii tuliyopewa bure na mwenyezi mungu badala ya kuweka chungwa zako kwenye kikapu kimoja.
 
" Wakati mwingine na nyinyi mjifunze hayo mambo ya kitaalamu kulikoni kuuliza tu hivi hivi. Unajua ungekuwa na wewe unauliza kwa hoja - "unajua kwamba hiki kitu hiki ingekuwa umeme wa jua miezi miwili tu upo" - tungeweza kufanya hivyo." Kikwete anamwambia mwandishi wa BBC.
hiyo statement hapo juu siyo sahihi kwani technologia ya solar power ina zaidi ya miaka kumi sasa walikuwa wapi siku zote achana na miezi 2
anayoitaja vipi kuhusu miaka 5 iliyopita walikuwa wapi? anatumia kigezo cha miezi miwili kama njia ya kukwepa swali kwani tatizo la umeme lina miaka kama ishirini toka lianze alikuwa wapi miaka yote ku develop altenatives za kuzalisha umeme.

Tusisahau, kuwa Kikwete ni mwanasiasa mahiri,
mwanasiasa mahiri hakimbii midahalo.
 
JF bana wananiachaga hoi wakati mwingine.... badala ya kujadili ishu at hand, wanajadili mleta ishu..... kweli ukiwa ni mwenyechuki hata zuri la umchukiaye hulioni!

Tofauti na unavyodai, wengi tunajitahidi kutafsiri tafsiri ya Maggid kuhusu mahojiano ya BBC na JK na tafsiri tunayopata ni kuwa hakuna tofauti yoyote kati ya majibu aliyotoa Kikwete na tafsiri anayotoa Maggid. Kikwete kahojiwa na BBC kuhusu matatizo ya Umeme Tanzania na amekiri yako nje ya uwezo wake na tafsiri ya Maggid ni kuwa matatizo ya Umeme Tanzania yako nje ya uwezo wa Raisi wetu.

Maggid hana tatizo na Watanzania kuendelea kuwa gizani, tatizo la Maggid ni kuwa kuna Watanzania wanathubutu kumlaumu Kikwete ambaye amekiri kutokuwa na uwezo wa kulitatua tatizo la Umeme. Maggid anadai Kikwete alikwenda kwenye mahojiano na takwimu mfukoni zinazoonyesha kuongezeka kwa uzalishaji wa Umeme toka 2009, lakini hapo hapo tunaendelea kubaki gizani - tafsiri, my foot !
 
Nimeipenda hii: Tusisahau kuwa Kikwete ni mwanasiasa mahiri. Kweli ukipenda chongo...

Kwa hakika huyu Majjid simfahamu sana lakini nashindwa kuelewa mtu kama huyu anatetea nini? Mwanasiasa mahiri hawezi kutoa majibu kama yale kabisa. Mwanasiasa mahiri angeweza kuyajibu yale maswali kwa hoja zenye substance hata kama hana data za uhakika. Mwanasiasa mahiri anaweza kukwepa kujibu swali wala usigundue kwamba hakujibu swali. JK alichoweza kutamka kwenye yale mahojiano ni mvua tu; zile other options like Jua, upepo etc yule mtangazaji ali-introduce yeye. Halafu alikuwa ana-interrupt sana (hana composure) kama mtu anayetapata hajui lakusema. In short yeye alitakiwa aeleze ni vipi wameweza kutumia other options than mvua kujaribu kutatua tatizo la umeme. Na kama hizo njia nyingine zimeshindikana then where are we going from here? Yeye anaanza na blame game kwamba matatizo ameyakuta. Well, alipokuwa anapigania uraisi 2005 si alijua haya matatizo yako? Aliporudi temu ya pili si aliyajua yapo? Kwahiyo alitegemea nani ayamalize wakati yeye ndio amepigania mwenyewe kuwa leader(kinara) wakuyamaliza matatizo hayo. Kusema amekuja akayakuta matatizo haisaidii. Yeye mwenyewe alishakuwa waziri wa nishati na madini sijui alikuwa na vision ipi; atuambie basi maana amesema haya matatizo ni ya siku nyingi. Je wakati huo bado option ilikua yakutegemea mvua tu? Kikwete na-kukaa kote kwenye wizara nyeti leave alone as a President anatoa majibu mepesi hivyo? If he has no plan then why is he there? Labda Majid atusaidie kwenye hilo.
 
Back
Top Bottom